KIONGOZI WA MUSLIM BROTHERHOOD AFIKISHWA MAHAKAMANI MISRI

Kiongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, amefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake.Hata hivyo mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Februari 11 mwaka 2014,Wadadisi wanasema ni sehemu ya kampeini ya serikali dhidi ya vuguvugu hilo baada ya jeshi kumuondoa mamlakani aliyekuwa rais Mohamed Morsi.Mohamed Badie -- aliyefikishwa mahakamani na viongozi wengine wa kundi hilo, alikanusha madai kua alitumia kundi hilo kuchochea ghasia.Miongoni mwa washitakiwa wenza wa Badie ni pamoja na Isam al-Iryan, Muhammad al-Biltaji, Basim Udah na Safwat Hijazi. Makosa mengine wanayokabiliwa nayo ni pamoja na kuunda genge la kuwahangaisha watu, uharibifu wa mali ya watu binafsi na kumiliki silaha kinyune na sheria.Makosa wanayokabiliwa nayo yanatokana na ghasia za mwezi Julai ambapo makabiliano yalizuka kati ya wafuasi elfu tano wa Mohammed Morsi pamoja na majeshi katika eneo la Giza na katika msikiti wa Al-Istiqamah baada ya kungo'olewa mamlakani kwa Mohammed Morsi.Hata hivyo Badie Alihoji kwa nini uchunguzi haukufanyika kuhusu kifo cha mwanawe pamoja na kuteketezwa kwa makao makuu ya Brotherhood.Wanafunzi katika chuo kikuu cha Al Azhar wameendelea kuandamana na kulazimisha polisi kuingia chuoni humo ili kusitisha vurugu zao.

NELSON MANDELA IN HIS LAST SPEECH AS ANC PRESIDENT, DECEMBER 1997

" There is a heavy responsibility for a leader elected unopposed. He may use that powerful position to settle scores with his detractors, to marginalise... to get rid of them and surround themselves with yes-men and women. His first duty is to ally the concerns of his colleagues to enable them to discuss freely without fear within internal structures.- Nelson Mandela in his last speech as ANC president, December, 1997.

TANZANIA BARA YATIMIZA MIAKA 52 YA UHURU

HAPPY INDEPENDENT DAY TANZANIA MAINLAND!!! 
HERI YA SIKU YA UHURU TANZANIA BARA!!! 
Mnamo tarehe 9 Desemba 1961, Baba wa taifa Mwl. Julius K. Nyerere pamoja na viongozi wenzie wa TANU walifanikiwa kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika kwa wakati ule (sasa Tanzania) kutoka katika utawala wa Waingereza chini ya Gavana Richard Turnbull. Siku hiyo bendera ya Uingereza ilishushwa na bendera ya Tanganyika huru ilianza kupepea nchini. Enzi za ukoloni Tanzania ambayo kipindi hicho iliitwa Tanganyika, iliwahi kutawaliwa na utawala wa kikatili wa Ujerumani, na baadaye Uingereza. Baada ya Uhuru Mwl. Nyerere alikuwa Waziri Mkuu na baadaye Rais wa kwanza. Katika miaka hii 52 ya uhuru Tanganyika iliungana na Zanzibar mnamo 26 Aprili 1964 na kuunda JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. Toka uhuru tumepitia Mawaziri Wakuu 10, wa sasa akiwa ni Mizengo Kayanza Peter Pinda na pia Marais 4 ambao ni 1. Mwl. Julius Kambarage Nyerere 2. Ali Hassan Mwinyi 3. Benjamin William Mkapa 4. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndo mtawala kwa sasa.
 WITO KWA WATANZANIA NI KUDUMISHA AMANI NA KUEPUKANA NA MIGOGORO YA KIDINI NA UKABILA INAWEZA KULIGAWA TAIFA PIA KUDUMISHA UMOJA,USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO ILI TAIFA LETU LIWEZE KUSONGA MBELE. 
WITO KWA SERIKALI NI KUHAKIKISHA INAILINDA AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOTE. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!

WACHINA WAJIHUSISHA NA UKAHABA DSM


Amini Usiamini Wachina sasa Wameamua kuwekeza mpaka kwenye Ukahaba , Kama unataka kushuhudia hilo basi tembele katika fukwe za bahari ya hindi ukajionee wadada wa kichana wana vyouza mapenzi kama karanga...Bei zao ni kuanzia 20,000 mpaka 60,000.

INDIA, UFARANSA NA MAREKANI ZAOMBOLEZA KIPEKEE



Johannesburg.Wakati Bara la Afrika likiendelea na maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini na mkombozi aliyepinga siasa za ubaguzi za makaburu, Nelson Mandela, mataifa mengine duniani yameonyesha kufanya maombelezo katika namna mbalimbali.Pamoja na kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Mandela na wananchi wa Afrika Kusini, viongozi wa mataifa makubwa duniani wameonyesha kuguswa na msiba huo kiasi cha kuomboleza kwa namna tofauti tofauti.India Hii inaweza kuwa ni nchi mojawapo ambayo imetangaza siku nyingi zaidi za maombolezo kwa ajili ya kifo cha Nelson Mandela kutoka nje ya Bara la Afrika.Baada ya kupata taarifa za kifo cha Mandela, Serikali ya India kupitia Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Manmohan Singh aliwatangazia siku tano za maombelezo na kuamuru bendera zipeperushwe nusu mlingoti katika kipindi hicho cha maombolezo.Sambamba na hilo, Singh alimwelezea namna kiongozi huyo wa Afrika alivyokuwa shujaa katika kupinga mfumo wa kibaguzi.UfaransaKuonyesha kuwa taifa hili pia limeguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huu, jengo refu zaidi mjini Paris la Eiffel Tower liliwashwa taa zenye rangi zilizopo kwenye Bendera ya Afrika Kusini.Picha zilizopigwa katika jengo hilo mpaka siku ya jana, linaionyesha likiwa limenakshiwa na taa zenye rangi tano za bendera hiyo zikiwemo nyekundu, kijani, nyeusi, njano na nyeupe.MarekaniTaifa hili lenye nguvu duniani limeonyesha heshima kubwa kwa Nelson Mandela kwa kupeperusha bendera zake nusu mlingoti nchi nzima na kuweka siku tatu za maombolezo.Kana kwamba hiyo haitoshi taa zenye rangi ya Bendera ya Afrika Kusini zilionekana kung’arisha jengo la Empire state lililopo NewYork na Hoteli ya Omni iliyopo Dallas.

RAIS KIKWETE ASHAURIWA AMNG'OE WAZIRI PINDA

Rais Jakaya Kikwete, ameshauriwa kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikielezwa sababu kuwa ndiye kikwazo katika utendaji wa Serikali na kwamba akiachwa ataipeleka pabaya Serikali na CCM.Kikwete pia ameshauriwa kumfukuza kazi Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, kwa kushindwa kukabiliana na matatizo ya ubadhirifu katika halmashauri nchini.“Kama (Rais) unaitakia mema nchi na CCM kuchukua hatua za kuwafukuza kazi Pinda na Waziri Ghasia,” alisema Mbunge wa Mwibara, Khangi Lugola (CCM), juzi alipochangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka jana.“Kwa nini Watanzania wafe kwa kunyimwa misaada na wafadhili kwa sababu ya mtu mmoja tu Pinda, kwa ajili ya Ghasia ameiendesha Tamisemi kama Saccos ama Vikoba?” alihoji. “Mchawi wetu ... ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekuwa mpole mno hawajibiki,” alisema Mh. Lugola na kuongeza, “Kuanzia jana (juzi) Waziri Mkuu anahudhuria mahafali.”Wakati Lugola akizungumza mawaziri waliokuwepo bungeni ni wanne, manaibu mawaziri wawiliwawili, wakati mawaziri wote 53.

RIPOTI ZA CAG, KAMATI KUWANG'OA MAWAZIRI?

“Tutawatumia mawaziri vivuli kuhakikisha mawaziri mizigo wanang’oka nafasi zao kwa masilahi na mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu” – John Mnyika. Kuna kila dalili kuwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na zile za Kamati za Bunge zinazosimamia fedha za umma, huenda zikawang’oa baadhi ya mawaziri.Hofu kuu inaonekana kuwakumba baadhi ya mawaziri huku waziri mmoja mwandamizi alisema; “Wengi wetu tumeshikwa na kihoro, hatujui nini kitatokea.”Ni ripoti za aina hiyo zilizowasilishwa bungeni Aprili 2012, zilisababisha kuwapo shinikizo kwa Rais Jakaya Kikwete kupangua baraza lake la mawaziri, Mei 4, 2012 na kuwatupa nje mawaziri hao.Katika panguapangua hiyo, Rais Kikwete aliwatosa mawaziri sita akiwemo Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko na Mbunge wa Moshi Vijijini,Dk Cyril Chami.Wengine waliotoswa kwa shinikizo hilo la wabunge ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.Pia Naibu Waziri wa Uchukuzi wa wakati huo, Athuman Mfutakamba alitoswa sanjari na Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya.Katika mkutano huu wa 14 unaoendelea, zipo tetesi kuwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejipanga kuwang’oa mawaziri kamili sita na manaibu mawaziri saba kwa kushindwa kuwajibika.“Hizi siku nne za taarifa za kamati, inawatia kiwewe baadhi ya mawaziri na hakuna ubishi ripoti hizi zinaweza kuchochea kuwapo uamuzi mgumu,” alidokeza mmoja wa mawaziri waandamizi.Mbunge wa Ubungo na Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, John Mnyika, alisema pia kila waziri kivuli wa wizara ambayo imeonekana kuongozwa na waziri mzigo, amepewa maelekezo maalumu.

WALINDA AMANI ZAIDI WAHITAJIKA AFRIKA YA KATI

Majeshi ya Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, yanaongeza kasi ya juhudi zao dhidi ya vurugu na kuzieneza katika sehemu nyengine za taifa hilo ili kurejesha utulivu baada ya mapigano ya kidini.Wanajeshi zaidi wa Ufaransa walishika doria katika mji mkuu Bangui huku wengine wakiingia nchini humo kupitia Cameroon.Msemaji wa jeshi hilo amesema kuna wanajeshi zaidi watahitajika kwenda maeneo ya Kaskazini na Magharibi, Ufaransa, inaongeza idadi ya wanajeshi wake nchini humo hadi 1,600, kuisaidia wanajeshi wanaolinda Amani kukabiliana na vurugu kati ya waisilamu na wakristo.Afrika ya Kati imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu Michel Djotodia kumng’oa mamlakani aliyekuwa Rais Francis Bozize.Djotodia amejitangaza kuwa kiongozi wa kwanza wa waisilamu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya wakristo.Kundi la waasi la Seleka ambalo lilimuingiza mamlakani Djotodia, linatuhumiwa kwa kuwaua wakristo .Duru zinasema kuwa mamia ya watu waliuawa wiki jana katika vita vinavyochochewa na waasi wa Seleka.Rais wa Ufaransa, Francis Hollande amesema viongozi wa Afrika lazima wahakikishe kuwa wanadhibiti ulinzi na usalama katika mataifa yao.

KANYE WEST AZINGUANA NA RAIS OBAMA

Rapper Kanye West amemtolea Uvivu Rais Barack Obama wa Marekani kwa kumzuia kutaja jina lake popote na wala la Mpenzi wake Kim Kardashian...Hii inakuja kama ni kujibu mapigo baada ya Rais Obama kumuita Kanye kuwa ni "Jack Ass" yaani mtu mjinga ama Chizi hivi ...Mwaka 2009 kwa mara ya kwanza Obama alimwita Kanye Jack Ass baada ya Kanye Kupinga ushindi wa Taylor Swift kushinda tuzo ya Best Female Video MTV ..Kanye West alivamia jukwaa na kupinga uteuzi huo....Juzi Tena katika Mahojiona fulani na TV moja Huko Marekani Obama Aliulizwa Jay Z na Kanye Yupi Unamchagua Ombana Akajibu Jay Z, na Obama akaulizwa kama bado anamchukulia Kanye kama Jack Ass ..na akajibu hivi: “He is a jackass, but he’s talented." alisema Obama.

WANAWAKE WALIOMUUNGA MKONO MORSI WAACHILIWA

Mahakama ya rufaa nchini Misri imeamuru kuachiliwa huru kwa wanawake, 21 wakiwemo wasichana saba waliofungwa jela mwezi jana kwa kuandaa maandamano ya kumuunga mkono aliyekuwa Rais Mohammed Morsi.Watoto hao wamepewa kifungo cha nje cha miezi mitatu. Mahakama hiyo pia ilipunguza kifungo cha miaka 11 walichokuwa wamepewa wanawake hao 14.Mahakama iliwapata na hatia mwezi jana ya kuwa sehemu ya kundi la kigaidi lililokuwa linatatiza usafiri wa magari, kufanya hujuma na kutumia nguvu kufanya vitendo vyao.Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa hukumu hiyo.Mmoja wa wanaharakati hao walitaja hukumu hiyo kama ya wazimu.Wanawake hao walifikishwa mahakamani wakiwa wamevalia nguo nyeupe huku wakiwa wamebeba maua ya waridi.Aidha wanawake hao na watoto walishiriki maandamano ya kumuunga mkono aliyekuwa rais Morsi na jamaa zao wanasema ni maandamano ya kwanza waliyowahi kushiriki na kuyaendesha bila vurugu.Mamia ya watu wameuawa nchini Misri tangu hatua ya kumwondoa Morsi madarakani mwezi Julai kusababisha maandamano na vurugu nyingi. SOURCE: BBC Swahili

CCM WALIPOKUJA KUKAGUA UJENZI MWAKALELI

Kinana akishirili katika ujenzi Mwakaleli

Dr. Asha Rose Migiro na Nape wakishiriki ketika ujenzi
Dr. Asha Rose Migiro akizungumza na wanafunzi wa Mwakaleli
Katibu mwenezi wa CCM akizungumza na wanafunzi wa Mwakaleli
Prof. David Mwakyusa akizungumza na wanafunzi wa Mwakaleli, akiwaasa kusoma kwa bidna kuepukana na mahusiano kwani UKIMWI unaua.
Wanafunzi wa kidato cha sita Mwakaleli wakiwa na Dr. Asha Rose Migiro nambunge wa vuti maalumu Mbeya Dr. Mary Mwanjelwa kwtika picha.







SOURCE: CCM BLOG

WABUNGE NCHINI UGANDA WANUNULIWA iPADS

Kumezuka malalamiko nchini Uganda baada ya wabunge kununuliwa tabiti au (iPads) kwa pesa za Umma.Afisaa mkuu wa Bunge amesema kuwa tabiti hizo zitawafanya wabunge kuwa makini wakati wa vikao vya bunge.Kamishna wa bunge Emmanuel Dombo amesema kuwa wabunge sasa wanaweza kupata stakabadhi zao rasmi wakati hata wakiwa nje ya ofisi zao au wakiwa safarini.Pia alisema kuwa pesa walizonunulia iPad hizo zitasaidia kuepuka kutumia kiwango kikubwa cha karatasi na kupunguza gharama ya matumizi.Wabunge wote wa bunge la Uganda ambao idadi yao ni 375, wanunuliwa zilizogharimu kima cha dola laki tatu na sabini.Wakosoaji wanahoji ikiwa wanasiasa wanajua hata kuzitumia tabiti hizo na kusema kuwa tayari wananchi wanalipa pesa nyingi sana kwa mishahara ya wabungeMwaka jana wabunge wa Uganda walipiga kura kutaka mishahara na marupurupu yao kuongezwa kwa asilimia arobaini.Pia walipokea marupurupu ya zaidi ya dola 40,000 ili kujinunulia gari jipya.Mbunge wa Uganda kwa sasa hulipwa, dola elfu nane , ingawa nchi hiyo inakumbwa na matatizo ya kiuchumi.Wananchi wanasema kua hatua hii ya serikali ni kuharibu pesa za mlipa kodi, ikizingatiwa kuwa wabunge hao wanalipwa mishahara ya juu ambayo inawawezesha kujinunulia vifaa hivyo wao wenyewe.

DUNIA YAOMBOLEZA KIFO CHA MANDELA

Rais wa Malawi Joyce Banda, "Wakati kama huu, sote tumepata mshtuko. Sio kuwa hatukujua kitatokea, lakini ni huzuni kwa tulichopoteza. Ningependa kuelezea masikitiko yangu kwa kumpoteza kijana wa Afrika Dr.Nelson Mandela kwasababu vita alivyopigana sio tu dhidi ya ubaguzi wa rangi bali ni vita dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote dhidi ya binadamu.Na ndio maana vijana, na wazee, wake kwa waume, weupe na weusi tajiri na masikini wote wamejihusisha na yeye na vitu alivyopigania."Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, "Kifo cha mandela. Huyu alikuwa mwakilishi wa utu duniani.Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa wengine wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe.Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa wengine wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe.Katika ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko, amekuwa mfano mwema wa utangamano na sioni uwezekano wa kupatikana mwingine kama yeye katika miaka mingi ijayo."

RAIS KIKWETE ATANGAZA MAOMBOLEZO SIKU TATU TANZANIA

Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.Rais Jakaya Kikwete wa pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.Rais Jakaya Kikwete wa nchi hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote zitapepea nusu mlingoti.Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.Kufuatia kifo hicho Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote."Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.Rais Kikwete amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi."Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake". Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".

AFRIKA MASHARIKI YAOMBOLEZA KIFO CHA NELSON MANDELA

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ametangaza siku tatu za maombolezi, kufuatia kifo cha mzee Nelson Mandela, akisema kua Afrika na dunia nzima kwa ujumla imempoteza shujaa mkubwa sana katika karne ya 20 na 21.Kikwete alisema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kua Mandela ni kiongozi wa kipekee na mtu aliyeenziwa sana na dunia nzima pamoja na watu wa Afrika Kusini baada ya kupigania sana demokrasia nchini Afrika Kusini.Kikwete alisema mfano wa Mandela unapaswa kuigwa na watu wote duniani .Kwa upande wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesema kuwa Mandela alikuwa mfano mzuri wa umuhimu wa kuwa na matumaini na kuwataka watu kuwa na uelewa wa kuwasamehe bila masharti wale wote wanaotukuosea.Naye Rais wa Rwanda Paul Kagame,amesema kua Mandela ataendelea kuishi kwenye mioyo ya wengi wetu.Naye Rais mstaafu Daniel Moi ambaye alikuwa madarakani wakati Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amempongeza Mandela kwa kuhakikisha utulivu wa kisiasa barani Afrika na kuwa mfano bora kwa viongozi wengine.Naye Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema kuwa Mzee Mandela, pamoja na washirika wake, Albert Luthuli, Walter Sisulu, Govan Mbeki, Oliver Thambo na wengine wengi,walijitolea maisha yao kuleta demokrasia nchini Afrika Kusini.Walifanya kila walichoweza kuhakikisha kwa wanawakomboa watu wa taifa lao.Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Museveni amesema ni jukumu la vijana sasa kuiga mfano wa Mandela kuhakikisha kuwa Afrika inalindwa dhidi ya ukoloni mambo leo na kutengwa.