Posts

MABAKI YA NDEGE YA MISRI YAPATIKANA

Image
Mamlaka ya Misri inasema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo. Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha ya kwanza ya masalio hayo. Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo. Chanzo: BBC

MOVIE: X-MEN APOCALYPSE RELEASED TODAY

Image
  Release date: May 27, 2016 Director: Bryan Singer Starring: James McAvoy Jennifer Lawrence Oscar Isaac Michael Fassbender Rose Byrne Sophie Turner Synopsis: In this comic-book adventure set in the 1980s, the X-Men are forced to confront an ancient mutant called Apocalypse (Oscar Isaac). After the resurrected beast recruits a super-team to take over the world and destroy hunmanity, Professor X (James McAvoy) and his charges must come to the rescue for the fate of the planet. The film co-stars Michael Fassbender, Jennifer Lawrence and Olivia Munn.

OBAMA AZURU HIROSHIMA JAPAN

Image
Obama amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000. Baada ya kuweka shada ya maua katika bustani ya amani eneo la Hiroshima-Japan, rais Obama alitoa hotuba ya kumbukumbu ya mashambulizi hayo ya Hiroshima huku akisisitiza matumaini kuwa uhusiano kati ya Japan na Marekani utazidisha matumaini katika juhudi za kutupilia mbali matumizi ya silaha za atomiki. Obama amekuwa rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000. Obama amefanya ziara hiyo ya kihistoria baada ya mkutano wa viongozi wa nchi saba tajiri kiviwanda duniani ambapo viongzo hao wamekubali kuimarisha uchumi wa dunia. Upatanisho Shambulizi la bomu la kwanza la atomiki eneo la Hiroshima mwaka 1945 na pia Nagasaki lilisaba...

FURAHIA WIKENDI KWA KUANGALIA MUVI HIZI 5 KALI MPYA

Image
JINA LA MUVI: KILL ZONE 2 STAR: TONY JAA (kutoka Ong Bak)  After his true identity is exposed, undercover cop Kit ( Wu Jing ) is sent to a corrupt Thai prison by the gang he infiltrated, while his police unit erases all evidence that he was ever an officer. There, a guard named Chai ( Tony Jaa ) discovers that Kit is a bone-marrow match for his daughter, who desperately needs a transplant. The unlikely partners must find a way to secretly escape from the brutal prison and save Chai's daughter. Pou-Soi Cheang directed this martial-arts action thriller. JINA LA MUVI: LAST DAYS IN THE DESERT This biblical drama follows Jesus Christ (here referred to as " Yeshua " and played by Ewan McGregor ) during the 40 days he spent fasting and wandering in the desert. He is approached by a demon (also McGregor ) during his travels, who challenges him to help a troubled family living in the wilderness. Ciarán Hinds , Tye Sheridan , and Ayelet Zurer co-star as the mem...

HEZBOLLAH YATAJA SABABU YA KUUAWA KIONGOZI WAO

Image
 Kundi la Waislamu wa madhehebu ya Kishia la Hezbollah nchini Lebanon limetaja sababu ya kifo cha kiongozi wake wa ngazi ya juu wa kijeshi, Mustafa Badreddine kuwa kimetokana na makombora ya mizinga liliofanyika karibu na uwanja wa ndege wa Damascus nchini Syria.  Hezbollah lilitangaza  kifo cha Badreddine hapo jana na alifanyiwa mazishi ya kijeshi siku hiyo hiyo katika eneo la ngome la kundi hilo huko kusini mwa Beirut. Taarifa ya kundi hilo imesema mashambulizi hayo yamefanywa na kundi linaloitwa Takfiri. Takfiri ni neno linalotumiwa na kundi hilo la Kisunni kwa kuonesha msimamo mkali, kundi lenye kujihami na silaha, lililo na itikadi kali. Badreddine alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kundi la Hezbollah walioshutumiwa mwaka 2005 kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri. Chanzo: Deutsche Welle (DW)

TEGEMEA PAMBANO KUTOKA KWA MAYWEATHER NA CONOR McGREGOR

Image
 Floyd Mayweather   Conor McGregor Mwanamasumbwi Floyd Mayweather amesema kuwa yeye ndiye aleanzisha uvumi wa kupambana na Conor McGregor ambaye anapambana kwa mtindo wa Mixed Martial Art (MMA). McGregor alipost picha kwenye mtandao wa Twitter  iliyomuonesha yeye na Mayweather wakwa uso kwa uso. Mayweather, mwanamasumbwi aliyestaafu mwenye miaka 39 amesema kuwa atahitaji kiasi cha fedha Dollar za kimarekani Milioni 100 sawa na Euro Milioni 69.3 kupambana na McGregor raia wa Ireland mwenye umri wa miaka 27. "Muwe makini kusikiliza, linaweza kuwa pambano kati ya mcheza boxing na MMA" Mayweather aliiambia fighthype.com "Ni pendekezo nililolitoa mimi, inaweza isiwe tetesi" aliongeza Mayweather. Baba yake Mayweather alisema kuwa mwanaye huyo (Mayweather) aliwahi kumwambia kuwa atapambana na mwanamasumbwi yeyote kutoka MMA ambapo McGregor aliiambia BT Sport kuwa anataka pambano la Dola Bilioni na Muamerika, Floyd Mayweather. McGregor, a...

ANGALIA VIDEO YA JENNIFER LOPEZ-AIN'T YOUR MAMA HAPA

Image
Jennifer Lopez ameachia video ya wimbo wake Ain't your Mama May 6 ambapo mpaka sasa wimbo huo umetazawa na watazamaji zaidi ya milioni na laki saba. Kama bado hujapata nafasi ya kuangalia video hiyo tazama hapa kwa hisani ya VENANCE BLOG kisha toa maoni yako kuhusu video hiyo. Like Page yangu Facebook Nifuate Twitter Nifolo Instagram

DOWNLOAD AUDIO KUTOKA UPRISE MUSIC: JVP SQUAD-HUSTLE ZA KITAA

Image
Ngoma imefanywa Uprise Music na producer Fragger. Ngoma inaitwa Hustle za Mtaa imefanywa na JVP Squad ndani kasimama Ng'itu the Hustler na Fizzo. Sikiliza na kudownload kisha toa maoni yako hapa.  BOFYA HAPA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD  

UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA TANZANIA NA UGANDA SASA NI RASMI

Image
BOMBA la mafuta ghafi kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda, sasa ni rasmi kwamba litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga, ambako ndiko meli kubwa za mafuta, zitakapotia nanga kubeba mafuta hayo kwenda sehemu mbalimbali duniani. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia bandari hiyo. Kwa hatua hiyo, bomba hilo linalotakiwa kuwa limekamilika ifikapo 2018, litaingilia Mkoa wa Kagera kutoka nchini Uganda na kupita katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi Bandari ya Tanga. Rais Museveni Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ndiye aliyetangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika jijini Kampala jana. “Ujumbe wa Tanzania uliokamilisha mazungumzo hayo na kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo, uliongozwa na Dk Augustine Mahiga, ...

MALAWI IMETEKETEZA TANI 2 ZA PEMBE ZA NDOVU KUTOKA TANZANIA

Image
Malawi imeteketeza tani 2.6 ya pembe za ndovu ambazo zilinaswa na maafisa wa usalama zikitokea nchi jirani ya Tanzania. Meno hiyo 781 ya tembo ambayo inakisiwa kugharimu takriban dola milioni tatu ilipatikana baada ya operesheni dhidi ya ulanguzi na uwidaji haramu. Mkurugenzi wa idara inayosimamia mbuga za wanyama pori Bright Kumchedwa, amesema kuwa hiyo ni ishara ya kwanza na dhabiti kutoka kwa Malawi kuwa haitaruhusu tena ardhi yake kutumika kulangua bidhaa za uwindaji haramu. Hafla ya hiyo ya kihistoria ilifanyika katika eneo la Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo. Kenya inatarajiwa kutekeleza hatua kama hiyo mwishoni mwa mwezi huu. Kenya imekamata takriban tani 120 ya meno ya ndovu. Chanzo: BBC

ZITTO KABWE: RAIS AMELIINGIZIA TAIFA HASARA YA TSH. BILIONI 36

Image
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais John Pombe Magufuli ameliingizia taifa hasara ya bilioni 36 mpaka sasa toka alipoingia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia jumla ya bilioni 36.   "Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Rais, kwa kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe.  Wakati Rais John Magufuli anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa amba...

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MAREKANI: TRUMP NA RUBIO WATOFAUTIANA KUHUSU UISLAM

Image
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa moja kwa moja runingani. Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu wengi wanapenda Wamerekani. ''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi. Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani. Ikilinganishwa na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya sera zao. ''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema. Lakini katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wen...

JANET JACKSON AAHIRISHA KUFANYA ZIARA YA MUZIKI ULAYA KUFUATIA MAUZO MABAYA YA TIKETI

Image
Janet Jackson amefuta ziara yake kimuziki 'Unbreakable' barani Ulaya kufuatia mauzo mabaya ya tiketi barani humo. 'Alikuwa anaelekea kushindwa vibaya' kilisema chanzo cha habari. Muuza tiket mkuu alimuandikia barua pepe Janet mapema wiki hii kuhusu kurudishwa kwa hela za watu waliokuwa wamenunua tiketi. Hii ni wiki tatu kabla Janet alikuwa aende kufanya onesho jijini London, 'haitawezekana kwa sasa kusema ni lini tutapanga tena tarehe mpya ya onesho kwa hiyo tunarudisha hela kwa wale waliokuwa wamenunua tiketi' iliandikwa hivyo barua pepe hiyo. Upande wa Janet haukuzungumzia kuhusu kufutwa kwa onesho hilo lakini chanzo cha habari kilisema kuwa ni kufuatia mauzo mabay ya tiketi. 'Alikuwa anaelekea kushindwa vibaya, msanii anapofuta au kuahirisha ziara ya muziki sababu huwa ni mauzo mabaya ya tiketi' kilisema chanzo hicho na kuongeza 'ni bora kuahirisha kuliko kufanya onesho ukumbi ukiwa haujajaa watu haswa kwa msanii Janet Jackson'. Cha...

MECHI KATI YA LEICESTER NA WEST BROM FAHAMU HAYA

Image
Mchezo wa leo kati ya Leicester city na West Bromwich Albion utapigwa katika dimba la King Power Stadium, ambapo Leicester watakuwa ni wenyeji wa dimba hilo. Mtanange utaanza saa 4 na dakika 45 usiku saa za Afrika Mashariki. Novemba 1, 2013, West Brom alimfunga Leicester goli moja bila katika dimba la King Power Stadium. Mwaka 2015, April 11 West Brom wakiwa wenyeji katika dimba la nyumbani, The Hawthorns walipigwa bao tatu dhidi ya mbili na Leicister city. Lakini pia October 31, mwaka jana 2015, West Brom akiwa mwenyeji kwenye dimba la The Hawthorns alifungwa na Leicester city magoli 3 kwa mawili kama mechi iliyopita. Leicester City inaongoza ligi ikiwa na pointi 56 ambapo imecheza mechi 27 imeshinda mechi 16, imetoka sare mechi 8, na kupoteza mechi 3 ikiwa na magoli ya kifunga 20. Kwa upande wa West Brom wao wapo katika nafasi ya 13 wakiwa wamecheza mechi 27, wameshinda mechi 9, sare mechi 8 na kupoteza mechi 10 wakiwa wmemfungwa magoli10. West Brom wana pointi...

MAMBO YA KUFAHAMU KATI YA CHELSEA NA NORWICH CITY

Image
Chelsea imeshinda mechi saba na haijapoteza katika mechi tisa ilizokutana na Norwich City kwenye EPL. Norwich City imefenikiwa kuifunga Chelsea magoli manne tu na kushindwa katika mechi nne ambazo walikutana mara ya mwisho na The Blues. Steven Naismith wa Norwich City amefanikiwa kuifunga Chelsea magoli sita katima mechi saba walizokutana na The Blues EPL. Norwich City imeshinda mechi nne tu, sare nne na kupotezaechi nane katika mechi 16 ilizocheza katika dimba lao la nyumbani, Carrow Road. (W4 D4 L8). Norwich City imepata magoli 10 tu katika dimba lao la nyumbani, hii ni baada ya kushinda mechi mbili kati ya tano za EPL katika dimba hilo. Katika mechi 7 za EPL na kufunga magoli 7 pamoja na kuwa na jumla ya magoli 19 kwenye ligi. Chelsea imeshuhudia wachezaji wake 15 wakiifungia magoli timu hiyo msimu huu. Rekodi ambayo ni ya juu zaidi katika mashindani msimu huu. Guus Hiddink amepoteza mechi moja tu kati ya mechi 23 kama kocha na meneja wa klabu katika...