WAFAHAMU MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOFARIKI WAKIWA MADARAKANI
Leo nimekuandikia orodha ya marais 10 waliofariki wakiwa madarakani. Tuanze kuhesabu sasa:
10. Lansana Conte, Rais wa Guinea
Baada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana
akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi
ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni
rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya
aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi.
9. Omar Bongo, Rais wa Gabon
Saratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha Rais Omar
Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka
42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni
kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa
akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa
huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini.
8. Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-Bissau
Joao Bernardo Vieira rais wa Guinea-Bissau aliuwawa nchi mwake Machi
2009, akiwa na umri wa miaka 69. Alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa
miaka 31. 1978 alikuwa waziri mkuu na kuchukua madaraka 1980
na alitawala kwa miaka 19. Alibadilika na kuwa kiongozi wa umma na
aliongoza miaka minne mingine zaidi. 2005 alishinda tena uchaguzi wa
uraisi.
7. Umaru Musa Yar’Adua, Rais wa Nigeria
Umaru Musa Yar’Adua, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 mwaka 2011
akisumbuliwa na matatizo ya moyo
nchini Nigeria. Alikuwa madarakani kwa miaka mitatu pekee. Alikosekana
katika kampeni za uchaguzi kwa sababu za kiafya. Baada ya kuchaguliwa
kwake 2007, afya yake ilidhoofika kwa haraka.
6. Muammar Gadhafi, kiongozi na mwana mapinduzi wa Libya
Mwathirika wa mauaji, Muammar Gadhafi aliuawa akiwa na umri wa miaka
69 na vikosi vya waasi katika mazingira yasiyoeleweka nchini Libya,
baada ya kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Aliuondoa
uongozi wa kifalme bila ya kumwaga damu wakati wa mapinduzi ya kijeshi
ya mwaka 1969 lakini utawala wake ulifikia kikomo baada ya matokeo ya
vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni.
5. Malam Bacai Sanha, Rais wa Guinea-Bissau
Kiongozi wa nne kufariki mwaka 2012 alikuwa ni Malam Bacai Sanha rais
wa Guinea-Bissau. Aliugua ugonjwa wa kisukari na alifariki mjini Paris
baada ya miaka minne kama rais akiwa na umri wa miaka 64. Katika kipindi
chote cha utawala wake alisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya
yalosababisha kwenda hospitali mara nyingi.
4. Bingu wa Mutharika, Rais wa Malawi
Rais mwingine aliyefariki mwaka 2012 ni Bingu wa Mutharika, rais wa
Malawi. Alipata mshutuko wa moyo mwezi Aprili na kufariki siku mbili
baadae akiwa na umri wa miaka 78. Uongozi wake ulikuwa ni wa miaka nane
na alipata mafanikio makubwa katika sera zake za kilimo na chakula. Sifa
yake iliharibika kufuatia maandamano makubwa yalopinga ununuzi wa ndege
ya rais iliyogharimu Dola milioni 14
3. John Atta Mills, Rais wa Ghana
Pia mwaka 2012, John Atta Mills, rais wa Ghana alifariki akiwa
nyumbani kwake kwa mshutuko wa moyo na saratani ya koo akiwa na umri wa
miaka 68. Alishinda uchaguzi wa rais wa 2008 alishika madaraka kwa miaka
mitatu pekee. Alianzisha mikakati mingi ya kiuchumi na mageuzi ya
kiuchumi yalomletea sifa kutoka ndani na nje ya nchi.
2. Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia
Meles Zenawi alifariki Agosti 2012 nchini Ubelgiji akiwa na umri wa
miaka 57 kwa maambukizi yasiyojulikana. Ameiongoza Ethiopia kwa miaka 5
kama rais kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 na kama Waziri Mkuu kwa miaka 17
kuanzia 1995 hadi 2012. Anajulikana kwa kuanzisha mfumo wa siasa wa
vyama vingi, lakini pia kwa ukandamizaji wa maandamano halali ya watu wa
Oromia wa kaskazini mwa Ethiopia.
1. Michael Sata, Rais wa Zambia
Michael Sata ni kiongozi wa hivi karibuni aliyefariki madarakani
akiwa na umri wa miaka 77 kwa maradhi ambayo hayakuwekwa wazi Oktoba 28
2014, nchini Uingereza. Baada ya uchaguzi wa 2011, uvumi juu ya afya
yake ulisambaa nchini Zambia. Kukosekana kwake katika shughuli kubwa za
kitaifa kuliibua wasiwasi wa afya yake ingawa msemaji wake alisema
alikuwa katika afya nzuri.
Chanzo: DW Idhaa ya Kiswahili.
Comments
Post a Comment