WANASAYANSI WAGUNDUA UHAI KATIKA SAYARI YA SATURN

Sayari ya Saturn
Sayari ya Sarateni "Saturn"

Mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia.

Tathmini hii inatokea kufuatia uchunguzi katika sayari hiyo yenye kilomita 500 uliofanywa na Cassini.

Uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa maisha, hapa duniani.

Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi.

"Tuna uhakika kuwa kitu chenye uhai kinaweza kuishi kwenye bahari ya Enceladus lakini lazima tufanye utafiti zaidi," alisema mwanasayansi wa Cassini kutoka Taasisi ya Utafiti ya Southwest, San Antonio, Dkt. Hunter Waite.

"Iwapo hakuna maisha huko, ni sawa, lakini ikiwa maisha yapo itakuwa bora zaidi," alieleza BBC.
Bahari iliyopo kwenye Enceladus inakisiwa kuwa na kina kirefusana sana na yapo majimaji kwa sababu ya joto linalotokana na mvuto wa mara kwa mara kutoka kwenye sayari ya Saturn.

Cassini tayari amedhibitisha kwamba maji hayo yanashikana na sakafu ya bahari kutokana na aina ya chumvi na silika ambayo pia imeonekana katika mashimo.
 
Lakini wanachotaka kujua sana wanasayansi ni ikiwa maswala fulani yanayotendeka duniani pia yanaweza kufanyika katika Enceladus - kitu kinachoitwa serpentinisation, ambayo hutengeneza gesi ya hidrojeni.

"Kwa viumbe hai, hidrojeni huwa ni kama kama pipi - ni chakula wanachokienzi," alieleza Dkt Chris McKay, mwanabiolojia wa maswala ya anga wa shirika la Nasa.

"Ni nzuri sana kwa kuvipa nguvu, na inaweza kusaidia viumbe vidogo sana. Kupata hidrojeni itakuwa vizuri sana na itakuwa moja ya ushahidi utakaoonyesha uwezekano wa kuwepo na uhai."

Viumbe hai anavyozungumzia Dkt McKay vinaitwa methanojeni kwa sababu vinatengeneza gesi ya metheni vinapogusana na hidrojeni na gesi ya kaboni .

Nasa, ambayo inaongoza ujumbe wa Cassini , ilitakikana kufanya tangazo la hidrojeni miezi michache baada ya uchunguzi wa mwisho waroketi ya mwezini, Oktoba mwaka wa 2015.

Ziara ya Cassini sasa inakamilika . Baada ya kuizunguka Saturn kwa muda wa miaka 12, inaendelea kuishiwa na mafuta na sasa itawachiliwa kuingia kwenye anga ya dunia hiyo ya Saturn mwezi Septemba, kuhakikisha kuwa haiwezi kugongana na Enceladus na kusababisha kuchafuka kwake.


Chanzo: BBC

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017