LEO AGOSTI 6 KATIKA HISTORIA

Leo ni Agosti 6, 2018 ikiwa ni siku ya 218 katika mwaka 2018. Zimesalia siku 147 katika mwaka huu. Nakukaribisha tena katika muendelezo ya Leo Katika Historia. Kwa leo nimekuletea matukio kadhaa yaliyopata kutokea katika historia ya dunia, na tuanze kuyahesabu matukio hayo:

MATUKIO

1787 - Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Marekani ilianza kujadiliwa huko Philadelphia.

1890 - Hukumu ya kuuawa kwa kiti cha umeme ilianza kutekelezwa katika gereza la Auburn huko New York, Marekani ambapo William Kemmier alihukumiwa kifo katika kiti cha umeme kwa kumuua mpenzi wake Matilda Ziegler kwa shoka. Adhabu hii ya kifo ilipendekezwa mwaka 1881 na Dk. Albert Southwick baada kushuhudia mlevi akiuawa kwa shoti ya umeme. Katika kutekeleza adhabu hii zilitumika volti 700 za umeme na katika sekunde 17 umeme ulifeli kabla Kemmier hajafariki na baadaye waliongeza umeme hadi volti 1,030 ndani ya dakika 2 na ndipo Kemmier alifariki.
Kiti cha Umeme kilichotumika kutekeleza adhabu ya kifo kwa Kemmier.

1904 - Jeshi la Japan lililokua nchini Korea lilizunguka Jeshi la Urusi ambalo lilizidiwa nguvu na kuamua kurudi nyuma katika jimbo la Manchuria.

1945 - Ndege ya Marekani B-29 ikiongozwa na rubani Paul Tibbets ilidondosha bomu la nyuklia katika jimbo la Hiroshima. Bomu hilo liliua watu waliofikia 80,000 na pia watu 35,000 walijeruhiwa na inakadiriwa kua baadaye mwishoni mwa mwaka huo watu wengine 60,000 walifariki kwa madhara ya bomu hilo. Kulikua na majengo 90,000 katika mji wa Hiroshima lakini baada ya bomu kulipuka yalibaki majengo 28,000 tu, madakatari walikua 200 lakini waliosalia walikua 20 tu, manesi walikua 1,754 lakini walisalia 150 tu.
Ndege aina ya B-29 iliyodondosha bomu la nyuklia huko Hiroshima.
Baada ya bomu kudondoshwa hali ilikua hivi. 

Hivi ndiyo Hiroshima ilivyojengwa kwa sasa. 

1962 - Jamaica ilipata Uhuru wake kamili kutoka kwa Uingereza baada ya kutawaliwa kwa miaka 300.

1973 - Mwanamuziki wa Marekani Steve Wonder alipata ajali ya gari iliyopelekea kupoteza fahamu kwa siku 4.

1993 - Papa John Paul II alichapisha makala iliyohusu Umuhimu wa Kanisa Katoliki katika kufundisha maadili.

KUZALIWA

1809 - Mtunzi wa mashairi wa Uingereza Alfred Lord Tennyson alizaliwa. Moja kati ya mashairi yake maarufu ni "The Charge of the Light Bregade" la mwaka 1850.

1881 - Alexander Flemming mgunduzi wa dawa aina ya Penicillin mwaka 1928 alizaliwa.

1911 - Muigizaji na mchekeshaji wa Marekani Lucille Ball alizaliwa. 

1934 - Piers Anthony Dillingham Jacob mwandishi wa riwaya za kisayansi na matukio ya ajabu na ya kusimumua alizaliwa. 

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA