CELEBRITY: SHANIA TWAIN ANATIMIZA MIAKA 53 LEO AGOSTI 28, 2018

KUZALIWA 

Celebrity wetu wa leo ni Shania Twain. Jina lake la kuzaliwa ni Eilleen Regina Edwards lakini umaarufu wake umetokana na jina lilizoeleka la Shania Twain. Wengine wanamuita Malkia wa Muziki wa Country.  Alizaliwa mnamo Agosti 28, 1965 leo anatimiza miaka 53 ya kuwepo duniani. Alizaliwa huko Windsor, Ontario, Canada akiwa ni mmoja kati ya mabinti 3 wa Clarence na Sharon (Morison) Edwards. Yeye ndiye mkubwa. Alipokua na miaka 6 mama yake aliolewa tena na Jerry Twain ambaye alimchukua kama mwanaye. Alianza kuimba katika vilabu vya pombe na alipokua na miaka 13 alionekana katika The Tommy Hunter Show. Alipokua na umri wa miaka 22 wazazi wake waliuawa katika ajali na hivyo akaacha sanaa muziki ili awalee wadogo zake Mark na Darryl pamoja na dada zake wawili aliozaliwa nao kwa baba yake na mama yake mzazi. Mwaka 1991 alibadilisha jina lake alilopewa na wazazi wake na kujiita Shania Twain na hapo ndipo jina hili lilipokua.  Mwaka huo huo pia alisaini mkataba na lebo ya muziki ya Mercury Nashville.
Shania siku za hivi Karibuni.


KUOLEWA

Shania amewahi kufunga ndoa mbili ambapo ndoa ya kwanza alifunga na Robert John Lange Desemba 28, 1993 na ilidumu hadi Juni 9, 2010. Katika ndoa hii walifanikiwa kupata mtoto 1 kabla hawajaachana. Baadaye January 1, 2011 aliolewa na Frederic Nicolas Thiebaud ambaye yuko naye mpaka sasa. Hawajabahatika kupata mtoto. 

TUZO


Shania amewahi kushinda tuzo kadhaa na kutajwa katika nyingine:

Mwaka 1996 alitajwa katika tuzo za Grammy kama msanii bora chipukizi lakini hakufanikiwa kutwaa tuzo hiyo.


Mwaka 1997 aliteuliwa kuwania tuzo za Gemini katika kipengele cha mtumbuizaji bora katika vipindi mbalimbali vya television, huku pia hakufanikiwa kutwaa tuzo.

Mwaka 1998 aliteuliwa kuwania tuzo za MTV kama Video Bora ya Msanii wa Kike: You're Still the One. Huku pia hakufanikiwa kutwaa tuzo hiyo. Mwaka huu alishinda tuzo ya Grammy na wimbo wake wa From this Moment on.

Mwaka 1999 aliteuliwa kuwania tuzo ya Grammy kama Wimbo wa Mwaka: You're Still the One, pia hakufanikiwa kupata tuzo hiyo. 

Mwaka 2004 alifanikiwa kutwaa tuzo ya Bambi katika kipengele cha Pop Kimataifa. 

Mwaka 2005 Grammy walimchagua katika vipengele viwili; mtumbuizaji bora wa kike wa muziki wa country na kolabo bora ya country. Bado hakufanikiwa pia kutwaa tuzo. 

Mwaka 2011 alitwaa tuzo kama Nyota wa tuzo za Walk of Fame. 
Shania Twain katika video ya For evre and for always. 

ALBUM ZAKE

Shania Twain (1993)
The Woman In Me (1995)
Come Over (1998)
Up (2003)
Now (2017)

MENGINE KUHUSU SHANIA TWAIN

Anakula mboga za majani na alipendekezwa kua na mvuto kutokana na hili.

Mwaka 1995 aliorodheshwa kama Mtu mwenye majibu Halisi anapoulizwa maswali katika jarida la People Weekly.

Amewahi kukaa kwenye namba za juu za muziki duniani kwa wimbo wake You're Still the One ambayo ilishika namba 1 kwenye chati ya Billboard mara 7. Pia alishika namba 2 katika chati za Hot 100 kwa wimbo huo mwaka 1998.

Wimbo wake "Love Gets Me Everytime" ulikua ni wimbo ulioshika nafasi ya juu zaidi ya Billboard kwa wiki 5 katika nyimbo za country tangu wimbo wa mwisho wa Dolly Parton "Here You Come Again" uliposhika nafasi hiyo mwaka 1997.

Mwaka 1999 alitajwa kama mtumbuizaji bora wa muziki wa country na mwaka huo huo CMA walimtuza tuzo ya mwaka ya mafanikio katika muziki huo.

Mwaka 1999 aliuza nakala milioni 19 za albam yake ya Come Over nchini Marekani peke yake.

Mwaka 2003 aliwahi kushinda tuzo ya Juno ka Chaguo la Mashabiki.

Album yake ya Come Over (mauzo na matamasha) viliingiza dola za Marekani milioni 40 nchini Australia pekee. Hii inaifanya kuwa miongoni mwa album zilizowahi kushika chati za juu za muda wote nchini humo.

Alishika namba 39 katika orodha ya Jarida la Maxim kama mwanamke mwenye mvuto katika wanawake 100 waliotajwa katika orodha hiyo ya mwaka 2005.

Album yake ya Up (2002) iliuza nakala milioni 2 nchini Marekani ndani ya mwezi 1 tangu ilipowekwa sokoni.

Alipokua mdogo alikua na aibu na alikua Tom boy.

Amekua katika familia maskini ambayo chakula tu ilikua ni tabu. Shania alikua akienda shule bila kula kutokana na hali ya maisha kifedha nyumbani kwao.

Anapenda kushinda nyumbani na kupika. 
Anaamini kwamba yeye ni kama watu wengine.

Ni miongoni mwa wasanii wa 4 kutoka nchini Canada waliowahi kushika namba za juu katika chati ya Billboard tangu kuanzishwa kwake mwaka 1944. Wengine kutoka Canada ni Hank Snow, Anne Murray na Terry Klark.

Aliwahi kusema kwamba anapendezwa na majukumu wanayofanya wanaume katika maisha ya kila siku.

Shania anawasema kuwa anasikitika siku zote kwa kua ndoa yake ya awali alivunjika.

Anao wafuasi 863K katika mtandao wa Instagram. Katika mtandao wa Twitter anao wafuasi 901K. Katika mtandao wa Facebook anao wafuasi zaidi ya milioni 5. Ukurasa wake wa YouTube umetazamwa na watu bilioni 1.2 huku akiwa na subscribers zaidi ya bilioni 1.1.

Haya ni machache kati ya mengi niliyokuandalia kuhusu mwanamuziki Shania Twain. Kama una maoni usisite kuniandikia kupitia barua pepe: venancegilbert@gmail.com ama ujumbe Whatsapp 0712586027. Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG na karibu tena kwa mengine mengi. 

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017