Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kwa nafsi yake ametoa matumaini kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini kuhusu hatima yao ya mkopo wa Elimu ya Juu alipokuwa akihudhuria sherehe ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Rais Magufuli amebainisha haya, namnukuu; "Tunapopitia katika challenge hii muivumilie serikali kutengeneza utaratibu ulio mzuri, ninafahamu, katika bajeti ya mwaka 2015/2016, fedha iliyotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa sababu Mh. Waziri umezungumza hapa zilikuwa bilioni 340 ambazo zilikjuwa zinatosha karibu wanafunzi tisini elfu (90,000) baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani ili kutimiza yale tuliyokuwa tumeahidi tuliongeza fedha hizo za mkopo hadi kfikia bilioni 473 bajeti ilikuwa ya bilioni 340 tukaongeza zikafika bilioni 473 kutokana na makusanyo na tukaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi 124,358 mwaka huu ameeleza ni zaidi ya bilioni 483 zimepitishwa katika bajeti k...