AFARIKI URAMBO TABORA KWA KUNYWA VIROBA 12 VYA KONYAGI KATIKA MASHINDANO
Tukio hilo lilitokea juzi tarehe 12 Juni 2013 katika wilaya ya Urambo mkoani Tabora akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa niaba ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo Kaimu Kamanda, Edward Lukombe amemtaja marehemu kuwa ni Juvenali Wambura mwenye umri wa miaka 42, inadaiwa kuwa siku ya tukio baadhi ya wanywaji katika glosari moja waliandaa shindano ambalo si rasmi kuwa mnywaji atakayekunywa viroba 12 ataondoka na zawadi ya pesa taslimu ambapo inadaiwa marehemu alijigamba kuwa angekunywa viroba vyote na hivyo kuibuka mshindi inadaiwa kuwa marehemu alianza kunywa viroba hivyo kwa kasi ya ajabu ambapo alipomaliza kunywa kiroba cha mwisho cha 12 aliishiwa nguvu na hivyo wenzake kulazimika kumpeleka katika hospitali ya wilaya ya urambo kwa matibabu lakini bahati mbaya akafariki dunia muda mfupi.
Kaimu kamanda huyo amesema kuwa licha ya marehemu kunywa viroba vyote hivyo inaelekea hakuwa amepata lishe ya kutosha siku hiyo.
Kaimu kamanda huyo ametahadharisha wanywaji mkoani humo kunywa kwa wastani na kuwa wamekula na sio kunywa kwa mashindano ili kuepuka madhara kama hayo.
Venance ©Juni, 2013
Comments
Post a Comment