BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

Ramani ya Afrika.
Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo:


1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia.

2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti.

3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takribani 25% ya lugha zote duniani zinazungumzwa barani Afrika huku kukiwa na lugha za makabila zaidi ya 2,000.

4. Afrika ni bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani ambao wanakadiriwa kuwa bilioni 1.1 huku zaidi ya 50% ya wakazi wake wakiwa ni vijana wenye umri chini ya miaka 25. Inakadiriwa kwamba mpaka kufikia mwaka 2050 bara la Afrika litakuwa na takribani watu bilioni 2.3. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za idadi ya watu iliyotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015.

5. Takribani 40% ya wazee wakazi wa bara hili hawajui kusoma na kuandika.

6. Vita ya pili ya Kongo ndiyo vita hatari kutokea duniani baada ya Vita ya Pili ya dunia. Vita hii iligharimu uhai wa watu takribani milioni 5.4

7. Jangwa la Sahara ni kubwa kuliko yote duniani na ukubwa wake ni zaidi ya nchi ya Marekani.

8. Kuna zaidi ya wachina milioni 1 katika baraka la Afrika. Nchi ya Angola ikiwa na zaidi ya wachina 350,000.

9. Kiwango cha ukataji miti barani Afrika ni mara mbili ya kiwango chote cha ukataji miti duniani. Zaidi ya hekta milioni 4 zinakatwa miti barani hapa kila mwaka.

10. Ziwa Victoria ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika huku likiwa ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani na kuwa na maji laini duniani.

11. Wanyama kama vile twiga, pundamilia, viboko, sokwe na nyumbu ni wanyama pekee wanaopatikana katika bara hili.

12. Ziwa Nyasa ambalo kwa jina jingina linaitwa Ziwa Malawi ndilo ziwa lenye aina nyingi za samaki (fish species) kuliko maziwa mengine duniani.

13. Bara hili lina zaidi ya asilimia 85 ya Tembo wote wanaopatikana duniani kote, pia, 99% ya Simba waliosalia duniani wanapatikana katika bara hili. 

14. Mto Naili ambao una urefu wa kilomita 6,650 ni mto mrefu kuliko yote duniani na unapatikana katika bara hili.

15. Mbuga ya Serengeti ambayo inapatikana nchini Tanzania ni hifadhi pekee ambayo ina kundi kubwa la wanyama duniani ikiwa na pundamilia zaidi ya 750,000. Katika hifadhi hii nyumbu zaidi ya milioni 1.2 huhama kila mwaka kutoka hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania kuelekea katika hifadhi ya Masai Mara iliyoko Kenya. Katika kundi hilo la nyumbu wanaohama kila mwaka kutafuta malisho wanyama kama pundamilia, swala na pofu huwepo katika uhamaji huo ambalo ni tukio la kipekee duniani.

16. Bara la Afrika lina zaidi ya 25% ya aina ya ndege wote wanaopatikana duniani.

17. Zaidi ya mabwawa 1,270 yamejengwa kandokando ya mito barani hapa. Mabwawa haya yana kazi kubwa ya kuzalisha umeme unaotumia ngumu za maji.

18. Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa na bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya bara la Asia. Afrika ina takribani watu bilioni 1.2 na hii ni kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa mwaka 2015. Hii ni sawa na 16% ya idadi yote ya watu waliopo duniani.

19.  Afrika ni bara la pili kwa kuwa na joto baada ya bara la Australia.

20. Uislamu ni dini yenye wafuasi wengi barani Afrika ikifuatiwa na dini ya Kikristo huku ikikadiriwa kwamba takribani 38% ya Wakristo wote wataishi kusini mwa jangwa la Sahara mpaka kufikia mwaka 2050.

21. Afrika ni bara lililopo katika nyuzi 0 (0°) katika mstari wa grinwichi meridiani na ikweta.

22. Nchi kubwa kuliko zote barani Afrika ni Algeria ikiwa na eneo la kilomita za mraba milioni 2.381 ikifuatiwa na DR Congo yenye eneo la kilomita za mraba 2.844 wakati nchi ndogo kuliko zote ni Shelisheli yenye eneo la kilomita za mraba 459.

23. Nigeria ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika ikiwa na takribani watu wanaokadiriwa kufika milioni 218.5 hadi kufikia mwezi Septemba 2023. Hii ni sawa na 18% ya watu wote wanaoishi barani hapa. Pia, hii ni sawa na 2% ya watu wote wanaoishi duniani.

24. Umbali mfupi kati ya Ulaya na Afrika ni kilomita 14 sawa na maili 8.7 ukipitia mlango bahari wa Gibraltar.

24. Maporomoko ya Victoria yaliyopo kati ya mpaka wa Zambia na Zimbabwe ni maporoko ya makubwa zaidi ya maji kuliko yote duniani. Pia, ni moja kati ya maajabu saba ya dunia.

25. Kiboko ni mnyama hatari sana barani Afrika kuliko hata Simba na Chui. Anaua watu wengi kuliko Simba na Mamba wakijumlishwa kwa pamoja.

26. Takribani 90% ya wagonjwa wa Malaria duniani kote wanapatikana barani hapa. Ugonjwa huu unaua takribani watoto 30,000 kila mwaka.


27. Nchini Eswatini (Swaziland) katika kila watu 4 kati yao 1 ni muathirika wa UKIMWI.


28. Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na walemavu wengi wa ngozi (albino) kuliko nchi nyingine duniani. Wakati katika mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara ikikadiriwa kuwa mtu 1 katika watu 5,000 hadi 15,000 ana ualbino, kwa Tanzania mtu 1 katika watu 1,500 ana ualbino. Hii inaifanya Tanzania kuwa na watu wengi wenye ulemavu huu wa ngozi kuliko nchi nyingine duniani kote. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. 


29. Misri ni nchi inayoongoza kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watalii kuliko nchi nyingine barani hapa. Inapokea watalii zaidi ya milioni 10 kila mwaka 


30. Bendera ya nchi ya Msumbiji ni bendera pekee barani Afrika kuwa bendera ya taifa yenye silaha aina ya AK-47. Silaha hiyo inaashiria ulinzi wa nchi hiyo. Msumbiji ni nchi pekee yenye bendera yenye silaha ya aina hiyo duniani. Nchi nyingine zenye bendera zenye silaha duniani ni Guatemala na Haiti.


31. Bara la Afrika lilikuwa limeungana na mabara mengine miaka mingi iliyopita, lilitengana na mabara hayo katika kipindi cha kijiolojia (taaluma ya miamba na muundo wa ndani wa dunia) katika kipindi cha kijiolojia kiitwacho Mesozoic.


32. Ustaarabu (Civilization) ulianzia barani Afrika. Misri inapata sifa hii kwa kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa ustaarabu wa kifarao ambao ulianza mwaka 3300 kabla ya Kristo.


33. Shelisheli ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na pato kubwa la taifa (GNP). Pato lake linakadiriwa kuwa takribani dola za marekani milioni  15,400 huku Sudan Kusini ikiwa ndiyo yenye pato dogo zaidi ambalo linakadiriwa kuwa dola milioni 245.9.


34. Jangwa la Sahara ndilo jangwa lenye joto zaidi kuliko yote duniani. Linachukua eneo la mraba takribani milioni 9.1 ya majangwa yote duniani.

35. Kama jinsi ilivyo katika bara la Asia, barani hapa pia watu hutembea takribani maili 3.7 kila siku kutafuta maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.


36. Madagascar ni kisiwa kikubwa kuliko vyote barani Afrika na kisiwa cha 4 kwa ukubwa duniani. Kinapatikana mashariki mwa bahari ya Hindi.


37. Tembo ni mnyama mkubwa kuliko wote duniani na anakadiriwa kuwa na uzito wa tani 6 hadi 7 anapatikana barani Afrika pekee huku Twiga akiwa ni mnyama mrefu kuliko wote dunani naye anapatikana Afrika tu. Pia, mnyama anayekimbia sana kuliko wote ambaye ni Duma anapatikana Afrika pekee huku Mamba akiwa ni mnyama mkubwa kuliko wote katika jamii ya reptilia naye anapatiakana Afrika pekee.


38. Mabaki ya mtu wa kale zaidi yalipatikana barani hapa nchini Ethiopia. Mabaki hayo yanaaminika kuwepo toka miaka laki 2 iliyopita. Charles Darwin alikua akishikilia dai hili lakini lilipingwa na waz
ungu mpaka ilipogundulika katika karne ya 20.

39. Inakadiriwa kwamba takribani watu milioni 12.5 walitekwa barani hapa na kuuzwa katika bara la Amerika kama watumwa kati ya mwaka 1525 hadi 1866.


40. Wakati nchi ya Misri inasifika kwa umaarufu wa kuwa na mapiramidi mengi duniani, Sudan ni nchi pekee yenye idadi kubwa ya mapiramidi hayo ambayo yanakadiriwa kufikia 223 hii ikiwa ni mara mbili ya mapiramidi yote yanayopatikana nchini Misri.


41. Nchini Kenya kuna kabila linalojulikana kama Kalenjin ambalo ni kabila maarufu kwa kutoa wakimbiaji wanaoongoza kwa mbio za riadha duniani.


42. Taasisi ya Elimu kongwe kuliko zote duniani ambayo bado inatumika mpaka leo ipo barani hapa. Taasisi hiyo ni Chuo Kikuu cha Al-Karaouine ambayo iko Morocco. Taasisi hii ilianza kama madrasa na ilianzishwa mwaka 859 baada ya Kristo na ilianzishwa na Fatima Al-Fihri.


43. Takribani 60% ya bara la Afrika ni kame. Sehemu hii inasababishwa na uwepo wa majangwa ya Kalahari, Sahara na Namib.


45. Bara la Afrika lina 30% ya madini yote yanayopatikana duniani.


46. Nigeria ni nchi ya 4 kwa kuzalisha mafuta duniani. Nchi 10 zinazoongoza kwa kuzalisha mafuta barani hapa ni Nigeria, Algeria, Angola, Libya, Misri, Sudan, Guinea ya Ikweta, Congo Brazzaville, Gabon na Afrika ya Kusini.


47. Bara hili lina 40% ya akiba madini ya dhahabu, 60% ya ziada ya madini ya shaba na 90% ya madini ya platini.


48. Zaidi ya 55% ya nguvu kazi ya Afrika wanajihusisha na kilimo cha mazao ya chakula ambayo pia ni sekta inayokuza uchumi barani hapa.


49. Zaidi ya 90% ya udongo wa bara hili sio rafiki kwa kilimo, ni 0.25% ya udongo ambayo ni rafiki kwa kilimo barani hapa.


50. Zaidi ya watu milioni 300 barani hapa wanategemea maji yanayotoka chini kwa matumizi ya kunywa. Maji ni tatizo katika bara hili.


51. Bara la Afrika lina naeneo zaidi ya 3,000 yanayolindwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya utalii duniani. Takribani maeneo 198 ya bahari, maeneo 129 yanayohifadhiwa na UNESCO kama maeneo ya urithi wa kujivunia na maeneo 80 chepechepe (wetland) ambayo ni ni muhimu kimataifa.


52. Afrika ni bara maskini kuliko yote duniani. Pato lake ni 3.1% ya pato lote la dunia kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia.


53. Wayunani wa kale na Warumi walitumia neno Afrika wakimaanisha ukanda wa kaskazini mwa Afrika peke yake. Katika lugha ya kilatini Afrika ina maana ya ~enye hali ya jua. Wayunani wanatambua kama Aphrike wakiwa na maana kwamba ~isiyo na baridi.


54. Afrika ni bara pekee lenye kingo fupi za kanda za pwani licha ya kua bara la pili kwa ukubwa.


55. Katika bara hili wanawake wanakadiriwa kufanya kazi masaa mengi kuliko wanaume. Wanawake hufanya kazi masaa 12 hadi 14 kwa siku barani hapa.


56. Chura mkubwa zaidi kuliko wote duniani maarufu kwa jina la Goliath anapatikana nchini Guinea ya Ikweta.


57. Benin ni nchi pekee duniani ambayo inashikiria rekodi ya kuwa nchi yenye vizazi mapacha kuliko nyingine zaidi duniani. Katika kila vizazi 1,000 nchini Benin 27.9 ni vizazi vya watoto mapacha. Takwimu ya dunia ni utokeaji wa vizazi mapacha 13.6 katika vizazi 1,000.


58. Niger ni nchi inayoongoza kwa kuwa wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuwa na vizazi. Inakadiriwa kua kila mwanamke nchini humo ana watoto 6.62. Burundi ni nchi inayofuatia baada ya Niger ikiwa na 6.04 na hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016 kutoka mtandao wa Statista "The Statistical Portal"


59. Kahun ni jiji la kwanza chini ya mipango miji duniani. Jiji hili lipo nchini Misri. 


60. Afrika ni bara linaloongoza kwa vifo vya Mama na mtoto wakati wa kujifungua.


61. Takribani watu milioni 589 kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi bila umeme. Hii ni sawa na 20% tu wakati 80% wakiishi kwa kutegemea vyanzo vingine vya nishati kama vile kuni na mkaa kwa ajaili ya kupikia.


62. Inakadiriwa kwamba mtoto 1 katika 3 kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika wana utapiamlo.


63. Bara la Afrika linakadiriwa kua na watumiaji wa mtandao (Internet) milioni 453.3 ambao ni sawa na 35.2% ya wakazi wote wa bara hili. mpaka kufikia Desemba 31, 2017 huku kukiwa na watumiaji milioni 177 wa Facebook. Mwaka 2000 bara la Afrika lilikua na watumiaji wa mtandao milioni 4.5. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa mtandao wa Internet World Stats.


64. Nchi zote 54 za bara hili ni nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Morocco iliwahi kujitoa katika umoja huu na baadaye iliamua kurejea tena. Umoja huu ulianzishwa mwaka 1963 kama OAU na baadaye ulibadilishwa kua AU mwaka 2002. Makao yake makuu yapo Addis Ababa, Ethiopia.

65. Bara la Afrika ndilo lenye nchi nyingi kuliko bara lilingine duniani.



Orodha hii imeandaliwa kwa msaada wa mtandao. Haya ni baadhi ya machache kati ya mengi unayopaswa kuyafahamu na ni jukumu lako kutafuta mengine mengi ya kufahamu. Kwa maoni na ushauri niandikie kupitia:
📧 venancegilbert@gmail.com
📞 0753400208.

PREMIER: A POEM BY VENANCE GILBERT FOR CELEBRATING THE WORLD MOTHERS' DAY 2018



Venance Gilbert: A composer of this poem.

Today is a very special day to all Mothers in the World. It is called World Mothers' Day. As one among the people who were raised by a mother, I found an interest in holding a pen and a piece of paper at least to write the few from the collection of what I did as I was growing up and my mother was there for me to make sure that I grow up wisely and intelligently. On March 28, 2017 I completed the long lasting composition of this poem. IT IS VERY SPECIAL FOR MY DEAR MAMA FLORENTINA AND ALL MOTHERS' IN THE WORLD. May be your mother has passed away (sorry for the loss) but due to spiritual faith, we believe that the resting mothers in heaven can hear our voices, so you can also recite the poem for your mom and she will hear you in one way or another. The poem is called Premier. I welcome you once again to this field of language use. I have hired a very simple language in composing this poem, it is very understood and straightforward:

Poem: Premier
Poet: Venance Gilbert
Composition: March 28, 2017

My premier
That genuine premier of me
I say genuine since he skilled me to be material
Premier I know you are delighted of me
Your harvest is gratified of you most
My premier, my duplicate
You accentuate me to premise on goodness
Those generations when I operated capricious
Honorably your pampering is now honoured
Not only me some folks also say
But premier they never be fluent in it loud
In a nutshell this blameless make-up ensued after you
And this is why I say you are packed with conceit.

Premier
Into blackness and perky you hiked
Probably some are uncovered in this
But them handier certainly not branded this
Premier you are the only that Supernatural being gifted me
Your depth gloss upon me like not any gilt
And I see your craving never catch antediluvian
Above and beyond it is protracted fixed interminably
Just like no one can sort out healthier than you
This has building I for one I am at the moment
What else can I for one say? I hearting you premier.

I dredge up those generations I was vulgar
Those livings when the deeds was unworldly
I also hark back to the switch into teens
A tick when I operated sagacious
Premier you performed in conformity with the phase
You drafted the role and set me on the route
I was half-hearten but you never let that alive in me
If you could leave me, who else would carry me delicately?
Undeniably, Not any. I treasure you premier.

Premier
Where I wailed you also get in
Just to spectacle that the realm was not only mine
And when entirety put me downcast
You battled my angle, you bout for me
Your maws could voice to me devotedly
If you give up I will despond
Be solid I am with you to soar the massif
And we scrabbled collectedly directioning to the ultimate
And our flight was at least efficacious
God, take the appreciations for the exquisite premier

Premier
In our day as I let my big hand ink about you
I summon up those beings you contended on hard working
At the phase I didn’t grasp but you adage for me
My produce work, work hard, work as you can
If you work, you have a warranty to live healthier
The troop will worth your being there in time off
But if you no toil, publics will be drowsy of you
Thank you premier, I grasp it in their gates.

Premier
Our life-cycle is an encyclopedia
There is no way it apt the lone script
I set aside those archetype existences you stressed
You lodged the rising germs inside me
And their fruit is seen in prospect
Premier, I worth how you upturned me
I upkeep and pledge to animate in noble
Sometime I wish to amend the wheel
To reword the deportment, but you discern
That I was just on the rise, thank you premier one.



Thank you for taking time and interest in reciting this 6 stanzas poem. If you have anything to comment or advice please leave your comment below or you can write to me through:
 ðŸ“§ venancegilbert@gmail.com
📞 0753400208.

ZIJUE FAIDA NA HASARA ZA KUWA NA AKAUNTI BINAFSI "PRIVATE" KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM


Uhali gani mpenzi msomaji wa segment yetu ya Fahamu? Nakukaribisha katika segment yetu ya kila siku ya Fahamu, kama ilivyo kawaida, hapa nakufahamisha mambo kadhaaa ambayo labda hukuyafahamu ama uliyafahamu ila si kwa kina basi huwa nakufahamisha hapa. Kumekuwepo na akaunti nyingi binafsi hasa hasa zile za watoto wa kike kwenye mtandao wa Instagram. Kuna faida na hasara za kuweka akaunti yako kuwa binafsi na hasara zake pia. Leo nakuletea mada kuhusu faida na hasara za kuwa na akaunti binafsi ambazo hizi ndizo zinazotofautisha kua na akaunti huru na binafsi:
Related image
Huu ni mfano wa akaunti binafsi ya Instagram ukiitembelea
FAIDA ZAKE
1. KUA NA MAMLAKA YA KURUHUSU AMA KUTORUHUSU NANI AKUFUATE
Unapaokuwa na akaunti private ya instagram basi unakua na uwezo wa kuamua mwenyewe kwamba nani akufuate (following) na nani asikufuate kwa mfano unaweza kuzuia watu ambao ni wanafamilia ikiwa akaunti yako ina mambo yako ya siri lakini hii haizuii wao kuangalia kwa maana bado wanaweza kutumia majina usiyoyafahamu. Kila anayetaka kua mfuasi wako anapata ruhusa kutoka kwako kabla ya kua mfuasi. Huu ni usalama binafsi kwa namna moja ama nyingine.

2. INAZUIA MUINGILIANO NA MITANDAO NA TOVUTI NYINGINE
Unapokuwa na akaunti binafsi unazuia muingiliano wa mitandao mingine na tovuti nyingine kwa mfano muingiliano wa tovuti nyingine hii inakupunguzia uwezo wa kupata wafuasi wapya kwa maana.

3. INAZUIA WATU KUDOWNLOAD PICHA NA VIDEO UNAZOWEKA
Hii kwa namna moja ama nyingine inaweza kua ni faid na pia hasara kwa namna nyingine. Instagrama inazuuia uwezo wa watu kudownload picha na video zako kama akaunti yako ni private hii inatokana na kufunga link ya kudownload. Hii ni kwa wafuasi wako kwa maana ndiyo wenye uwezo wa kuiona akaunti yako.

4. INAZUIA WATU KUWAONA WAFUASI WAKO NA WALE ULIOWAFUATA
Kama bado hujakubaliana na ombi la mtu kukufuata inakua ni vigumu kwa yeye kuwaona wafusai wako hii ni kwa sababu sera ya faragha inazuia isntagram kutoa taarifa zako kama hizi; wafuasi na uliowafuata, picha na video zako lakini hii haizuii wasifu wako (bio) kutoonekana.


HASARA ZAKE
1. INAKUPUNGUZIA IDADI YA WAFUASI
Wapo watu ambao kwa namna moja huja kwenye akaunti yako kuangalia picha na video unazoweka ili wakufuate mtandaoni hapo hivyo wanapokuta akaunti yako ni binafsi na kutoona taarifa zako kama vile picha na ama makala zako basi wanaamua hata kutokukufuata kabisa. Kuna wakayti unashea na watu picha yako katika mitandao ya Facebook na Twitter na hivyo watu wakavutiwa na kukufuata lakini wanapokuta aaunti yako ni binafsi wanaamua kuachana na akaunti yako.

2. INAPUNGUZA MUINGILIANO
Unapokua na akaunti binafsi unapunguza uwezo wa watu kuingiliana na akaunti yako kwa mfano kupata watembeleaji wapya, kufanya biashara na watu kupitiaa Instagram na hata kufanya matangazo na mtaandao wa Instagram (Sponsored links) Ni lazima iwe akaunti huru kwa umma ili uweze kupata miingiliano kama hii na mingineyo.

3. INAKUPUNGUZIA WATEJA KAMA NI AKAUNTI YA BIASHARA
Kama wewe ni mfanya biashara na akaunti yako unaiendeza kwa msingi wa kuwa akaunti binafsi fahamu kwamba unapunguza idadi kubwa sana ya wateja yako. Hii inafanya watembeleaji wapya wasiwe na uwezo wa kuziona picha zako za matangazo ya biashara. Instagram ni mahala pazuri sana kutangaza biashara yako kwa vile inaruhusu picha na maelezo yake.

4. INACHOSHA KUPITIA MAOMBI YA WATU WANAOTAKA KUKUFUATA
Inaweza kua suala la kawaida kupitia maombi ya watu wanaotaka kukufuata lakini ni usumbufu pia na inachosha kupitia maombi yote has pale idadi ya watu wanaotaka kukufuata inapokuwa kubwa. Unapokua na akaunti huru unapata tu taarifa kwamba mtu fulani kakufuata basi.


Kwa Maoni na Ushauri wasiliana nami kwa moja kati ya njia hizi:
Barua pepe: venancegilbert@gmail.com
Simu: 0712586027 (na WhatsApp pia) na 0753400208.

ALI KIBA - MVUMO WA RADI WATCH VIDEO & DOWNLOAD MP3


Ali Kiba ameachia audio na video ya Wimbo wake mpya Unaoitwa Mvumo wa Radi.

Kudownload audio    BOFYA HAPA

Kudownload video    BOFYA HAPA


Kutazama video hii hapa chini



GOODALL MWANASAYANSI WA AUSTRALIA (104) AMEJITOA UHAI WAKE NCHINI USWISI

David Goodall 
Mwanasayansi David Goodall, 104, aliyesafiri kutoka Australia hadi Uswisi ili kujitoa uhai amefariki katika kliniki moja nchini Uswisi, shirika linalotetea haki za watu wanaotaka kufa limetangaza.

Mwanaikolojia huyo ambaye pia alikuwa mtaalamu wa mimea hakuwa anaugua lakini alisema aliamua kujitoa uhai kutokana na kudhoofika kwa 'ubora wa maisha yake'.
Image result for david goodall
Goodall mwaka 1984 enzi za ujana.
Bw Goodall alikuwa amezua mjadala kutokana na safari yake ya kutoka Australia kwenda kujitoa uhai.
Muda mfupi kabla ya kifo chake, alisema alikuwa na "furaha kuhitimisha" maisha yake.

"Maisha yangu yamekuwa dhaifu sana kwa mwaka mmoja hivi uliopita na hivyo basi nina furaha kuyahitimisha," alisema akiwa amezingirwa na jamaa wake kadhaa.

"Nafikiria, kuangaziwa kwa kisa changu kutachangia kutetea haki za wazee kuruhusiwa kujitoa uhai, jambo ambalo nimekuwa nikitaka."

Mtazame Goodall katika video hii hapa chini:



Alifariki mwendo wa saa sita unusu mchana katika kliniki ya Life Cycle mjini Basel baada ya kudungwa sindano ya Nembutal, kwa mujibu wa Philip Nitschke mwanzilishi wa shirika la Exit International lililomsaidia kujitoa uhai.

"Najuta kufika umri huu," Dkt Goodall alisema mwezi uliopita katika sherehe ya kuzaliwa kwake, katika mahojiano na shirika la utangazaji la Australia.
Image result for david goodall

"Sina raha. Nataka kufa. Sio jambo la kuhuzunisha, kinachohuzunisha ni kwamba mtu anazuiwa kufa."
Ni jimbo moja pekee Australia lililohalalisha kujitoa uhai mwaka jana kufuatia mjadala mkali uliozusha mgawanyiko, lakini ili mtu kuruhusiwa, ni sharti awe anaugua mahututi.

Je ni mataifa gani mengine yanaruhusu kujitoa uhai?

  • Uswizi, ni nchi pekee iliyo na vituo vinavyotoa huduma hiyo kwa raia wa mataifa mengine.
  • Uholanzi, Ubelgiji na Luxembourg zinaruhusu, hata kwa watoto lakini katika hali maalum.
  • Colombia inaruhusu kujitoa uhai kwa hiari wakati mgonjwa akiwa hatibiki.
  • Majimbo sita ya Marekani - Oregon, Washington, Vermont, Montana, California na Colorado - yannaruhusu kwa wagonjwa mahututi wasio tibika.
  • Canada ililifuata jimbo la Quebec kuruhusu hilo mnamo 2016.
    Jamaa zake Goodall watajumuika naye huko Uswizi
    Jamaa zake Goodall walijumuika naye huko Uswisi kabla ya kifo chake.

Mjadala unazua mgawanyiko Afrika

Katika nchi nyingi tu Afrika, njia zote za kujitoa uhai zinatizamwa kama mauaji. Wataalamu barani Afrika wamepinga wito wa watu kutaka kujitoa uhai kwa hiari. Mjadala mkubwa umezuka kuhusu kinachotajwa kuwa 'kuuawa kwa huruma' hususani kwa wagonjwa walio mahututi na wasioweza kutibika

Lakini mkutano wa muungano wa wataalamu wa afya duniani katika mkutano mapema mwaka huu mjini Abuja Nigeria waliamua kwamba hatua hiyo inakwenda kinyume na kiapo cha matabibu na inakwenda kinyume na imani na maadili ya jamii za Kiafrika badala yake viongozi katika muungano hao wametaka kuboreshwa kwa huduma za kuwashughulukia wagonjwa mahututi wasioweza kutibika.

Masuala yaliozingatiwa katika kuptisha uamuzi huo ni sheria, dini, jamii na tamaduni, saikolojia na upana wa maadili kuhusu suala hilo. Wataalamu wa mataifa kutoka Afrika kusini, Kenya, Botswana, Zambia na Cote D'ivore (Ivory Coast) walipinga hoja hiyo ya kujitoa uhai kwa hiari wakisisitiza inakwenda kinyume na maadili ya utoaji matibabu.


 Chanzo: BBC

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI ATIMIZA MIAKA 93: TUJIKUMBUSHE HISTORIA YAKE KWA UFUPI

Mei 8, 1925 wkati huo Tanganyika ikiwa ni koloni la Uingereza alizaliwa Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mzee Ali Hassan Mwinyi.

Image result for MWINYI in marathon 

Alipoingia madarakani kumpokea aliyekuwa Rais wa Awamu ya kwanza,Mwalimu Julius Nyerere mnamo tarehe 5 Novemba mwaka 1985, watanzania wachache sana (kama wapo) waliweza kutabiri kwamba miaka kumi baadaye na zaidi baada ya kustaafu rasmi, ataibuka kuwa mmojawapo wa maraisi wa Tanzania ambao watabakia kupendwa na kuheshimika kwa namna ya kipekee kabisa. Tunadiriki kusema “namna ya kipekee” kwa sababu ukweli unabakia kwamba inapofanyika tathmini ya uongozi wake, bado mtu au watu mbalimbali wanakuwa na maoni yao tofauti tofauti kuhusiana na suala hilo. Utoaji huo wa tathmini ni suala ambalo haliwezi kukoma leo wala kesho, ni tukio linaloendea na litakaloendelea, vizazi mpaka vizazi. Huo ndio uzuri au ubaya wa historia na muda (history and time) huwa vina jinsi ya kipekee katika kutoa hukumu zao.

Mpaka anakabidhi madaraka yake ya Urais kwa Rais wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa mnamo tarehe 23 November mwaka 1995, jina ambalo wengi tulipenda kulitumia ni “Mzee Ruksa” ingawa kamwe hatukuwahi kusahau kwamba jina lake kamili ni Ali Hassan Mwinyi, Raisi wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Ali Hassan Mwinyi alizaliwa tarehe 8 mwezi wa tano (Mei) mwaka 1923 katika kijiji cha Kivure,wilayani Kisarawe, mkoa wa Pwani,Tanzania Bara. Kama wengi wa viongozi wetu, Mwinyi naye alizaliwa katika iliyokuwa Tanganyika. Akiwa bado mwenye umri mdogo sana familia yake ilihamia Zanzibar. Kwa maana hiyo Mwinyi ni mzaliwa wa bara aliyekulia na kuendelea kuishi visiwani Zanzibar.

Alianza safari yake kielimu huko visiwani Zanzibar katika shule ya msingi Mangapwani kuanzia mwaka 1933 hadi 1936 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Dole kwa ajili ya elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1937 mpaka mwaka 1942. Baada ya hapo alijiunga na Chuo Cha Ualimu Zanzibar kusomea ualimu kuanzia mwaka 1943 mpaka 1944.
Mwinyi katika picha rasmi ya wakati wa utawala wake.

Kuanzia mwaka 1945 mpaka mwaka 1950 alirejea tena katika shule ya Mangapwani,shule aliyosomea,safari hii akiwa sio mwanafunzi tena bali Mwalimu.Kuanzia mwaka 1950 mpaka 1954 alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo wakati huo huo alikuwa akiongeza elimu yake kwa njia ya posta ambapo alijipatia General Certificate in Education (GCE) na pia alikuwa amejiunga na Durban University Institute of Education, United Kingdom (kwa njia ya posta tena) kusomea stashahada ya ualimu. Baada ya hapo alijiunga tena na Chuo Cha Ualimu Zanzibar kama mkufunzi kuanzia mwaka 1956 mpaka mwaka 1961 huku pia akiendelea kujisomea kwa njia ya posta kutoka Regent Institute kilichopo London nchini Uingereza ambapo alijipatia cheti cha ufundishaji lugha ya kiingereza.

Kuanzia mwaka 1961 mpaka 1962 alijiunga na Hall University, Uingereza katika Tutors’ Attachment Course. Mzee Mwinyi pia ana cheti ya lugha ya kiarabu alichokipatia Cairo nchini Misri kati ya mwaka 1972 na 1974.

Safari yake ya kisiasa aliianza rasmi mwaka 1964 alipojiunga na Afro Shiraz Party (ASP) huko Zanzibar ambapo alikitumikia chama katika ngazi na nafasi mbalimbali. Kati ya mwaka 1964 na 1965 alikuwa ni Katibu Mkuu wa muda katika wizara ya elimu Zanzibar kabla hajateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi katika iliyokuwa Zanzibar State Trading Corporation (ZSTC).Hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1965 na mwaka 1970. Pia katika miaka hiyo hiyo,kuanzia mwaka 1966 mpaka 1970, Mwinyi alikuwa mweka hazina msaidizi katika tawi la ASP la Makadara,Zanzibar. Wakati huo huo pia kati ya mwaka 1964 mpaka 1977 alikuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)
Majukumu mengine aliyokuwa nayo miaka hiyo ni pamoja na uenyekiti wa Zanzibar Censorship Board (1964-1965), Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na pia mwenyekiti wa Baraza la Chakula na Lishe.

Mwinyi (kushoto) akiwa na maraisi wenzake wastaafu Benjamini Mkapa (kulia) na Jakaya Mrisho Kikwete (katikati)

Kuanzia mwaka 1972 mpaka 1975, Mwinyi alikuwa ni Waziri wa Afya wa Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia 1975 mpaka 1977. Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri cheo alichokitumikia mpaka mwaka 1982 aliporejea nyumbani na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii cheo ambacho alikutumia kwa muda mfupi tu kwani mwaka 1983 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Raisi.
Mwaka 1984, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Raisi wa Zanzibar wakati huo,Alhaj Aboud Jumbe, Mwinyi alichaguliwa kuwa Raisi wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na wakati huo huo Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuanzia mwezi August mwaka huo huo wa 1984 Mwinyi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi cheo alichoendelea nacho mpaka mwaka 1990 baada ya kung’atuka kwa Hayati Mwalimu Nyerere kutoka katika kukiongoza Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Mwinyi (wa pili kutoka kushoto) akishuhudia mchezo wa bao kati ya hayati Mwalimu Nyerere (wa pili kutoka kulia) na mzee mmoja wa Butiama(jina halijulikani).Wengine wanaoshuhudia ni Mama Maria Nyerere(kulia) na kaka yake Nyerere,Chief Burito(wa tatu kutoka kulia).Picha ilipigwa Butiama.

Lakini kabla ya hapo, mwaka 1985,Mwinyi alichaguliwa kuwa Raisi wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kustaafu kwa Mwalimu Nyerere. Mwinyi ni mtaalamu wa lugha ya Kiswahili na pia hupenda michezo hususani jogging. Mwinyi ameoa wake wawili (Sitti Mwinyi na Khadija Mwinyi), ana watoto na wajukuu. Anaishi Msasani jijini Dar-es-salaam.

Related image
Rai mstaafu Mwinyi akiwa na wastaafu wenziye Mkapa, Kikwete na Rais Magufuli. Picha kwa hisani ya Mwananchi Communication Limited.
MAKALA HII NI HAKIMILIKI YA JEFF MSANGI MWANDISHI WA TOVUTI YA BONGOCELEBRITY.

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda.

Zaidi ya watu milioni 15 katika bara hili huitumia lugha hii kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya Muungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika.

TANZANIA

Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa.
Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVITA, TATAKI (zamani TUKI pia TAKILUKI) na UKUTA. Pia vyuo vikuu mbalimbali vya Bara na Visiwani vilianza kufundisha Kiswahili kuanzia Shahada za Awali, Uzamili na Uzamivu kama vile Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha TanzaniA, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino n.k.

KENYA

Kiswahili nchini Kenya ni lugha rasmi na pia ni lugha ya Taifa. Rais wa kwanza wa taifa la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta alitoa kauli kwamba Kiswahili kinafaa kutumika kama lugha rasmi ya Kenya mwaka 1969. Mwaka 1975 kiswahili kilianza kutumika bungeni.Serikali ya Kenya ilianzisha somo la Kiswahili katika Idara ya Lugha za Kiafrika na Isimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Kuanzia miaka ya themanini mwishoni, takribani vyuo vikuu vyote vilivyoanzishwa na Serikali vilifundisha masomo ya Kiswahili kwa lugha ya hii.

UGANDA

Mwaka 1960, Serikali ya Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo. Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima. Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro hata kabla ya ukoloni mwaka 1862. Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.
Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi.
Wikendi hii Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, Keneth Cimara imeipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Katika warsha ya siku mbili iliyokamilika mwishoni mwa juma katika hoteli ya Imperial Royal mjini Kamapla iliyowajumuisha walimu wa vyuo vikuu, shule za upili na taasisi mbalimbali nchini Uganda.
Keneth Cimara amesema miaka ya themani raia wengi wa Uganda walikiona Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwanyanganya mali zao, aidha kuwatendea uhalifu.
Cimara ameongeza kwamba sasa Serikali ya Uganda ni miongoni mwa mataifa ya Jumuia ya Afrika Mashariki ambayo yameweka mikakati ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahi kama anavyosema tena Katibu mtendaji.


RWANDA

Kiswahili ni lugha rasmi nchini Rwanda. Kabla ya mwaka 1994, wakati wa mauaji ya kimbali lugha ya kiswahili ilizungumzwa kwenye miji tofauti nchini Rwanda.
Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.
Mwaka wa 1976-1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule za upili na chuo Kikuu Cha Rwanda

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Kiswahili kiliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya 19. Kiswahili kilianza kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo, kuelekea kandokando ya mto Kongo.

Pia kuna wazungumzaji wachache katika nchi za Burundi, Msumbiji, Comoros, Malawi , Madagascar na Zambia.


Chanzo: BBC

MIAKA 5 YA VENANCE BLOG NAWASHUKURU SANA KUWEPO HAPA TANGU KUANZISHWA KWAKE MEI 2013

VENANCE BLOG ilianzishwa Mei 2, 2013.

Alhamis ya tarehe 2 Mei, 2013 nilitimiza kiu yangu ya kufungua Blog hii, lilikuwa ni wazo lililoishi toka mwaka 2012 nilipoanza kufahamu matumizi ya mtandao na tarehe hiyo lengo hili lilitimia. Huu ni mwaka wa 5 sasa nikiwa katika tasnia hii.

Kuna wakati majukumu ya kitaaluma shuleni yanakaba sana mpaka nashindwa kuwa active kutokana na kufanya kazi hii nikiwa bado masomoni toka mwaka 2013 mpaka sasa.

Kuwepo kwa Blog hii kumesaidia baadhi ya watu kupata taarifa na habari nyingine kwa mfano zile za kielimu hasa wakati wa selection za vyuo vikuu. VENANCE BLOG imekua msaada kwa baadhi ya watu, nimekua nikiwapa taarifa za habari hizi hasa wale walio katika mazingira ya kutokua na access ya mtandao.

Pamoja na mengine mengi kama haya nimekua nikiitumia Blog hii kama platform ya kuchapisha mashairi yangu ambayo nimekua nikiyaandika kwa nyakati tofauti tofauti. Nawashukuruni sana wasomaji wangu kwa kutembelea Blog hii na kuyasoma mashairi hayo na pia kutumia muda wenu kutoa maoni kadiri inavyowapendeza. Asanteni sana.

Aidha nimekua nikiandika habari za kitaifa, kimataifa, siasa, udaku, nyimbo mpya, video mpya, habari za masuala ya anga, Teknolojia, Michezo, nimekua nikiandika pia nukuu kutoka kwa wanafalsafa wakubwa dunia na watu wengineo kama vile wanasiasa, wanamuziki, wanaharakati wa masuala tofauti tofauti n.k. Aidha nimekua nikiandika habari za mitindo na mambo mengine kadha wa kadha.

Habari, Picha, Matukio na mambo mengine ninayoyachapisha hapa nimekua nikipitia kwa ukaribu katika vyanzo makini kama vile Habari Leo, Mwananchi, BBC, DW, VoA, Jarida la Mitindo la Vogue, Forbes, Kitabu cha kumbukumbu cha rekodi za dunia Guinness, Blogs za watu binafsi, taasisi na kadhalika.

Katika mwaka huu wa 5 naahidi kuendelea kufanya kazi hii kwa ukaribu kabisa na watu, moja ya mpango wa hivi karibuni ni kuanza kuandika habari za matangazo ya kazi pamoja na kuongeza zaidi taarifa za nafasi za masomo ya nje ya nchi (scholarship) ambayo hii tayari nimeanza kuifanyia kazi. Pia kuna mengine mengi yanakuja katika Blog hii. Endelea kufuatilia VENANCE BLOG na nakushukuru sana kuendelea kuwa msomaji wa Blog hii.


Kwa maoni na mengineyo, wasiliana nami kwa moja kati ya njia hizi:
barua pepe: venancegilbert@gmail.com

Simu ya mkononi: 0753400208.