MANCHESTER CITY YAIBURUZA VIBAYA CRYSTAL PALACE
Klabu ya Manchester City imerudi katika nafasi yake ya tatu katika ligi ya Uingereza baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Crystal Palace ambayo imeshindwa kwa mara ya tatu mfululizo.
City ilihitaji dakika mbili pekee kupata bao la kwanza baada ya David Silva kufunga baada ya kurudi kutoka kuuguza jereha.
Wenyeji waliongeza bao la pili dakika tatu katika kipindi cha pili wakati Vincent Kompany alipopiga mkwaju ulioingia katika kona ya ya juu ya goli na baadaye Kevin De Bruyne akafunga bao la tatu.
Ndoto ya Palace ilithibitishwa baada ya Raheem Sterling kufunga bao la nne kabla ya beki Otamendi kufunga bao la tano katika dakika za lala salama.
Kikosi hicho cha Sam Allardyce kiko pointi tano juu ya eneo la kushushwa daraja na kinaweza kuwa hatarini iwapo klabu za Hull City na Swansea zitaibuka washindi siku ya Jumamosi.
Comments
Post a Comment