KANYE WEST AMEFUTA AKAUNTI ZAKE KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na makumi ya mamilioni ya wafuasi.
Sababu hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema.
Alimshtumu mwanamuziki mwenza Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo.
Mkewe nyota wa Raality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.
Amekuwa akijikuza pamoja na kampuni ya kuuza nguo ya mumewe.
Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake.
Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao.
West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump.
Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba.
Comments
Post a Comment