Posts

ACTION MUVI MPYA INATOKA AGUST 2, SNIPER: GHOST SHOOTER

Image
Muvi inaitwa Sniper: Ghost Shooter inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 2 Agost mwaka huu (siku chache kutoka leo kama siku 5 mbele). Imechezwa na Chad Michael Collins, Billy Zane, Dennis Haysbert na wengine wengi. STORI KWA UFUPI Masnaipa wenye akili Chad Collins (katika muvi hii ameigiza kama Brandon Beckett) na Billy Zane (katika muvi hii anaitwa Richard Miller) wanapewa jukumu la kulinda bomba la gesi ili lisiharibiwe na magaidi. Wanapokuwa katika mambano na maadui inapelekea masnaipa wenzao wengine kuuawa na adui asiyefahamika alipo lakini yeye akiwa anafahamu wao (Richard na Brandon) walipojificha. Hofu inazidi kutanda hadi kufikia safu ya ulinzi kushutumiwa kushirikiana na maadui. Kuna mmoja kati yao anashirikiana na upande wa maadui? Je, mpango ni mwanzo wa mpango mwingine kumjua msaliti? Je, Kanali atatumia muda mwingi kuamua nini kifanyike? Haya yote utayapata katika muvi hii Sniper: Ghost Shooter kuanzia Agost 2, mwaka huu katika tovuti na application za kupakua muvi...

CHADEMA 'YAIBIPU' POLISI

Image
Ni wazi sasa kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeamua kujipima nguvu na Jeshi la Polisi baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kutangaza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Septemba mosi, mwaka huu. Kamati Kuu hiyo katika maazimio yake yaliyosomwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ilisisitiza kuwa azma yake hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kupinga agizo la jeshi hilo la kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Sababu nyingine zilizoisukuma Kamati Kuu kufikia azma hiyo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ni pamoja na kupinga zuio la urushwaji wa moja kwa moja wa mijadala ya Bunge, kupinga wabunge wa upinzani kudhibitiwa bungeni, kuingiliwa kwa mhimili wa mahakama, upuuzwaji wa utawala wa sheria na haki ya kupata habari. Katika hatua nyingine, Kamati Kuu ya Chadema imezindua operesheni Ukuta yenye lengo la kupambana na kile ilichokiita kuwa ni udikteta nchini, huku ikitangaza kus...

WAZIRI MKUU WA NEPAL KHADGA PRASAD OLI AMEJIUZURU

Image
Waziri Mkuu wa Nepal Khadga Prasad Oli amejiuziru wadhifa wake ikiwa ni muda mchache kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika Bunge la nchi hiyo. Inadaiwa katika kura hiyo Oli angeshindwa. Oli mwenye umri wa miaka 64 alishinikizwa kujiuzuru na wapinzani wa chama chake kufuatia kutoheshimu mgawanyo wa madaraka ambao ndiyo uliompa Uwaziri mkuu miezi 9 iliyopita. "Nimekwisha wasilisha barua yangu ya kujiuzuru kwa Rais nilipokutana naye kabla hata ya Bunge" amesikika akisema Oli aliponukuliwa na The Reuters katika Bunge la Nepal. Oli aliyezaliwa kaskazini mwa Nepal Fenruari 22 mwaka 1952 alikuwa mwanachawa wa Nepal Communist Party mwaka 1970 baada ya kuvutiwa na viongozi wa kikomunisti alipokuwa kijana. Amewahi kutumikia kifungo cha miaka 14 jela. Oli aliingia madarakani Oktoba mwaka jana huku akikosolewa sana na kuwepo kwa maandamano kufuatia kushindwa kuchukua hatua katika tetemeko lililowaacha wananchi katika umaskini mkubwa. Zaidi ya watu 50 wali...

BARAZA LA MITIHANI LIMETANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016

Image
Matokeo ya Kidato cha Sita 2016 yametoka, unaweza kuyaona kwa kubofya  HAPA

SATELITE YA JUNO YAFIKA KATIKA SAYARI YA JUPITA

Image
Satelite ya Juno ikiwa imewasili katika sayari ya Jupita. Satelite ya Juno inayokuwa inayoongozwa taasisi ya Utafiti wa Anga NASA iliyoko nchini Marekani imefanikiwa kufika katika sayari ya Jupita ambayo ni sayari ya tano katika mfumo wa jua kutoka kwenye jua. Satelite hiyo ya Juno iliondoka duniani miaka mitano iliyopita ambayo ilikuwa na rocket engine kuiongoza satelite hiyo mpaka kuifika satelite hiyo.. Wattafiti wanapanga kuitumia satelite hiyo kuichunguza sayari hiyo kwa jina. Wanadai kuwa muonekano wa sayari hiyo na kemia yake unaweza kuichunguza zaidi sayari hii ambayo ni kubwa kuliko zote katika mfumo wa jua toka ilipotengenezwa zaidi ys miaka bilioni 4 na nusu iliyopita. Hakuna chombo kilichofanikiwa kupita au kuisogelea sayari hiyo ya Jupita kutokana na mionzi iliyopo katika sayari hii kama chombo hicho hakijalindwa na vifaa maalumu vya kieletroniki ambavyo vinazuia mionzi hiyo kupenya. Mahesabu ya haraka yanaonesha kuwa satelite hiyo imeundwa kwa miyonzi zenye...

MAN WATER AELEZA SABABU ZA KUWARUDISHA WAKONGWE KWENYE MUZIKI

Image
Producer Man Water wa combinataion sound, ameelezea sababu ya kupenda kuwarudisha wasanii wa kitambo kwenye game, ambao tayari walishapotea kimuziki. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Man Water amesema hupenda kufanya hivyo kwani ana imani wasanii hao bado wana uwezo mkubwa, na kwa kuwa alitoka nao mbali kikazi. “Kurudisha wasanii waliopotea mimi na kuwa nao karibu kwa sababu ni watu wangu ambao nimetoka nao mbali, najua hustle zao tulipita wote, na kwa sababu mi mwenzao bado nimebaki kwenye game, sasa nikiwaita wale nawaambia jinsi gani game ya sasa ilivyo na wabadilike vipi ili waweze kurudi”, alisema Man Water. Man Water alishawahi kumrudisha kwenye game msanii 20% , Alikiba, Lady Jaydee na wengine, huku bado akiwa na mpango wa kuendelea kuwarudisha wasanii wengine kama Mr. Nice. Chanzo: EATV

MABAKI YA NDEGE YA MISRI YAPATIKANA

Image
Mamlaka ya Misri inasema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo. Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha ya kwanza ya masalio hayo. Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo. Chanzo: BBC

MOVIE: X-MEN APOCALYPSE RELEASED TODAY

Image
  Release date: May 27, 2016 Director: Bryan Singer Starring: James McAvoy Jennifer Lawrence Oscar Isaac Michael Fassbender Rose Byrne Sophie Turner Synopsis: In this comic-book adventure set in the 1980s, the X-Men are forced to confront an ancient mutant called Apocalypse (Oscar Isaac). After the resurrected beast recruits a super-team to take over the world and destroy hunmanity, Professor X (James McAvoy) and his charges must come to the rescue for the fate of the planet. The film co-stars Michael Fassbender, Jennifer Lawrence and Olivia Munn.

OBAMA AZURU HIROSHIMA JAPAN

Image
Obama amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000. Baada ya kuweka shada ya maua katika bustani ya amani eneo la Hiroshima-Japan, rais Obama alitoa hotuba ya kumbukumbu ya mashambulizi hayo ya Hiroshima huku akisisitiza matumaini kuwa uhusiano kati ya Japan na Marekani utazidisha matumaini katika juhudi za kutupilia mbali matumizi ya silaha za atomiki. Obama amekuwa rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru eneo la mji wa Hiroshima ambalo Marekani ilishambulia kwa kutumia bomu la kwanza la atomiki mwaka 1945 na kuua takriban watu 140,000. Obama amefanya ziara hiyo ya kihistoria baada ya mkutano wa viongozi wa nchi saba tajiri kiviwanda duniani ambapo viongzo hao wamekubali kuimarisha uchumi wa dunia. Upatanisho Shambulizi la bomu la kwanza la atomiki eneo la Hiroshima mwaka 1945 na pia Nagasaki lilisaba...

FURAHIA WIKENDI KWA KUANGALIA MUVI HIZI 5 KALI MPYA

Image
JINA LA MUVI: KILL ZONE 2 STAR: TONY JAA (kutoka Ong Bak)  After his true identity is exposed, undercover cop Kit ( Wu Jing ) is sent to a corrupt Thai prison by the gang he infiltrated, while his police unit erases all evidence that he was ever an officer. There, a guard named Chai ( Tony Jaa ) discovers that Kit is a bone-marrow match for his daughter, who desperately needs a transplant. The unlikely partners must find a way to secretly escape from the brutal prison and save Chai's daughter. Pou-Soi Cheang directed this martial-arts action thriller. JINA LA MUVI: LAST DAYS IN THE DESERT This biblical drama follows Jesus Christ (here referred to as " Yeshua " and played by Ewan McGregor ) during the 40 days he spent fasting and wandering in the desert. He is approached by a demon (also McGregor ) during his travels, who challenges him to help a troubled family living in the wilderness. Ciarán Hinds , Tye Sheridan , and Ayelet Zurer co-star as the mem...

HEZBOLLAH YATAJA SABABU YA KUUAWA KIONGOZI WAO

Image
 Kundi la Waislamu wa madhehebu ya Kishia la Hezbollah nchini Lebanon limetaja sababu ya kifo cha kiongozi wake wa ngazi ya juu wa kijeshi, Mustafa Badreddine kuwa kimetokana na makombora ya mizinga liliofanyika karibu na uwanja wa ndege wa Damascus nchini Syria.  Hezbollah lilitangaza  kifo cha Badreddine hapo jana na alifanyiwa mazishi ya kijeshi siku hiyo hiyo katika eneo la ngome la kundi hilo huko kusini mwa Beirut. Taarifa ya kundi hilo imesema mashambulizi hayo yamefanywa na kundi linaloitwa Takfiri. Takfiri ni neno linalotumiwa na kundi hilo la Kisunni kwa kuonesha msimamo mkali, kundi lenye kujihami na silaha, lililo na itikadi kali. Badreddine alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kundi la Hezbollah walioshutumiwa mwaka 2005 kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri. Chanzo: Deutsche Welle (DW)

TEGEMEA PAMBANO KUTOKA KWA MAYWEATHER NA CONOR McGREGOR

Image
 Floyd Mayweather   Conor McGregor Mwanamasumbwi Floyd Mayweather amesema kuwa yeye ndiye aleanzisha uvumi wa kupambana na Conor McGregor ambaye anapambana kwa mtindo wa Mixed Martial Art (MMA). McGregor alipost picha kwenye mtandao wa Twitter  iliyomuonesha yeye na Mayweather wakwa uso kwa uso. Mayweather, mwanamasumbwi aliyestaafu mwenye miaka 39 amesema kuwa atahitaji kiasi cha fedha Dollar za kimarekani Milioni 100 sawa na Euro Milioni 69.3 kupambana na McGregor raia wa Ireland mwenye umri wa miaka 27. "Muwe makini kusikiliza, linaweza kuwa pambano kati ya mcheza boxing na MMA" Mayweather aliiambia fighthype.com "Ni pendekezo nililolitoa mimi, inaweza isiwe tetesi" aliongeza Mayweather. Baba yake Mayweather alisema kuwa mwanaye huyo (Mayweather) aliwahi kumwambia kuwa atapambana na mwanamasumbwi yeyote kutoka MMA ambapo McGregor aliiambia BT Sport kuwa anataka pambano la Dola Bilioni na Muamerika, Floyd Mayweather. McGregor, a...

ANGALIA VIDEO YA JENNIFER LOPEZ-AIN'T YOUR MAMA HAPA

Image
Jennifer Lopez ameachia video ya wimbo wake Ain't your Mama May 6 ambapo mpaka sasa wimbo huo umetazawa na watazamaji zaidi ya milioni na laki saba. Kama bado hujapata nafasi ya kuangalia video hiyo tazama hapa kwa hisani ya VENANCE BLOG kisha toa maoni yako kuhusu video hiyo. Like Page yangu Facebook Nifuate Twitter Nifolo Instagram

DOWNLOAD AUDIO KUTOKA UPRISE MUSIC: JVP SQUAD-HUSTLE ZA KITAA

Image
Ngoma imefanywa Uprise Music na producer Fragger. Ngoma inaitwa Hustle za Mtaa imefanywa na JVP Squad ndani kasimama Ng'itu the Hustler na Fizzo. Sikiliza na kudownload kisha toa maoni yako hapa.  BOFYA HAPA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD  

UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA TANZANIA NA UGANDA SASA NI RASMI

Image
BOMBA la mafuta ghafi kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda, sasa ni rasmi kwamba litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga, ambako ndiko meli kubwa za mafuta, zitakapotia nanga kubeba mafuta hayo kwenda sehemu mbalimbali duniani. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia bandari hiyo. Kwa hatua hiyo, bomba hilo linalotakiwa kuwa limekamilika ifikapo 2018, litaingilia Mkoa wa Kagera kutoka nchini Uganda na kupita katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi Bandari ya Tanga. Rais Museveni Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ndiye aliyetangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika jijini Kampala jana. “Ujumbe wa Tanzania uliokamilisha mazungumzo hayo na kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo, uliongozwa na Dk Augustine Mahiga, ...