Posts

UONGOZI LEADERSHIP ESSAY COMPETITION FOR AFRICAN STUDENTS. FULLY-FUNDED TO JOHANNESBURG SOUTH AFRICA

Image
African citizens between the age of 18-25 are invited to submit an essay for this year’s Leadership Essay Contest organised by the Institute of African Leadership for Sustainable Development (UONGOZI Institute). Application Deadline:  14 th  July, 2017 (5pm GMT). Eligible Countries:  African countries To be taken at (country):  South Africa About the Award:  The essay contest aims to provide a space for the youth of Africa and the next generation of leaders in the region to contribute to important discussions on leadership. Type:  Essay Contest Eligibility:  The contest is open to all African citizens between the age of 18 – 25 years old, to write about their perspective on leadership as it relates to peace and security in Africa. The essays should respond to the following question: “If you were a leader, what would you do to ensure that peace and security is achieved and sustained in Africa?” The essays should be no more...

WABUNGE: "BILA KILIMO KWANZA HAKUNA SERIKALI YA VIWANDA"

Image
  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamesema bila kuwekeza katika kilimo, azima ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda haitatimia. Kadhalika, wameipongeza Serikali kwa kuondoa tozo 108 zilizokuwa kero kwa wakulima na kuitaka Serikali kuhakikisha tozo zilizoondolewa zinawanufaisha zaidi wakulima na Watanzania, badala ya kuwanufaisha wafanyabiashara pekee. Waliyasema hayo jana kwa nyakati tofauti bungeni Dodoma wakati wakichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Fedha 2017/18. Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile (CCM), alisema kama Tanzania inataka kuwa ya viwanda, haina budi kuwekeza katika utafiti kwa ajili ya sekta ya kilimo ili kubaini namna bora zaidi za kutumia rasilimali na fursa zilizopo ili kuimarisha kilimo na hivyo kusaidia kufikia haraka azima ya kujenga Tanzania ya viwanda. Alisema tayari fursa za kuinua kilimo na kukifanya uti wa mgongo nchini zimea...

TRUMP AWASILI SAUDI ARABIA

Image
Rais Donald Trump  akikaribishwa  kwa bashasha  kubwa  na  ukoo  wa  kifalme  wa  Saudi Arabia  jana , wakati  akiweka  kando, japokuwa  kwa  muda  tu , utata mkubwa  unaoukumba utawala  wake  mjini  Washington. Rais Trump akilakiwa mjini Riyadh Trump  amewazawadia  wenyeji wake  mpango  wa mauzo  ya  bilioni 110  wa  silaha  wenye  lengo  la  kuimarisha  usalama  wa  Saudi  Arabia pamoja  na  makubaliano  kadhaa  ya  kibishara. "Hii  ni  siku  muhimu  sana, uwekezaji  mkubwa  katika  Marekani ," Trump  alisema wakati wa  mkutano  na  mwanamfalme Mohammed bin Nayef. Rais Trump (Kushoto) akisalimiana na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz(kulia) Ziara  katika  mji  mkuu  wa  Saudi Arabia...

KOREA KASKAZINI IMEFANYA JARIBIO LINGINE LA KOMBORA

Image
Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa Korea Kaskazini imefanyia majaribio kombora lingine. Ofisi ya kijeshi nchini Korea Kusini inasema kuwa kombora hilo lilirushwa siku ya Jumapili jioni saa za Korea. Jaribio hilo linafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kulifanyia majaribio kombora lingine ambalo inadai kuwa ni jipya na ambalo lina uwezo wa kubeba silaha kubwa ya nyuklia. W achambuzi wanasema kwamba huko mbeleni linaweza kuifikia Alaska. Jumatatu iliyopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliitaka Korea K askazini kusitisha majaribio kama hayo. Baraza hilo la UN lilisisitiza umuhimu wa nchi hiyo kuachana na hatua hizo. Korea Kaskazini inafahamika kwa kuunda zana za nyuklia na imefanya jumla ya jaribio matano ya nyuklia na ya makombora yenye uwezo wa kusafirisha zana hizo hadi maeneo inayolenga. Korea Kusini inasema kuwa jaribio la hivi punde lilifanyiwa eneo la Pukchang magharibi mwa nchi. Chanzo: BBC & DW

VIDEO: JAY 2 THE HUSTLER X CAST BEEZY - TIME IS NOW (OFFICIAL VIDEO)

Image
 

MGAHAWA WAKUMBWA NA KASHFA YA KUUZA NYAMA YA BINADAMU

Image
Mgahawa mmoja mjini London umekumbwa na habari bandia za kuuza nyama ya mtu. Wafanyikazi katika mkahawa wa Karri Twist katika eneo la New Cross nchini Uingereza wamehangaishwa kwa kupigiwa simu kutoka kwa wateja wanaosema ''Kwa nini hamujafunga''?. Mkahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu la mkahawa huo. Na watu wengine waliamini mzaha huo. Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari cha channel23news.com, mtandao ambao wateja wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja kwa moja katika mtandao wa fecbook. Shinra Begum ambaye ndio mmiliki wake aliambia Newsbeat kwamba biashara hiyo ya familia imekumbwa na wakati mgumu tangu habari hiyo ilipochapishwa siku ya Alhamisi. ''Wakati watu walipoanza kunipigia simu na kuuliza iwapo tulikuw...

NDEGE YA MAREKANI YAZUILIWA NA NDEGE ZA CHINA

Image
Ndege mbili za kijeshi za China zimeizuia 'vibaya' ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani. Ndege hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa bahari ya China. Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.  China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na maji hayo yenye utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake ,hatua ambayo imesababisha wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili. ''Swala hilo linaangaziwa na China kupitia njia mwafaka ya kidiplomasia mbali na zile za kijeshi'', msemaji wa jeshi la angani la Marekani Luteni kanali Lori Hodge amesema. ''Uzuizi huo haukufanywa kwa njia ya ''utaalamu'' kutokana na hali ya rubani wa ndege hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili'', aliongezea akisema uchungzi wa kijeshi unaendelea. ...

MABOMU YASABABISHA WATU ZAIDI YA ELFU 50 KUHAMA UJERUMANI

Image
Operesheni kubwa ya kuwaondoa wakaazi wengi wa mji wa Hanover ulioko kaskazini mwa Ujerumani, inaendelea, ya kuwahamisha zaidi ya watu elfu 50 baada ya mabomu makubwa ya wakati wa vita vya dunia, kupatikana kama hayajalipuka. Wakaazi hao wanatarajiwa kuondoka majumbani mwao baadaye leo, ili kuwapa nafasi wataalamu wa kutegua mabomu, kuhamishia mahala salama mabomu hayo ambayo yanakisiwa kuwa matano. Operesheni hiyo itachukua siku nzima, na hata zaidi ikiwa mabomu mengineyatapatikana. Washambuliaji walivamia mji wa Hanover mara 125 kwa mabomu, wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. Haki miliki ya picha Getty Images.     Wataalamu wanaamini kuwa mabomu ambayo hayakulipuka huenda yako chini ya jengo hili                 Zaidi ya asilimia 20 ya mabomu yaliyoangushwa mjini humo hayakulipuka. Baadhi ya mabomu mengine yalikuwa na vifaa vinavyochuku...

WAPIGANAJI WA HAMAS WAPATA KIONGOZI MPYA

Image
Ismael Haniyeh ndio kiongozi mpya wa kundi la Hamas Wapiganaji wa Palestina Hamas wamepata kiongozi mpya. Kiongozi huyo ni Ismail Haniyeh ambaye hadi hivi karibuni alikuwa ndio kiongozi wa kundi hilo katika ukanda wa Gaza. Akijulikana kama kiongozi anayetumia akili nyingi wakati wa kutatua maswala, anachukua mahala pake Khaled Meshaal ambaye ameliongoza kundi hilo akiwa ughaibuni kwa miongo miwili. Uchaguzi wa kiongozi mpya ulifanyika kupitia njia ya Video Link kati ya wajumbe waliopo katika ukanda wa Gaza na wale waliopo nchini Qatar ambako Meshaal ana makao yake. Mwandishi wa BBC anasema kuwa bwana Meshaal anaachia ngazi wakati ambapo Hamas limeanza kulegeza msimamo wa kisiasa. Kwa mara ya kwanza wiki iliopita katika sera mpya kundi hilo liliwachilia wito wake wa kuiharibu Israel. Hamas bado lina wapiganaji wake katika eneo la Gaza na bado linaaminika kuwa kundi la kigaidi na Israel Marekani na mataifa ya bara Ulaya. Chanzo: BBC

MANCHESTER CITY YAIBURUZA VIBAYA CRYSTAL PALACE

Image
Klabu ya Manchester City imerudi katika nafasi yake ya tatu katika ligi ya Uingereza baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Crystal Palace ambayo imeshindwa kwa mara ya tatu mfululizo. City ilihitaji dakika mbili pekee kupata bao la kwanza baada ya David Silva kufunga baada ya kurudi kutoka kuuguza jereha. Wenyeji waliongeza bao la pili dakika tatu katika kipindi cha pili wakati Vincent Kompany alipopiga mkwaju ulioingia katika kona ya ya juu ya goli na baadaye Kevin De Bruyne akafunga bao la tatu. Ndoto ya Palace ilithibitishwa baada ya Raheem Sterling kufunga bao la nne kabla ya beki Otamendi kufunga bao la tano katika dakika za lala salama. Kikosi hicho cha Sam Allardyce kiko pointi tano juu ya eneo la kushushwa daraja na kinaweza kuwa hatarini iwapo klabu za Hull City na Swansea zitaibuka washindi siku ya Jumamosi.

RAIS MAGUFULI AMETUMA SALAMU ZA POLE KWA WAFIWA WA AJALI ARUSHA

Image
Hii hapa chini ni taarifa kama ilivyoandikwa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko mkubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea leo saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha. Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu. Kufuatia ajali hiyo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na imesababisha uchungu, hu...

KANYE WEST AMEFUTA AKAUNTI ZAKE KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Image
Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na makumi ya mamilioni ya wafuasi. Sababu hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema. Alimshtumu mwanamuziki mwenza Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo. Mkewe nyota wa Raality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51. Haki miliki ya picha TWITTER Image caption Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati mashabiki walipojaribu kuwasiliana na msanii huyo Amekuwa akijikuza pamoja na kampuni ya kuuza nguo ya mumewe. Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake. Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao. Haki miliki ya picha TWITTER Image captio...

MFAHAMU KARL MARX KWA UFUPI: DUNIA INAMKUMBUKA LEO

Image
Karl Mark alikuwa ni mwanafalsafa na mwanamapinduzi wa Ujerumani aliyeandika vitabu vya The Communist Manifesto na  Das Capital vitabu ambavyo vilikuwa vikipingana na mfumo wa kibepari na kuunda mfumo wa Ukomunisti ama Ujamaa kama alivyoutafsiri hayati Mwalimu JK Nyerere. Karl Marx alizaliwa Mei 5, 1818. Alianza kuchunguza nadharia za kijamii alipokuwa Chuo Kikuu na wenzie waliounda kikundi chao kilichoitwa Young Hegelians. Hiki kilikuwa ni kikundi kilichokuwa kinaamini katika falsafa za mwalimu wao aliyeitwa Hegel. Marx alikuwa mwandishi wa habari na machapisho yake kuhusu Ukomunisti vilipelekea yeye kufukuzwa Ujerumani na Ufaransa. Mwaka 1848 alichapisha kitabu chake cha The Communist Manifesto akiwa na Friedrich Engels ambacho kilipelekea kufukuzwa Ujerumani na kukimbilia London, Uingereza, huko pia aliandika kitabu cha Das Kapital ambako ndiko alikoishi mpaka alipoiaga dunia. Karl Marx alikuwa ni miongoni mwa watoto 9 wa Heinrich Marx na Henrietta Marx huko Tr...