OBAMA AWATAHADHARISHA WAPIGA KURA KUHUSU TRUMP

Rais Barrack Obama amewahimiza wafuasi wa chama cha Democratic kumpigia kura Hillary Clinton na kuonya kwamba Donald Trump ni tishio kwa haki za kijamii, taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla.


Rais wa Marekani Barrack Obama amewahimiza wafuasi wote wa chama cha Democratic kumpigia kura kwa wingi Hillary Clinton siku ya uchaguzi wiki ijayo na kuonya kwamba Donald Trump mgombea urais wa chama cha Republican ni tishio kwa haki za kijamii ambazo ziliafikiwa kupitia hali ngumu , taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla.

Akigusia chaguo la rais siku ya Jumanne wiki ijayo, rais Barrack Obama alimpuuzilia mbali Trump kuwa mtu asiyestahili kabisa kuwa rais.

Kufikia sasa Clinton bado anaonyesha uwezekano wa kuwa rais wa 45 wa Marekani lakini huku zikiwa zimesalia siku sita kabla ya uchaguzi huo mkuu, wafuasi wa chama cha Demokratic bado wako chonjo hasa kutokana na mienendo ya Trump isiyotabirika.

Obama aliwaambia wapiga kura katika mji wa Chapel Hill kuwa hatima ya taifa hilo imo mikononi mwao . Aliongeza kwa kusema, „"hatima ya dunia inawategemea nyinyi, wapiga kura wa North Carolina itawabidi kuhakikisha munachukuwa hatua katika mwelekeo bora."

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton

Wikileaks yaendelea kutoa barua pepe

Huku kampeini hizo zikipamba moto, barua pepe nyingine za siri zinazomhusu Hillary Clinton zilitolewa hapo jana na mtandao wa wikileaks unaofanya udukuzi na kuchapisha taarifa za siri, hizi zikiwa sehemu ya barua pepe zinazotolewa na mtandao huo kila siku tangu mwezi uliopita.

Mtandao huo umesema kuwa unanuia kutoa barua pepe hizo zilizoibwa kutoka kwa akaunti ya mkuu wa kampeini ya Hillary Clinton , Podesta kila siku katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Hata hivyo msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani John Kirby alisema hapo jana kuwa wizara hio haitatoa taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo ya stakabadhi zilizoibwa lakini akasema kuwa juhudi za wizara hiyo za kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vya habari kuhusiana na kipindi cha kuhudumu kwa Hillary katika wizara hiyo mara nyingine ilihitajika kuwasiliana na waakilishi wake kuhakikisha kuwepo kwa usawa.

Kundi la kampeini la Clinton hata hivyo limekuwa likionya kuwa mtandao huo wa wikileaks umeharibu barua pepe zilizoibwa na wadukuzi ambao huenda wanafanyia kazi serikali ya Urusi.

Chanzo: DW

MAJINA YA MKOPO MZUMBE MWAKA WA KWANZA 2016/2017 HAYA HAPA


Chuo Kikuu Mzumbe kimetoa majina ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza walionufaika na Mkopo wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017. 

Ili kuona majina haya kwa simu hakikisha una Office App kwenye simu yako (WPS Office, OfficeSuite ama Polaris Office n.k.)


MAJINA YA WALIOCHAGULIWA MZUMBE AWAMU YA TATU HAYA HAPA (BATCH/ROUND 3)

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Chuo Kikuu Mzumbe, imetoa majina ya waliochaguliwa chuoni hapo kwa awamu ya tatu (Third Batch/Round)

Tumia mojawapo kati ya Browser hizi kuangalia selection hizo; UC Browser, Mozilla Firefox, Google Chrome au Dolphin Browser, Opera Mini haitaonesha baadhi ya vipengele katika kudownload majina haya. Link itakupeleka moja kwa moja juu kabisa kutakuwa na mshale wa kupakua majina hayo, bofya hapo na majina yatashuka moja kwa moja.

👉BOFYA HAPA KUONA NA KUDOWNLOAD MAJINA👈

HAYA HAPA MAJINA YA HOSTEL MZUMBE MWAKA WA KWANZA (JINA LA HOSTELI NA NAMBA YA CHUMBA)

Haya hapa majina ya Hosteli mwaka wa kwanza Mzumbe (Jina la Hosteli pamoja na namba ya Chumba unachotakiwa kuishi) 

RAIS MAGUFULI AAHIDI KUENDELEA KUTOA MIKOPO 2016/2017 KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NA KUTOA RAI SUALA HILO KUSHUGHULIKIWA

Tokeo la picha la magufuli udsm leo oktoba 21

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kwa nafsi yake ametoa matumaini kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini kuhusu hatima yao ya mkopo wa Elimu ya Juu alipokuwa akihudhuria sherehe ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Rais Magufuli amebainisha haya, namnukuu;

"Tunapopitia katika challenge hii muivumilie serikali kutengeneza utaratibu ulio mzuri, ninafahamu, katika bajeti ya mwaka 2015/2016, fedha iliyotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa sababu Mh. Waziri umezungumza hapa zilikuwa bilioni 340 ambazo  zilikjuwa zinatosha karibu wanafunzi tisini elfu (90,000)  baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani  ili kutimiza yale tuliyokuwa tumeahidi tuliongeza fedha hizo za mkopo hadi kfikia bilioni 473 bajeti ilikuwa ya bilioni 340 tukaongeza zikafika bilioni 473 kutokana na makusanyo na tukaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi 124,358 mwaka huu ameeleza ni zaidi ya bilioni 483 zimepitishwa katika bajeti  kwa hiyo wanafunzi wengi zaidi watapata mkopo ninafahamu kwa mfano wanafunzi wanaoendelea ambao wako karibu 93,000 wote wamekuwa accommodated kwenye mkopo pamoja na wanafunzi wapya ambao nafikiri ni zaidi ya 25,000 lakini ni lazima kweli nikiri hapakuwepo na coordination palitakiwa kwanza vyuo vyote vya elinu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua kwa sababu wapo wengine walifungua mwezi mzima uliopita wako wengine wamefungua jana wako wengine watafungua keshokutwa ukishafungua haraka haraka wanafunzi wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawambia kufanya registration lazima walipe wakati Bodi ya Mikopo haijatoa orodha ya majina ya vijana ambao watakaokopeshwa ni contradiction.

Palikuwa pawepo na communication kati ya Bodi ya Mikopo sijui ni TCUsijui ni nani, Wizara ya Elimu na Wizara ya Fedha kwamba katika orodha ya wanafunzi watakaopata mikopo ni hawa hapa majina yao ni haya hapa mnapeleka majina hayo na orodha, amount ya fedha zinazotakiwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Fedha nao wanaprocess zao fedha hizi tunazitoa baadaye zikishapelekwa kwenye benki kwenye hizo akaunti za wanafunzi, mngeweza mkafungua vyuo hapakuwa na sababu ya kufungua mwezi mzima kabla wanafunzi wanakaa pale hajui kama atapata mkopo au hatapata mkopo halafu unamwambia hakuna registration  kwa sababu hujapata mkopo inaleta usumbufu wa ajabu, na hilo.

Nitoe wito kwa Wizara ya Elimu na hili nasema kwa dhati lengo la serikali si kuleta usumbufu kwa wanfunzi  lakini ni ukweli pia kwamba haitatoa mikopo kwa wanafunzi ambao wenye uwezo unamkuta mtoto wa Profesa Rwekaza na wewe upate mkopo mtoto wa Ndalichako naye apate mkopo mtoto wa Katibu Mkuu Kijazi naye apate mkopo haiwezekani mkopo huu umelenga kwa ajili ya kutoa watoto masikini lakini nafahamu na ninasikia hata katika Bodi ya Mikopo kule kuna upendeleo upendeleo wa aina fulani katika kutoa mkopo hata ambao hawastahili wanapewa mikopo na ambao hawastahili wananyimwa mkopo sasa hili Waziri na Bodi zinazohusika mulisimamie sitaki siku moja nije huko kwenye Bodi ya mikopo nichukue orodha ya wanafunzi wote niangalie shule walizosoma na particulars walizozijaza halafu nije nipewe majina ya watu ambao hawakustahili kupewa mkopo wanafunzi 25 wa mwaka huu siwezi kushindwa kusoma kwa siku 1 ntapekua page by page 25,000 ukigawa kwa masaa 12 ambayo naweza nikajifungia kila jina naweza nikalisoma kwa sekunde ngapi ninajua naweza, sasa tusifikie huko.

Ninashukuru Waziri baada ya kuona hii changamoto ukawa umelileta hili suala haraka haraka na tukatoa instruction Wizara ya Fedha watoe bilioni 80 za mwanzo haraka haraka na nimeambiwa zimeshatolewa, sasa niwaombe wanafunzi msiwe na haraka haraka kwa sababu katika changamoto hizi ambazo zinapita ndani ya serikali wanafunzi hewa, mikopo hewa, mishahara hewa hatutaki hela yetu ipotee ovyo pameshatokea changamoto na najua haitatokea tena vyuo vikuu vitakuwa vinafunguliwa siku ambapo wana uhakika na fedha zitakuwa zimeshapelekwa kwenye wanafunzi.

Lakini pia pamekuwa na utitiri mwingi mno wa vyuo vikuu unakuta shule ilikuwa inaitwa sekondari leo ukisoma kwenye orodha nayo inaitwa Chuo Kikuu na saa nyingine inafikia wanafunzi unaanza kuwagombania, Chuo Kikuu kwa mfano cha Dodoma kina capacity ya kuweka wanafunzi mpaka 45,000 waliopo ni 30,000 lakini unakuta kinafunguliwa chuo kingine Bagamoyo kina wanafunzi 20 mabweni hayapo maabara hayapo natoa mfano tu labda nimesema Bagamoyo kingine kinafunguliwa Chato.

Sasa ninachotaka kutoa wito kwa Bodi, TCU, Wizara hebu mpitie vizuri hivi vyuo mnatoa vibali mnatoa vibali mno vya kuanzisha chuo kikuu kila mahali wakati vyuo vilivyopo havijajaa watu na mnawachanganya saa nyingine hawa watoto kwa sababu mnakuwa mnawagombania, na vyuo vikuu vingine havina walimu unakuta mwalimu leo yuko  Dar es Salaam kesho yuko Mbeya keshokutwa yuko Iringa keshokutwa Moshi ataconcentrate namna gani kufundisha kwa hiyo matatizo haya mengine yameletelezwa na nyinyi mnnaopendwa kuitwa maVice Chancellors wenye vyuo vilivyopo sijasema wewe (akimaanisha Prof. Rwekaza, VC wa UDSM) kwa hiyo nikuombe Waziri simamia hili, kwanu kuna ubaya gani tukiwa hata na vyuo vikuu vinne tu kila chuo kina watu milioni moja moja watu wako palepale wanalipwa mshahara mzuri na wanaconcentrate vizuri."


KWA MSAADA KUTOKA KWA MWANAFUNZI ALIYEFATILIA SPEECH HII CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NA KUSAMBAZA KWA WATANZANIA.

MFAHAMU HILLARY CLINTON KWA MAMBO HAYA 15

Tokeo la picha la hillary clinton
Jina Kamili: Hillary Diane Rodham Clinton
Kuzaliwa: Oktoba 26, 1947
Alikozaliwa: Chicago, Illinois

Kwa Ufupi

Alipochaguliwa kuwa Seneta mwaka 2001 alikuwa mwanamke wa kwanza First Lady kuwa mtumishi wa serikali. Baadaye alikuwa Katibu Mkuu wa Ikulu ya Marekani mwaka 2009 akitumikia wadhifa huo hadi mwaka 2013 katika utawala wa Rais Barrack Obama. Mwaka huu (2016), amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha The Democratics.

Tokeo la picha la hillary clinton
Hillary alizaliwa  Oktoba 26, 1947 huko Chicago, Illinois. Alipata Shahada yake ya Sheria kutoka Yale University. Alifunga ndoa na mwanafunzi mwenziye aliyekuwa akisoma sheria Bill Clinton mwaka 1975. Baadaye alitumikia taifa la Marekani kama First lady  mwaka 1993 hadi 2001, na baadaye akiwa Seneta mwaka 2001 hadi 2009. Mapema mwaka 2007 Clinton alitangaza kugombea Urais nchini Marekani. Katika kura za maoni mwaka 2008 alichuana na Barrack Obama lakini kura hazikumruhusu kugombea Urais kwa ticket ya Democratic. Rais Obama alipoingia madarakani alimchagua kuwa Katibu Mkuu mwaka 2009 hadi 2013.

HillaryRodham ni mtoto  mkubwa katika familia ya Hugh Rodham na Dorothy Emma Howell Rodham. Ana wadogo zake wawili wanaume; Hugh Jr. aliyezaliwa 1950 na Anthony aliyezliwa 1954.

Kama kijana Hillary aliingia katika siasa na kumfanyia kampeni mgombea wa chama cha Republican Barry Goldwater mwak 1954. Alivutiwa kufanya kazi za umma baada ya kusikia hotuba ya Martin Luther King Jr. huko Chicago na hapo alijiunga na chama cha Democratic mwaka 1968.

Elimu

Tokeo la picha la hillary clinton at yale
Hillary enzi za Yale
Hillary alisoma Wellesley College ambapo alikuwa akishiriki katika masuala ya siasa shuleni na alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa darasa lake kabla hajahitimu mwaka 1959. Baadaye alijiunga na Shule ya Sheria Yale ambako alikutana na Bill Clinton. Alitunukiwa Shahada ya Heshima katika sheria mwaka 1973 na aliendelea na alijiunga na Kituo cha masomo ya watoto Yale ambako alisoma kozi za masomo ya watoto na madawa nakwa mwaka mmoja.

Ndoa

Tokeo la picha la hillary clinton and bill wedding
Hillary na Bill Clinton siku ya harusi yao 1975

Alifunga ndoa na Bill Clinton mwaka 1975 na wana mtoto mmoja anayeitwa Chelsea. Ndoa hii ipo katika orodha ya watu maarufu duniani ambao wameanza mahusiano tokea wakiwa masomoni. Hillary alipomaliza chuo kwa wakti ule alikaa mwaka mzima chuoni hapo akimsubiri mpenzi wake Bill Clinton ahitimu masomo yake.

Vitabu alivyoandika

1996- It Takes a Village
1997- The Unuque Voice of Hillary Clinton
1998- Dear Socks, Dear Buddy
 2000- An Invitation to the White House
2003- Living History
2014- Hard Choices
2015- Solutions: American Leaders Speak Out on Criminal Justice
2016- Stronger Together

First Lady wa Marekani

Tokeo la picha la the clintons during bill inauguration
Siku ya kiapo, Bill Clinton kama Rais akiwa na mkewe Hillary na binti yao Chelsea

Katika Uchaguzi wa mwaka 1992 Hillary alishiriki vyema katika kuaslimia wapiga kura, kuhutubia na kuwa miongoni mwa washauri wakuu wa Bill Clinton.


MAMBO 15 UNAYOPASWA KUFAHAMU KUHUSU HILLARY CLINTON

15. Ameshinda tuzo ya Grammy mwaka 1997 lakini sio tuzo ya muziki. Ni kuhusu kitabu chake cha It Takes a Village lakini sio pekee aliyeshinda tuzo hizo, Obama pia alishachukua tuzo hii katika kitabu chake pia.

14. Hillary hajaendesha gari toka mwak 1996 alilisema hili mwaka 2012.

13.  Mama yake Bill Clinton (mama mkwe wa Hillary) hakufikiria kwamba Hillary ni mzuri sana kuwa na mwanaye kuwa hana mvuto.

12. Moja kati ya kesi za awali za Hillary kama mwanasheria ilikuwa inahusisha Panya.

11. Hillary Clinton mwanzoni alikuwa mfuasi wa chama cha Republican kabla ya kuhamia Democratic mwaka 1968 baada ya kuvutiwa na moja kati ya hotuba za Martin Luther King Jr.

10.Katika utawala waRais Bill Clinton FBI walichukua picha za viganja (fingerprints) vya Bill na Hillary kuona kama wawili hao waliweza kuangalia nyaraka za FBI.Ilibainika kwamba hawakuhusika kuangalia nyaraka hizo lakini miaka miwili baadaye zilikutwa nyumbani kwa Hillary zikiwa na alama za viganja vyake.

9. Utambulisho wake wa Huduma za Siri ni "Evergreen" na alipewa utambulisho huu akiwa First lady na Huduma za Siri.Amekua akitumia utambulisho huu hata katika kampeni zake za Urais. Katika kipindi cha 2008 alipokuwa akigombea utambulisho huu ulirejeshwa tena. Bill Clinton pia amekuwa akitumia utambulisho wa "Eagle" katika kipindi cha harakati za mkewe kuelekea Ikulu .

8. Ni First lady pekee ambaye amegombea Useneta na kushinda kiti hicho akiwa pia ni First lady. Alikuwa Seneta wa New York mwaka 2001 na kukabidhiwa Ofisi Januari 3 mwaka huo.

7. Jarida la Sheria la Marekani 'The National Law Journal' lilimtaja Hillary kuwa miongoni mwa wanasheria 100 wenye ushawishi nchini humo mwaka 1988 na 1991. Umahiri wake katik sheria ulimfanya awe na pesa nyingi hata kumshinda mumewe Bill aliyekuwa Gavana wa Arkansas kwa wakati huo. Umahili wa Clinton ktik sheria ulichangia pia kwa kiasi kikubwa kumfanya Bill awe Rais wa nchi hiyo kwa kipindi hicho.

6. Ni Katibu Mkuu aliyesafiri kuliko makatibu wengine katika Historia katika kipindi chake cha miaka 4. Alizuru nchi 112 na kusafiri kwa ndege maili milioni 1 na kutumia 25% ya kipindi chake katika safari.

5. Amekuwa akituhumiwa kujihusisha na Usagaji "mapenzi ya jinsia moja". Baadhi ya watu wamekuwa wakithibitisha hili kwa mfano Edward Klein ambaye ameandika ktika kitabu chake The Truth About Hillary kuwa amekuwa akishiriki usagaji na msaidizi wake Huma Abedin na wasagaji wengine.

4. Hillary na mumewe Bill waliwahi kuitwa Mahakamani kutoa ushahidi kuhusika katik scandal ya Whitewater Development. Hata hivyo baadaye hawakukutwa na hatia ya kufanya mabaya katika scandal hiyo.

3. Hillary aliamua kutumia jina la Clinton baada ya kushawishiwa na wapiga kura wa Arkansas. Baada ya ndoa yao Hillary aliendelea kutumia jina lake la Hillary Rodham, Wapiga kura hao walitaka kujua kama ndoa yao ni ndoa kweli ama fasheni tu hivyo Hillary akaamua kutumia jina la Hillary Rodham Clinton. Kwa hiyo ili kufanya mumewe ashinde katika Uchaguzi kuwa Gavana wa jimbo la Arkansas aliamua kujiita Hillary Rodham Clinton.

2. Alishiriki katika jopo la wanasheria 43 kumtia hatiani Rais Richard Nixon. Wanajopo wenzie walimtuhumu kama muongo na kutofuata maadili ya kumtia hatiani Rais Nixon. Bosi wa Hillary alisema mara kwa mara Hillary alikuwa akikosea katik kuuliza maswali lakini hakuwa na uwezo wa kumfukuza Hillary kazi.

1. Japokuwa alipmba kurasa za jarida la The Vogue mwaka 1998, alikataa kuonekana katika Jarida hilo mwaka 2007 kwa kuhofia kuwa mfeministi sana kitu ambacho kingeleta shida katika mbio zake za uchaguzi wa Urais mwaka 2008.








Tokeo la picha la hillary clinton
 Tokeo la picha la hillary clinton

MAKALA HII IMEHARIRIWA KWA HISANI YA MTANDAO.

VIDEO: TRUMP AKATAA KUJIBU SWALI KUHUSU KUKUBALI MATOKEO KAMA ATASHINDA KWENYE UCHAGUZI

Ni katika Mdahalo wa tatu na wa mwisho ukiofanyika Nevada, Las Vegas.

Swali liliulizwa kwa Bwana Trump "utakubali matokeo ya Urais baada ya kushindwa na mpinzania wako Hillary Clinton?"

Trump hakujibu moja kwa moja, alisema "nitaliangalia hilo kwa wakati huo".

Awali ya hapo Rais Obama alishangazwa na kutokujiamini kwa Trump kuhusu kuwa na mashaka na Uchaguzi hata kabla ya Uchaguzi wenyewe kufanyika.

Nitakuandalia makala kamili kutoka kwenye Mdahalo huo.

Hii hapa video ikimuonesha Trump alivyokataa kujibu swali aliloulizwa:

Video kwa hisani ya France24.

WALIOCHAGULIWA MZUMBE AWAMU YA PILI MAJINA HAYA HAPA

Chuo Kikuu Mzumbe kimetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kwa ngazi ya Cheti, Stashahada na Shahada kwa awamu ya pili.


>>>BOFYA HAPA KUANGALIA MAJINA<<<

HAYA HAPA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA AWAMU YA PILI RUAHA, MWALIMU NYERERE & ECKERNFORDE

Hapa kuna selection za Vyuo vitatu; Ruaha, Mwalimu Nyerere na Eckernforde

1. KWA RUAHA CATHOLIC UNIVERSITY (RUCU)
👉BOFYA HAPA👈


2. KWA MWALIMU NYERERE MEMORIAL ACADEMY (MNMA)
👉BOFYA HAPA👈


3. KWA ECKERNFORDE TANGA UNIVERSITY (ETU)
👉BOFYA HAPA👈

WALIOCHAGULIWA MZUMBE MAJINA YAO YAKO HAPA (FIRST BATCH/ROUND 1)

Chuo Kikuu Mzzumbe kimetangaza majina ya waliochaguliwa chuoni hapo.

👉BOFYA HAPA KUDOWNLOAD MAJINA👈

WALIOCHAGULIWA UDSM, DUCE, MUCE & IFM AWAMU YA PILI HAWA HAPA



Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na matawi yake DUCE na Mkwawa (MUCE) pamoja na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM) vimetoa majina ya waliochaguliwa awamu ya pili kujiunga na chuo hicho.

1. KWA UDSM, DUCE NA MKWAWA (MUCE)
👉BOFYA HAPA👈


2. KWA IFM
👉BOFYA HAPA👈


3. KWA IFM MWANZA
👉BOFYA HAPA👈

ORODHA YA MAJINA WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI (AWAMU YA PILI)

Hii ni list ya majina ya vyuo vilivyotoa majina ya waliochaguliwa leo October 5, 2016.

1. KWA CHUO KIKUU SAUT AWAMU YA KWANZA NA PILI ZOTE
👉BOFYA HPA👈

2. KWA TEKU
👉BOFYA HAPA👈

3. KWA ARCHBISHOP JAMES (AJUCO)
👉BOFYA HAPA👈

4. KWA JORDAN ROUND 1 & 2
👉BOFYA HAPA👈

5. KWA BUGANDO (CUHAS)
👉BOFYA HAPA👈



Endelea kufuatilia Blog hii kwa selection za vyuo vingine zaidi kwa round zilizosalia.

WALIOCHAGULIWA JORDAN (AWAMU 1 & 2)

Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan kimetangaza majina ya waliochaguliwa chuoni hapo mwaka wa masomo 2016/2017.

👉BOFYA HAPA KUONA MAJINA👈

SELECTED STUDENTS TO JOIN KAMPALA INTERNATINONAL UNIVERSITY FOR ACADEMIC YEAR 2016/2017 (FIRST & SECOND BATCHES)

Chuo Kikuu chq Kimataifa cha Kampala (KIU) kimetoa majina ya awamu ya kwanza na ya pili (first and second batches) za wanafunzi waliochaguliwa chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

👉BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD NA KUANAGALIA MAJINA HAYO👈