WABUNGE: "BILA KILIMO KWANZA HAKUNA SERIKALI YA VIWANDA"

 
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamesema bila kuwekeza katika kilimo, azima ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda haitatimia.

Kadhalika, wameipongeza Serikali kwa kuondoa tozo 108 zilizokuwa kero kwa wakulima na kuitaka Serikali kuhakikisha tozo zilizoondolewa zinawanufaisha zaidi wakulima na Watanzania, badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara pekee. Waliyasema hayo jana kwa nyakati tofauti bungeni Dodoma wakati wakichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Fedha 2017/18.

Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile (CCM), alisema kama Tanzania inataka kuwa ya viwanda, haina budi kuwekeza katika utafiti kwa ajili ya sekta ya kilimo ili kubaini namna bora zaidi za kutumia rasilimali na fursa zilizopo ili kuimarisha kilimo na hivyo kusaidia kufikia haraka azima ya kujenga Tanzania ya viwanda. Alisema tayari fursa za kuinua kilimo na kukifanya uti wa mgongo nchini zimeanza kuonekana kwani kwa sasa Tanzania ndiyo inayouza vyakula na bidhaa za biashara katika nchi mbalimbali duniani zikiwemo nchi za Sudan, Kenya na Uganda wanaonunua mazao ya chakula kama mahindi.

“Nchi kama India inanunua kwetu korosho, choroko na tumbaku. Kwa sasa mipango ni kuipeleka nchi kwenye viwanda ni wakati muafaka wa kuwekeza kwenye kilimo kwa kufanya utafiti za kisayansi za namna bora ya kuendeleza kilimo chetu kwa sababu kilimo ndio ajira, chakula na fedha,” alisisitiza. Alisema Tanzania inasifika kwa kufanya utafiti, lakini pamoja na kuwa na uwezo huo bado haujatumika vizuri kuendeleza mambo ya msingi yakiwamo maeneo ya kilimo, mifugo na uvuvi.

“Kwa mfano sisi ndio wenye eneo kubwa katika Ziwa Victoria, lakini takwimu za kidunia zinaonesha Uganda yenye sehemu ndogo katika ziwa hilo ndiyo inayoshika nafasi ya juu; ya sita duniani kwa uvuvi huku sisi Tanzania tukishika nafasi ya nane,” alisema. Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (CCM) aliitaka serikali iwekeze kwenye utafiti wa kilimo ili kuyabaini maeneo ya kijiografia na kisayansi yanayoweza kuikuza kwa kasi sekta hiyo ya kilimo inayokwenda sambamba na sekta ya viwanda.

“Kwa mfano Morogoro ina udongo wenye rutuba na mito inayotiririsha maji kwa mwaka mzima, utafiti ukifanyika wa namna bora ya kutumia rasilimali hizo, ni wazi kuwa Morogoro pekee inaweza kulisha Tanzania nzima,” alisema. Pamoja na hayo mbunge huyo alisema si kweli utitiri wa kodi zilizofutwa na serikali umewalenga zaidi wafanyabiashara na wenye kampuni na si wakulima kwa kuwa wafanyabiashara na kampuni hizo kutokana na kufutwa kwa tozo hizo kuanzia sasa watanunua mazao na bidhaa hiyo kwa bei inayostahili.

Kwa upande wake Mbunge wa Hanang, Mary Nagu (CCM), alisema serikali haina budi kuzingatia kuwa kilimo ndicho kinachochangia ajira kwa Watanzania takribani asilimia 65, kinachozalisha chakula kwa Watanzania kwa asilimia 100 na kuingiza asilimia 28 katika pato la taifa. “Hii ni sekta muhimu sana, ni vema Serikali ione umuhimu wa kuifanyia mageuzi sekta ya kilimo na kuongeza bajeti ya wizara ya kilimo kwani hali ilivyo sasa badala ya kilimo kukua, kinashuka kwa kasi,”alisema.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2011 kilimo kilikuwa kwa wastani wa asilimia 3.5 lakini miaka sita baadaye yaani mwaka2016 kilimo hicho kilishuka na ukuaji wake kufikia asilimia 1.7 hali inayozidisha umasikini kwa Watanzania,” alisema Dk Nagu. Alisema pamoja na ukuaji wa kilimo pia bajeti ya Wizara ya Kilimo imekuwa ilishuka badala ya kupanda kila mwaka kwani mwaka 2011 bajeti ya Wizara hiyo ilikuwa asilimia 7.8 ya bajeti nzima ya Serikali, lakini katika bajeti ya mwaka 2016, bajeti ya Wizara hiyo ilishuka na kufikia asilimia 4.9.

Nagu aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika Serikali ya Awamu ya Nne, kupongeza hatua ya Serikali kuondoa utitiri wa kodi zenye kero kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, aliitaka Serikali ihakikishe kuwa hatua hiyo inawanufaisha zaidi wakulima, wafugaji na wavuvi na si kwa wafanyabiashara.

Kwa upande wake mbunge wa Malindi, Ally Saleh (CUF) aliishauri serikali iwekeze zaidi kwenye fikra za kuleta mabadiliko ya kilimo, mifugo na uvuvi kutokana na ukweli kuwa Tanzania imebarikiwa rasilimali kama vile maziwa, mito, bahari na mikoa yenye rutuba ambayo endapo itatumiwa vema itakuza sekta hizo.
“Sasa hivi tuna tatizo gani, badala ya kilimo kwenda mbele kinashuka. Leo hii haiwezekani sisi tunaongoza kwa kuwa na ng’ombe wengi kuliko Kenya, lakini wao wanatuzidi kwa kuzalisha maziwa. Tunahitaji fikra mpya,” alisema. Alisema Tanzania kuna hekta takribani milioni 13.5 zinazolimika na hekta milioni 1.5 za mikoko, pia ni nchi ya tatu Afrika lakini pia nchi ya 11 duniani kwa kuwa na wingi wa mifugo, lakini bado rasilimali hizo haijatumiwa vizuri.

Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), aliishauri Serikali iwekeze zaidi katika kilimo kupitia mbolea ya uhakika, dawa za mimea, masoko na miundombinu bora kwa kuwa huo ndio usalama wa watanzania katika chakula.


Chanzo: Habari Leo

TRUMP AWASILI SAUDI ARABIA

Rais Donald Trump  akikaribishwa  kwa bashasha  kubwa  na  ukoo  wa  kifalme  wa  Saudi Arabia  jana , wakati  akiweka  kando, japokuwa  kwa  muda  tu , utata mkubwa  unaoukumba utawala  wake  mjini  Washington.
Saudi Arabien - Donald Trump zu Besuch in Riad (picture-alliance/dpa/AP/E. Vucci)
Rais Trump akilakiwa mjini Riyadh
Trump  amewazawadia  wenyeji wake  mpango  wa mauzo  ya  bilioni 110  wa  silaha  wenye  lengo  la  kuimarisha  usalama  wa  Saudi  Arabia pamoja  na  makubaliano  kadhaa  ya  kibishara.
"Hii  ni  siku  muhimu  sana, uwekezaji  mkubwa  katika  Marekani ," Trump  alisema wakati wa  mkutano  na  mwanamfalme Mohammed bin Nayef.
Auslandreise US-Präsident Trump in Saudi-Arabien (Getty Images/AFP/M. Ngan)
Rais Trump (Kushoto) akisalimiana na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz(kulia)
Ziara  katika  mji  mkuu  wa  Saudi Arabia  ilikuwa  ni ziara  ya  kwanza  ya  Trump  nje  ya nchi  akiwa  rais, ikiwa  ni  ziara  itakayokuwa  na vituo  vitano ambayo  itamchukua  katika mataifa  ya  mashariki  ya  kati  hadi  Ulaya. Ni  rais  pekee  wa  Marekani kuifanya  Saudi Arabia , ama  taifa  lolote  lenye  Waislamu  wengi kuwa  kituo  chake  cha  kwanza  nje  ya nchi.
Trump  aliwasili  mjini  Riyadh akizongwa  na  hatua  yake  ya  kumfuta  kazi  mkurugenzi  wa FBI James Comey  na  hali  ya  kufichuka zaidi  juu  ya  uchunguzi  wa  serikali  kuu kuhusiana  na  uwezekano  wa  mahusiano  ya kampeni  na  Urusi.
Akikimbia  mambo  mjini Washington  na  kukumbatiwa  na  familia  ya  kifalme inaonekana kumpa  nguvu  Trump.
Melania  hakufunika nywele
Baada  ya  safari  ya  usiku  kucha , rais  alilakiwa  katika  uwanja  wa  ndege  na  Mfalme Salman , hali  iliyoonekana kuwa  ni  ya  aina  ya  kipekee  kwa  kuwa  mfalme  hakuonekana mwaka  jana  wakati  wa  kumlaki rais Barack Obama  katika  ziara  yake  ya  mwisho  nchini Saudi  Arabia.
Saudi Arabien US-Präsident Trump und König Salman bin Abdulaziz al-Saud unterzeichnen Verträge (Getty Images/AFP/M. Ngan)
Rais Trump akitia saini makubaliano ya mauzo ya silaha pamoja na mfalme Salman bin Abdulaziz al-Saud
Trump  aliongozana  katika  ziara  yake  hiyo  na  mkewe Melania  Trump, ambaye  alivalia suti  nyeusi na  mkanda  wa  dhahabu, lakini  hakufunika  nywele  zake  katika  nchi  hiyo  ya kifalme  ambayo ni  ya  kihafidhina  zaidi, kwa  mujibu  wa  utamaduni  wa  ujumbe  wa kimagharibi.
Mapokezi  makubwa  ya  Trump  yanaakisi  kiwango  ambacho  Saudi  Arabia  imekuwa hairidhishwi  na  Obama. Wasaudi  kwa  kiasi  kikubwa  hawakumuamini  Obama  kuhusiana na  mahusiano  yake  na  Iran na  wamekasirishwa  na  mtazamo  wake  wa  kujizuwia kuhusiana  na  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe  nchini  Syria.
Auslandreise US-Präsident Trump in Saudi-Arabien - Melania Trump (Getty Images/AFP/M. Ngan)
Mke wa rais wa Marekani Melania Trump(kushoto) akiwa pamoja na mwanamfalme Muhammad nin nayef bin Abdulaziz al-Saud
Wairani wachagua rais
Wakati  Trump  anawasili , Wairani  walikuwa  wamemchagua  tayari  Hassan Rouhani , mmoja  kati  ya  washirika  wa  Obama   katika  makubaliano  ya  kihistoria  yaliyokuwa  na lengo  la  kudhibiti  nia  ya  Iran  ya  kujipatia  silaha  za  kinyuklia, kwa  muhula  wa  pili  wa miaka  minne kuwa  rais, akielezea  msukumo  wake  kwa  ajili  ya  uhuru  zaidi  na kuzijongelea  zaidi  nchi  nyingine  duniani.
Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani  Rex Tillerson  amesema  ana  matumaini Rouhani  atatumia  kipindi chake  hicho  kipya  madarakani  "kuanza  mchakato  wa kuvunjilia  mbali  mtandao  wa kigaidi  wa  Iran."
Donald Trump, Melania Trump, König Salman (picture alliance/AP Photo/E.Vucci)
Rais Trump akiwasili katika kasri la mfalme wa Saudi Arabia



Trump  hakutoa  matamshi yeyote  katika  siku  yake  ya  kwanza  nje  ya  nchi  na  alitumia muda  wake  mwingi  akitembea  kati ya  vyumba  mbali  mbali  vya  kasri  la  mfalme.
Chanzo: DW

KOREA KASKAZINI IMEFANYA JARIBIO LINGINE LA KOMBORA

Korea Kaskazini yalifanyia majaribio kombora lingineJeshi la Korea Kusini linasema kuwa Korea Kaskazini imefanyia majaribio kombora lingine.Ofisi ya kijeshi nchini Korea Kusini inasema kuwa kombora hilo lilirushwa siku ya Jumapili jioni saa za Korea.

Jaribio hilo linafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kulifanyia majaribio kombora lingine ambalo inadai kuwa ni jipya na ambalo lina uwezo wa kubeba silaha kubwa ya nyuklia. Wachambuzi wanasema kwamba huko mbeleni linaweza kuifikia Alaska.

Jumatatu iliyopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio kama hayo.

Baraza hilo la UN lilisisitiza umuhimu wa nchi hiyo kuachana na hatua hizo.Korea Kaskazini inafahamika kwa kuunda zana za nyuklia na imefanya jumla ya jaribio matano ya nyuklia na ya makombora yenye uwezo wa kusafirisha zana hizo hadi maeneo inayolenga.

Korea Kusini inasema kuwa jaribio la hivi punde lilifanyiwa eneo la Pukchang magharibi mwa nchi.

Chanzo: BBC & DW

VIDEO: JAY 2 THE HUSTLER X CAST BEEZY - TIME IS NOW (OFFICIAL VIDEO)

 

MGAHAWA WAKUMBWA NA KASHFA YA KUUZA NYAMA YA BINADAMU

Mkahawa wakumbwa na habari bandia za kuuza ''nyama ya binadamu''Mgahawa mmoja mjini London umekumbwa na habari bandia za kuuza nyama ya mtu.

Wafanyikazi katika mkahawa wa Karri Twist katika eneo la New Cross nchini Uingereza wamehangaishwa kwa kupigiwa simu kutoka kwa wateja wanaosema ''Kwa nini hamujafunga''?.
Mkahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu la mkahawa huo.

Na watu wengine waliamini mzaha huo.
Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari cha channel23news.com, mtandao ambao wateja wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja kwa moja katika mtandao wa fecbook.

Shinra Begum ambaye ndio mmiliki wake aliambia Newsbeat kwamba biashara hiyo ya familia imekumbwa na wakati mgumu tangu habari hiyo ilipochapishwa siku ya Alhamisi.
''Wakati watu walipoanza kunipigia simu na kuuliza iwapo tulikuwa tukiuza nyama ya binadamu sikuamini''.

''Nilishtuka nilipoaana habari hiyo katika mtandao na kuendelea kusambazwa katika mtandao wa facebook''.

Sasa watu wametishia kulivunja jengo letu na nimelazimika kuketi chini na mteja ili kumuelezea kwamba yote hayo ni madai ya uwongo.

Shinra anasema kuwa alilazimika kuripoti kwa maafisa wa polisi kwa sababu lilikuwa swala lililomtia wasiwasi mkubwa.

Njia ya pekee ambapo Karri Twist iliweza kukabiliana na chuki hiyo ni kupitia kuchapisha katika mtandao wao ili kuhakikisha kwamba watu wanajua kwamba hilo halikuwa la kweli.

Chanzo: BBC

NDEGE YA MAREKANI YAZUILIWA NA NDEGE ZA CHINA

Ndege za China zaizuia ndege ya MarekaniNdege mbili za kijeshi za China zimeizuia 'vibaya' ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani.

Ndege hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa bahari ya China.
Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini. 

China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na maji hayo yenye utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake ,hatua ambayo imesababisha wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.
''Swala hilo linaangaziwa na China kupitia njia mwafaka ya kidiplomasia mbali na zile za kijeshi'', msemaji wa jeshi la angani la Marekani Luteni kanali Lori Hodge amesema.
''Uzuizi huo haukufanywa kwa njia ya ''utaalamu'' kutokana na hali ya rubani wa ndege hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili'', aliongezea akisema uchungzi wa kijeshi unaendelea.
Bahari hiyo ya kusini mwa China
Bahari ya Kusini mwa China
Mnamo mwezi Februari , ndege moja ya Marekani ilianza kile Washington ilielezea kuwa doria yake ya kawaida kusini mwa bahari ya China ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.
Ndege na meli hizo zilielekea katika eneo hilo licha ya onyo kutoka China dhidi ya kutoa changamoto yoyote kwa uhuru wa China katika eneo hilo.

Kwa nini bahari hiyo ya kusini mwa China inazozaniwa?
Mnamo mwezi Mei 2016 ndege mbili za kijeshi za China zilizuia ndege nyengine ya Marekani iliokuwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China.

Wakati huo, jeshi la Marekani lilisema kuwa ilikuwa ikipiga doria ya kawaida katika eneo hilo.

Chanzo: BBC

MABOMU YASABABISHA WATU ZAIDI YA ELFU 50 KUHAMA UJERUMANI

Mabomu kutoka vita vya pili vya dunia bado yako Hannover

Operesheni kubwa ya kuwaondoa wakaazi wengi wa mji wa Hanover ulioko kaskazini mwa Ujerumani, inaendelea, ya kuwahamisha zaidi ya watu elfu 50 baada ya mabomu makubwa ya wakati wa vita vya dunia, kupatikana kama hayajalipuka.
Wakaazi hao wanatarajiwa kuondoka majumbani mwao baadaye leo, ili kuwapa nafasi wataalamu wa kutegua mabomu, kuhamishia mahala salama mabomu hayo ambayo yanakisiwa kuwa matano.

Operesheni hiyo itachukua siku nzima, na hata zaidi ikiwa mabomu mengineyatapatikana.
Washambuliaji walivamia mji wa Hanover mara 125 kwa mabomu, wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.
Wataalamu wanaamini kuwa mabomu ambayo hayakulipuka huenda yako chini ya jengo hiliHaki miliki ya picha Getty Images.    Wataalamu wanaamini kuwa mabomu ambayo hayakulipuka huenda yako chini ya jengo hili                
Zaidi ya asilimia 20 ya mabomu yaliyoangushwa mjini humo hayakulipuka.
Baadhi ya mabomu mengine yalikuwa na vifaa vinavyochukua muda mrefu kulipuka, na ambayo kwa sasa yameanza kuoza, na kusababisha hatari kubwa.


Chanzo: BBC

WAPIGANAJI WA HAMAS WAPATA KIONGOZI MPYA

Ismael Haniyeh ndio kiongozi mpya wa kundi la Hamas
Ismael Haniyeh ndio kiongozi mpya wa kundi la Hamas
Wapiganaji wa Palestina Hamas wamepata kiongozi mpya.
Kiongozi huyo ni Ismail Haniyeh ambaye hadi hivi karibuni alikuwa ndio kiongozi wa kundi hilo katika ukanda wa Gaza.
Akijulikana kama kiongozi anayetumia akili nyingi wakati wa kutatua maswala, anachukua mahala pake Khaled Meshaal ambaye ameliongoza kundi hilo akiwa ughaibuni kwa miongo miwili.
Uchaguzi wa kiongozi mpya ulifanyika kupitia njia ya Video Link kati ya wajumbe waliopo katika ukanda wa Gaza na wale waliopo nchini Qatar ambako Meshaal ana makao yake.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa bwana Meshaal anaachia ngazi wakati ambapo Hamas limeanza kulegeza msimamo wa kisiasa.
Kwa mara ya kwanza wiki iliopita katika sera mpya kundi hilo liliwachilia wito wake wa kuiharibu Israel.
Hamas bado lina wapiganaji wake katika eneo la Gaza na bado linaaminika kuwa kundi la kigaidi na Israel Marekani na mataifa ya bara Ulaya.

Chanzo: BBC

MANCHESTER CITY YAIBURUZA VIBAYA CRYSTAL PALACE

Tokeo la picha la Machester City
Klabu ya Manchester City imerudi katika nafasi yake ya tatu katika ligi ya Uingereza baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Crystal Palace ambayo imeshindwa kwa mara ya tatu mfululizo.
City ilihitaji dakika mbili pekee kupata bao la kwanza baada ya David Silva kufunga baada ya kurudi kutoka kuuguza jereha.
Wenyeji waliongeza bao la pili dakika tatu katika kipindi cha pili wakati Vincent Kompany alipopiga mkwaju ulioingia katika kona ya ya juu ya goli na baadaye Kevin De Bruyne akafunga bao la tatu.
Ndoto ya Palace ilithibitishwa baada ya Raheem Sterling kufunga bao la nne kabla ya beki Otamendi kufunga bao la tano katika dakika za lala salama.
Kikosi hicho cha Sam Allardyce kiko pointi tano juu ya eneo la kushushwa daraja na kinaweza kuwa hatarini iwapo klabu za Hull City na Swansea zitaibuka washindi siku ya Jumamosi.

RAIS MAGUFULI AMETUMA SALAMU ZA POLE KWA WAFIWA WA AJALI ARUSHA

Tokeo la picha la magufuli
Hii hapa chini ni taarifa kama ilivyoandikwa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko mkubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea leo saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.
Kufuatia ajali hiyo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na taifa kwa ujumla.
"Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo naomba unifikishie pole nyingi kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, walimu na dereva waliopoteza maisha, hiki ni kipindi kigumu kwetu sote, na uwaambie naungana nao katika majonzi na maombi.
"Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu" Amesema Rais Magufuli.

KANYE WEST AMEFUTA AKAUNTI ZAKE KATIKA MITANDAO YA KIJAMII


Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na makumi ya mamilioni ya wafuasi.
Sababu hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema.
Alimshtumu mwanamuziki mwenza Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo.
Mkewe nyota wa Raality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.
Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati mashabiki walipojaribu kuwasiliana na msanii huyoHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionHivi ndivyo ilivyokuwa wakati mashabiki walipojaribu kuwasiliana na msanii huyo
Amekuwa akijikuza pamoja na kampuni ya kuuza nguo ya mumewe.
Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake.
Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika mtandaoo wa Twitter wa mkewe Kim KardashianHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionHivi ndivyo ilivyokuwa katika mtandaoo wa Twitter wa mkewe Kim Kardashian
West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump.
Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba.

MFAHAMU KARL MARX KWA UFUPI: DUNIA INAMKUMBUKA LEO

Karl Mark alikuwa ni mwanafalsafa na mwanamapinduzi wa Ujerumani aliyeandika vitabu vya The Communist Manifesto na Das Capital vitabu ambavyo vilikuwa vikipingana na mfumo wa kibepari na kuunda mfumo wa Ukomunisti ama Ujamaa kama alivyoutafsiri hayati Mwalimu JK Nyerere.

Karl Marx alizaliwa Mei 5, 1818. Alianza kuchunguza nadharia za kijamii alipokuwa Chuo Kikuu na wenzie waliounda kikundi chao kilichoitwa Young Hegelians. Hiki kilikuwa ni kikundi kilichokuwa kinaamini katika falsafa za mwalimu wao aliyeitwa Hegel. Marx alikuwa mwandishi wa habari na machapisho yake kuhusu Ukomunisti vilipelekea yeye kufukuzwa Ujerumani na Ufaransa. Mwaka 1848 alichapisha kitabu chake cha The Communist Manifesto akiwa na Friedrich Engels ambacho kilipelekea kufukuzwa Ujerumani na kukimbilia London, Uingereza, huko pia aliandika kitabu cha Das Kapital ambako ndiko alikoishi mpaka alipoiaga dunia.

Karl Marx alikuwa ni miongoni mwa watoto 9 wa Heinrich Marx na Henrietta Marx huko Trier Prussia ya zamani (kwa sasa Ujerumani) Baba yake alikuwa mwanasheria aliyefanikiwa sana na alikuwa mwanaharakati aliyependa mabadiliko nchini Prussia. Japokuwa wazazi wake walikuwa na asili ya Kiyahudi, baba yake Marx alihamia katika Ukristu mwaka 1816 alipokuwa na umri wa miaka 3.

Marx alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida. Alisomea nyumbani hadi alipokuwa na umri wa miaka 12 na kisha alipelekwa Jesuit High School alikosoma kwa muda wa miaka 5 kuanzia 1830 hadi 1835.

Mwaka 1835 Marx alijiunga na Chuo Kikuu cha Bonn. Chuo hiki kilikuwa na Itikadi za kuipinga serikali. Marx alijiunga na maisha ya uanafunzi katika chuo hiki. Katika semista mbili chuoni hapo, alifungwa kwa ulevi na kuvuruga amani chuoni hapo, kuwa na madeni lakini pia kushiriki katika falsafa zilizokinzana na chuo. Mwisho wa mwaka baba yake Marx alimsisitiza kuwa serious na masomo katika Chuo Kikuu cha Berlin.

Katika Chuo Kikuu Berlin alisomea fani ya sheria na falsafa ambako alikutana na falsafa za mwalimu wake George Hegel ambaye alikuwa profesa katika chuo hicho mpaka alipofariki mwaka 1895. Baadaye Marx alijiunga na kikundi cha Young Hegelians ambacho pia kulikuwa na Bruno Bauer na Ludwig Feuerbach ambao walikosoa kuanzishwa kwa siku za kisiasa na kidini nchini humo. Kuna mengi yalijiri Marx alipokuwa Berlin.
Tokeo la picha la marx and bruno bauer
Bruno Bauer
Marx hakutulia wala kuishia hapo. Mwaka 1841 alitunukiwa Shahada yake ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Jena lakini harakati zake za kisiasa zilipelekea yeye kutokuaminiwa na kuwa mwalimu katika chuo chochote nchini Ujerumani. Alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari na mwaka 1842 alikuwa Mhariri wa Rheinische Zeitung ambalo lilikuwa ni gazeti la wanaharakati wa usawa huko Cologne, Ujerumani. Mwaka mmoja baadaye serikali ililifuta gazeti hilo kuanzia April 1, 1843. Marx aliacha kazi hapo Machi 18. Miezi mitatu baadaye alimuoa Jenny von Westephalen  na Oktoba walihamia Paris, Ufaransa.
Tokeo la picha la karl marx and his family
Marx akiwa na mkewe Jenny von Westephalen
Mji wa Paris ulikuwa ni kitovu cha harakati za kisiasa barani Ulaya mwaka 1843. Huko Marx akiwa na Arnold Ruge, walianzisha gazeti la uchambuzi wa kisiasa lilioitwa Deutsch-Franzosische Jahrbucher (German-French Annals) jambo moja tu ndilo lilikuwa likichapishwa katika gazeti hili kabla Marx na Ruge hawajatofautiana kiitikadi hadi kupelekea gazeti hilo kupotea kwenye ramani lakini Agosti 1844, gazeti hilo liliwaleta pamoja Marx na Friedrich Engels kama mwandishi mshiriki ambaye alikuwa msaidizi wake na rafiki yake hadi kifo. Pamoja, wawili hao walianza kuandika makala za kukosoa mawazo ya Bruno Bauer ambaye alikuwa ni mshiriki katika kikundi cha Young Hegelians. Mwaka 1845 Marx na Engels walichapisha makala yao iliyojulikana kama The Holy Family.


Baadaye katika mwaka huo, Marx alihamia Ubeligiji baada ya kufukuzwa nchini Ufaransa ambako aliandika katika gazeti la Vorwarts! ambalo lilikuwa na itikadi ambazo baadaye zingepelekea kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kikomunisti. Alipokuwa Ubeligiji, Marx alipokelewa na Moses Hess, na baadaye aliachana kabisa na siasa za Young Hegelians. Alipokuwa nchini humo aliandika The German Ideology ambako ndiko alipoandika nadharia yake inayojulikana kama Historical Materialism. Marx hakupata mtu wa kuruhusu kuchapisha makala yake. The German Ideology na Theses on Feuerbach hayakuchapisha makala hiyo hadi alipofariki. Nadharia hii inawataka watu kushiriki kwa vitendo kupinga uonevu.


Tokeo la picha la Karl marx and engels
Karl Marx & Friedrich Engels
Mwanzoni mwa mwaka 1846, Mark alianzisha Communist Correspondence Committee katika juhudi zake za kuunganisha ukomunisti barani Ulaya. Waingereza walivutiwa na sera zake na kuitisha mkutano na kuunda shirikisho lao Communist League na mwaka 1847 katika mkutano wao mkuu uliofanyika London, shirikisho hilo liliwaomba Marx na Engels kuandika Manifest der Kommunistischen Partei (Manifesto of the Communist Party)

The Communist Manifesto ni miongoni mwa kazi maarufu za Marx ambayo ilichapishwa mwaka 1848 na baadaye mwaka 1849 Marx alifukuzwa nchini Ubeligiji. Alikwenda Ufaransa ambako alianzisha vuguvugu la Mapinduzi nchini humo ambako pia alifukuzwa. Prussia ilikataa kumpokea Marx na hivyo alihamia London japokuwa Uingerza ilikataa kumpa uraia nchini humo hadi kifo chake.

Marx alipokuwa London alisaidia kuundwa kwa shirikisho la wanataaluma wa Ujerumani German Workers' Educational Society lakini pia Shirikisho la Kikomunisti The Communist League. Aliendelea kufanya kazi kama mwandishi japokuwa safari hii alizuiwa na baadhi ya itikadi zake. Alifanya kazi katika The New York Daily Tribune kwa miaka 10 kuanzia 1852-1862 lakini hakulipwa , aliishi kwa kusaidiwa na rafiki yake Engels.

Marx aliutazama mfumo wa kibepari zaidi na mwaka 1867 alichapisha toleo la kwanza la kitabu chake Das Kapital. Baadaye alitumia muda wake kupitia chapisho hilo na akawa akilifanyia masahihisho na kuongeza baadhi ya vitu. Matoleo mawili yaliyofuata baadaye ambayo hata hakuyakamilisha yaliunganishwa na kuchapishwa na Engels.

Marx alifariki kwa ugonjwa wa mapafu unaojulikana kitaalamu kama pleurisy alipokuwa London Machi 14, 1883. Katika kaburi lake kuna maandishi ya kitabu chake The Communist Manifesto yenye maana wafanyakazi wote waungane.



MAKALA HII IMEANDALIWA KWA MSAADA WA MTANDAO INAWEZA KUFANYIWA MAREKEBISHO MUDA WOWOTE PANAPOHITAJIKA.