FIFA itatoa zawadi ya dola milioni mbili kwa kila mojawapo ya timu tano za Afrika zilizofuzu kucheza kombe la dunia kuzisaidia katika maandalizi, amesema rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF. Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia, zimefuzu kushiriki katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi, na rais wa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad, alismea katika taarifa kwamba fedha hizo zitatumika "kushughulikia mapema, suala la bonasi za wachezaji." "Migogoro juu ya malipo katika michuano iliyopita ilipelekea kuwepo na hali zilizoathiri vibaya taswira ya soka barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kuathiri kwa kiwango kikubwa utendaji wa timu viwanjani," aliongeza. Mwaka uliopita, shirikisho la kandanda la Nigeria (NFF) lilisaini makubaliano na wachezaji wake wakiahidi kujiepusha na migogoro ya bonasi na malipo ambayo imeharibu kampeni zao za nyuma za kombe la dunia. Wachezaji wa timu ya Nigeria, Sup...
Comments
Post a Comment