Venance Blog:
Jaji mkuu wa mahakama ya juu zaidi ya kikatiba ameapishwa nchini Misri kuwa rais wa muda baada ya jeshi kumng'oa mamlakani rais aliyechaguliwa naraia kwa njia ya kidemokrasia na kushinda kwa wingi wa kura, Mohammed Morsi.
Viongozi duniani wamepokea kwa tahadhari matukio yanayojiri huko Misri. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amewaambia waandishi kwambaanaangalia kwa umakini hatua iliyochukuliwa na jeshi la Misri.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza , William Hague, amesema Uingereza haiungi mkono uvamizi huo wa kijeshi lakini haina budi kuitambua hatua hiyo na kusogea mbele. Hata hivyo alikataa kulishutumu jeshi kwa kumpindua Morsi akisema ni uvamizi ulioungwa mkono na watu wengi.
Mfalme Abdalla wa Saudia ametuma ujumbe wa hongera kwa kaimu rais wa Misri akisema kwamba uteuzi wake unajiri katika wakati muhimu.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.
Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjiniCairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.
Jana nilikuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea Kusini, leo tuangalie upande wa pili kwa akina dada ambao ni warembo zaidi. #10. Han Ye Seul Han Ye Seul alizaliwa chini Marekani japokuwa ana asili ya Korea. Anaigiza series na filamu za kawaida. Alionekana katika Nonstop 4 na pia ameigiza katika muvi kama vile Couple or Truble, Birth of a Beauty, Miss Gold Digger na Penny Pincher. Baada ya kupata umaarufu nchini Korea aliamua kufuta uraia wake wa Marekani na kuamua kuwa raia wa Korea Kusini. #9. Song Hye Kyo Song Hye Kyo alipata umaarufu katika tasnia ya muvi nchini Korea katika muvi kama vile Autumn in My Heart, All In, Full House, The World They Live In na nyinginezo. Ni mwenye furaha na amekuwa akiigiza muvi zake vizuri sana. #8. Lee Da Hae Lee Da Hae ni muigizaji maarufu nchini Korea Kusini. Ameigiza katika My Girl, Green Rose, The Slave Hunter, Miss Ripley na Hotel King. Ameigiza pia katika muvi za Kichina kama vile Actually Lob...
Pole kwa Rais Morsi
ReplyDelete