MAJARIBIO KATI YA ChatGPT, BING CHAT NA GOOGLE BARD
Maendeleo ya teknolojia ya Akili Bandia (AI) yamebadilisha jinsi tunavyofanya kazi na mambo mengine mengi katika miezi ya hivi karibuni na hivyo kumpa karibu mtu yeyote uwezo wa kuandika msimbo (code), kuunda sanaa na hata kuwekeza. Kwa watumiaji wa kitaalamu na wale wenye mapenzi na teknolojia, programu zalishi za AI, kama vile ChatGPT, huangazia uwezo wa hali ya juu ili kuunda maudhui yenye ubora kutokana na maelezo rahisi anayotoa mtumiaji. Microsoft imeongeza GPT-4 katika Bing, OpenAI inaongeza uwezo mpya kwenye ChatGPT na Bard inaunganisha kwenye mfumo mzima wa Google yani kwamba chochote kinachoweza kupatikana kupitia Google utakipata kwenye Bard pia. Uwepo wa robotisogozi hizi 3 za hivi punde za AI kunaweza kumtatanisha mtumiaji ipi inamfaa zaidi. Kujua ipi kati ya robotisogozi tatu maarufu za AI ni bora kuandika msimbo, kutoa maandishi, au kusaidia kuunda wasifu ni changamoto, kwa hivyo nakueleza hapa tofauti kubwa zaidi ili uweze kuchagua inayolingana na mahitaji y...