Uganda imetoa tahadhari kwamba kundi la wanamgambo la Al Shabaab linapanga kutumia malori ya mafuta kama mabomu katika mahambulizi yao.
Taarifa hii inakuja siku moja baada ya polisi kuwakamata washukiwa wawili wa ugaidi waliokuwa na mabomu wakinuia kutekeleza mashambulizi mjini Mombasa.
Mkuu wa polisi wa Uganda,Kale Kayihura, amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba idara ya polisi na ujasusi zina taarifa za kuthibitishwa kuwa kundi la Al-Shabaab linapanga kulipua malori ya mafuta nchini Uganda na kusababisha uharibifu mkubwa.
Ameshauri wananchi kuwa waangalifu na waweze kutoa taarifa zozote kwa polisi.
Uganda na Kenya ziko na wanajeshi wake nchini Somalia kusaidia wanajeshi wa Somalia na wale wa Muungano wa Afrika kupambana na kundi la Al Shabaab.
Wapiganaji hao wamekiri kufanya mashambulizi katika nchi hizo mbili na kutishia mashambulizi zaidi ikiwa Kenya haitaondoa wanajeshi wake kutoka Somalia.
Kundi la Al Shabaab liliwaua watu 76 katika mji mkuu wa Uganda Kampala mwaka 2010.
Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda. Zaidi ya watu milioni 1 5 katika bara hili huitumia lugha hi i kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya M uungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika. TANZANIA Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa. Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVI...
Comments
Post a Comment