Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kuaga miili ya waliokufa katika tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Maafa zaidi yameripotiwa katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea juzi mkoani Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo kuongezeka na kufikia watu 16, huku wengine 253 wakijeruhiwa na kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo, pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule yameanguka. Tukio hilo limemfanya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kulazimika kufanya ziara ya ghafla ya kuwatembelea waathirika wa tetemeko hilo, ambalo limedaiwa kusababisha tafrani pia katika nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki za Kenya na Rwanda. Katika hatua nyingine, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo eneo la Tengeru, mkoani Arusha kimeeleza mpango wa kuanza kufunga vifaa vitakavyotoa ishara ya matukio ya matetemeko ya ardhi kabla majanga ha...