KUTOKA OMBA OMBA MPAKA KUWA MWANDISHI NA MUUZAJI BORA WA RIWAYA

Jean-Marie Roughol 
Kwa takribani miongo 3 (miaka 30) , Jean-Marie Roughol aliishi maisha ya dhiki sana kama omba omba huko Arc de Triomphe, Paris Ufaransa. Ni miongoni mwa wamafamilia waliokuwa wakimiliki utajiri na maduka makubwa ya nguo na sehemu za starehe.

Wapo waliomdharau kama ilivyokawaida kwa omba omba yeyete, wapo waliomrushia sarafu walipokuwa wakitembea wapo waliompatia note nakadhalika lakini wapo pia ambao waliompa kipande cha kutembea tembea kwenye muvi zao.

Baada ya kukutana na aliyekuwa Waziri serikalini ambaye alimsidia kuchapisha kitabu kuhusu maisha ya dhiki aliyokuwa akiishi, maisha ya Roughol yamekuwa ni kile anchoita yeye "muujiza".

Matajiri walionunua kitabu chake ambacho kimeuza karinu nakala elfu 50 na kitabu cha tatu katikaa orodha ya vitabu vya Jamii ya Kifaransa, "French Society" muuzaji huyu (Roughol) kwa sasa anamiliki nyumba yake, anatafuta kazi lakini pia yupo katika maandalizia ya kuandaa kitabu ambaco kitakuwa ni muendelezo wa kitabu chake hicho cha sasa.


"Nimepewa nafasi katika maisha. Ni muujiza kwangu na sitamani tena kurudi mtaaniSitaki kuwakatisha tamaa watu walionisaidia nna kuwa na imani na mimi" Roughol alizungumza hayo katika mahojiano na The Observer. "sasa nakwenda kutafuta kazi hata kama ni kuosha vyombo mgahawani. Sasas ni zamu yangu kuwasaidia watu mtaani.Mtu yeyote anaweza kuwaona mtaani. Unaweza kua kiongozi na ukapoteza kazi, au ukawa katika janga la moto au ukawa na malipo kidogo ya uzeeni ambayo hata hayatoshi kukidhi maisha yako lakini bado upo hapo ulipo. Na wale wasiokuwa mtaani wanatakiwa kuwa na mshikamano kwa sababu inawezekana wakawa wao"

"Sihisi kama nimeona zaidi ya umaskini" George Orwell aliandika katika Down and Out in Paris zaidi ya miaka 80 iliyopita. 'Bado naweza kuchagua kitu kimoja ama viwili nilivyojifunza katika maisha ya dhiki, sitafikiri tena kua omba omba wote ni waongo ama kudhani uwa omba omba anaweza kutoka katika umasikini huo kwa kumpa kalamu. ama kushangazwa na mtu aliyeishiwa nguvu bila kufanya kazi au hata labda kujisogeza karibu na jeshi la Wokovu ama kufurshia chakula kizuri katika mgahawa nadhifu. Huu ni mwanzo"

"Sikuwahi kufikiria kama maisha yangu yangekuwa ya kuomba omba katika mitaa ya Paris ili niweze kuishi" Roughol anaandika "sikuwahi kufikiri pia kama nitakuja ulala mitaani usiku... hakika ninawajibka kwa yaliyotokea katika maisha yangu, lakini maisha yangu hayakuanza vizuri: huu sio utani: ni kweli"

Roughol alizaliwa mwaka 1968, mama yake alimtelekeza na baba yake alimtuma akatafute wazazi kokote kule nchini Ufaransa. Akiwa kwenye treni aliandika "Nilikuwa na furaha, nilishawishiwa nitawaona tembo. Nilikuwa nikiangalia nje ya dirisha kuwaona tembo hao".

Mama yake wa hiari alikuwa mkali sana, alikuwa akimpa vyakula vilivyooza na maji ambayo si safi na salama na pia alikuwa akimfungia kwenye sehemu kama banda. Anasema, "hakukuwa na chochote, hakukuwa na upendo, nakukuwa na chakula; watu hawa walilipwa kwa kulea watoto hivyo mimi nilikuwa kipato kwao"

Anakumbuka pia jinsi alivyowahi kulala na panya waliokuwa na ukubwa sawa na paka.

Maisha yake yalianza kubadilika alipoamua kuchunga baiskeli ya Jean-Louis Debre, 72, aliyewahi kuwa Waziri katika serikali ya Ufaransa baada ya hapo Waziri huyo alimshawishi Roughol kuandika kuhusu maisha yake.

"Nilimwambia mengine hayana umuhimu na nilitaka kujua kuhusu maisha yake, kwa nini alikuwa omba omba" Debre anaeleza katika Dibaji ya kitabu. "ni kwa nini watu mashuhuri tu, au wale wanaotaka kuwa wanasiasa, nyota wa TV, radio, sinema wanaruhusiwa kuelezea maisha yao ya awali? Je wale wasiofahamika hawana chochote cha kusema kuhusu maisha yao ya awali? Roughol amenifundisha zaidi ya kile nilichomfanyia."

Kitabu hicho "Je tape la manche" (I’m begging) kilichapishwa mwaka juzi 2015 lakini hakikuwa maarufu sana hadi kufikia miezi kadhaa alipopokea cheki kutoka kwa wasambazaji wa kitabu chake hicho, cheki hiyo ilimruhusu Roughol kuanza maisha mapya.




Jean-Louis Debré with Jean-Marie Roughol
Roughol (kulia) na aliyemsaidia Debre (kushoto) aliyewahi kuwa Waziri katika serikali ya Ufaransa.


Leo, Roughol anamheshimu sana Debre kama mkombozi wa maisha yake. "miaka miwili iliyopita, sikuweza kufikiri kuwa hapa nilipo sasa. Jean-Louis ni baba ambaye sikutarajia kwa naye. Bado yuko pamoja nami na hajaniacha. Anasema maisha yangu yameanza kuimarika na sasa nina jukumu la kuhakikisha naendelea kutembea mwenyewe. Yuko sahihi" anasema Ruoughol.




MAKALA HII IMETAFSIRIWA KUTOKA THE GUARDIAN.


UNGANA NA VENANCE BLOG MITANDAONI
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: @venancegilbert
email: venancegilbert@gmail.com & venanceblog@gmail.com

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017