RAIA WA AFRIKA KUSINI WAKESHA WAKIMUOMBEA RAIS NELSON MANDELA

Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto. Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika. Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu. Awali mwanawe wa kike, Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema. Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabariwanapaswa kumheshimu babaake. Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi. "leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela. Bwana Zuma alifutilia mbali safariyake ya Msumbiji ili kumtembeleaMandela hospitalini. Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

ORODHA YA MAJINA WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI (AWAMU YA PILI)

BEYONCÉ FT JAY Z-DRUNK IN LOVE SONG LYRICS

ABIRIA 52 WALIOKWAMA KATIKA MELI HUKO ANTAKTIKA WAOKOLEWA

CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER