Kwa tamaduni za kiafrika na jinsi tulivyozoea, mtu anapofiwa hasa na Mama yake mzazi humchukua muda sana kabla ya kurudi katika utaratibu wa kawaida, hii imekuwa tofauti kwa Zari ambaye siku chache tu baada ya msiba ameonekana na Diamond wakiponda raha huku wakijirekodi video na kuzituma katika mtandao wa Instagram hali iliyopelekea mashabiki kuliongelea sana suala hilo.
Diamond Platnumz amefunguka baada ya kuonekana kukerwa na maneno ya watu katika mtandao wa Instgram na kuyaandika haya:
"Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa misiba ya watu.... Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehemu tulivu apetiwepetiwe apate faraja!...sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia... Pambaneni na mahusiano yenu...! Nina siku 5 za kumpetipeti...! leo ndio kwanza Ya kwanza 😛"
![]() |
Hii ni screenshoot ya ujumbe huo aliotuma Diamond Platnumz kwenye mtandao wa Instagram huku akiwa ametag eneo Mombasa, Kenya. |
WASILIANA NA VENANCE BLOG:
Facebook page: VENANCE BLOG
Twitter: @Venancetz
Instagram: @venanceblog
email: venancegilbert@gmail.com
0 comments:
Post a Comment