MECHI YA ATLETICO & REAL MADRID KULINDWA NA POLISI 2,000
Walinzi zaidi ya 2,000 watatumiwa
kudumisha usalama na kudhibiti mashabiki wakati wa mechi ya nusufainali
ya mkondo wa kwanza kati ya Real Madrid na Atletico Madrid katika Ligi
ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mechi hiyo itakayochezewa Santiago Bernabeu
siku ya Jumanne imeorodheshwa kama yenye "hatari kubwa" na usalama
"utaimarishwa", maafisa wasimamizi wa jiji la Madrid walisema Ijumaa.
UEFA wameamrisha usalama katika mechi za klabu Ulaya uimarishwe baada ya
shambulio kwenye basi la timu ya Borussia Dortmund mnamo 11 Aprili.
Atletico watakuwa na mashabiki 4,000 katika uwanja huo wa Real unaotoshea mashabiki 80,000.
Kawaida ni mashabiki wachache sana husafiri kuhudhuria mechi za ugenini Uhispania.
Idadi
ya walinzi tarehe 2 Mei itakuwa ya juu zaidi ya waliokuwepo wakati wa
mechi iliyopita ya Real Ulaya dhidi ya Bayern Munich polisi wa
kukabiliana na fujo walipokabiliana na mashabiki wageni wakati wa
mapumziko.
Kulikuwa pia na fujo mechi ya robofainali ya Atletico nyumbani, polisi wakikabiliana na mashabiki wa Leicester City.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment