RAIS PUTIN AMEAGIZA WANADIPLOMASIA 755 WA MAREKANI KUONDOKA URUSI

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu.

Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo.

Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo.

Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani.

Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Estonia, makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence, alisema anatumai kwamba mienendo ya serikali ya Urusi itabadilika.

Mashirika ya ujasusi nchini Marekani yanaamini kuwa Urusi ilijaribu kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kwa lengo la kumsaidia Donald Trump kupata ushindi.
Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.


Chanzo: BBC

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017