KIONGOZI WA AL SHABAAB AJISALIMISHA
Mmoja wa viongozi wakuu wa zamani wa kundi la wapiganaji wa Al-shabaab, Hassa Dahir Aweyes amewasili mjini Mogadishu chini ya ulinzi mkali wa vikosi vya serikali.
Hata hivyo haijulikani iwapo kiongozi huyo amesalimu amri auameamua kujiunga na vikosi hivyo vya serikali.
Ijumaa iliopita, umoja wa mataifaulitangaza kuwa Bwana Hassa Dahir alikuwa amejisalimisha kwavikosi vya serikali ya Somali lakinimadai hayo yakapingwa na wazee wa koo za taifa hilo.
Kiongozi huyo alikuwa amechukua hifadhi katika mji wa Kazkazini wa Adado baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya kambi tofauti za wapiganaji wa Al Shabaab juma lililopita.
Kiongozi huyo ametajwa kama gaidi na umoja wa mataifa pamoja na serikali ya marekani.
©2013 Venance
Comments
Post a Comment