RAIS MAGUFULI AAHIDI KUENDELEA KUTOA MIKOPO 2016/2017 KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NA KUTOA RAI SUALA HILO KUSHUGHULIKIWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kwa nafsi yake ametoa matumaini kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini kuhusu hatima yao ya mkopo wa Elimu ya Juu alipokuwa akihudhuria sherehe ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Rais Magufuli amebainisha haya, namnukuu;
"Tunapopitia katika challenge hii muivumilie serikali kutengeneza utaratibu ulio mzuri, ninafahamu, katika bajeti ya mwaka 2015/2016, fedha iliyotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa sababu Mh. Waziri umezungumza hapa zilikuwa bilioni 340 ambazo zilikjuwa zinatosha karibu wanafunzi tisini elfu (90,000) baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani ili kutimiza yale tuliyokuwa tumeahidi tuliongeza fedha hizo za mkopo hadi kfikia bilioni 473 bajeti ilikuwa ya bilioni 340 tukaongeza zikafika bilioni 473 kutokana na makusanyo na tukaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi 124,358 mwaka huu ameeleza ni zaidi ya bilioni 483 zimepitishwa katika bajeti kwa hiyo wanafunzi wengi zaidi watapata mkopo ninafahamu kwa mfano wanafunzi wanaoendelea ambao wako karibu 93,000 wote wamekuwa accommodated kwenye mkopo pamoja na wanafunzi wapya ambao nafikiri ni zaidi ya 25,000 lakini ni lazima kweli nikiri hapakuwepo na coordination palitakiwa kwanza vyuo vyote vya elinu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua kwa sababu wapo wengine walifungua mwezi mzima uliopita wako wengine wamefungua jana wako wengine watafungua keshokutwa ukishafungua haraka haraka wanafunzi wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawambia kufanya registration lazima walipe wakati Bodi ya Mikopo haijatoa orodha ya majina ya vijana ambao watakaokopeshwa ni contradiction.
Palikuwa pawepo na communication kati ya Bodi ya Mikopo sijui ni TCUsijui ni nani, Wizara ya Elimu na Wizara ya Fedha kwamba katika orodha ya wanafunzi watakaopata mikopo ni hawa hapa majina yao ni haya hapa mnapeleka majina hayo na orodha, amount ya fedha zinazotakiwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Fedha nao wanaprocess zao fedha hizi tunazitoa baadaye zikishapelekwa kwenye benki kwenye hizo akaunti za wanafunzi, mngeweza mkafungua vyuo hapakuwa na sababu ya kufungua mwezi mzima kabla wanafunzi wanakaa pale hajui kama atapata mkopo au hatapata mkopo halafu unamwambia hakuna registration kwa sababu hujapata mkopo inaleta usumbufu wa ajabu, na hilo.
Nitoe wito kwa Wizara ya Elimu na hili nasema kwa dhati lengo la serikali si kuleta usumbufu kwa wanfunzi lakini ni ukweli pia kwamba haitatoa mikopo kwa wanafunzi ambao wenye uwezo unamkuta mtoto wa Profesa Rwekaza na wewe upate mkopo mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo mtoto wa Katibu Mkuu Kijazi naye apate mkopo haiwezekani mkopo huu umelenga kwa ajili ya kutoa watoto masikini lakini nafahamu na ninasikia hata katika Bodi ya Mikopo kule kuna upendeleo upendeleo wa aina fulani katika kutoa mkopo hata ambao hawastahili wanapewa mikopo na ambao hawastahili wananyimwa mkopo sasa hili Waziri na Bodi zinazohusika mulisimamie sitaki siku moja nije huko kwenye Bodi ya mikopo nichukue orodha ya wanafunzi wote niangalie shule walizosoma na particulars walizozijaza halafu nije nipewe majina ya watu ambao hawakustahili kupewa mkopo wanafunzi 25 wa mwaka huu siwezi kushindwa kusoma kwa siku 1 ntapekua page by page 25,000 ukigawa kwa masaa 12 ambayo naweza nikajifungia kila jina naweza nikalisoma kwa sekunde ngapi ninajua naweza, sasa tusifikie huko.
Ninashukuru Waziri baada ya kuona hii changamoto ukawa umelileta hili suala haraka haraka na tukatoa instruction Wizara ya Fedha watoe bilioni 80 za mwanzo haraka haraka na nimeambiwa zimeshatolewa, sasa niwaombe wanafunzi msiwe na haraka haraka kwa sababu katika changamoto hizi ambazo zinapita ndani ya serikali wanafunzi hewa, mikopo hewa, mishahara hewa hatutaki hela yetu ipotee ovyo pameshatokea changamoto na najua haitatokea tena vyuo vikuu vitakuwa vinafunguliwa siku ambapo wana uhakika na fedha zitakuwa zimeshapelekwa kwenye wanafunzi.
Lakini pia pamekuwa na utitiri mwingi mno wa vyuo vikuu unakuta shule ilikuwa inaitwa sekondari leo ukisoma kwenye orodha nayo inaitwa Chuo Kikuu na saa nyingine inafikia wanafunzi unaanza kuwagombania, Chuo Kikuu kwa mfano cha Dodoma kina capacity ya kuweka wanafunzi mpaka 45,000 waliopo ni 30,000 lakini unakuta kinafunguliwa chuo kingine Bagamoyo kina wanafunzi 20 mabweni hayapo maabara hayapo natoa mfano tu labda nimesema Bagamoyo kingine kinafunguliwa Chato.
Sasa ninachotaka kutoa wito kwa Bodi, TCU, Wizara hebu mpitie vizuri hivi vyuo mnatoa vibali mnatoa vibali mno vya kuanzisha chuo kikuu kila mahali wakati vyuo vilivyopo havijajaa watu na mnawachanganya saa nyingine hawa watoto kwa sababu mnakuwa mnawagombania, na vyuo vikuu vingine havina walimu unakuta mwalimu leo yuko Dar es Salaam kesho yuko Mbeya keshokutwa yuko Iringa keshokutwa Moshi ataconcentrate namna gani kufundisha kwa hiyo matatizo haya mengine yameletelezwa na nyinyi mnnaopendwa kuitwa maVice Chancellors wenye vyuo vilivyopo sijasema wewe (akimaanisha Prof. Rwekaza, VC wa UDSM) kwa hiyo nikuombe Waziri simamia hili, kwanu kuna ubaya gani tukiwa hata na vyuo vikuu vinne tu kila chuo kina watu milioni moja moja watu wako palepale wanalipwa mshahara mzuri na wanaconcentrate vizuri."
Comments
Post a Comment