TEGEMEA PAMBANO KUTOKA KWA MAYWEATHER NA CONOR McGREGOR

 Floyd Mayweather

Conor McGregor
Mwanamasumbwi Floyd Mayweather amesema kuwa yeye ndiye aleanzisha uvumi wa kupambana na Conor McGregor ambaye anapambana kwa mtindo wa Mixed Martial Art (MMA).


McGregor alipost picha kwenye mtandao wa Twitter  iliyomuonesha yeye na Mayweather wakwa uso kwa uso.


Mayweather, mwanamasumbwi aliyestaafu mwenye miaka 39 amesema kuwa atahitaji kiasi cha fedha Dollar za kimarekani Milioni 100 sawa na Euro Milioni 69.3 kupambana na McGregor raia wa Ireland mwenye umri wa miaka 27.

"Muwe makini kusikiliza, linaweza kuwa pambano kati ya mcheza boxing na MMA" Mayweather aliiambia fighthype.com

"Ni pendekezo nililolitoa mimi, inaweza isiwe tetesi" aliongeza Mayweather.

Baba yake Mayweather alisema kuwa mwanaye huyo (Mayweather) aliwahi kumwambia kuwa atapambana na mwanamasumbwi yeyote kutoka MMA ambapo McGregor aliiambia BT Sport kuwa anataka pambano la Dola Bilioni na Muamerika, Floyd Mayweather.

McGregor, aliyeshindwa pambano lake hvi karibuni alipokuwa akipambana na Nate Diaz aliondolewa kwenye pambano la UFC 200 CARD mwezi uliopita baada ya kugomea kutimiza baadhi ya vigezo vilivyotaka kushiriki pambano hilo.

Pambano la 49 na la mwisho kutoka kwa Mayweather dhidi ya ANDRE BERTO mwezi wa tisa mwaka jana lilimfanya aamue uamuzi ambao haukutegemewa na wengi, ambapo alisema, "kazi yangu imefikia mwisho, na hii ni taarifa rasmi".

CHANZO: BBC

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017