TAHLISO YATOA WIKI MOJA KWA SERIKALI KUTOA MIKOPO
Shirikisho la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) limetoa muda wa wiki moja kwa wanafunzi waliokosa mikopo licha ya kuwa na vigezo vyote ikiwemo uhitaji kusikilizwa na serikali kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.
Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bwana Stanslaus Peter, katika kikao cha pamoja kilichohusisha marais wa vyuo vyote nchini, waliokutana Jijini Dar es Salaam leo, kujadili sintofahamu inayowakumba wanafunzi wanaojiunga mwaka wa kwanza katika vyuo mbalimbali nchini.
Stanslaus amesema kuwa kuna kundi kubwa la wanafunzi ambao wameondolewa kwenye orodha ya wanufaika, na wengine kunyimwa kabisa ama kwa visingizio au bila sababu, jambo linalowafanya waishi katika mazingira magumu na kuhatarisha hatma yao kimasomo.
Amesema wamekubalina kuwa, endapo serikali haitafanyia kazi ombi hilo ndani ya wiki moja, basi shirikisho hilo litachukua hatua ikiwa ni pamojana kuhamasisha wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu kuungana na wale wa mwaka kwanza katika kudai haki hiyo.
Chanzo: EATV
Comments
Post a Comment