NDEGE YA MAREKANI YAZUILIWA NA NDEGE ZA CHINA
Ndege mbili za kijeshi za China zimeizuia 'vibaya' ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani.
Ndege
hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya
kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa
bahari ya China.
Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.
China
imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na maji hayo yenye
utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake ,hatua ambayo imesababisha
wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.
''Swala hilo linaangaziwa na China kupitia njia mwafaka ya
kidiplomasia mbali na zile za kijeshi'', msemaji wa jeshi la angani la
Marekani Luteni kanali Lori Hodge amesema.
''Uzuizi huo
haukufanywa kwa njia ya ''utaalamu'' kutokana na hali ya rubani wa ndege
hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili'', aliongezea akisema
uchungzi wa kijeshi unaendelea.
Bahari ya Kusini mwa China |
Mnamo mwezi Februari , ndege moja ya Marekani
ilianza kile Washington ilielezea kuwa doria yake ya kawaida kusini mwa
bahari ya China ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.
Ndege
na meli hizo zilielekea katika eneo hilo licha ya onyo kutoka China
dhidi ya kutoa changamoto yoyote kwa uhuru wa China katika eneo hilo.
Kwa nini bahari hiyo ya kusini mwa China inazozaniwa?
Mnamo
mwezi Mei 2016 ndege mbili za kijeshi za China zilizuia ndege nyengine
ya Marekani iliokuwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China.
Wakati huo, jeshi la Marekani lilisema kuwa ilikuwa ikipiga doria ya kawaida katika eneo hilo.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment