ATUHUMIWA KUKUTWA UTUPU AKIFUKUA KABURI

MKAZI wa Kijiji cha Ikola katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi , Richard Clavery ( 34 ) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kufukua kaburi la mwanamke, aliyekufa na kuzikwa kaburini humo. Mtu huyo anatuhumiwa kukutwa na waombolezaji, akiwa amevua nguo zake zote na kuzitundika juu ya msalaba, uliosimikwa kaburini hapo. Mwendesha Mashitaka, Godfrey Luzabila alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa, Februari 25 mwaka huu kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 18 mwaka huu saa nne usiku nyumbani kwa dada wa marehemu, Lenada Sakafu katika kijiji cha Ikola . Luzabila alidai usiku wa tukio hilo, mtuhumiwa alifika nyumbani kwa Lenada Sakafu na kufukua maiti ya mdogo wa Lenada, Tabu Omera aliyekuwa amezikwa kaburini siku tatu kabla ya tukio hilo. Kaburi alimozikwa marehemu, lilikuwa katika eneo la nyumba ya Lenada. Alidai usiku huo, Lenada akiwa nyumbani hapo pamoja na waombolezaji, wakiwemo majirani na ndugu, ghafla alitokea mtoto wa Lenada, aitwaye Brandina ambaye aliwaeleza kuwa ameona mtu nje ya nyumba yao akifukua kaburi la Tabu. Waombolezaji hao papo hapo walitoka nje na kumkuta Clavery akifukua kaburi hilo, huku akiwa amevua nguo zake zote na kuzitundika juu ya msalaba uliosimikwa kaburini hapo. Walipomsemesha mtuhumiwa huyo, alijifanya amepandisha majini na kujaribu kutoroka. Mtuhumiwa alikana shitaka hilo. Hakimu Ntengwa alilazimika kuahirisha shauri hilo hadi Machi 6 , mwaka huu litakapotajwa tena. Hakimu aliamuru mshtakiwa arejeshwe rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, ambapo alitakiwa adhaminiwe na mtu mmoja kwa kiasi cha Sh milioni moja . Chanzo: Habari Leo

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU