MECHI YA ATLETICO & REAL MADRID KULINDWA NA POLISI 2,000
![]() |
Polisi wa kukabiliana na fujo walikabiliana na mashabiki wa Bayern Munich mnamo 18 Aprili |
Walinzi zaidi ya 2,000 watatumiwa
kudumisha usalama na kudhibiti mashabiki wakati wa mechi ya nusufainali
ya mkondo wa kwanza kati ya Real Madrid na Atletico Madrid katika Ligi
ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mechi hiyo itakayochezewa Santiago Bernabeu
siku ya Jumanne imeorodheshwa kama yenye "hatari kubwa" na usalama
"utaimarishwa", maafisa wasimamizi wa jiji la Madrid walisema Ijumaa.
UEFA wameamrisha usalama katika mechi za klabu Ulaya uimarishwe baada ya
shambulio kwenye basi la timu ya Borussia Dortmund mnamo 11 Aprili.
Atletico watakuwa na mashabiki 4,000 katika uwanja huo wa Real unaotoshea mashabiki 80,000.
Kawaida ni mashabiki wachache sana husafiri kuhudhuria mechi za ugenini Uhispania.
Idadi
ya walinzi tarehe 2 Mei itakuwa ya juu zaidi ya waliokuwepo wakati wa
mechi iliyopita ya Real Ulaya dhidi ya Bayern Munich polisi wa
kukabiliana na fujo walipokabiliana na mashabiki wageni wakati wa
mapumziko.
Kulikuwa pia na fujo mechi ya robofainali ya Atletico nyumbani, polisi wakikabiliana na mashabiki wa Leicester City.
Chanzo: BBC
WAFAHAMU MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOFARIKI WAKIWA MADARAKANI
Leo nimekuandikia orodha ya marais 10 waliofariki wakiwa madarakani. Tuanze kuhesabu sasa:
10. Lansana Conte, Rais wa Guinea
Baada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana
akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi
ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni
rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya
aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi.
9. Omar Bongo, Rais wa Gabon
Saratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha Rais Omar
Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka
42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni
kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa
akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa
huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini.
8. Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-Bissau
Joao Bernardo Vieira rais wa Guinea-Bissau aliuwawa nchi mwake Machi
2009, akiwa na umri wa miaka 69. Alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa
miaka 31. 1978 alikuwa waziri mkuu na kuchukua madaraka 1980
na alitawala kwa miaka 19. Alibadilika na kuwa kiongozi wa umma na
aliongoza miaka minne mingine zaidi. 2005 alishinda tena uchaguzi wa
uraisi.
7. Umaru Musa Yar’Adua, Rais wa Nigeria
Umaru Musa Yar’Adua, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 mwaka 2011
akisumbuliwa na matatizo ya moyo
nchini Nigeria. Alikuwa madarakani kwa miaka mitatu pekee. Alikosekana
katika kampeni za uchaguzi kwa sababu za kiafya. Baada ya kuchaguliwa
kwake 2007, afya yake ilidhoofika kwa haraka.
6. Muammar Gadhafi, kiongozi na mwana mapinduzi wa Libya
Mwathirika wa mauaji, Muammar Gadhafi aliuawa akiwa na umri wa miaka
69 na vikosi vya waasi katika mazingira yasiyoeleweka nchini Libya,
baada ya kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Aliuondoa
uongozi wa kifalme bila ya kumwaga damu wakati wa mapinduzi ya kijeshi
ya mwaka 1969 lakini utawala wake ulifikia kikomo baada ya matokeo ya
vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni.
5. Malam Bacai Sanha, Rais wa Guinea-Bissau
Kiongozi wa nne kufariki mwaka 2012 alikuwa ni Malam Bacai Sanha rais
wa Guinea-Bissau. Aliugua ugonjwa wa kisukari na alifariki mjini Paris
baada ya miaka minne kama rais akiwa na umri wa miaka 64. Katika kipindi
chote cha utawala wake alisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya
yalosababisha kwenda hospitali mara nyingi.
4. Bingu wa Mutharika, Rais wa Malawi
Rais mwingine aliyefariki mwaka 2012 ni Bingu wa Mutharika, rais wa
Malawi. Alipata mshutuko wa moyo mwezi Aprili na kufariki siku mbili
baadae akiwa na umri wa miaka 78. Uongozi wake ulikuwa ni wa miaka nane
na alipata mafanikio makubwa katika sera zake za kilimo na chakula. Sifa
yake iliharibika kufuatia maandamano makubwa yalopinga ununuzi wa ndege
ya rais iliyogharimu Dola milioni 14
3. John Atta Mills, Rais wa Ghana
Pia mwaka 2012, John Atta Mills, rais wa Ghana alifariki akiwa
nyumbani kwake kwa mshutuko wa moyo na saratani ya koo akiwa na umri wa
miaka 68. Alishinda uchaguzi wa rais wa 2008 alishika madaraka kwa miaka
mitatu pekee. Alianzisha mikakati mingi ya kiuchumi na mageuzi ya
kiuchumi yalomletea sifa kutoka ndani na nje ya nchi.
2. Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia
Meles Zenawi alifariki Agosti 2012 nchini Ubelgiji akiwa na umri wa
miaka 57 kwa maambukizi yasiyojulikana. Ameiongoza Ethiopia kwa miaka 5
kama rais kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 na kama Waziri Mkuu kwa miaka 17
kuanzia 1995 hadi 2012. Anajulikana kwa kuanzisha mfumo wa siasa wa
vyama vingi, lakini pia kwa ukandamizaji wa maandamano halali ya watu wa
Oromia wa kaskazini mwa Ethiopia.
1. Michael Sata, Rais wa Zambia
Michael Sata ni kiongozi wa hivi karibuni aliyefariki madarakani
akiwa na umri wa miaka 77 kwa maradhi ambayo hayakuwekwa wazi Oktoba 28
2014, nchini Uingereza. Baada ya uchaguzi wa 2011, uvumi juu ya afya
yake ulisambaa nchini Zambia. Kukosekana kwake katika shughuli kubwa za
kitaifa kuliibua wasiwasi wa afya yake ingawa msemaji wake alisema
alikuwa katika afya nzuri.
Chanzo: DW Idhaa ya Kiswahili.
THE WHEEL A POEM BY VENANCE GILBERT
![]() |
Venance on the sitting benches of Vikenge Hostels, Mzumbe University Main Campus Morogoro |
Poet: Venance Gilbert
Poem: The Wheel
Composition: October 18, 2016
Publication: April 20, 2017
Copyright: Venance Gilbert 2016
Copyright: Venance Gilbert 2016
The wheel was moving
But I never noticed
second counted, minutes gone,
hours died, days were numbered
weeks moved, months and years passed
I noticed it as the matter of living.
Mental pictures remind me
those days when the moments existed
Sometimes I wish to restore and start
I find the wheel moving fast following the line
Like the train on its pathway
Happy birthday takes back to those moments.
Today I am youth
Full capable to place the mind on motion
I often regret when I remember the moment
The moment when I was the driver of the wheel
But now the wheel drives, how possible?
I never drove it well and careful at the moment,
Drive the wheel careful before it drive you on its pathway.
WANASAYANSI WAGUNDUA UHAI KATIKA SAYARI YA SATURN
![]() |
Sayari ya Sarateni "Saturn" |
Mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia.
Uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa maisha, hapa duniani.
Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi.
"Tuna uhakika kuwa kitu chenye uhai kinaweza kuishi kwenye bahari ya Enceladus lakini lazima tufanye utafiti zaidi," alisema mwanasayansi wa Cassini kutoka Taasisi ya Utafiti ya Southwest, San Antonio, Dkt. Hunter Waite.
"Iwapo hakuna maisha huko, ni sawa, lakini ikiwa maisha yapo itakuwa bora zaidi," alieleza BBC.
Bahari iliyopo kwenye Enceladus inakisiwa kuwa na kina kirefusana sana na yapo majimaji kwa sababu ya joto linalotokana na mvuto wa mara kwa mara kutoka kwenye sayari ya Saturn.
Cassini tayari amedhibitisha kwamba maji hayo yanashikana na sakafu ya bahari kutokana na aina ya chumvi na silika ambayo pia imeonekana katika mashimo.
Lakini wanachotaka kujua sana wanasayansi ni ikiwa maswala fulani yanayotendeka duniani pia yanaweza kufanyika katika Enceladus - kitu kinachoitwa serpentinisation, ambayo hutengeneza gesi ya hidrojeni.
"Kwa viumbe hai, hidrojeni huwa ni kama kama pipi - ni chakula wanachokienzi," alieleza Dkt Chris McKay, mwanabiolojia wa maswala ya anga wa shirika la Nasa.
"Ni nzuri sana kwa kuvipa nguvu, na inaweza kusaidia viumbe vidogo sana. Kupata hidrojeni itakuwa vizuri sana na itakuwa moja ya ushahidi utakaoonyesha uwezekano wa kuwepo na uhai."
Viumbe hai anavyozungumzia Dkt McKay vinaitwa methanojeni kwa sababu vinatengeneza gesi ya metheni vinapogusana na hidrojeni na gesi ya kaboni .
Nasa, ambayo inaongoza ujumbe wa Cassini , ilitakikana kufanya tangazo la hidrojeni miezi michache baada ya uchunguzi wa mwisho waroketi ya mwezini, Oktoba mwaka wa 2015.
Ziara ya Cassini sasa inakamilika . Baada ya kuizunguka Saturn kwa muda wa miaka 12, inaendelea kuishiwa na mafuta na sasa itawachiliwa kuingia kwenye anga ya dunia hiyo ya Saturn mwezi Septemba, kuhakikisha kuwa haiwezi kugongana na Enceladus na kusababisha kuchafuka kwake.
Chanzo: BBC
DOWNLOAD ACHA NIKAE KIMYA DOWNLOAD PLATNUMZ NEW SONG
Huu ni wimbo mpya kuhusu hali inayoendelea nchini hivi sasa. Diamond pia ameamua kuzungumza kwa namna yake.
WELCOME ON BOARD: A POEM BY VENANCE GILBERT
Poem: Welcome on Board
Poet: Venance Gilbert
Date composed: January 3, 2017.
Copyright: Venance Gilbert.
If it would be
changing
Possibly this might
be like pressing next
Particularly on
a DVD player
But this does
not let us press
Welcome on
board; you are now part of us.
If be it swotting
Feasibly this
may be pacing another course
Chiefly at
school, college or varsity
But this does
not rest on on papers
Welcome on
board; you are now part of us.
If it would be
moving
Positively this
would be rambling
Definitely to beings
But this does
not hinge on our feet strength
Welcome on
board; you are now part of us.
If be it breathing
Certainly this
would be breathing in
Specifically in
all the livings
But this does
not need breathing structures
Welcome on board;
you are now part of us.
We have now trodden
on another numeral
Each of us has
to go through nippy revolution
Or reasonably style
headway
Never welcome
him on board as part of us
Let us welcome
him with fresh hallucinations
Welcome on
board; you are now part of us.
KUTOKA OMBA OMBA MPAKA KUWA MWANDISHI NA MUUZAJI BORA WA RIWAYA

Kwa takribani miongo 3 (miaka 30) , Jean-Marie Roughol aliishi maisha ya dhiki sana kama omba omba huko Arc de Triomphe, Paris Ufaransa. Ni miongoni mwa wamafamilia waliokuwa wakimiliki utajiri na maduka makubwa ya nguo na sehemu za starehe.
Wapo waliomdharau kama ilivyokawaida kwa omba omba yeyete, wapo waliomrushia sarafu walipokuwa wakitembea wapo waliompatia note nakadhalika lakini wapo pia ambao waliompa kipande cha kutembea tembea kwenye muvi zao.
Baada ya kukutana na aliyekuwa Waziri serikalini ambaye alimsidia kuchapisha kitabu kuhusu maisha ya dhiki aliyokuwa akiishi, maisha ya Roughol yamekuwa ni kile anchoita yeye "muujiza".
Matajiri walionunua kitabu chake ambacho kimeuza karinu nakala elfu 50 na kitabu cha tatu katikaa orodha ya vitabu vya Jamii ya Kifaransa, "French Society" muuzaji huyu (Roughol) kwa sasa anamiliki nyumba yake, anatafuta kazi lakini pia yupo katika maandalizia ya kuandaa kitabu ambaco kitakuwa ni muendelezo wa kitabu chake hicho cha sasa.
"Nimepewa nafasi katika maisha. Ni muujiza kwangu na sitamani tena kurudi mtaaniSitaki kuwakatisha tamaa watu walionisaidia nna kuwa na imani na mimi" Roughol alizungumza hayo katika mahojiano na The Observer. "sasa nakwenda kutafuta kazi hata kama ni kuosha vyombo mgahawani. Sasas ni zamu yangu kuwasaidia watu mtaani.Mtu yeyote anaweza kuwaona mtaani. Unaweza kua kiongozi na ukapoteza kazi, au ukawa katika janga la moto au ukawa na malipo kidogo ya uzeeni ambayo hata hayatoshi kukidhi maisha yako lakini bado upo hapo ulipo. Na wale wasiokuwa mtaani wanatakiwa kuwa na mshikamano kwa sababu inawezekana wakawa wao"
"Sihisi kama nimeona zaidi ya umaskini" George Orwell aliandika katika Down and Out in Paris zaidi ya miaka 80 iliyopita. 'Bado naweza kuchagua kitu kimoja ama viwili nilivyojifunza katika maisha ya dhiki, sitafikiri tena kua omba omba wote ni waongo ama kudhani uwa omba omba anaweza kutoka katika umasikini huo kwa kumpa kalamu. ama kushangazwa na mtu aliyeishiwa nguvu bila kufanya kazi au hata labda kujisogeza karibu na jeshi la Wokovu ama kufurshia chakula kizuri katika mgahawa nadhifu. Huu ni mwanzo"
"Sikuwahi kufikiria kama maisha yangu yangekuwa ya kuomba omba katika mitaa ya Paris ili niweze kuishi" Roughol anaandika "sikuwahi kufikiri pia kama nitakuja ulala mitaani usiku... hakika ninawajibka kwa yaliyotokea katika maisha yangu, lakini maisha yangu hayakuanza vizuri: huu sio utani: ni kweli"
Roughol alizaliwa mwaka 1968, mama yake alimtelekeza na baba yake alimtuma akatafute wazazi kokote kule nchini Ufaransa. Akiwa kwenye treni aliandika "Nilikuwa na furaha, nilishawishiwa nitawaona tembo. Nilikuwa nikiangalia nje ya dirisha kuwaona tembo hao".
Mama yake wa hiari alikuwa mkali sana, alikuwa akimpa vyakula vilivyooza na maji ambayo si safi na salama na pia alikuwa akimfungia kwenye sehemu kama banda. Anasema, "hakukuwa na chochote, hakukuwa na upendo, nakukuwa na chakula; watu hawa walilipwa kwa kulea watoto hivyo mimi nilikuwa kipato kwao"
Anakumbuka pia jinsi alivyowahi kulala na panya waliokuwa na ukubwa sawa na paka.
Maisha yake yalianza kubadilika alipoamua kuchunga baiskeli ya Jean-Louis Debre, 72, aliyewahi kuwa Waziri katika serikali ya Ufaransa baada ya hapo Waziri huyo alimshawishi Roughol kuandika kuhusu maisha yake.
"Nilimwambia mengine hayana umuhimu na nilitaka kujua kuhusu maisha yake, kwa nini alikuwa omba omba" Debre anaeleza katika Dibaji ya kitabu. "ni kwa nini watu mashuhuri tu, au wale wanaotaka kuwa wanasiasa, nyota wa TV, radio, sinema wanaruhusiwa kuelezea maisha yao ya awali? Je wale wasiofahamika hawana chochote cha kusema kuhusu maisha yao ya awali? Roughol amenifundisha zaidi ya kile nilichomfanyia."
Kitabu hicho "Je tape la manche" (I’m begging) kilichapishwa mwaka juzi 2015 lakini hakikuwa maarufu sana hadi kufikia miezi kadhaa alipopokea cheki kutoka kwa wasambazaji wa kitabu chake hicho, cheki hiyo ilimruhusu Roughol kuanza maisha mapya.
![]() |
Roughol (kulia) na aliyemsaidia Debre (kushoto) aliyewahi kuwa Waziri katika serikali ya Ufaransa. |
Leo, Roughol anamheshimu sana Debre kama mkombozi wa maisha yake. "miaka miwili iliyopita, sikuweza kufikiri kuwa hapa nilipo sasa. Jean-Louis ni baba ambaye sikutarajia kwa naye. Bado yuko pamoja nami na hajaniacha. Anasema maisha yangu yameanza kuimarika na sasa nina jukumu la kuhakikisha naendelea kutembea mwenyewe. Yuko sahihi" anasema Ruoughol.
MAKALA HII IMETAFSIRIWA KUTOKA THE GUARDIAN.
UNGANA NA VENANCE BLOG MITANDAONI
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: @venancegilbert
email: venancegilbert@gmail.com & venanceblog@gmail.com
FAHAMU WATU AU MAMBO YALIYOTAFUTWA SANA GOOGLE MWAKA 2016
Kila mwisho wa mwaka Mtandao wa Google hutoa orodha ya yale yaliyotafutwa kupitia mtandao huo. Tutaangalia katika nyanja za kiujumla, habari za dunia, watu, bidhaa za kiteknolojia, habari za michezo duniani, vifo, muvi/sinema, wasanii na vipindi vya runinga. Katika kila nyanja tutaangalia mambo au watu 10. Tuanze kuangalia trends hizo:
KIUJUMLA
1. Pokeman Go
2. iPhone 7
3. Donald Trump
4. Prince
5. Powerball
6. David Bowie
7. Deadpool
8. Olympics
9. Slither.io
10. Sucide Squad
HABARI ZA DUNIA
1. Uchaguzi wa Marekani (US Election)
2. Olympics
3. Brexit
4. Mauaji ya Orlando (Orlando Shooting)
5. Virusi vya Zika
6. Panama Papers
7. Nice
8. Brussels
9. Mauaji ya Dallas (Dallas Shooting)
10. Tetemeko la ardhi Kumamoto (Kumamoto Earthquake)
WATU
1. Donald Trump
2. Hillary Clinton
3. Michael Phelps
4. Melania Trump
5. Simone Biles
6. Bernie Sanders
7. Steven Avery
8. Celine Dion
9. Ryan Lochte
10. Tom Hiddleston
BIDHAA
1. iPhone 7
2. Freedom 251
3. iPhone SE
4. iPhone 6S
5. Google Pixel
6. Samsung Galaxy S7
7. iPhone 7 Plus
8. Note 7
9. Nintendo Switch
10. Samsung J7
HABARI ZA MICHEZO KIDUNIA
1. Rio Olympics
2. World Series
3. Tour de France
4. Wimbledon
5. Australian Open
6. EK 2016
7. T20 World Cup
8. Copa América
9. Royal Rumble
10. Ryder Cup
VIFO
1. Prince
2. David Bowie
3. Christina Grimmie
4. Alan Rickman
5. Muhammad Ali
6. Leonard Cohen
7. Juan Gabriel
8. Kimbo Slice
9. Gene Wilder
10. José Fernández
MUVI
1. Deadpool
2. Suicide Squad
3. The Revenant
4. Captain America Civil War
5. Batman v Superman
6. Doctor Strange
7. Finding Dory
8. Zootopia
9' The Conjuring 2
10. Hacksaw Ridge
WANAMUZIKI
1. Céline Dion
VIPINDI VYA RUNINGA
1. Stranger Things
2. Westworld
3. Luke Cage
4. Game of Thrones
5. Black Mirror
6. Fuller House
7. The Crown
8. The Night Of
9. Descendants of the Sun
10. Soy Luna
TAARIFA HII IMEANDALIWA KWA MSAADA KUTOKA GOOGLE.
Sogea karibu na VENANCE BLOG kwenye mitandao ya kijamii
facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: @venancegilbert
Barua pepe (e-mails): venancegilbert@gmail.com & venanceblog@gmail.com
KUELEKEA MWISHONI 2016 LADY JAY DEE KAYAANDIKA HAYA INSTAGRAM
"Kiukweli comeback yangu ya 2016 ilikuwa kubwa sana kuliko watu wengi walivyoitegemea mbali na changamoto ngumu na nyingi nilizowahi kupitia na ninazoendelea kuzipitia kuliko msanii yeyote yule wa kike wala wa kiume Tanzania nadiriki kusema bado nimesimama Imara *Kejeli *Dhihaka *Mabezo *Kutengwa *Story za kusingiziwa ikiwemo kuambiwa nyumba yangu inauzwa sijui inapigwa mnada na mengine yote mnayoyajua ni vitu vinavyovunja moyo sana. Ila Wa Tanzania ninawaheshimu sana linapokuja swala la kupigania kitu mnachokipenda. Hivi bila nyie si ningekuwa marehemu??? Bila fans JayDee ni nani??? Ninawashukuru kwa kuniamsha. Ninawashukuru kwa kuniamini. Ninawashukuru kwa kunipa nguvu na jeuri. Kuanzia Ndindindi mpaka Together *Mliijaza Mlimani City *Mkajaza mikoa niliyopita. Nawaomba muendelee kujaa 2017. Ili kuwadhihirishia wanadamu kuwa Mungu huwa ni mmoja tu. Happy new year to my fans all around the world. Nawapenda hata nikinuna. Kaeni tayari kwa album ya WOMAN 2017."
Hiyo ilikuwa ni sehemu ya kwanza, aliyoiandika jana na hii hapa chini ni sehemu ya pili:
"Kama nilivyoeleza hapo awali mwaka 2015 vitu vingi vilisimama ili nijpange upya. Na 2016 vitu vingi vilianza kurudi Ikiwemo kuendelea kuperform na Band yangu THE BAND ambayo niliondoa jina la MACHOZI BAND na tulizunguka sehemu nyingi nchini. Mwaka 2017 nitarudisha kitu kingine ambacho kimekuwa kikiulizwa na watu wengi sana kutokana na kutokuwepo hewani kwa takribani mwaka na nusu. DIARY YA LADY JAYDEE Itarudi tena kwa mfumo na muonekano wa tofauti na wa mwanzo ukizingatia maisha yangu pia yamebadilika Hivyo naomba sponsor kujitokeza kwa wingi pia kwani mambo yakuwa ni moto sana. Itakuwa ni kuhusu misha yangu binafsi ya kimuziki, kibiashara, mapenzi na kila kinachonizunguka. Kaeni tayari kwa Msimu mpya wa Diary ya Lady JayDee yenye production bora zaidi ya jana. Diary ya Lady JayDee pia itapatikana kwenye YouTube channel yangu fanya kusubscribe"
Hii ni sehemu ya pili aliyoiandika katika mtandao wa Instagram. Kama kuna lolote usikose kutembelea VENANCE BLOG kwa mengine zaidi. Jay Dee anapatikana Instagram @jidejaydee
Unaweza kulike VENANCE BLOG facebook kwa kubofya HAPA
Nifolo kwenye Twitter @Venancetz au bofya HAPA
Nipo Instagram pia @venancegilbert au bofya HAPA
TATHIMINI KWA UFUPI CHELSEA vs EVERTON KABLA YA MECHI SAA 2:30 EAT
Timu hizi mbili zimekutana katika michezo 49 ambapo Chelsea imeshinda mechi 22 na Everton imeshinda mechi 10 na kudroo mechi 17. Chelsea imeshinda nyumbani mechi 13 wakati Everton imeshinda mechi 9. Nje, Chelsea imeshinda mechi 9 wakati Everton imeshinda 2.
Katika mechi 3 zilizopita Chelsea ilifungwa na Everton magoli 2 kwa nunge, hii ilikuwa mechi ya Machi 12, 2016. Lakini pia mechi ya Januari 16, 2016 timu hizi zilitoka sare ya magoli 3. Na ile ya Septemba 12, 2015 Chelsea alipigwa magoli 3 kwa 1.
Katika msomu huu Chelsea ipo katika nafasi ya 4 wakati Everton ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi. Chelsea imeshinda 70% ya mechi ilizocheza huku Everton ikishinda 50%. Mechi za nyumbani Chelsea ina asilimia 80% dhidi ya mpinzani wake Everton 50% huku mechi zilizopigwa nje Chelsea ana 60% na Everton 40%. Chelsea ina wastani wa 2.1 katika magoli iloshinda wakati Everton ana wastani wa 1.5 Lakini pia Chelsea imefungwa wastani wa 0.9 wakati Everton ina 0.8.