KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MAREKANI: TRUMP NA RUBIO WATOFAUTIANA KUHUSU UISLAM
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa moja kwa moja runingani.
Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu wengi wanapenda Wamerekani.
''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi.
Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani.
Ikilinganishwa na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya sera zao.
''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema.
Lakini katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana naye kwamba familia za magaidi ziangamizwe.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment