MFAHAMU HILLARY CLINTON KWA MAMBO HAYA 15

Tokeo la picha la hillary clinton
Jina Kamili: Hillary Diane Rodham Clinton
Kuzaliwa: Oktoba 26, 1947
Alikozaliwa: Chicago, Illinois

Kwa Ufupi

Alipochaguliwa kuwa Seneta mwaka 2001 alikuwa mwanamke wa kwanza First Lady kuwa mtumishi wa serikali. Baadaye alikuwa Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani mwaka 2009 akitumikia wadhifa huo hadi mwaka 2013 katika utawala wa Rais Barrack Obama. Mwaka huu (2016), amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha The Democratics.

Tokeo la picha la hillary clinton
Hillary alizaliwa  Oktoba 26, 1947 huko Chicago, Illinois. Alipata Shahada yake ya Sheria kutoka Yale University. Alifunga ndoa na mwanafunzi mwenziye aliyekuwa akisoma sheria Bill Clinton mwaka 1975. Baadaye alitumikia taifa la Marekani kama First lady  mwaka 1993 hadi 2001, na baadaye akiwa Seneta mwaka 2001 hadi 2009. Mapema mwaka 2007 Clinton alitangaza kugombea Urais nchini Marekani. Katika kura za maoni mwaka 2008 alichuana na Barrack Obama lakini kura hazikumruhusu kugombea Urais kwa ticket ya Democratic. Rais Obama alipoingia madarakani alimchagua kuwa Katibu Mkuu mwaka 2009 hadi 2013.

HillaryRodham ni mtoto  mkubwa katika familia ya Hugh Rodham na Dorothy Emma Howell Rodham. Ana wadogo zake wawili wanaume; Hugh Jr. aliyezaliwa 1950 na Anthony aliyezliwa 1954.

Kama kijana Hillary aliingia katika siasa na kumfanyia kampeni mgombea wa chama cha Republican Barry Goldwater mwak 1954. Alivutiwa kufanya kazi za umma baada ya kusikia hotuba ya Martin Luther King Jr. huko Chicago na hapo alijiunga na chama cha Democratic mwaka 1968.

Elimu

Tokeo la picha la hillary clinton at yale
Hillary enzi za Yale
Hillary alisoma Wellesley College ambapo alikuwa akishiriki katika masuala ya siasa shuleni na alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa darasa lake kabla hajahitimu mwaka 1959. Baadaye alijiunga na Shule ya Sheria Yale ambako alikutana na Bill Clinton. Alitunukiwa Shahada ya Heshima katika sheria mwaka 1973 na aliendelea na alijiunga na Kituo cha masomo ya watoto Yale ambako alisoma kozi za masomo ya watoto na madawa nakwa mwaka mmoja.

Ndoa

Tokeo la picha la hillary clinton and bill wedding
Hillary na Bill Clinton siku ya harusi yao 1975

Alifunga ndoa na Bill Clinton mwaka 1975 na wana mtoto mmoja anayeitwa Chelsea. Ndoa hii ipo katika orodha ya watu maarufu duniani ambao wameanza mahusiano tokea wakiwa masomoni. Hillary alipomaliza chuo kwa wakti ule alikaa mwaka mzima chuoni hapo akimsubiri mpenzi wake Bill Clinton ahitimu masomo yake.

Vitabu alivyoandika

1996- It Takes a Village
1997- The Unuque Voice of Hillary Clinton
1998- Dear Socks, Dear Buddy
 2000- An Invitation to the White House
2003- Living History
2014- Hard Choices
2015- Solutions: American Leaders Speak Out on Criminal Justice
2016- Stronger Together

First Lady wa Marekani

Tokeo la picha la the clintons during bill inauguration
Siku ya kiapo, Bill Clinton kama Rais akiwa na mkewe Hillary na binti yao Chelsea

Katika Uchaguzi wa mwaka 1992 Hillary alishiriki vyema katika kuaslimia wapiga kura, kuhutubia na kuwa miongoni mwa washauri wakuu wa Bill Clinton.


MAMBO 15 UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU HILLARY CLINTON

15. Ameshinda tuzo ya Grammy mwaka 1997 lakini sio tuzo ya muziki. Ni kuhusu kitabu chake cha It Takes a Village lakini sio pekee aliyeshinda tuzo hizo, Obama pia alishachukua tuzo hii katika kitabu chake pia.

14. Hillary hajaendesha gari toka mwak 1996 alilisema hili mwaka 2012.

13.  Mama yake Bill Clinton (mama mkwe wa Hillary) hakufikiria kwamba Hillary ni mzuri sana kuwa na mwanaye kuwa hana mvuto.

12. Moja kati ya kesi za awali za Hillary kama mwanasheria ilikuwa inahusisha Panya.

11. Hillary Clinton mwanzoni alikuwa mfuasi wa chama cha Republican kabla ya kuhamia Democratic mwaka 1968 baada ya kuvutiwa na moja kati ya hotuba za Martin Luther King Jr.

10.Katika utawala waRais Bill Clinton FBI walichukua picha za viganja (fingerprints) vya Bill na Hillary kuona kama wawili hao waliweza kuangalia nyaraka za FBI.Ilibainika kwamba hawakuhusika kuangalia nyaraka hizo lakini miaka miwili baadaye zilikutwa nyumbani kwa Hillary zikiwa na alama za viganja vyake.

9. Utambulisho wake wa Huduma za Siri ni "Evergreen" na alipewa utambulisho huu akiwa First lady na Huduma za Siri.Amekua akitumia utambulisho huu hata katika kampeni zake za Urais. Katika kipindi cha 2008 alipokuwa akigombea utambulisho huu ulirejeshwa tena. Bill Clinton pia amekuwa akitumia utambulisho wa "Eagle" katika kipindi cha harakati za mkewe kuelekea Ikulu .

8. Ni First lady pekee ambaye amegombea Useneta na kushinda kiti hicho akiwa pia ni First lady. Alikuwa Seneta wa New York mwaka 2001 na kukabidhiwa Ofisi Januari 3 mwaka huo.

7. Jarida la Sheria la Marekani 'The National Law Journal' lilimtaja Hillary kuwa miongoni mwa wanasheria 100 wenye ushawishi nchini humo mwaka 1988 na 1991. Umahiri wake katik sheria ulimfanya awe na pesa nyingi hata kumshinda mumewe Bill aliyekuwa Gavana wa Arkansas kwa wakati huo. Umahili wa Clinton ktik sheria ulichangia pia kwa kiasi kikubwa kumfanya Bill awe Rais wa nchi hiyo kwa kipindi hicho.

6. Ni Katibu Mkuu aliyesafiri kuliko makatibu wengine katika Historia katika kipindi chake cha miaka 4. Alizuru nchi 112 na kusafiri kwa ndege maili milioni 1 na kutumia 25% ya kipindi chake katika safari.

5. Amekuwa akituhumiwa kujihusisha na Usagaji "mapenzi ya jinsia moja". Baadhi ya watu wamekuwa wakithibitisha hili kwa mfano Edward Klein ambaye ameandika ktika kitabu chake The Truth About Hillary kuwa amekuwa akishiriki usagaji na msaidizi wake Huma Abedin na wasagaji wengine.

4. Hillary na mumewe Bill waliwahi kuitwa Mahakamani kutoa ushahidi kuhusika katik scandal ya Whitewater Development. Hata hivyo baadaye hawakukutwa na hatia ya kufanya mabaya katika scandal hiyo.

3. Hillary aliamua kutumia jina la Clinton baada ya kushawishiwa na wapiga kura wa Arkansas. Baada ya ndoa yao Hillary aliendelea kutumia jina lake la Hillary Rodham, Wapiga kura hao walitaka kujua kama ndoa yao ni ndoa kweli ama fasheni tu hivyo Hillary akaamua kutumia jina la Hillary Rodham Clinton. Kwa hiyo ili kufanya mumewe ashinde katika Uchaguzi kuwa Gavana wa jimbo la Arkansas aliamua kujiita Hillary Rodham Clinton.

2. Alishiriki katika jopo la wanasheria 43 kumtia hatiani Rais Richard Nixon. Wanajopo wenzie walimtuhumu kama muongo na kutofuata maadili ya kumtia hatiani Rais Nixon. Bosi wa Hillary alisema mara kwa mara Hillary alikuwa akikosea katik kuuliza maswali lakini hakuwa na uwezo wa kumfukuza Hillary kazi.

1. Japokuwa alipmba kurasa za jarida la The Vogue mwaka 1998, alikataa kuonekana katika Jarida hilo mwaka 2007 kwa kuhofia kuwa mfeministi sana kitu ambacho kingeleta shida katika mbio zake za uchaguzi wa Urais mwaka 2008.








Tokeo la picha la hillary clinton
 Tokeo la picha la hillary clinton

MAKALA HII IMEHARIRIWA KWA HISANI YA MTANDAO.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017