WALIOCHAGULIWA BUGANDO (CUHAS) MAJINA HAYA HAPA

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Kikatoliki (Bugando) (CUHAS) kimetoa majina ya wanafunzi mbalimbali waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho.

BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA

Aidha unaweza kutuma jina lako na index ya form four au six bila kusahau kozi uliyoomba chuoni hapo kwenda namba 0753400208 na utaangaliziwa jina bure kabisa.

WALIOCHAGULIWA UDSM, DUCE NA MKWAWA BATCH 1 MAJINA HAYA HAPA



Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na matawi yake DUCE na MKWAWA (MUCE) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kozi mbalimbali za shahada chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.



Unaweza kutuma jina lako, pamoja na namba ya kidato ya cha 4 au 6 kwenda namba 0753400208 na utaangaliziwa jina BURE. Kumbuka kutuma jina lako, index ya 4 au 6 na chuo unachotaka kuangalia hata kama ni zaidi ya kimoja. Mfano: Venance Gilbert s2509/0575/2012 (iv) au s0494/0141/2015 (vi) Mzumbe, MUHAS, SUA, UDSM, UDOM, SAUT n.k. kwenda 0753400208. Huduma hii ni BURE.

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA UDOM BACHELOR DEGREE YAPO HAPA


Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Ili kuona matokeo haya kwa njia ya  simu hakikisha simu yako ina WPS Office, Polaris Office n.k. kisha BONYEZA HAPA KUANGALIA MAJINA HAYO

VENANCE BLOG IKO NA WEWE, UKISHINDWA KUANGALIA MAJINA HAYO TUMA UJUMBE MFUPI (SMS) UKIANDIKA JINA LAKO NA INDEX YA KIDATO CHA 4 AU 6 KWENDA NAMBA 0753400208 UTAANGALIZIWA JINA LAKO BURE KABISA KUPEWA MAJIBU.

WALIOCHAGULIWA KOZI ZA SHAHADA CBE KAMPASI YA DAR ES SALAAM

Chuo cha Elimu ya Biashara kimetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa kwanza wa masomo 2016/2017.
Majina yapo hapa. Kumbuka hili ni toleo la kwanza (First Batch). BOFYA HAPA KUANGALIA

WALIOCHAGULIWA KOZI MBALIMBALI ZA SHAHADA IFM

  Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) imetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kusoma kozi mbalimbali za Shahada katika fani mbali mbali chuoni hapo.

Majina hayo yako hapa. BOFYA HAPA KUONA MAJINA HAYO

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA KAMPAS YA MBEYA HAYA HAPA



Chuo Kikuu Tumaini Makumira kampus ya Mbeya kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Chuo hicho kwa kozi za Shahada ya Elimu na Sanaa (Bachelor of Arts with Education BA.Ed) na Shahada ya Elimu katika Sanaa (Bachelor of Education in Arts BED). Majina hayo yapo kwenye tovuti ya Chuo toka juzi Septemba 15.

KUANGALIA BA.Ed BOFYA HAPA

KUANGALIA BEd BOFYA HAPA

Aidha taarifa zote za Chuo hiko unaweza kuzipata kwa KUBOFYA HAPA

VENANCE BLOG IKO NA WEWE KWA TAARIFA ZOTE ZA VYUO MBALIMBALI NCHINI. ENDELEA KUWA NAMI.

HILLARY CLINTON AMEREJEA KATIKA KAMPENI NA KUMSHAMBULIA TRUMP

Mgombea wa chama cha Democratic katika kinyan'ganyiro cha urais nchini Marekani Hillary Clinton amerejea tena katika kampeni na kutoa kauli ya tahadhari dhidi ya mpinzani wake Donald Trump.

Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton akiwahutubia wafuasi wake North Carolina
Mgombea wa chama cha Democrats Hillary Clinton akiwahutubia wafuasi wake North Carolina

Akizungumza katika mikutano miwili tofauti ya kampeni kwenye majimbo mawili, North Carolina na Washington, Hillary Clinton alisema amefurahi kurejea katika kampeni hizo baada ya hapo awali kushauriwa na madaktari kubakia nyumbani hadi atakapopata nafuu kutokana na maradhi ya homa ya mapafu yaliyokuwa yakimkabili.

Hali ya afya ya Hillary Clinton ilidhoofika wakati wa kumbukumbu ya mika 15 tangu yalipofanyika mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani tarehe 11/9/ 2001.

"Ni jambo jema kuwa nimerejea katika kampeni" alisema mgombea huyo wa chama cha Democratic huku akishangiliwa na wafuasi wake alipohutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la Greensboro, North Carolina.

Hillary Clinton alitangaza kuendelea na mikutano ya kampeni katika majimbo ambayo mgombea wa chama cha Republican Donald Trump amekwishafanya mikutano yake ya kampeni ikiwa ni pamoja na jimbo la Florida ambalo kila mgombea anawania kulichukua.

Wakati suala la afya ya wagombea wote wawili likizua mjadala katika mikutano ya kampeni ya viongozi hao , Hillary Clinton alienda mbali zaidi kwa kutoa taarifa zinazohusiana na afya yake akisema ni mwenye afya njema na anaweza vema kutekeleza majukumu ya uongozi. Kwa upande mwingine wakati mgombea wa chama cha Republican Donald Trump akionekana kuwa na uzito mkubwa daktari wake alithibitisha kuwa mgombea huyo ana afya njema.
Hillary Clinton amshambulia Trump
Bildkombo Donald Trump und Hillary Clinton
Akizungumza katika mikutano hiyo ya kampeni Hillary Clinton hakusita kumshambulia kwa maneno Donald Trump kutokana na kauli ya awali aliyoitoa akikataa kusema iwapo ana amini kuwa Rais Barack Obama ni mzaliwa wa Marekani na pia kumkashifu mchungaji mwenye asili ya Afrika ambapo Trump alitembelea kanisa lake mjini Michigan wiki hii.

Kwa miaka kadhaa Donald Trump alikuwa akiendesha harakati akihoji kama Rais Barack Obama amezaliwa nchini Marekani na kutumia majukwaa kutangaza kuwa Rais huyo wa sasa wa Marekani alizaliwa nje ya nchi hiyo na kuwa hakusitahili kuwa Rais wa nchi hiyo kwa mujibu wa katiba ya Marekani.

Hapo jana wakati Trump alipohojiwa na gazeti la Washington Post iwapo ana amini kuwa Rais Obama alizaliwa mjini Hawaii, alishindwa kutoa jibu kwa mara nyingine akisema atajibu swali hilo wakati muafaka utakapowadia. Hata hivyo taarifa iliyotolewa baadaye na waratibu wa mikutano ya kampeni ya mgombea huyo ilisema Trump ana amini kuwa Rais Obama alizaliwa nchini Marekani.

" Baada ya kufanikiwa kupata cheti cha kuzaliwa cha Rais Barack Obama wakati wengine wameshindwa , Donald Trump sasa ana amini kuwa Rais Obama ni mzaliwa wa Marekani " ilisisitiza taarifa hiyo.

Aidha mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton alisema kitendo cha Trump kumshambulia mchungaji kinazidi kumnyima sifa Trump za kuwa Rais wa nchi hiyo na kuwataka wapiga kura kumkataa wakati wa uchaguzi wa mwezi Novemba.


Chanzo: DW

MTU MMOJA AMEJITOA MUHANGA NA KUUA WATU 16 KATIKA MSIKITI WA MOHMAND PAKISTAN

Takribani watu 16 wameuawa na wengine 35 kujeruhiwa katika swala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Mohmand huko Pakistan.

Duru za habari zinasema kuwa mtu huyo aliyejitoa muhanga ameua watu 16 na wengine 35 kujeruhiwa walipokuwa wakihudhuria swala ya Ijumaa kaskazini mashariki mwa  Pakistan.

Shambulio hilo limetokea katika kijiji cha Anbar Tehsil katika wilaya inayokaliwa na kabila la Mohmand ambapo jeshi la Pakistan limekuwa likipambana na kundi la Taliban.

"Swala ya Ijumaa ilikuwa ikiendelea msikitini hapo wakati ambapo mshambuliaji huyo wa kujitoa muhanga alijilipua na kuua waumini 16 na kujeruhi wengine 35" kiongozi mmoja wa Mohmand aliliambia shirika la habari la AFP.

Hakujatokea taarifa zozote kuhusu shambulio hilo, lakini kundi la Taliban linashutumiwa kuhusika na shambulio hilo kwa kuwa limekuwa likifanya mashambulio katika maeneo ya mahakama, shule na misikiti.

Jeshi la Pakistan limekuwa likifanya operesheni toka Juni 2014 kuangamiza makundi yote ya kigaidi yaliweka ngome kaskazini mashariki mwa maeneo hayo ili kuepusha vifo vya watu wasio na hatia toka 2004.


Chanzo: Al Jazeera

LEO SEPTEMBA 14 KATIKA HISTORIA

Rapa Nas Escobar alizaliwa September 13, 1973.
Leo ni Jumatano Septemba 14, 2016. Ni siku ya 258 katika mwaka 2016. Zimesalia siku 108 kuukamilisha mwaka 2016.

MATUKIO

1960 - Iraq, Iran, Kuwait na Saudi Arabia ziliunda jumuiya ya OPEC.

1979 - Nur Muhammad Tarak, Rais na na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Afghanistan aliuawa katika mapinduzi ambapo Waziri Mkuu Hafizullah Amin alishika madaraka.



KUZALIWA

1849 - Mwanasaikolojia wa Urusi, Ivan Pavlov.

1864 - Robert Cecil,  miongoni mwa waanzilishi wa Jumuiya ya Mataifa alizaliwa.

1879 - Margaret Sanger, wakili na muanzilishi wa Uzazi wa mpango.

1973 - Rapa Nas Escobar alizaliwa. 

NEW AUDIO: DOWNLOAD BARAKA DA PRINCE FT ALI KIBA-NISAMEHE MP3

Baraka Da Prince akishirikiana na Ali Kiba wanakusikilizisha kitu hiki hapa kipya, wimbo unaitwa Nisamehe umefanyikwa kwa Imma the Boy.


DOWNLOAD HAPA

TCU IMERUHUSU UDAHILI VYUO VIKUU AWAMU YA PILI

Tume ya Vyuo Vikuu nchini Tanzania (TCU) imeruhusu awamu ya pili ya udahili kwa wanafunzi waliokosa vyuo kwa kukosa sifa katika udahili wa awamu ya kwanza na wale ambao hawakuomba kudahiliwa kabisa.

Aidha TCU inakumbusha kwamba wale waliokwisha omba na hawakupangiwa kwa kukosa sifa stahiki za vyuo walivyopangiwa hawatatakiwa kulipia tena.

Pia wadahiliwa wapya wanatakiwa kulipia kiasi cha fedha za kitanzania Tsh. Elfu Hamsini (50,000/=) kama gharama za udahili. Fedha hii huwa hairudishwi.

Vilevile TCU inakumbusha kwamba kozi ambazo zimejaa tayari hazitaonekana kwenye mfumo wa Udahili (CAS).

Aidha TCU inawakumbusha waombaji kuwa mwisho wa kutuma maombi ya udahili ni Septemba 23 na hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza kwa wale watakaoshindw kuomba vyuo katika muda huo ulioongezwa.


MAELEZO ZAIDI BOFYA HAPA

IGGY AZALEA ASISITIZA YEYE NA FRENCH MONTANA NI MARAFIKI TU

Iggy Azalea amekataa kuwa na uhusiano na French Montana japo wameonekana mara kadhaa wakiwa sehemu za starehe pamoja.
Rapper huyo wa kike ameuambia mtandao wa TMZ kuwa hana mpenzi kwa sasa hivyo yeye na French Montana ni marafiki tu.
“We are Single, I’m single,” amesema Iggy. “just friends.”
Wiki kadhaa zilizopita Iggy alidai kuwa yeye na French Montana kuna wimbo wamefanya ila hawana mahusiano yoyote lakini baada ya wiki moja wawili hao walionekana wakiwa wanakula bata pamoja huko Cabo San Lucas, Mexico. Walionekana pia wakibusiana.

LEO SEPTEMBA 13 KATIKA HISTORIA

Tarehe kama ya leo Septemba 13' Tupac Shakur alifariki.
Leo Septemba 13 siku ya 257 katika mwaka 2016, zimesalia siku 109 kuukamilisha mwaka 2016.


MATUKIO

1759 - Vikosi vya majeshi ya Uingerza viliyashinda majeshi ya Ufaransa katija mapigano kwenye nyanda za Abraham huko Quebec.

1914 - Wanaharakati wa Ireland waliomba msaada kwa wajerumani.

1940 - Italia iliivamia Misri.

1945 - Vikosi vya majeshi ya Uingereza viliingia Japan kupunguza uwezo wa jeshi la Japan.

1993 - Mkataba wa amani kusitisha mapigano Israel na Palestina ulisainiwa.


VIFO

1996 - Mwanamuziki 2Pac Shakur alifariki.


KWA MSAADA WA MTANDAO.

CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER


Leo katika kipengele cha Celebrity wa siku tunaye Paul Walker ambaye kwa sasa ni maremu. Kwa nini Paul Walker leo? Kwa sababu leo ni tarehe ambayo alizaliwa mwaka 1973 huko California. Na tuangalie historia yake ili kumfahamu zaidi.

KUZALIWA

Paul Walker alizaliwa Septemba 12, 1973 huko Glendale, Calfornia nchini Marekani. 

ELIMU

Alipata Elimu yake katika Village Christian School.

KAZI

Paul Walker alikuwa muigizaji nchini Marekani ambapo alianza kazi hiyo katika televisheni mbalimbali kama vile katika vipindi vya The Young and the Restless na Touched by an Angel. Alipata umaarufu katika movie za vijana kama vile She's All That na Varsity Blues. Walker alipata umaarufu zaidi katika movie za Brian O'Conner ambapo zinahusisha uendeshaji wa magari mitaani 'The Fast and the Furious'. Alishiriki pia katika filamu kama vile Eight Below, Timeline, Into the Blue, Joy Ride na Running Scared.

Mbali na uigizaji, Walker pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha The Coty Prestige fragrance brand, Davidoff Cool Water for Men na alishiriki katika Chanel zinazoonesha Matukio ya kijiografia chini Marekani katika mfululizo wa vipindi vya Expedition Great White.

Pia alianzisha kikundi cha kusaidia jamii haswa wale wanaokumbwa na majanga ya asili kilichoitwa Reach Out WorldWide (ROWW).

Mpaka mauti yanamfika, Walker alikuwa anaigiza movie 3 ambazo ni Hours (2013), Brick Mansions (2014) na Furious 7 (2015). Wiz Khalifa alimuimbia wimbo wa heshima 'See You Again' ambao ulitumika kama soundtrack ya Furious 7. Wimbo huo ulitajwa kushiriki tuzo za Golden Globe Awards katika kipengele cha Wimbo Bora katika Tuzo ya 73 ya Golden Globe Wards.

MIAKA YA UMAARUFU

Paul Walker alikuwa maarufu kati ya mwaka 1984 hadi mwaka 2013 alipofikwa na mauti.

UTAJIRI ALIOKUWA NAO

Mpaka anafariki alikadiriwa kuwa na utajiri uliofikia dola za kimarekani bilioni 25 kwa makadirio ya mwaka 2014.


MAISHA YAKE

Walker alizaliwa Glendale California na alikuwa ni mtoto wa Cherly ambaye alikuwa mwanamitindo na baba yake Paul William Walker III alikuwa ni mkandarasi na mwanamasumbwi aliyeshinda ubingwa wa Golden Gloves mara mbili.

Paul Walker baada ya kumaliza elimu ya pili (kwa Tanzania kidato cha 5 & 6) alijiunga na vyuo mbali mbali Kusini mwa California akisomea baiolojia ya viumbe wa majini.


DINI

Walker alikuwa ni muumini wa Dini ya Kikristu. Kanisa lake linaitwa Nondenominational Christianity ambalo mwanzo lilijulikana kama The Church of  Jesus Christ of Latter-day Saints.

FAMILIA

Aliacha mtoto mmoja aitwaye Meadow Walker. Pia alikuwa na Ndugu wawili wa kiume; Cody Walker na Caleb Walker.

KIFO

Paul Walker alifariki Novemba 30, 2013 katika ajali mbaya ya gari ambayo alikuwepo yeye na rafiki yake Roger Rodas miaka 38. Siku hiyo Walker akiwa na Roger walikuwa wakielekea katika taasisi yake ya kusaidia watu ROWW ambapo iliwalenga waanga wa kimbunga Typhoon Haiyan (Yolanda). Siku hiyo Roger ndiye aliyekuwa dereva huku Paul akiwa kama abiria. Inadaiwa kuwa Roger aliendesha gari kwa umbali wa maili 45 kwa saa sawa na kilomita 72 kwa saa na baadae gari yao Porsche Carrera GT ilipiga mzinga maeneo ya Kelly Johnson Parkway huko Valencia Santa Clarita California na badae gari yao iliungua. Ajali ilionekana kwenye camera ya ulinzi iliyokuwa maeneo hayo.
Hapa ndipo majivu ya mwili wa Paul Walker yalipozikwa.


Mwaka 2014 uchunguzi zaidi ulionesha kuwa chanzo cha ajali kilikuwa ni mwendokasi ambapo alidaiwa kuwa gari ilikimbizwa katika mwendokasi wa kilomita 103 kwa saa.

Majivu ya mwili wa Paul Walker yalizikwa huko Forest Lawn Memorial Park, Hollywood Hills nchini Marekani.







Hapa akiwa na wenzie wa Fast and Furious.




MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PAUL WALKER MAHALA PEMA PEPONI.

AMINA!. 

UCHAMBUZI KWA MSAADA WA WIKIPEDIA PICHA KWA HISANI YA MTANDAO.

LEO SEPTEMBA 12 KATIKA HISTORIA

Tarehe kama ya leo Septemba 12, 1973 muigizaji wa Marekani, Paul Walker alizaliwa huko Glendale, Califonia.Alifariki Novemba 30, 2013.
Leo ni tarehe 12 Septemba, siku ya 256 katika mwaka 2016, zimesalia siku 110 kuukamilisha mwaka 2016.

MATUKIO

Leo kuna matukio mengi sana hata hivyo tuyaangalie kama ifuatavyo:

1217 - Mfalme wa Ufaransa Prince Louis na Mfalme wa Uingerza Henry III walisaini mkataba wa amani.

1624 - Meli ya kwanza kupita chini ya maji ilijaribiwa katika Mto Thames kwa ajili ya kutumiwa na Mfalme James I huko Uingereza.

1662 - John Flamsteed aliona nusu ya kupatwa kwa jua na ikampelekea kuvutiwa na elimu ya anga (unajimu)

1703 - Jeshi la Uingereza chini ya Archiduke Charles wa Austria waliwasili nchini Ureno.

1722 - Vikosi vya Urusi viliteka Baku na Derbent huko Persia ambayo kwa sasa ni Iran.

1751 - Amsterdam ilikataa kuanzisha makazi ya Wayahudi.

1753 - Mnajimu wa Ufaransa Charles Messier bila kutarajia aligundua gesi ya miamba (crab nebula) na akaanza utafiti wake (Messier Catalogue)

1848 - Uswisi iliunganisha mataifa yake kupata taifa moja la Uswisi.

1878 - Mfalme Leopold II wa Ubelgiji alifungua Mkutano wa Kongo.

1885 - Rekodi ya kwanza ya magoli 35 katika mechi ya ligi daraja la kwanza iliwekwa.

1890 - Cecil Rhodes alifika Harare, Zimbabwe kwa wakati ule ikiitwa Fort Salisbury.

1909 - Waarabu walivamia Gedara Palestina.

1919 - Adolf Hitler aliungana na Chama cha Wafanyakazi wa Ujerumani akiwa mwanachama wa saba lakini hakukubaliana na lengo la chama hicho badala yake alisisitiza Utaifa (Harakati za nchi binafsi) na kusisitiza chuki dhidi ya Wayahudi.

1922 - Mwanariadha Paavo Nurmi aliweka rekodi ya dunia kwa kukimbia umbali wa mita 5000 sawa na kilomita 5 kwa daika 14:35.4

1928 - Kimbunga Hurricane kiliua watu 6,000.

1934 - Estonia, Lativia & walisaini mkataba wa Baltic Entente dhidi ya Muungano wa nchi za Kisovieti.

1941 - Meli ya kwanza ya kijerumani katika vita ya pili ya Dunia ilitekwa na meli za Marekani.

1943 - Taifa la Skorzeny lilimuachia Benito Nussolini huko Gran Sasso.

1944 - Vikosi vya Marekani viliingia nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza.

1950 - Serikali ya Ubelgiji iliwafukuza wafanyakazi wote wa kikomunisti.

1956 - Wanafunzi weusi waliruhusiwa kusoma shule ya Ckay Ky huko Marekani.

1958 - Marekani ilifanya jaribio lake la Nyuklia katika uwanja wa majaribio wa Nevada.

1958 - Muhandisi Jack Kilby alifanya jaribio la sakiti ya kompyuta aliyogundua kwa msimamizi wake.

1959 - Muungano wa nchi za kisovieti (USSR) ulituma chombo Luna 2 kwenda kwenye mwezi.

1961 - Urusi ilifanya jaribio lake la nyuklia huko Novaya Zemlya.

1971 - Urusi ilituma chombo chake kwenye mwezi Luna 16.

1973 - Urusi ilifanya tena jaribio la Nyuklia huko Novaya Zemlya.

1974 - Mfalme Haile Sellasie alipinduliwa nchini Ethiopia.

1978 - Fidel Castro alitembelea Addis Ababa Ethiopia.

1979 - Indonesia ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambalo lilikuwa na ukubwa wa 8.1 katika kipimo cha Richter.

1984 - Ethiopia iliunda Jamhuri ya Kisoshalisti.

1987 - Ethiopia ilianza kufuata utawala wa Katiba.

1992 - Mae Jemison alikuwa mwanamke wa kwanza Mmarwkani mweusi kwenda angani.

1999 - Indonesia ilisema itaruhusu walinzi wa amani Mashariki mwa Timor.

2005 - Israel iliondosha majeshi na vikosi vyake kutoka ukanda wa Gaza.

2007 - Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alitangaza nia yake ya kujiuzulu wadhifa huo.

2007 - Rais wa zamani wa Ufilipino Joseph Estrada kwa kosa na wizi wa fedha za serikali.

2010 - Lady Gaga na Eminem walichukua tuzo za MTV Video Music.

2012 - Kampuni ya Apple ilitangaza na kuonesha simu zao iPhone 5 na iOS 6.

2015 - Watalii 12 waliuawa bila kukusudia na Jeshi la Misri Magahribi mwa Jangwa la Misri wakidhaniwa kuwa ni waasi.




KUZALIWA

1575 -  Mtafiti wa Uingereza Henry Hudson.

1913 - Mwanaridha Jesse Owen.

1973 - Muigizaji Paul Walker.

1977 - Muigizaji Connor Frante.

1978 - Muigizaji Benjamin McKenzie.

1981 - Muigizaji na Mwanamuziki Jennifer Hudson.



IMEANDALIWA KWA MSAADA WA MTANDAO.