TRUMP AWASILI SAUDI ARABIA
Rais Donald Trump akikaribishwa kwa bashasha kubwa na ukoo wa kifalme wa Saudi Arabia jana , wakati akiweka kando, japokuwa kwa muda tu , utata mkubwa unaoukumba utawala wake mjini Washington.
Trump amewazawadia wenyeji wake mpango wa mauzo ya bilioni 110 wa silaha wenye lengo la kuimarisha usalama wa Saudi Arabia pamoja na makubaliano kadhaa ya kibishara.
"Hii ni siku muhimu sana, uwekezaji mkubwa katika Marekani ," Trump alisema wakati wa mkutano na mwanamfalme Mohammed bin Nayef.
Ziara katika mji mkuu wa Saudi Arabia ilikuwa ni ziara ya kwanza ya Trump nje ya nchi akiwa rais, ikiwa ni ziara itakayokuwa na vituo vitano ambayo itamchukua katika mataifa ya mashariki ya kati hadi Ulaya. Ni rais pekee wa Marekani kuifanya Saudi Arabia , ama taifa lolote lenye Waislamu wengi kuwa kituo chake cha kwanza nje ya nchi.
Trump aliwasili mjini Riyadh akizongwa na hatua yake ya kumfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey na hali ya kufichuka zaidi juu ya uchunguzi wa serikali kuu kuhusiana na uwezekano wa mahusiano ya kampeni na Urusi.
Akikimbia mambo mjini Washington na kukumbatiwa na familia ya kifalme inaonekana kumpa nguvu Trump.
Melania hakufunika nywele
Baada ya safari ya usiku kucha , rais alilakiwa katika uwanja wa ndege na Mfalme Salman , hali iliyoonekana kuwa ni ya aina ya kipekee kwa kuwa mfalme hakuonekana mwaka jana wakati wa kumlaki rais Barack Obama katika ziara yake ya mwisho nchini Saudi Arabia.
Rais Trump akitia saini makubaliano ya mauzo ya silaha pamoja na mfalme Salman bin Abdulaziz al-Saud
Trump aliongozana katika ziara yake hiyo na mkewe Melania Trump, ambaye alivalia suti nyeusi na mkanda wa dhahabu, lakini hakufunika nywele zake katika nchi hiyo ya kifalme ambayo ni ya kihafidhina zaidi, kwa mujibu wa utamaduni wa ujumbe wa kimagharibi.
Mapokezi makubwa ya Trump yanaakisi kiwango ambacho Saudi Arabia imekuwa hairidhishwi na Obama. Wasaudi kwa kiasi kikubwa hawakumuamini Obama kuhusiana na mahusiano yake na Iran na wamekasirishwa na mtazamo wake wa kujizuwia kuhusiana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Mke wa rais wa Marekani Melania Trump(kushoto) akiwa pamoja na mwanamfalme Muhammad nin nayef bin Abdulaziz al-Saud
Wairani wachagua rais
Wakati Trump anawasili , Wairani walikuwa wamemchagua tayari Hassan Rouhani , mmoja kati ya washirika wa Obama katika makubaliano ya kihistoria yaliyokuwa na lengo la kudhibiti nia ya Iran ya kujipatia silaha za kinyuklia, kwa muhula wa pili wa miaka minne kuwa rais, akielezea msukumo wake kwa ajili ya uhuru zaidi na kuzijongelea zaidi nchi nyingine duniani.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema ana matumaini Rouhani atatumia kipindi chake hicho kipya madarakani "kuanza mchakato wa kuvunjilia mbali mtandao wa kigaidi wa Iran."
Trump hakutoa matamshi yeyote katika siku yake ya kwanza nje ya nchi na alitumia muda wake mwingi akitembea kati ya vyumba mbali mbali vya kasri la mfalme.
Chanzo: DW
Comments
Post a Comment