KUELEKEA MWISHONI 2016 LADY JAY DEE KAYAANDIKA HAYA INSTAGRAM



Kuelekea mwisho wa mwaka 2016 msanii mkongwe Lady Jay Dee ameyaandika haya katika mtandao wa Instagram:

"Kiukweli comeback yangu ya 2016 ilikuwa kubwa sana kuliko watu wengi walivyoitegemea mbali na changamoto ngumu na nyingi nilizowahi kupitia na ninazoendelea kuzipitia kuliko msanii yeyote yule wa kike wala wa kiume Tanzania nadiriki kusema bado nimesimama Imara *Kejeli *Dhihaka *Mabezo *Kutengwa *Story za kusingiziwa ikiwemo kuambiwa nyumba yangu inauzwa sijui inapigwa mnada na mengine yote mnayoyajua ni vitu vinavyovunja moyo sana. Ila Wa Tanzania ninawaheshimu sana linapokuja swala la kupigania kitu mnachokipenda. Hivi bila nyie si ningekuwa marehemu??? Bila fans JayDee ni nani??? Ninawashukuru kwa kuniamsha. Ninawashukuru kwa kuniamini. Ninawashukuru kwa kunipa nguvu na jeuri. Kuanzia Ndindindi mpaka Together *Mliijaza Mlimani City *Mkajaza mikoa niliyopita. Nawaomba muendelee kujaa 2017. Ili kuwadhihirishia wanadamu kuwa Mungu huwa ni mmoja tu. Happy new year to my fans all around the world. Nawapenda hata nikinuna. Kaeni tayari kwa album ya WOMAN 2017."

Hiyo ilikuwa ni sehemu ya kwanza, aliyoiandika jana na hii hapa chini ni sehemu ya pili:

"Kama nilivyoeleza hapo awali mwaka 2015 vitu vingi  vilisimama ili nijpange upya. Na 2016 vitu vingi vilianza kurudi Ikiwemo kuendelea kuperform na Band yangu THE BAND ambayo niliondoa jina la MACHOZI BAND na tulizunguka sehemu nyingi nchini. Mwaka 2017 nitarudisha kitu kingine ambacho kimekuwa kikiulizwa na watu wengi sana kutokana na kutokuwepo hewani kwa takribani mwaka na nusu. DIARY YA LADY JAYDEE Itarudi tena kwa mfumo na muonekano wa tofauti na wa mwanzo ukizingatia maisha yangu pia yamebadilika Hivyo naomba sponsor kujitokeza kwa wingi pia kwani mambo yakuwa ni moto sana. Itakuwa ni kuhusu misha yangu binafsi ya kimuziki, kibiashara, mapenzi na kila kinachonizunguka. Kaeni tayari kwa Msimu mpya wa Diary ya Lady JayDee yenye production bora zaidi ya jana. Diary ya Lady JayDee pia itapatikana kwenye YouTube channel yangu fanya kusubscribe"

Hii ni sehemu ya pili aliyoiandika katika mtandao wa Instagram. Kama kuna lolote usikose kutembelea VENANCE BLOG kwa mengine zaidi. Jay Dee anapatikana Instagram @jidejaydee





 Unaweza kulike VENANCE BLOG facebook kwa kubofya HAPA
Nifolo kwenye Twitter @Venancetz au bofya HAPA
Nipo Instagram pia @venancegilbert au bofya HAPA

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017