Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7 wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani na athari zake. Chanzo: DW
Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda. Zaidi ya watu milioni 1 5 katika bara hili huitumia lugha hi i kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya M uungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika. TANZANIA Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa. Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVI...
Uhali gani msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG? Nakukaribisha katika darasa jipya la kufahamu mambo kadha wa kadha kama yanavyokuwa yakipigiwa kura na watu kutoka vyanzo tofauti kama vile tovuti, mitandao ya kijamii, watu wenye ushawishi, majarida n.k. Basi kwa kuanza leo nakuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea. Vigezo vilivyotumika husemwa na mtandao husika unaotoa orodha hiyo. Ili kurahisisha kazi hii, mimi kama Blogger ntakuletea orodha hizi kila siku kwa lugha ya Kiswahili. Na tuanze sasa, tunaanzia Korea Kusini kuangalia waigizaji wa kiume wenye mvuto kwa mwaka 2017: # 10. Lee Byung-Hun Lee Byung-Hyun ni muimbaji, mwanamitindo na muigizaji kutokea Korea ya Kusini. Anamiliki kampuni yake ya BH Entertainment. Ni muhitimu wa masuala ya filam na maigizo katika Chuo Kikuu Chung Ang. Anazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kikorea na Kimandarin lakini pia ni mfuasi wa dini ya Budha. Alizaliwa Julai 12, 1972 katika jimbo la Gyeonggi Korea ya Kusini. Alianz...
KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa ...
Jana nilikuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea Kusini, leo tuangalie upande wa pili kwa akina dada ambao ni warembo zaidi. #10. Han Ye Seul Han Ye Seul alizaliwa chini Marekani japokuwa ana asili ya Korea. Anaigiza series na filamu za kawaida. Alionekana katika Nonstop 4 na pia ameigiza katika muvi kama vile Couple or Truble, Birth of a Beauty, Miss Gold Digger na Penny Pincher. Baada ya kupata umaarufu nchini Korea aliamua kufuta uraia wake wa Marekani na kuamua kuwa raia wa Korea Kusini. #9. Song Hye Kyo Song Hye Kyo alipata umaarufu katika tasnia ya muvi nchini Korea katika muvi kama vile Autumn in My Heart, All In, Full House, The World They Live In na nyinginezo. Ni mwenye furaha na amekuwa akiigiza muvi zake vizuri sana. #8. Lee Da Hae Lee Da Hae ni muigizaji maarufu nchini Korea Kusini. Ameigiza katika My Girl, Green Rose, The Slave Hunter, Miss Ripley na Hotel King. Ameigiza pia katika muvi za Kichina kama vile Actually Lob...
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na maarifa kwa watahiniwa waliofanya mtihani mwaka 2017. Kuangalia matokeo BOFYA HAPA
Bibi kizee mmoja mwenye umri wa miaka 85 raia wa Marekani na ambaye amekuwa akiiba vito vya thamani kwa zaidi ya miaka 60 amehukumiwa tena kwa kosa la wizi. Doris Payne, anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dola 690, kutoka katika duka moja la uuzaji wa vitu vya thamani la Saks katika kiunga kimoja mjini Atlanta-Marekani. Wakili wake anatafuta namna ataachiwa huru kwa sababu ya kudorora kwa afya yake. Payne, ambaye maisha yake ya wizi yaliwekwa katika filamu mwaka 2013, amewahi kufungwa jela mara kadhaa kwa makosa mengi tu ya wizi na uhalifu. Wakuu nchini Marekani wanasema kuwa, ametumia majina 22 ya bandia tangu alipoiba almasi kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 23, na akaweza kukwepa kutiwa mbaroni. Muungano wa Walinzi wa vitu vya thamani JSA, kampuni moja kubwa ya kibiashara, ilituma tahadhari kwa maduka yote yanayouza bidhaa na mapambo ya thamani kujihadhari na mwizi huyo sugu mapema miaka ya 70. Rais wa kampuni hiyo kubwa alitaja tabia ya bi kizee huyo ...
Picha kwa hisani ya Debt.org 1.0 UTANGULIZI Nilipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu nilisikia manung'uniko miongoni mwa wanafunzi wenzangu wengi wa vyuo vikuu ambayo yalitokana na taaluma wanazosoma. Kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea manung'uniko hayo miongoni mwa wasomi hawa tukiachilia mbali suala la ucheleweshwaji wa mikopo miongoni mwa wasomi hawa (kwa sasa changamoto hii inapungua kadiri siku zinavyosonga). Tatizo lingine ambalo linawasumbua wasomi hawa ni suala la uchaguzi wa taaluma gani akaisome Chuo Kikuu. Uchaguzi wa taaluma (career choice) ni jambo nyeti sana na la kuzingatia kwa muhitimu yeyote wa elimu ya kuanzia kidato cha nne. Jamii yetu ya Tanzania haifahamu kwa undani kuhusu umuhimu wajambo hili lakini huku ndiko msingi hundaliwa. Mtu anapohitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano ama ngazi ya astashahada (certificate) na stashahada (diploma) hapo ndipo uchanguzi wa taaluma huanza. Kwa kuandika makala haya ninakusudia ...
10. YUSUF MANJI Manji ni mmiliki wa mali zisizohamishika hasa majengo kwa ajili ya makazi ya watu na biashara. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya Quality Group of Companies. Anajihusisha pia na vipuli vya magari. Haya yamemfanya kua miongoni mwa matajiri wa juu zaidi nchini. 9. FIDA RASHID Fida ni muanzilishi wa kampuni ya Africarrier Group. Hii ni kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. Pia kampuni hii inahusika na usambazaji wa magali ya kampuni ya Eicher na Golden Dragon hapa nchini. Hii imefanya kampuni yake kufanya vyema sana katika idara hii. Fida pia ni mmiliki wa mali zisizohamishika pamoja na majengo kama Zahra Tower na Raha Tower. Amekua mjasiriamali anayetengeneza zaidi mazingira mazuri ya biashara zake kama wafanyavyo wengine. 8. GHALIB SAID MOHAMMED Ghalib Mohammed alikua akifanya biashara ya korosho hapo awali na biashara nyingine akishirikiana na baba yake. Baadaye Ghalib Said aliamua kuanzisha kampuni yake na kuiita GSM Group ambayo inajihusisha...
Comments
Post a Comment