Posts

TATHIMINI KWA UFUPI CHELSEA vs EVERTON KABLA YA MECHI SAA 2:30 EAT

Image
Timu hizi mbili zimekutana katika michezo 49 ambapo Chelsea imeshinda mechi 22 na Everton imeshinda mechi 10 na kudroo mechi 17. Chelsea imeshinda nyumbani mechi 13 wakati Everton imeshinda mechi 9. Nje, Chelsea imeshinda mechi 9 wakati Everton imeshinda 2. Katika mechi 3 zilizopita Chelsea ilifungwa na Everton magoli 2 kwa nunge, hii ilikuwa mechi ya Machi 12, 2016. Lakini pia mechi ya Januari 16, 2016 timu hizi zilitoka sare ya magoli 3. Na ile ya Septemba 12, 2015 Chelsea alipigwa magoli 3 kwa 1. Katika msomu huu Chelsea ipo katika nafasi ya 4 wakati Everton ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi. Chelsea imeshinda 70% ya mechi ilizocheza huku Everton ikishinda 50%. Mechi za nyumbani Chelsea ina asilimia 80% dhidi ya mpinzani wake Everton 50% huku mechi zilizopigwa nje Chelsea ana 60% na Everton 40%. Chelsea ina wastani wa 2.1 katika magoli iloshinda wakati Everton ana wastani wa 1.5 Lakini pia Chelsea imefungwa wastani wa 0.9 wakati Everton ina 0.8.

TAHLISO YATOA WIKI MOJA KWA SERIKALI KUTOA MIKOPO

Image
Shirikisho la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) limetoa muda wa wiki moja kwa wanafunzi waliokosa mikopo licha ya kuwa na vigezo vyote ikiwemo uhitaji kusikilizwa na serikali kabla hatua nyingine hazijachukuliwa. Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bwana Stanslaus Peter, katika kikao cha pamoja kilichohusisha marais wa vyuo vyote nchini, waliokutana Jijini Dar es Salaam leo, kujadili sintofahamu inayowakumba wanafunzi wanaojiunga mwaka wa kwanza katika vyuo mbalimbali nchini. Stanslaus amesema kuwa kuna kundi kubwa la wanafunzi ambao wameondolewa kwenye orodha ya wanufaika, na wengine kunyimwa kabisa ama kwa visingizio au bila sababu, jambo linalowafanya waishi katika mazingira magumu na kuhatarisha hatma yao kimasomo. Amesema wamekubalina kuwa, endapo serikali haitafanyia kazi ombi hilo ndani ya wiki moja, basi shirikisho hilo litachukua hatua ikiwa ni pamojana kuhamasisha wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu...

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

Image
Google Inc. kupitia teknolojia yao ya Android wanakuja na Version nyingine 7.0 na 7.1 Android Nougat. Katika historia ya version za Android zilizowahi kuwagunduliwa version ya Kwanza ilikuwa Android Alpha 1.0 ya mwaka 2007. Hapo katikati zikaletwa Zombie Arts, Jeally Bean, KitKat, Lollipop na Mashallow. Sasa ni zamu ya Android Nougat. TUANGALIE SIFA ZA ANDROID NOUGAT 7 Android Nougat ipo kwa ajili hako. Ina njia nyingi za kufanya uhisi teknolojia hii ni ya kwako. Kwa mujiu wa Android, Nougat ni toleo zuri kuwahi kutolewa katika teknolojia hii. 1. Ni Mfumo wa Uendeshaji (Operating System, OS) unaotumia lugha yako. Inayasogeza karibu maneno ya lugha yako ikiwa na emoj mpya na uwezo wa kutumia lugha 2 kwa wakati mmoja. Ina zaidi ya emoj 1500 ikijumuisha emoj mpya 72. 2. Inakuruhusu kufanya mambo 2 kwa wakati mmoja. Sasa unaweza kutumia vitumizi viwili (applications) kwa kugusa mara mbili (double trap) na kutumia vitumizi viwili pande mbili. Kwa mfano, unaweza...

BATCH 4 WALIOCHAGULIWA MZUMBE (DEGREE, DIPLOMA, CERTIFICATE & TRANSFER)

Image
Yafuatayo ni majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Mzumbe kwa awamu ya 4 kwa mwaka 2016/2017. Pia yapo na majina ya waliohamishwa kutoka kwingineko kwenda Mzumbe. 👉BOFYA HAPA KUONA NA KUPAKUA MAJINA HAYO👈

SIMBA YAZIONYA AFRICAN LYON NA PRISONS

Image
Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema ari waliyokuwa nayo hivi sasa ana uhakika wa kupata pointi sita nyingine kwenye mechi mbili zilizobaki kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara. Akizungumza na gazeti hili jana, Mkude alisema pointi sita walizozipata Shinyanga dhidi ya Mwadui na Stand United, zimedhihirisha ubora waliokuwa nao msimu huu na atahakikisha wanaendelea na kasi hiyo ili kutimiza kile ambacho wamekikusudia. “Lengo ni ubingwa na kwakuwa tunautaka ubingwa kwanza lazima tumalize kinara kwenye mzunguko wa kwanza kwa kuchukua pointi zote sita kwenye michezo yetu miwili iliyobaki na baadaye tujipange kwa ajili ya mzunguko wa pili,” alisema Mkude. Simba imebakiwa na mechi dhidi ya Africany Lyon na Prisons. Mkude alisema anafurahi kuona kila mchezaji ndani ya kikosi chao akicheza kwa kujituma na kufuata kikamilifu maelekezo kutoka kwa wakuu wa benchi lao la ufundi na anaamini ari hiyo itaendelea hadi mwishoni mwa msimu huu na hatimaye kuwa mabingwa. “Hatuja...

SERIKALI IMEPELEKA TSH. BILIONI 177 KWENYE HALMASHAURI ZA WILAYA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imepeleka katika halmashauri nchini Sh bilioni 177 Oktoba mwaka huu kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha, amempongeza Rais John Magufuli, kwa kufikisha siku 365 za kuwapo madarakani na mafanikio makubwa ya utawala wake tangu alipopewa na Watanzania ridhaa ya kuwa Rais wa Tano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana. Licha ya pongezi zake, amewaomba Watanzania waendelee kumuunga mkono Rais Magufuli ili afanikishe zaidi dhamira yake njema ya kuwatumikia wananchi. Majaliwa aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma ambapo alizungumzia mambo mbalimbali katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu. Akizungumzia suala la fedha kupelekwa katika halmashauri, alisema serikali imechukua muda kupeleka fedha mara baada ya bajeti kupitishwa na Bunge kwa kuwa ilitaka kufanya mambo muhimu ya kujiridhisha. Aliyaja maeneo muhimu ambayo serikali ilitaka kuyafanyia kazi kabla ya kupeleka fedha kuwa ni kujiridh...

WAHAMIAJI 239 WAHOFIWA KUZAMA KATIKA AJALI YA MELI WAKITOKEA LIBYA

Image
Wahamiaji 239 wamehofiwa kuzama katika ajali ya meli wakitokea nchini Libya. Hii ni kwa mujibu wa habari kutoka shirika la Wakimbizi UNHCR. Msemaji wa UNHCR mjini Roma Italia amesema kuwa taarifa hizo zimethibitishwa na manusura wa ajali walipofikishwa katika ukingo wa bahari katika kisiwa cha Lampedusa. Mpaka sasa hakuna ambaye amekwishapatikana katika hao 239. Sami alisema kuwa watu 31 wamenusurika katika ajali za meli mbili zilizopata ajali baharini kufuatia dhoruba kali. Walisema kuwa watu 29 walinusurika katika meli ya kwanza huku wengine 120 hawajulikani walipo. Katika jitihada za kuokoa watu, wanawake 2 waliokuwa wakiogelea kujinusuru waliwambia waokoaji kuwa watu hao 120 walikufa katika meli hiyo. Katika matukio yote mawili, wengi wa wahamiaji hao wanaonekana kuwa ni raia kutoka eneo la Jangwa la Sahara. Leonard Doyle, msemaji mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) amesema kuwa watu 4,220 wamepoteza maisha katika mwaka huu 2016 kwenye ajali za meli katik...

OBAMA AWATAHADHARISHA WAPIGA KURA KUHUSU TRUMP

Image
Rais Barrack Obama amewahimiza wafuasi wa chama cha Democratic kumpigia kura Hillary Clinton na kuonya kwamba Donald Trump ni tishio kwa haki za kijamii, taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla. Rais wa Marekani Barrack Obama amewahimiza wafuasi wote wa chama cha Democratic kumpigia kura kwa wingi Hillary Clinton siku ya uchaguzi wiki ijayo na kuonya kwamba Donald Trump mgombea urais wa chama cha Republican ni tishio kwa haki za kijamii ambazo ziliafikiwa kupitia hali ngumu , taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla. Akigusia chaguo la rais siku ya Jumanne wiki ijayo, rais Barrack Obama alimpuuzilia mbali Trump kuwa mtu asiyestahili kabisa kuwa rais. Kufikia sasa Clinton bado anaonyesha uwezekano wa kuwa rais wa 45 wa Marekani lakini huku zikiwa zimesalia siku sita kabla ya uchaguzi huo mkuu, wafuasi wa chama cha Demokratic bado wako chonjo hasa kutokana na mienendo ya Trump isiyotabirika. Obama aliwaambia wapiga kura katika mji wa Chapel Hill kuwa hatima ya taifa h...

MAJINA YA MKOPO MZUMBE MWAKA WA KWANZA 2016/2017 HAYA HAPA

Image
Chuo Kikuu Mzumbe kimetoa majina ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza walionufaika na Mkopo wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.  Ili kuona majina haya kwa simu hakikisha una Office App kwenye simu yako (WPS Office, OfficeSuite ama Polaris Office n.k.) 👉BOFYA HAPA KUONA MAJINA NA KUDOWNLOAD👈

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA MZUMBE AWAMU YA TATU HAYA HAPA (BATCH/ROUND 3)

Image
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Chuo Kikuu Mzumbe, imetoa majina ya waliochaguliwa chuoni hapo kwa awamu ya tatu (Third Batch/Round) Tumia mojawapo kati ya Browser hizi kuangalia selection hizo; UC Browser, Mozilla Firefox, Google Chrome au Dolphin Browser, Opera Mini haitaonesha baadhi ya vipengele katika kudownload majina haya. Link itakupeleka moja kwa moja juu kabisa kutakuwa na mshale wa kupakua majina hayo, bofya hapo na majina yatashuka moja kwa moja. 👉BOFYA HAPA KUONA NA KUDOWNLOAD MAJINA👈

HAYA HAPA MAJINA YA HOSTEL MZUMBE MWAKA WA KWANZA (JINA LA HOSTELI NA NAMBA YA CHUMBA)

Image
Haya hapa majina ya Hosteli mwaka wa kwanza Mzumbe (Jina la Hosteli pamoja na namba ya Chumba unachotakiwa kuishi)  👉BOFYA HAPA KUONA MAJINA HAYO👈

RAIS MAGUFULI AAHIDI KUENDELEA KUTOA MIKOPO 2016/2017 KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NA KUTOA RAI SUALA HILO KUSHUGHULIKIWA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kwa nafsi yake ametoa matumaini kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini kuhusu hatima yao ya mkopo wa Elimu ya Juu alipokuwa akihudhuria sherehe ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Rais Magufuli amebainisha haya, namnukuu; "Tunapopitia katika challenge hii muivumilie serikali kutengeneza utaratibu ulio mzuri, ninafahamu, katika bajeti ya mwaka 2015/2016, fedha iliyotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa sababu Mh. Waziri umezungumza hapa zilikuwa bilioni 340 ambazo  zilikjuwa zinatosha karibu wanafunzi tisini elfu (90,000)  baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani  ili kutimiza yale tuliyokuwa tumeahidi tuliongeza fedha hizo za mkopo hadi kfikia bilioni 473 bajeti ilikuwa ya bilioni 340 tukaongeza zikafika bilioni 473 kutokana na makusanyo na tukaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi 124,358 mwaka huu ameeleza ni zaidi ya bilioni 483 zimepitishwa katika bajeti  k...

MFAHAMU HILLARY CLINTON KWA MAMBO HAYA 15

Image
Jina Kamili: Hillary Diane Rodham Clinton Kuzaliwa: Oktoba 26, 1947 Alikozaliwa: Chicago, Illinois Kwa Ufupi Alipochaguliwa kuwa Seneta mwaka 2001 alikuwa mwanamke wa kwanza First Lady kuwa mtumishi wa serikali. Baadaye alikuwa Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani mwaka 2009 akitumikia wadhifa huo hadi mwaka 2013 katika utawala wa Rais Barrack Obama. Mwaka huu (2016), amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha The Democratics. Hillary alizaliwa  Oktoba 26, 1947 huko Chicago, Illinois. Alipata Shahada yake ya Sheria kutoka Yale University. Alifunga ndoa na mwanafunzi mwenziye aliyekuwa akisoma sheria Bill Clinton mwaka 1975. Baadaye alitumikia taifa la Marekani kama First lady  mwaka 1993 hadi 2001, na baadaye akiwa Seneta mwaka 2001 hadi 2009. Mapema mwaka 2007 Clinton alitangaza kugombea Urais nchini Marekani. Katika kura za maoni mwaka 2008 alichuana na Barrack Obama lakini kura hazikumruhusu kugombea Urais kwa ticket ya Democratic. R...

VIDEO: TRUMP AKATAA KUJIBU SWALI KUHUSU KUKUBALI MATOKEO KAMA ATASHINDA KWENYE UCHAGUZI

Image
Ni katika Mdahalo wa tatu na wa mwisho ukiofanyika Nevada, Las Vegas. Swali liliulizwa kwa Bwana Trump "utakubali matokeo ya Urais baada ya kushindwa na mpinzania wako Hillary Clinton?" Trump hakujibu moja kwa moja, alisema "nitaliangalia hilo kwa wakati huo". Awali ya hapo Rais Obama alishangazwa na kutokujiamini kwa Trump kuhusu kuwa na mashaka na Uchaguzi hata kabla ya Uchaguzi wenyewe kufanyika. Nitakuandalia makala kamili kutoka kwenye Mdahalo huo. Hii hapa video ikimuonesha Trump alivyokataa kujibu swali aliloulizwa: Video kwa hisani ya France24.

WALIOCHAGULIWA MZUMBE AWAMU YA PILI MAJINA HAYA HAPA

Image
Chuo Kikuu Mzumbe kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kwa ngazi ya Cheti, Stashahada na Shahada kwa awamu ya pili. >>> BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA <<<