RAIS PUTIN AMEAGIZA WANADIPLOMASIA 755 WA MAREKANI KUONDOKA URUSI

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu.

Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo.

Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo.

Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.

Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.

Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kupata ushindi.
Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.


Chanzo: BBC

MMILIKI WA NGURDOTO HOTEL AFARIKI DUNIA


Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwananchi ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha.

Akihojiwa na gazeti la Mwananchi Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo.

Laswai, amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo.

Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.



Chanzo: Mwananchi

PICHA 20 KUTOKA KWA DIAMOND NA ZARI WAKIWA KENYA WALIZOPOST INSTAGRAM

Diamond na Zari wameendelea na starehe zao huko Mombasa Kenya huku team ya WCB ikitia mguu pia mahali hapo; Harmonize na Sallam walihusika pia. Hizi ni baadhi ya picha kutoka katika mapumziko hayo.

Hapa Zari aliamua kumtania shemeji yake Harmonize.

mkubwa Simba na Zari katika starehe zao



Harmonize alipata nafasi ya kusema chochote BClub



Katika picha hii Diamond kaandika caption ya kiingereza ambayo Kiwashili chake ni "namwambia Harmonize kwamba wenye chuki wote hawana maana. Tuna uwezo na ni matarijiri"

Unamuona Zari anavyozidi kupendeza kama ndo kwanza ana miaka 12

Kila mtu apambane na mahusiano yake tu.



Huu mkao sasa Zari alivyomtegea Mond afu anajifanya kama hana habari yuko busy na simu


Sallam alihusika pia B Club

Wanapendeza hawa wapendanao



unamuona Zari?



KWA PICHA, MATUKIO, HABARI NA MAELEZO KAMA HAYA NA MENGINE MENGI USISITE KUTEMBELEA VENANCE BLOG:
Facebook: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: @venanceblog
email: venancegilbert@gmail.com

DIAMOND AWAJIA JUU WANAOMSEMA ZARI KUHUSU MSIBA WA MAMA YAKE

Mwanamuziki wa Tanzania aliyeikamata Afrika na Dunia kwa uimbaji wake wa lugha ya Kiswahili, Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote, Baba Tee, Simba na majina mengineyo usiku wa leo amewajia juu hasa wadada wanaomsema mpenzi wake Zarina Hassan kufuatia kifo cha mama yake kilichotokea majuzi tu. Zari ameonekana na Diamond wakiwa katika starehe za mahusiano yao kitu kilichopelekea wadau na mashabiki wao kuliongelea suala hilo.

Kwa tamaduni za kiafrika na jinsi tulivyozoea, mtu anapofiwa hasa na Mama yake mzazi humchukua muda sana kabla ya kurudi katika utaratibu wa kawaida, hii imekuwa tofauti kwa Zari ambaye siku chache tu baada ya msiba ameonekana na Diamond wakiponda raha huku wakijirekodi video na kuzituma katika mtandao wa Instagram hali iliyopelekea mashabiki kuliongelea sana suala hilo.

Diamond Platnumz amefunguka baada ya kuonekana kukerwa na maneno ya watu katika mtandao wa Instgram na kuyaandika haya:
"Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa misiba ya watu.... Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehemu tulivu apetiwepetiwe apate faraja!...sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia... Pambaneni na mahusiano yenu...! Nina siku 5 za kumpetipeti...! leo ndio kwanza Ya kwanza 😛"

Hii ni screenshoot ya ujumbe huo aliotuma Diamond Platnumz kwenye mtandao wa Instagram huku akiwa ametag eneo Mombasa, Kenya.


WASILIANA NA VENANCE BLOG:
Facebook page: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: @venanceblog
email: venancegilbert@gmail.com

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU

Picha kwa hisani ya Debt.org

1.0 UTANGULIZI

Nilipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu nilisikia manung'uniko miongoni mwa wanafunzi wenzangu wengi wa vyuo vikuu ambayo yalitokana na taaluma wanazosoma. Kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea manung'uniko hayo miongoni mwa wasomi hawa tukiachilia mbali suala la ucheleweshwaji wa mikopo miongoni mwa wasomi hawa (kwa sasa changamoto hii inapungua kadiri siku zinavyosonga). Tatizo lingine ambalo linawasumbua wasomi hawa ni suala la uchaguzi wa taaluma gani akaisome Chuo Kikuu.

Uchaguzi wa taaluma (career choice) ni jambo nyeti sana na la kuzingatia kwa muhitimu yeyote wa elimu ya kuanzia kidato cha nne. Jamii yetu ya Tanzania haifahamu kwa undani kuhusu umuhimu wajambo hili lakini huku ndiko msingi hundaliwa. Mtu anapohitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano ama ngazi ya astashahada (certificate) na stashahada (diploma) hapo ndipo uchanguzi wa taaluma huanza. Kwa kuandika makala haya ninakusudia kutoa hamasa kwa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla kuwasaidia vijana hawa katika uchaguzi wa taaluma zao za baadaye kulingana na uwezo wao na mambo wanayoyapenda.

Uchaguzi wa taaluma huanza na uchaguzi wa michepuo/tahasusi (combination) anayokwenda kuisoma mwanafunzi shuleni. Hii huathiri kwa kiasi kikubwa taaluma yake kwa namna chanya ama hasi. Hapa ninamaanisha kwamba mchepuo atakaosoma una uhusiano mkubwa na taalumza zianzofundishwa chuo chuo kikuu ama kutokuwa na uhusiano kabisa. 

Kuna mambo kadhaa ambayo huwaathiri wanafunzi wawapo vyuo vikuu kwa kutozingatia uchaguzi wa taaluma. Mambo hayo yaweza kuwa; kutoendelea na masomo ya Chuo Kikuu kutokana na kufeli masomo (Discontinuation from studies), kufeli majaribio mara kwa mara kutokana na kutoridhika na kile wanachosomea ama ugumu wa masomo. Sababu kubwa hapa zaweza kuwa tatu; kwanza, uchaguzi wa taaluma kwa kufuata mkumbo wa marafiki pili, kushawishiwa ama kuchaguliwa taaluma na mzazi ama mtu yeyote aliyesoma taaluma husika na kupata mafanikio kwa hivyo na mchaguaji anaona naye asome taaluma husika ili afanikiwe na tatu, ni upepo wa upatikanaji wa mkopo kwa vyuo vikuu.

Tuwapo shuleni hasa kidato cha 5 & 6 wanafunzi wengi hua na ndoto kubwa sana wakati mwingine kuliko hata kutambua uwezo wao uko katika mambo yepi. Hili husababishwa na marafiki, suala hili linaitwa mkumbo. Kwa mfano wanafunzi wengi wa Kidato cha Sita hubagua taaluma za kusoma kutokana na matakwa yao bila kutambua uwezo wao. Wapo wengine ambao hawafikirii chochote zaidi ya kusikiliza marafiki zao wanataka kusoma taaluma zipi (mkumbo) matokeo yake baadaye wakiwa vyuoni huanza kujilaumu ama baadaye hushindwa kuendelea na masomo yaani 'Discontinuing from studies'.

Jambo lingine ni kushawishiwa ama kuchaguliwa taaluma ya kusoma na wazazi/mlezi; mara nyingi wazazi/mlezi huwalazimisha vijana wao wakasome taaluma fulani bila kutambua uwezo wa kijana husika. Lakini pia kwa sababu mzazi/mlezi kufanikiwa katika taaluma husika anamlazimisha kijana asome taaluma aliyosoma yeye. Wakati mwingine wazazi hualazimisha kabisa kwamba vijana wao wasipofuta maagizo wanayoambiwa watajijua wenyewe. Jambo hili huwa ni zito na changamoto sana kwa sababu wazazi/walezi mara nyingi ndiyo hugharamia fedha za masomo vijana wao wawapo masomoni.

Vilevile kuna suala la upatikanani wa mkopo. Hili ni suala ambalo linawalazimu wengi kusoma taaluma fulani Elimu/Ualimu wa Sayansi, Udaktari, Uuguzi na Uhandisi n. k. kwa sababu ya upatikanaji mkopo wa serikali ama ufadhili wa masomo. Wengi wao huchelewa kukubaliana na hali hii, lakini baadaye pia kutokana na ufadhili wa serikali hujikuta hawana namna kwa sababu ya hali ya familia kutoweza kugharamia masomo. Wengine hugundua mambo fulani katika taaluma husika na kuamua kukubaliana na hali na kuendelea na masomo. Huu ni mfano tu ila katika taaluma nyingine ambazo sijazitaja wapo wenye mambo kama haya.


2.0 MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIA WAKATI WA KUCHAGUA TAALUMA

Kuna mambo kadhaa unaweza kuyazingatia katika suala zima la kuchagua taaluma ya kusoma Chuo Kikuu, mambo hayo yaweza kuwa yafuatayo:

2.1. UJUZI ULIO NAO AMA KIPAJI

Japokuwa kuna baadhi ya taaluma haziihitaji ujuzi sana ni muhimu kutambua kuwa suala la ujuzi ni la muhimu katika kipi usomee. Mathelani ujuzi katika lugha, hesabu ama kuwa na uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu. Ujuzi ulio nao wewe utakusaidia kusoma vyema taaluma yako na kuifurahia huku ukiunoa zaidi ujuzi huo. hili pia linawahusu wenye vipaji, unaposoma taaluma inayokuza kipaji chako basi inekujenga zaidi kuwa na mtazamo mpana kuhusu kipaji na ndoto yako.

 2.2. MAMBO UPENDAYO

Baada ya kugundua ujuzi ama uwezo ulio nao, suala linalofuata ni kufahamu unapenda kufanya nini katika maisha yako baada ya kumaliza masomo. Lengo lako linatakiwa liwe kufanya jambo ambalo unalipenda, hii itakusaidia katika kuridhika na kuyafurahia masomo yako kwa kipindi chote utakochokuwa masomoni, utasoma kwa furaha sana na utakuwa umeridhika. Sanjari na hapo itakusaidia kujijenga vizuri kitaaluma na kukunoa vyema.

2.3. TAFUTA KITABU CHA CHUO KINACHOELEZEA KUHUSU CHUO (PROSPECTUS)

Prospectus ni kitabu kinachoelezea mambo yote ya msingi unayopaswa kuyafahamu kuhusu chuo. Kitabu hiki kinaelezea vizuri kuhusu taaluma mbalimbali zinazotolewa na chuo husika, hii inajumuisha na kozi ndogondogo ambazo hufundishwa kwa muda wote wa masomo kuanzia semista ya kwanza hadi ya mwisho. Kitabu hiki pia huonesha taarifa za kifedha kama ada inayotakiwa kulipwa kwa kila taaluma na michango mingine ya chuo. Muhimu zaidi kupitia kitabu hiki cha mwongozo ni kufahamu kuhusu taaluma utakayopenda kuisoma. Hapo utalinganisha  uwezo wako katika taaluma, yaani taaluma zipi utazimudu na zipi zinahitaji uongeze bidii. Pia kitabu hiki huwa na sifa za chini za kujiunga na masomo katika kila taaluma (mimimum entry qualification) hizi zinategea sana ufaulu wako wa Kidato cha Nne, Sita ama Diploma. Huna sababu ya kupata nakala ngumu ama kupiga simu kwenye chuo husika kwa sababu kitabu hiki huwekwa katika tovuti ya kila chuo.

2.4. PITIA KITABU CHA MWONGOZO CHA TCU (TCU GUIDEBOOK)

Kitabu hiki hutolewa kila mwaka wa masomo na Tume ya Vyuo Vikuu nchini. Hiki huwa na taaluma zinazotolewa na kila chuo pamoja na vigezo husika katika kila taaluma pamoja na ada yake. Taaluma ama chuo kisichokuwepo katika kitabu hiki huwa hakiruhusiwi kufanya udahili kwa mwaka husika. Katika kitabu hiki utakutana na vigezo vya chini ambavyo unatakiwa kukidhi ili kuingia katika ushindani wa taaluma husika. Mara nyingi ushindani unategemea na ufaulu wako kidato cha nne na kidato cha sita ama Diploma; jinsi ulivyofaulu vizuri ndivyo jinsi utakuwa katika nafasi za juu zaidi kuchaguliwa katika taaluma na chuo ulichotuma maombi. Vitabu vya Mwongozo hutolewa tofauti kwa Wahitimu wa Kidato cha Sita, Diploma wale wa Kutambuliwa kwa Kujifunza hapo Awali [Recognition for Prior Learning (RPL)]. Kila kimoja huainisha sifa kulingana na elimu husika.

2.5. CHAGUA TAALUMA UNAZOPENDA KULINGANA NA UWEZO NA VIPAUMBELE VYAKO

Katika hatua hii unatakiwa kuorodhesha taaluma unazotaka usoma. Kumbuka katika uchaguzi wako huo ni taaluma moja tu utatakiwa kusoma ama kwa kupangiwa na chuo kutokana na uchaguzi wako. Hili lisikupe shida kwa sababu wakati mwingine unaweza kubadili ukifika chuo ili mradi tu unavyo vigezo. Kuna baadhi ya vyuo huruhusu kubadili taaluma mwanzoni mwa semista ya kwanza. Vingine haviruhusu hivyo kama hujaipenda zaidi taaluma hiyo, unaweza kuahirisha mwaka wa masomo ama kuhama chuo. Nasisitiza kufanya uchaguzi sahihi zaidi ili kuepukana na kadhia hizo.

 2.6. USIFIKIRIE SANA KUHUSU UPATIKANAJI WA AJIRA

Wengi wetu tunasoma kwa kufikiria upatikanaji wa ajira, kwamba baada ya masomo tuuajiriwe ni sahihi pia lakini jambo la muhimu kwa sasa ni kusoma na kutengeneza wasifu mzuri katika masomo huku ukinoa kipaji na uwezo wako. Kumbuka umahiri wako ndiyo utakaokuajiri. Ukifika chuo masomo yawe kipaumbele wakati ukifanya mengine kama itakulazimu. Ukifikiria ajira kutokana na taaluma yako hutasoma kwa amani, soma mambo mazuri huja mbele ya safari.

2.7. CHAGUA CHUO NA TAALUMA KULINGANA NA UFAULU WAKO

Kumekuwepo na tabia ya watu kung'ang'ania kuchagua taaluma fulani ama vyuo fulani kutokana na jinsi wanavyopenda wao na sifa na hadhi za vyuo watakavyo pasipokuzingatia ufaulu wao. Wengi wamejikuta wakikosa nafasi za masomo kwa mwaka husika, hii inatokana na kung'ang'ania chuo kutokana na hadhi yake ilihali mtu ana ufalu mdogo kushindana na wenye ufaulu mkubwa. Hakikisha ufaulu wako unakidhi vigezo vya ushindani wa taaluma na vyuo unavyochagua. Kama ufaulu wako ni wa chini ni vyema kutafuta taaluma na vyuo ambazo entry qualifications zinaendana na ufaulu wako. Usipozingatia hili utapoteza muda kurudia zoezi la udahili ama utakosa kabisa nafasi kwa mwaka husika. Zingatia kwamba ufaulu wako ndiyo ushindani wako. Usipochaguliwa katika chuo na taaluma fulani hakikisha una mbadala mwingine wa chuo na si kung'ang'ania uchaguzi ambao hujachaguliwa. Na uzuri wa siku hizi ni kwamba usipochaguliwa taaluma fulani unapewa na sababu, usipuuze sababu hizo.

2.8. FANYA UAMUZI SAHIHI NA UTUME MAOMBI KATIKA VYUO UNAVYOVIPENDA

Baada ya kuridhika na machaguo yako ya taaluma, hakikisha umechagua machaguo sahihi bila kukurupuka na kisha tuma maombi vyuoni. Kwa sasa maombi yanatumwa kwenye vyuo husika ama kwa kupeleka maombi chuo moja kwa moja ama kwa kutumia njia ya mtandao na sio kupitia TCU kama ilivyokuwa miaka iliyopita. Njia ya mtandao ni rahisi sana ufatiliaji wake kuliko kupeleka maombi kwa njia ya barua.

 
3.0. MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA

Hapo juu nimeainisha mambo ya muhimu kwa uchaguzi wa taaluma hasa vyuo vya ndani. Hapa chini nimeeleza kwa ufupi mambo ya jumla kuhusu uchaguzi utakaoufanya, sababu nyingine zaweza kukinzana na maelezo hapo juu kuliangana na mtazamo wa mtu.

3.1. SOKO LA AJIRA

Kama wewe ni mtu wa kuzingatia sana soko la ajira ni muhimu kwako kufanya utafiti kufahamu taaluma ambazo zina wigo mpana wa ajira ama zinazoajiri sana na hata zile ambazo zina uchache wa wataalamu. Wigo mpana wa ajira ni kuingia katika idara mbalimbali za ajira na kuweza kuendana na idara hizo bila kufundishwa sana au tena baada ya kumaliza masomo. Ajira zinazoajiri sana ni zile ambazo tasisi huhitaji watu wengi mara nyingi kulingana na umuhimu wake ingawa taaluma zote ni muhimu. Ajira zenye uchache wa wataalamu ni zile ambazo watu hawajasoma sana taaluma hizo kutokana na upya wake.

3.2. MSHAHARA NA MUDA

Ijapokuwa jambo unalolipenda ni muhimu zaidi, suala la mshahara ni la muhimu pia. Zingatia mshahara na malupulupu mengine na faida utakazozipata katika taaluma unayotaka kusoma kulingana na matarajio yako ya baadaye. Suala la muda pia ni muhimu kwa sababu zipo taaluma zitakuhitaji kupatikana hata katika muda wa zaida hata baada ya saa za kawaida za kazi.

3.3. UWIANO KATI YA KAZI NA MAISHA

Chunguza namna taaluma unayochagua itaathiri muda wa kazi na maisha yako binafsi , familia na matarajio yako mengine.

3.4. UKUAJI NA MAENDELEO

Zingatia ukuaji wako kitaaluma na maendeleo yako binafsi. Chagua taaluma ambayo itakupa wigo mpana wa kukua na kuendelea binafsi na kuendeleza taaluma husika yaani kuwa na mchango chanya katika maisha yako na taaluma yenyewe.

3.5. MALENGO ENDELEVU

Fikiria kuhusu malengo yako katika miaka ijayo. Je taaluma hiyo itakusaidia kufika huko ama utakuwa mtu wa kujilaumu tu na kujuta kwa nini uliichagua kuisoma? Fikiria kwa makini sana.

3.6. AFYA YAKO NA UZIMA

Hakikisha kwamba unakuwa katika taaluma ambayo inajali afya yako na uzima. Zipo baadhi ya taaluma huchosha mwili na akili pia, ni muhimu kuzifahamu ili ufahamu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

3.7. MAZINGIRA NA UTAMADUNI WA KAZI

Baadhi ya taaluma zitakufanya uwe mtu wa kusafiri na kuhama hama sana. Hakikisha unakuwa tayari kumudu mambo hayo. Pia fikiria kuhusu utamaduni na miiko ya taaluma husika kama inaendana na tabia zako.

 

4.0. MUHTASARI NA MAELEZO MENGINE

Mara baada ya kufanya maombi kila Chuo hufanya utaratibu wa udahili kwa mfumo wa ushindani walioweka wenyewe lakini utaratibu huo lazima uendane na vigezo vya Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU). Katika zama hizi za kila Chuo kufanya udahili wenyewe kunawapa nafasi ya wao kuchagua wale wanaowataka kulingana na vigezo vyao, kwa hiyo unashauriwa kuangalia ufaulu wako hasa idadi ya alama ulizo nazo (cutting points) katika mchepuo/tahasusi uliyosoma Kidato cha Sita ama ufaulu wako katika ngazi ya Stashahada (Diploma) wakati mwingine hata matokeo ya Kidato cha Nne huangaliwa. Kwa ufupi ni kwamba wenye alama za juu huwa na uwezekano mkubwa wa kuchaguliwa ukilinganisha na wenye alama za chini.

Vyuo vinapomaliza uchambuzi na udahili hutangaza majina ya wale waliochaguliwa kujiunga na vyuo hivyo moja kwa moja ama waliochaguliwa hapo na kuchaguliwa kwingineko, kwa hiyo hapa mdahiliwa hutakiwa kuchagua chuo kimoja na taaluma moja na kisha kuthibitisha chuo na taaluma apendayo kuisoma. Aidha vyuo pia hutoa sababu za kwa nini wadahiliwa wengine hawakufanikiwa kuchaguliwa na mara nyingi sababu hizo si za kupuuzia hata kidogo hasa ukiambiwa hujafikisha alama za ushindani ama kutokidhi vigezo vya taaluma husika. Mdahiliwa hutakiwa kuzingatia sababu hizo za kutochaguliwa na kujaribu awamu nyingine. Utaratibu huwa ni uleule lakini katika awamu zinazofuata taaluma fulani huondolewa kwenye mfumo kutokana na kuuwa zimesjaa wadahiliwa na hii ndiyo maana unasisitizwa kusoma taarifa kwa kina kuhusu uchaguzi wako wa taaluma.

Utaratibu huendelea hivyo mpaka awamu zote zitakapokwisha. Jambo la muhimu ni kwamba kuna wakati usipozingatia baadhi ya maelezo unaweza kukosa nafasi ya chuo kwa mwaka husika hasa kutozingatia ufaulu wako ama niseme idadi ya alama ulizo nazo katika mchepuo ama Stashahada yako. Ni muhimu sana kuwa makini. Jambo lingine la muhimu tena ni kuhakikisha taarifa zako binafsi zinakua sahihi kwenye mfumo wa udahili. Zingatia yote niliyoyaeleza hapa kuepuka usumbufu.

Unaweza kumtafuta mtu mwenye ufahamu wa mambo haya akakuelekeza vizuri zaidi ama unaweza kuwasiliana name kwa namba nilizoweka hapa chini. Huwa natoa ushauri huu BURE kabisa niapokuwa na muda. Mawasiliano yangu yapo hapa chini.

 

Makala haya yameandaliwa na kuandikwa na

Venance Gilbert

Mwalimu, Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Lugha na Menejimenti (BED-LM)

Chuo Kikuu Mzumbe

venancegilbert@gmail.com

0753400208.

Yalichapishwa mara ya kwanza 25/07/2017 yamefanyiwa marekebisho 05/06/2024.

SCHOLARSHIPS FOR UNDERGRADUATE, GRADUATE AND PhD STUDIES

Tokeo la picha la VENANCE BLOG
The listed Universities below offer various scholarship programmes across the world. If you are interested you may follow the instruction basing on your status of education and interests of the course you wish to perform.



Rhodes Trust, Oxford University
Application Deadline: Various

China Three Gorges University, China
Application Deadline: July 7, 2017

Nanjing University of Information Science & Technology, China
Application Deadline: June 15, 2017

Beijing Sport University, China
Application Deadline: July 10, 2017

The Southeast Asian Regional Center for Graduate Study and Research in Agriculture (SEARCA)
Application Deadline: July 31, 2018

Durham University, United Kingdom
Application Deadline: July 28, 2017

University of New Mexico
Course Starts on June 12, 2017 

Queen Mary University of London, United Kingdom
Application Deadline: January 15, 2018

University of Ghana
Application Deadline: November 3, 2017

Plymouth University in United Kingdom
Application Deadline: June 30, 2017

University of Cape Town, South Africa
Application Deadline: July 31, 2017

Humboldt University of Berlin, Germany
Application Deadline: June 15, 2017

University of Maryland
Course Starts on August 21, 2017

European Commission
Application Deadline: September 8, 2017

Charles Sturt University, Australia
Application Deadline: June 12, 2017

Sapienza University of Rome, Italy
Application Deadline: July 31, 2017

University of Melbourne in Australia
Application Deadline: July 16, 2017

University of Zaragoza, Spain
Application Deadline: June 15, 2017

Trinity College Dublin, Ireland
Application Deadline: June 14, 2017

Penn State University and Coursera
MOOC starts from June 5, 2017

The Radio Television Digital News Association
Application Deadline: June 30, 2017

Government of Hong Kong
Application Deadline: June 19, 2017

University of Lausanne, Switzerland
Application Deadline: June 30, 2017

Uppsala University ,Sweden
Application Deadline: June 30, 2017

University of Greenwich, United Kingdom
Application Deadline: June 28, 2017

The Japan Foundation
Application Deadline: June 1, 2017

Government of Belize
Application Deadline: June 16, 2017

University of Sao Paulo, Brazil
Application Deadline: July 25, 2017

Oxford Internet Institute, UK
Application Deadline: June 26, 2017

University of North Carolina, USA
Application Deadline: August 2, 2017

University of Bristol, United Kingdom
Application Deadline: July 7, 2017

University of Newcastle, Australia
Application Deadline: June 30, 2017

Dublin City University, Ireland
Application Deadline: June 30, 2017

University of Cape Town, South Africa
Application Deadline: Open

University of Oslo, Norway
Application Deadline: June 26, 2017

University of New South Wales, Australia
Application Deadline: July10, 2017

Department of Science & Technology, India
Application Deadline: June 30, 2017

John S. Latsis Public Benefit Foundation
Application Deadline: June 7, 2017

Indian Institute of Management, Bangalore
Course Starts on August 3, 2017

RWTH Aachen University
Course Starts on July 19, 2017




Source: Scholarship Position