Maafisa wa serikali nchini Yemen wamesema kuwa zaidi ya wahamiaji arubaini wa Kiafrika wamezama baharini, baada ya mashua walimokuwa wakisafiria kuzama, katika pwani ya kusini mwa nchi hiyo. Manoari ya jeshi la Yemen ambalo lilikuwa katika eneo hilo, imefanikiwa kuwaokoa wahamiaji wengine wapatao thelathini. Wizara ya ulinzi nchini Yemen imesema kuwa mashua hiyo iliyokuwa ikisafirisha wahamiaji haramu, ilizama katika mkoa wa Kusini wa Shabwa, eneo ambako maelfu ya wahamiaji wa Kiafrika huwasili kila mwaka. Kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Uhamiaji la IOM, wengi wa wakimbizi wanaojaribu kuvuka guba la Eden, wanatoka Somalia na Ethiopia. Shirika hilo limesema kuwa wahamiaji hao hufanya safari ndefu na hatari ili kukwepa umasikini, unyanyazaji au vita katika mataifa yao. Baada ya kuwasili Yemen, wengi wao hutarajia kupata kazi nchini Saudi Arabia na mataifa ya Guba, lakini mamia ya wahamiaji wa Kiafrika hufa kila mwaka wakijaribu kuvuka eneo hilo la Guba wakitafuta maisha bora katika mataifa ya ngambo.

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

LIST OF UNDERGRADUATES SELECTED TO JOIN TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY (TIA) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

VIFAA VYA KUWATAMBUA WENYE UGONJWA WA EBOLA VYAINGIZWA NCHINI

TAZAMA HAPA MAGOLI 10 BORA YA KOMBE LA DUNIA 2018