MAANDAMANO DHIDI YA RAIS MORSI WA MISRI YAANZA

Raia wa Misri wamefanya maandamano makubwa kote nchini kumshinikiza rais wa taifa hilo Mohammed Morsi, kujiuzulu wakati wa maadhimisho yake ya kwanza tangu achukue hatamu ya taifa hilo. Ijapokuwa barabara za mji wa Cairo zina utulivu kufikia sasa, maafisa wa polisi wamewekwa katika kila sehemu ili kuzuia ghasia. Wapinzani wa rais huyo wanamkashifu kwa kushindwa kutatua maswala ya kimsingi kama vile uchumi pamoja na usalama na kudai kuwa zaidi ya raia millioni 22 wametia sahihi yakutaka uchaguzi mpya kufanyika mara moja. Aidha wanadai kuwa rais Morsi, ameweka ajenda ya Kiislamu ya chama chake cha Muslim brotherhood mbele kushinda mahitaji ya raia wa taifa hilo. Wafuasi wa rais huyo pia wameapa kufanya mikutano ya hadhara kumuunga mkono kiongozi wao ©2013 Venance

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017