RAIS KIKWETE AELEKEZA NGUVU KATIKA ELIMU YA KIDATO CHA 5 & 6
Rais Jakaya Kikwete akipokea tuzo maalum kutoka kwa Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jana. Picha na Ikulu Rais Jakaya Kikwete jana alitumia kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu kuaga wadau wa sekta hiyo, akisema sasa nguvu zielekezwe katika kujenga majengo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu ya sekondari. Rais Kikwete, ambaye alikiri kuwapo udhaifu katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, alisema mafanikio pia ni makubwa kiasi kwamba sasa hakuna wanafunzi wanaokosa nafasi ya kwenda sekondari baada ya kufaulu na hivyo nguvu sasa inatakiwa kuwekwa katika kuongeza miundombinu ya kidato cha tano na sita. Kikwete alitoa kauli hiyo jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa alipohutubia maelfu ya wakazi wa Dodoma, wakiwamo wanafunzi wa shule za sekondari na msing...