Posts

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018

Image
10. YUSUF MANJI Manji ni mmiliki wa mali zisizohamishika hasa majengo kwa ajili ya makazi ya watu na biashara. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya Quality Group of Companies. Anajihusisha pia na vipuli vya magari. Haya yamemfanya kua miongoni mwa matajiri wa juu zaidi nchini. 9. FIDA RASHID Fida ni muanzilishi wa kampuni ya Africarrier Group. Hii ni kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. Pia kampuni hii inahusika na usambazaji wa magali ya kampuni ya Eicher na Golden Dragon hapa nchini. Hii imefanya kampuni yake kufanya vyema sana katika idara hii. Fida pia ni mmiliki wa mali zisizohamishika pamoja na majengo kama Zahra Tower na Raha Tower. Amekua mjasiriamali anayetengeneza zaidi mazingira mazuri ya biashara zake kama wafanyavyo wengine. 8. GHALIB SAID MOHAMMED Ghalib Mohammed alikua akifanya biashara ya korosho hapo awali na biashara nyingine akishirikiana na baba yake. Baadaye Ghalib Said aliamua kuanzisha kampuni yake na kuiita GSM Group ambayo inajihusisha...

CELEBRITY: SHANIA TWAIN ANATIMIZA MIAKA 53 LEO AGOSTI 28, 2018

Image
KUZALIWA  Celebrity wetu wa leo ni Shania Twain. Jina lake la kuzaliwa ni  Eilleen Regina Edwards lakini umaarufu wake umetokana na jina lilizoeleka la Shania Twain. Wengine wanamuita Malkia wa Muziki wa Country.  Alizaliwa mnamo Agosti 28, 1965 leo anatimiza miaka 53 ya kuwepo duniani. Alizaliwa huko  Windsor, Ontario, Canada akiwa ni mmoja kati ya mabinti 3 wa Clarence na Sharon (Morison) Edwards. Yeye ndiye mkubwa. Alipokua na miaka 6 mama yake aliolewa tena na Jerry Twain ambaye alimchukua kama mwanaye. Alianza kuimba katika vilabu vya pombe na alipokua na miaka 13 alionekana katika The Tommy Hunter Show. Alipokua na umri wa miaka 22 wazazi wake waliuawa katika ajali na hivyo akaacha sanaa muziki ili awalee wadogo zake Mark na Darryl pamoja na dada zake wawili aliozaliwa nao kwa baba yake na mama yake mzazi. Mwaka 1991 alibadilisha jina lake alilopewa na wazazi wake na kujiita Shania Twain na hapo ndipo jina hili lilipokua.  Mwaka huo huo pia alisaini m...

LEO AGOSTI 6 KATIKA HISTORIA

Image
Leo ni Agosti 6, 2018 ikiwa ni siku ya 218 katika mwaka 2018. Zimesalia siku 147 katika mwaka huu. Nakukaribisha tena katika muendelezo ya Leo Katika Historia. Kwa leo nimekuletea matukio kadhaa yaliyopata kutokea katika historia ya dunia, na tuanze kuyahesabu matukio hayo: MATUKIO 1787 - Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Marekani ilianza kujadiliwa huko Philadelphia. 1890 - Hukumu ya kuuawa kwa kiti cha umeme ilianza kutekelezwa katika gereza la Auburn huko New York, Marekani ambapo William Kemmier alihukumiwa kifo katika kiti cha umeme kwa kumuua mpenzi wake Matilda Ziegler kwa shoka. Adhabu hii ya kifo ilipendekezwa mwaka 1881 na Dk. Albert Southwick baada kushuhudia mlevi akiuawa kwa shoti ya umeme. Katika kutekeleza adhabu hii zilitumika volti 700 za umeme na katika sekunde 17 umeme ulifeli kabla Kemmier hajafariki na baadaye waliongeza umeme hadi volti 1,030 ndani ya dakika 2 na ndipo Kemmier alifariki. Kiti cha Umeme kilichotumika kutekeleza adhabu ya kifo kwa Kemmier. ...

TAZAMA HAPA MAGOLI 10 BORA YA KOMBE LA DUNIA 2018

Image
Michuano ya Kombe la Dunia tayari imemalizika nchini Urusi jana Julai 15, 2018 ambapo Ufaransa ilii chapa 4 - 2 Croatia. Leo nakupa nafasi ya kuangalia magoli 10 bora yaliyofungwa katika michuano hii, magoli haya ni kama ifuatavyo: 10: Cristiano Ronaldo, Portugal vs Spain 09: Toni Kroos, Germany vs Sweden 08: Lionel Messi, Argentina vs Nigeria 07: Ricardo Quaresma, Portugal vs IR Iran 06: Nacho, Spain vs Portugal 05: Aleksandar Kolarov, Serbia vs Costa Rica 04: Angel Di Maria, Argentina vs France 03: Philippe Coutinho, Brazil vs Switzerland 02. Benjamin Pavard, France vs Argentina 01. Denis Cheryshev, Russia vs Croatia. Unaweza kutazama magoli hayo katika video hii hapa chini: Magoli haya ni kwa hisani ya Kwesé Sports ambao walikua ni washirika rasmi wa FIFA wa kuonesha michuano hii ya Kombe la Dunia 2018.

HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA & UALIMU 2018

Image
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Kidato cha Sita 2018 na yale ya wanafunzi wa Ualimu. Kuangalia matokeo hayo  BOFYA HAPA

FRIENDSHIP QUOTES OF THE DAY MAY 26, 2018

Image
Today I invite you to read these quotes of the day. Enjoy your day. 1.  One of the most beautiful qualities of true friendship is to understand and to be understood. ~Lucius Annaeus Seneca. 2.  Walking with a friend in the dark is better than walking alone in the light. ~Helen Keller. 3.  There is nothing on this earth more to be prized than true friendship. ~Thomas Aquinas. 4.  My best friend is the one who brings out the best in me. ~Henry Ford. 5.  It is one of the blessings of old friends that you can afford to be stupid with them. ~Ralph Waldo Emerson. 6.  The strong bond of friendship is not always a balanced equation; friendship is not always about giving and taking in equal shares. Instead, friendship is grounded in a feeling that you know exactly who will be there for you when you need something, no matter what or when. ~Simon Sinek. 7.  A friend is someone who gives you total freedom to be yourself. ~Jim Mo...

WAFUNGAJI BORA NA WALIOCHEZA MECHI NYINGI KATIKA KOMBE LA DUNIA 1930-2014

Image
WAFUNGAJI 5 WA MUDA WOTE 1. Miroslav Klose - Ujerumani Klose wakati wa droo ya kombe la dunia mwaka jana 2017. Amezaliwa Juni 9, 1978. Ana jumla ya magoli 16 katika michuano ya kombe la dunia na magoli 23 katika mechi za kufuzu, hii inafanya jumla ya magoli kuwa 29.   Aling'aa katika mechi ya awali kufuzu michuano hii ambapo Ujerumani iliichapa Abania 2-1 mwaka 2002.  Amecheza mechi 43; 24 zikiwa za kombe la dunia na 19 zikiwa za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza na timu yake wameshinda mechi 30 wamesuluhu mechi 8 na kupoteza mechi 5. Ana kadi 1 ya njano katika michuano ya FIFA na kadi 2 za njano katika hatua ya makundi kufuzu kucheza kombe la dunia. Mwaka 2006 alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas na mwaka 2014 alikuwepo katika kikosi cha Ujerumani walipotwaa kombe la dunia katika fainali dhidi ya Ajentina nchina Brazil. Klose wakati wa mechi ya robo fainali kati ya Ujerumani na Ufaransa katika dimba la Marakana Rio de Jeneiro Jula...

UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU TEKNOLOJIA YA 5G

Image
Logo rasmi ya teknolojia ya mtandao wa 5G. Katika teknolojia za mitandao ya simu iliyopita kulikua na suluhisho la matumizi ya sauti pekee katika mtandao wa 1G, sauti na jumbe za maneno katika mtandao wa 2G, kuliongezeka kufungua tovuti mbalimbali katika mtandao wa 3G na kuongezeka kwa kasi zaidi ya mtandao na kutazama video za moja kwa moja katika mtandao wa 4G. Mabadiliko kutoka 4G kwenda 5G yatasaidia si watumiaji wa mtandao tu bali pia wamiliki wa viwanda mbalimbali. Mabadiliko katika teknolojia ya simu na mtandao. Kwa teknolojia ya mtandao huu wa simu za mkononi kasi ya mtandao inatarajiwa kuwa mara 8 ya hii ya sasa mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2023 huku kukiwa na uhitaji wa teknolojia imara, viwango vikubwa vya data na wigo mpana wa matumizi ya mtandao huu tofauti na hii iliyopo sasa (4G). Vitumizi vipya kama vile 4K/8K vya kutazamia video mtandaoni moja kwa moja, uwezo wa mtandao ambao umeongezwa karibia na uhalisia pamoja matumizi ya data ambao kwa sasa yanach...