SIMBA YAZIONYA AFRICAN LYON NA PRISONS

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema ari waliyokuwa nayo hivi sasa ana uhakika wa kupata pointi sita nyingine kwenye mechi mbili zilizobaki kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkude alisema pointi sita walizozipata Shinyanga dhidi ya Mwadui na Stand United, zimedhihirisha ubora waliokuwa nao msimu huu na atahakikisha wanaendelea na kasi hiyo ili kutimiza kile ambacho wamekikusudia.

“Lengo ni ubingwa na kwakuwa tunautaka ubingwa kwanza lazima tumalize kinara kwenye mzunguko wa kwanza kwa kuchukua pointi zote sita kwenye michezo yetu miwili iliyobaki na baadaye tujipange kwa ajili ya mzunguko wa pili,” alisema Mkude.

Simba imebakiwa na mechi dhidi ya Africany Lyon na Prisons. Mkude alisema anafurahi kuona kila mchezaji ndani ya kikosi chao akicheza kwa kujituma na kufuata kikamilifu maelekezo kutoka kwa wakuu wa benchi lao la ufundi na anaamini ari hiyo itaendelea hadi mwishoni mwa msimu huu na hatimaye kuwa mabingwa.

“Hatujafungwa hata mchezo mmoja katika michezo 13 ambayo tumecheza hadi sasa hii ni rekodi nzuri lakini tunatakiwa kuiendeleza kwenye mechi zijazo ili tuweze kufanya vizuri zaidi na zaidi kwakuwa bado tuna safari ndefu hadi kufikia mwisho wa ligi,” alisema Mkude.

Nahodha huyo amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuendelea kuwasapoti katika mechi zao ili kushinda mtihani uliopo mbele yao ambao ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA, baada ya kufanya vibaya kwa misimu mitatu iliyopita jambo ambalo lilipoteza heshima yao.

Simba inatarajia kucheza na African Lyon keshokutwa na tayari imesharejea kutoka Shinyanga na kuweka kambi Ndege Beach. Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017