
MGAHAWA WAKUMBWA NA KASHFA YA KUUZA NYAMA YA BINADAMU

Mkahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu la mkahawa huo.
Na watu wengine waliamini mzaha huo.
Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari cha channel23news.com, mtandao ambao wateja wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja kwa moja katika mtandao wa fecbook.
Shinra Begum ambaye ndio mmiliki wake aliambia Newsbeat kwamba biashara hiyo ya familia imekumbwa na wakati mgumu tangu habari hiyo ilipochapishwa siku ya Alhamisi.
''Wakati watu walipoanza kunipigia simu na kuuliza iwapo tulikuwa tukiuza nyama ya binadamu sikuamini''.
''Nilishtuka nilipoaana habari hiyo katika mtandao na kuendelea kusambazwa katika mtandao wa facebook''.
Sasa watu wametishia kulivunja jengo letu na nimelazimika kuketi chini na mteja ili kumuelezea kwamba yote hayo ni madai ya uwongo.
Shinra anasema kuwa alilazimika kuripoti kwa maafisa wa polisi kwa sababu lilikuwa swala lililomtia wasiwasi mkubwa.
Njia ya pekee ambapo Karri Twist iliweza kukabiliana na chuki hiyo ni kupitia kuchapisha katika mtandao wao ili kuhakikisha kwamba watu wanajua kwamba hilo halikuwa la kweli.
Chanzo: BBC
NDEGE YA MAREKANI YAZUILIWA NA NDEGE ZA CHINA

Ndege
hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya
kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa
bahari ya China.
Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.
China
imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na maji hayo yenye
utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake ,hatua ambayo imesababisha
wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.
''Swala hilo linaangaziwa na China kupitia njia mwafaka ya
kidiplomasia mbali na zile za kijeshi'', msemaji wa jeshi la angani la
Marekani Luteni kanali Lori Hodge amesema.
''Uzuizi huo
haukufanywa kwa njia ya ''utaalamu'' kutokana na hali ya rubani wa ndege
hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili'', aliongezea akisema
uchungzi wa kijeshi unaendelea.
![]() |
Bahari ya Kusini mwa China |
Mnamo mwezi Februari , ndege moja ya Marekani
ilianza kile Washington ilielezea kuwa doria yake ya kawaida kusini mwa
bahari ya China ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.
Ndege
na meli hizo zilielekea katika eneo hilo licha ya onyo kutoka China
dhidi ya kutoa changamoto yoyote kwa uhuru wa China katika eneo hilo.
Kwa nini bahari hiyo ya kusini mwa China inazozaniwa?
Mnamo
mwezi Mei 2016 ndege mbili za kijeshi za China zilizuia ndege nyengine
ya Marekani iliokuwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China.
Wakati huo, jeshi la Marekani lilisema kuwa ilikuwa ikipiga doria ya kawaida katika eneo hilo.
Chanzo: BBC
MABOMU YASABABISHA WATU ZAIDI YA ELFU 50 KUHAMA UJERUMANI

Operesheni kubwa ya kuwaondoa wakaazi wengi wa mji wa Hanover ulioko kaskazini mwa Ujerumani, inaendelea, ya kuwahamisha zaidi ya watu elfu 50 baada ya mabomu makubwa ya wakati wa vita vya dunia, kupatikana kama hayajalipuka.
Wakaazi hao wanatarajiwa kuondoka majumbani mwao baadaye leo, ili kuwapa nafasi wataalamu wa kutegua mabomu, kuhamishia mahala salama mabomu hayo ambayo yanakisiwa kuwa matano.
Operesheni hiyo itachukua siku nzima, na hata zaidi ikiwa mabomu mengineyatapatikana.
Washambuliaji walivamia mji wa Hanover mara 125 kwa mabomu, wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Zaidi ya asilimia 20 ya mabomu yaliyoangushwa mjini humo hayakulipuka.
Baadhi ya mabomu mengine yalikuwa na vifaa vinavyochukua muda mrefu kulipuka, na ambayo kwa sasa yameanza kuoza, na kusababisha hatari kubwa.
Chanzo: BBC
WAPIGANAJI WA HAMAS WAPATA KIONGOZI MPYA
![]() |
Ismael Haniyeh ndio kiongozi mpya wa kundi la Hamas |
Wapiganaji wa Palestina Hamas wamepata kiongozi mpya.
Kiongozi huyo ni Ismail Haniyeh ambaye hadi hivi karibuni alikuwa ndio kiongozi wa kundi hilo katika ukanda wa Gaza.
Akijulikana kama kiongozi anayetumia akili nyingi wakati wa kutatua maswala, anachukua mahala pake Khaled Meshaal ambaye ameliongoza kundi hilo akiwa ughaibuni kwa miongo miwili.
Uchaguzi wa kiongozi mpya ulifanyika kupitia njia ya Video Link kati ya wajumbe waliopo katika ukanda wa Gaza na wale waliopo nchini Qatar ambako Meshaal ana makao yake.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa bwana Meshaal anaachia ngazi wakati ambapo Hamas limeanza kulegeza msimamo wa kisiasa.
Kwa mara ya kwanza wiki iliopita katika sera mpya kundi hilo liliwachilia wito wake wa kuiharibu Israel.
Hamas bado lina wapiganaji wake katika eneo la Gaza na bado linaaminika kuwa kundi la kigaidi na Israel Marekani na mataifa ya bara Ulaya.
Chanzo: BBC
MANCHESTER CITY YAIBURUZA VIBAYA CRYSTAL PALACE
Klabu ya Manchester City imerudi katika nafasi yake ya tatu katika ligi ya Uingereza baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya Crystal Palace ambayo imeshindwa kwa mara ya tatu mfululizo.
City ilihitaji dakika mbili pekee kupata bao la kwanza baada ya David Silva kufunga baada ya kurudi kutoka kuuguza jereha.
Wenyeji waliongeza bao la pili dakika tatu katika kipindi cha pili wakati Vincent Kompany alipopiga mkwaju ulioingia katika kona ya ya juu ya goli na baadaye Kevin De Bruyne akafunga bao la tatu.
Ndoto ya Palace ilithibitishwa baada ya Raheem Sterling kufunga bao la nne kabla ya beki Otamendi kufunga bao la tano katika dakika za lala salama.
Kikosi hicho cha Sam Allardyce kiko pointi tano juu ya eneo la kushushwa daraja na kinaweza kuwa hatarini iwapo klabu za Hull City na Swansea zitaibuka washindi siku ya Jumamosi.
RAIS MAGUFULI AMETUMA SALAMU ZA POLE KWA WAFIWA WA AJALI ARUSHA
Hii hapa chini ni taarifa kama ilivyoandikwa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko mkubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha vilivyotokea leo saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.
Kufuatia ajali hiyo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na taifa kwa ujumla.
"Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo naomba unifikishie pole nyingi kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, walimu na dereva waliopoteza maisha, hiki ni kipindi kigumu kwetu sote, na uwaambie naungana nao katika majonzi na maombi.
"Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu" Amesema Rais Magufuli.
KANYE WEST AMEFUTA AKAUNTI ZAKE KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Msanii wa muziki wa Rap nchini Marekani Kanye West amefuta akaunti zake za Twitter na zile za Instagram ambazo zilikuwa na makumi ya mamilioni ya wafuasi.
Sababu hazijulikani lakini mwezi Novemba mwaka jana alimaliza ziara yake mapema.
Alimshtumu mwanamuziki mwenza Jay Z kwa kujaribu kumuua na kuondoka katika jukwaa baada ya kutangaza kwamba atampigia kura rais wa Marekani Donald Trump wakati wa uchaguzi wa taifa hilo.
Mkewe nyota wa Raality TV Kim Kardashian amesalia katika mtandao wa Twitter na ana wafuasi milioni 51.

Amekuwa akijikuza pamoja na kampuni ya kuuza nguo ya mumewe.
Muda mfupi baada ya akaunti zake za mitandao kufungwa mkewe alichapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amechora nembo ya kampuni hiyo katika mkono wake.
Mashabiki walimsihi Kardashian amwambie mumewe arudi katika mtandao.

West alikuwa ameanza kuishi maisha ya ukimya katika mitandao ya kijamii mapema mwaka huu na alidaiwa kufuta ujumbe wake uliokuwa ukimuunga mkono rais Donald Trump.
Hatua yake pia ilijiri baada ya mkewe kuibiwa vito vyenye thamani ya dola milioni 10.5 mjini Paris mwezi Oktoba.
MFAHAMU KARL MARX KWA UFUPI: DUNIA INAMKUMBUKA LEO
Karl Mark alikuwa ni mwanafalsafa na mwanamapinduzi wa Ujerumani aliyeandika vitabu vya The Communist Manifesto na Das Capital vitabu ambavyo vilikuwa vikipingana na mfumo wa kibepari na kuunda mfumo wa Ukomunisti ama Ujamaa kama alivyoutafsiri hayati Mwalimu JK Nyerere.
Karl Marx alizaliwa Mei 5, 1818. Alianza kuchunguza nadharia za kijamii alipokuwa Chuo Kikuu na wenzie waliounda kikundi chao kilichoitwa Young Hegelians. Hiki kilikuwa ni kikundi kilichokuwa kinaamini katika falsafa za mwalimu wao aliyeitwa Hegel. Marx alikuwa mwandishi wa habari na machapisho yake kuhusu Ukomunisti vilipelekea yeye kufukuzwa Ujerumani na Ufaransa. Mwaka 1848 alichapisha kitabu chake cha The Communist Manifesto akiwa na Friedrich Engels ambacho kilipelekea kufukuzwa Ujerumani na kukimbilia London, Uingereza, huko pia aliandika kitabu cha Das Kapital ambako ndiko alikoishi mpaka alipoiaga dunia.
Karl Marx alikuwa ni miongoni mwa watoto 9 wa Heinrich Marx na Henrietta Marx huko Trier Prussia ya zamani (kwa sasa Ujerumani) Baba yake alikuwa mwanasheria aliyefanikiwa sana na alikuwa mwanaharakati aliyependa mabadiliko nchini Prussia. Japokuwa wazazi wake walikuwa na asili ya Kiyahudi, baba yake Marx alihamia katika Ukristu mwaka 1816 alipokuwa na umri wa miaka 3.
Marx alikuwa ni mwanafunzi wa kawaida. Alisomea nyumbani hadi alipokuwa na umri wa miaka 12 na kisha alipelekwa Jesuit High School alikosoma kwa muda wa miaka 5 kuanzia 1830 hadi 1835.
Mwaka 1835 Marx alijiunga na Chuo Kikuu cha Bonn. Chuo hiki kilikuwa na Itikadi za kuipinga serikali. Marx alijiunga na maisha ya uanafunzi katika chuo hiki. Katika semista mbili chuoni hapo, alifungwa kwa ulevi na kuvuruga amani chuoni hapo, kuwa na madeni lakini pia kushiriki katika falsafa zilizokinzana na chuo. Mwisho wa mwaka baba yake Marx alimsisitiza kuwa serious na masomo katika Chuo Kikuu cha Berlin.
Katika Chuo Kikuu Berlin alisomea fani ya sheria na falsafa ambako alikutana na falsafa za mwalimu wake George Hegel ambaye alikuwa profesa katika chuo hicho mpaka alipofariki mwaka 1895. Baadaye Marx alijiunga na kikundi cha Young Hegelians ambacho pia kulikuwa na Bruno Bauer na Ludwig Feuerbach ambao walikosoa kuanzishwa kwa siku za kisiasa na kidini nchini humo. Kuna mengi yalijiri Marx alipokuwa Berlin.
![]() |
Bruno Bauer |
Marx hakutulia wala kuishia hapo. Mwaka 1841 alitunukiwa Shahada yake ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Jena lakini harakati zake za kisiasa zilipelekea yeye kutokuaminiwa na kuwa mwalimu katika chuo chochote nchini Ujerumani. Alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari na mwaka 1842 alikuwa Mhariri wa Rheinische Zeitung ambalo lilikuwa ni gazeti la wanaharakati wa usawa huko Cologne, Ujerumani. Mwaka mmoja baadaye serikali ililifuta gazeti hilo kuanzia April 1, 1843. Marx aliacha kazi hapo Machi 18. Miezi mitatu baadaye alimuoa Jenny von Westephalen na Oktoba walihamia Paris, Ufaransa.
![]() |
Marx akiwa na mkewe Jenny von Westephalen |
Mji wa Paris ulikuwa ni kitovu cha harakati za kisiasa barani Ulaya mwaka 1843. Huko Marx akiwa na Arnold Ruge, walianzisha gazeti la uchambuzi wa kisiasa lilioitwa Deutsch-Franzosische Jahrbucher (German-French Annals) jambo moja tu ndilo lilikuwa likichapishwa katika gazeti hili kabla Marx na Ruge hawajatofautiana kiitikadi hadi kupelekea gazeti hilo kupotea kwenye ramani lakini Agosti 1844, gazeti hilo liliwaleta pamoja Marx na Friedrich Engels kama mwandishi mshiriki ambaye alikuwa msaidizi wake na rafiki yake hadi kifo. Pamoja, wawili hao walianza kuandika makala za kukosoa mawazo ya Bruno Bauer ambaye alikuwa ni mshiriki katika kikundi cha Young Hegelians. Mwaka 1845 Marx na Engels walichapisha makala yao iliyojulikana kama The Holy Family.
Baadaye katika mwaka huo, Marx alihamia Ubeligiji baada ya kufukuzwa nchini Ufaransa ambako aliandika katika gazeti la Vorwarts! ambalo lilikuwa na itikadi ambazo baadaye zingepelekea kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kikomunisti. Alipokuwa Ubeligiji, Marx alipokelewa na Moses Hess, na baadaye aliachana kabisa na siasa za Young Hegelians. Alipokuwa nchini humo aliandika The German Ideology ambako ndiko alipoandika nadharia yake inayojulikana kama Historical Materialism. Marx hakupata mtu wa kuruhusu kuchapisha makala yake. The German Ideology na Theses on Feuerbach hayakuchapisha makala hiyo hadi alipofariki. Nadharia hii inawataka watu kushiriki kwa vitendo kupinga uonevu.
Karl Marx & Friedrich Engels |
Mwanzoni mwa mwaka 1846, Mark alianzisha Communist Correspondence Committee katika juhudi zake za kuunganisha ukomunisti barani Ulaya. Waingereza walivutiwa na sera zake na kuitisha mkutano na kuunda shirikisho lao Communist League na mwaka 1847 katika mkutano wao mkuu uliofanyika London, shirikisho hilo liliwaomba Marx na Engels kuandika Manifest der Kommunistischen Partei (Manifesto of the Communist Party)
The Communist Manifesto ni miongoni mwa kazi maarufu za Marx ambayo ilichapishwa mwaka 1848 na baadaye mwaka 1849 Marx alifukuzwa nchini Ubeligiji. Alikwenda Ufaransa ambako alianzisha vuguvugu la Mapinduzi nchini humo ambako pia alifukuzwa. Prussia ilikataa kumpokea Marx na hivyo alihamia London japokuwa Uingerza ilikataa kumpa uraia nchini humo hadi kifo chake.
Marx alipokuwa London alisaidia kuundwa kwa shirikisho la wanataaluma wa Ujerumani German Workers' Educational Society lakini pia Shirikisho la Kikomunisti The Communist League. Aliendelea kufanya kazi kama mwandishi japokuwa safari hii alizuiwa na baadhi ya itikadi zake. Alifanya kazi katika The New York Daily Tribune kwa miaka 10 kuanzia 1852-1862 lakini hakulipwa , aliishi kwa kusaidiwa na rafiki yake Engels.
Marx aliutazama mfumo wa kibepari zaidi na mwaka 1867 alichapisha toleo la kwanza la kitabu chake Das Kapital. Baadaye alitumia muda wake kupitia chapisho hilo na akawa akilifanyia masahihisho na kuongeza baadhi ya vitu. Matoleo mawili yaliyofuata baadaye ambayo hata hakuyakamilisha yaliunganishwa na kuchapishwa na Engels.
Marx alifariki kwa ugonjwa wa mapafu unaojulikana kitaalamu kama pleurisy alipokuwa London Machi 14, 1883. Katika kaburi lake kuna maandishi ya kitabu chake The Communist Manifesto yenye maana wafanyakazi wote waungane.
MAKALA HII IMEANDALIWA KWA MSAADA WA MTANDAO INAWEZA KUFANYIWA MAREKEBISHO MUDA WOWOTE PANAPOHITAJIKA.
MECHI YA ATLETICO & REAL MADRID KULINDWA NA POLISI 2,000
![]() |
Polisi wa kukabiliana na fujo walikabiliana na mashabiki wa Bayern Munich mnamo 18 Aprili |
Walinzi zaidi ya 2,000 watatumiwa
kudumisha usalama na kudhibiti mashabiki wakati wa mechi ya nusufainali
ya mkondo wa kwanza kati ya Real Madrid na Atletico Madrid katika Ligi
ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mechi hiyo itakayochezewa Santiago Bernabeu
siku ya Jumanne imeorodheshwa kama yenye "hatari kubwa" na usalama
"utaimarishwa", maafisa wasimamizi wa jiji la Madrid walisema Ijumaa.
UEFA wameamrisha usalama katika mechi za klabu Ulaya uimarishwe baada ya
shambulio kwenye basi la timu ya Borussia Dortmund mnamo 11 Aprili.
Atletico watakuwa na mashabiki 4,000 katika uwanja huo wa Real unaotoshea mashabiki 80,000.
Kawaida ni mashabiki wachache sana husafiri kuhudhuria mechi za ugenini Uhispania.
Idadi
ya walinzi tarehe 2 Mei itakuwa ya juu zaidi ya waliokuwepo wakati wa
mechi iliyopita ya Real Ulaya dhidi ya Bayern Munich polisi wa
kukabiliana na fujo walipokabiliana na mashabiki wageni wakati wa
mapumziko.
Kulikuwa pia na fujo mechi ya robofainali ya Atletico nyumbani, polisi wakikabiliana na mashabiki wa Leicester City.
Chanzo: BBC
WAFAHAMU MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOFARIKI WAKIWA MADARAKANI
Leo nimekuandikia orodha ya marais 10 waliofariki wakiwa madarakani. Tuanze kuhesabu sasa:
10. Lansana Conte, Rais wa Guinea
Baada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana
akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi
ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni
rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya
aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi.
9. Omar Bongo, Rais wa Gabon
Saratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha Rais Omar
Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka
42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni
kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa
akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa
huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini.
8. Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-Bissau
Joao Bernardo Vieira rais wa Guinea-Bissau aliuwawa nchi mwake Machi
2009, akiwa na umri wa miaka 69. Alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa
miaka 31. 1978 alikuwa waziri mkuu na kuchukua madaraka 1980
na alitawala kwa miaka 19. Alibadilika na kuwa kiongozi wa umma na
aliongoza miaka minne mingine zaidi. 2005 alishinda tena uchaguzi wa
uraisi.
7. Umaru Musa Yar’Adua, Rais wa Nigeria
Umaru Musa Yar’Adua, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 mwaka 2011
akisumbuliwa na matatizo ya moyo
nchini Nigeria. Alikuwa madarakani kwa miaka mitatu pekee. Alikosekana
katika kampeni za uchaguzi kwa sababu za kiafya. Baada ya kuchaguliwa
kwake 2007, afya yake ilidhoofika kwa haraka.
6. Muammar Gadhafi, kiongozi na mwana mapinduzi wa Libya
Mwathirika wa mauaji, Muammar Gadhafi aliuawa akiwa na umri wa miaka
69 na vikosi vya waasi katika mazingira yasiyoeleweka nchini Libya,
baada ya kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Aliuondoa
uongozi wa kifalme bila ya kumwaga damu wakati wa mapinduzi ya kijeshi
ya mwaka 1969 lakini utawala wake ulifikia kikomo baada ya matokeo ya
vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni.
5. Malam Bacai Sanha, Rais wa Guinea-Bissau
Kiongozi wa nne kufariki mwaka 2012 alikuwa ni Malam Bacai Sanha rais
wa Guinea-Bissau. Aliugua ugonjwa wa kisukari na alifariki mjini Paris
baada ya miaka minne kama rais akiwa na umri wa miaka 64. Katika kipindi
chote cha utawala wake alisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya
yalosababisha kwenda hospitali mara nyingi.
4. Bingu wa Mutharika, Rais wa Malawi
Rais mwingine aliyefariki mwaka 2012 ni Bingu wa Mutharika, rais wa
Malawi. Alipata mshutuko wa moyo mwezi Aprili na kufariki siku mbili
baadae akiwa na umri wa miaka 78. Uongozi wake ulikuwa ni wa miaka nane
na alipata mafanikio makubwa katika sera zake za kilimo na chakula. Sifa
yake iliharibika kufuatia maandamano makubwa yalopinga ununuzi wa ndege
ya rais iliyogharimu Dola milioni 14
3. John Atta Mills, Rais wa Ghana
Pia mwaka 2012, John Atta Mills, rais wa Ghana alifariki akiwa
nyumbani kwake kwa mshutuko wa moyo na saratani ya koo akiwa na umri wa
miaka 68. Alishinda uchaguzi wa rais wa 2008 alishika madaraka kwa miaka
mitatu pekee. Alianzisha mikakati mingi ya kiuchumi na mageuzi ya
kiuchumi yalomletea sifa kutoka ndani na nje ya nchi.
2. Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia
Meles Zenawi alifariki Agosti 2012 nchini Ubelgiji akiwa na umri wa
miaka 57 kwa maambukizi yasiyojulikana. Ameiongoza Ethiopia kwa miaka 5
kama rais kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 na kama Waziri Mkuu kwa miaka 17
kuanzia 1995 hadi 2012. Anajulikana kwa kuanzisha mfumo wa siasa wa
vyama vingi, lakini pia kwa ukandamizaji wa maandamano halali ya watu wa
Oromia wa kaskazini mwa Ethiopia.
1. Michael Sata, Rais wa Zambia
Michael Sata ni kiongozi wa hivi karibuni aliyefariki madarakani
akiwa na umri wa miaka 77 kwa maradhi ambayo hayakuwekwa wazi Oktoba 28
2014, nchini Uingereza. Baada ya uchaguzi wa 2011, uvumi juu ya afya
yake ulisambaa nchini Zambia. Kukosekana kwake katika shughuli kubwa za
kitaifa kuliibua wasiwasi wa afya yake ingawa msemaji wake alisema
alikuwa katika afya nzuri.
Chanzo: DW Idhaa ya Kiswahili.
THE WHEEL A POEM BY VENANCE GILBERT
![]() |
Venance on the sitting benches of Vikenge Hostels, Mzumbe University Main Campus Morogoro |
Poet: Venance Gilbert
Poem: The Wheel
Composition: October 18, 2016
Publication: April 20, 2017
Copyright: Venance Gilbert 2016
Copyright: Venance Gilbert 2016
The wheel was moving
But I never noticed
second counted, minutes gone,
hours died, days were numbered
weeks moved, months and years passed
I noticed it as the matter of living.
Mental pictures remind me
those days when the moments existed
Sometimes I wish to restore and start
I find the wheel moving fast following the line
Like the train on its pathway
Happy birthday takes back to those moments.
Today I am youth
Full capable to place the mind on motion
I often regret when I remember the moment
The moment when I was the driver of the wheel
But now the wheel drives, how possible?
I never drove it well and careful at the moment,
Drive the wheel careful before it drive you on its pathway.