Posts

DOWNLOAD WIMBO MPYA: TOFA EMCEE-KUNG FU PANDA

Image
Anaitwa Christopher Robert jina la kazi ya sanaa 'Tofa Emcee'.  Tofa Emcee katika picha. Picha kwa hisani ya Facebook account Christoper TofaEmcee Robert Donload Kung Fu Panda kwa kubofya HAPA.

BEN POL AELEZEA ALIVYONUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA BOTI

Image
Msanii wa Bongo Fleva,Ben Pol amesimulia alivyonusurika kifo baada ya boti waliokuwa wakisafiria wakitokea visiwani Mbudya,jijini Dar kuzima ghafla katika ya bahari na kukaa kwa muda wa saa nzima bila kupata msaada. Ben Pol alisema kuwa baada boti kuzima maji yalianza kuingia ndani  na engine ya boti ikazimika na boti hiyo ikaanza kuzama kilichowaokoa walikuwa wamevaa makoti ya kuogelea ‘life jackets’. ‘’Baada ya kukaa kwa saa nzima baharini kwa bahati nzuri ilipita boti ya wavuvi ikatuona ikatuokoa ila mmoja wetu hakuwepo kati ya tuliokolewa na hatujamuona ambao ni wanawake watatu, watoto hao walikuwa watatu, wanaume tulikuwa nane, lakini mmoja ndiye hatujui alipo.’alisema Ben Pol.

VAN VICKER AKUMBWA NA MAFURIKO AKIELEKEA KWAKE

Image
Mafuriko makubwa yaliyoikumba jiji la Accra nchini Ghana usiku wa kuamkia juzi na kuleta maafa ya kuua watu 175 wakiwa wamejihifadhi kwenye kituo cha mafuta baada ya kituo hicho kulipuka moto,yamemkumba pia Staa wa filamu nchini humo Van Vicker akiwa barabarani akielekea nyumbani kwake. Kupitia akaunti yake Instagram Van Vicker aliandika kuwa ameshuhudia mafuriko kwa macho yake (live),huku taa za barabarani zikiwa haziwaki,kuna mashimo,matakataka,umeme ukiwa umekatika na barabara zilikuwa zimefurika maji, na magari yalikuwa yameharibika. Pia aliongeza kuwa waliokuwa wakitembea barabarani walikuwa wakitafuta pa kujihifadhi,madereva walipaniki na bado wakati huo mvua ilikuwa ikinyeesha na pia foleni ilikuwa kubwa na barabara ni ndogo. Ambapo alisema kuwa kawaida huwa inamchukua dakika 45 kwenda nyumbani kwake lakini siku hiyo ilimchukua masaa sita kufika nyumbani kwake. Chanzo; Udaku Specially

URUSI NA QATAR HUENDA ZISIANDAE KOMBE LA DUNIA

Image
Mkuu wa kamati ya uhasibu wa shirikisho la soka duniani FIFA Domenico Scala amesema huenda Urusi na Qatar zikapoteza nafasi za kuyaandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 mtawalia iwapo ushahidi utaonyesha kulikuwa na ufisadi katika shughuli ya kinyanganyiro cha kupata kibali cha kuandaa mashindano hayo. Scala hata hivyo amesema mpaka kufikia sasa hawajapokea ushahidi wowote wa kudhihirisha kuwa nchi hizo mbili zilitoa hongo. Matamshi yake ndiyo ya kwanza kutolewa na afisa wa ngazi ya juu wa FIFA kuwa kuna uwezekano nchi hizo zikapokonywa uenyeji wa mashindano hayo. Maafisa wa idara ya mahakama wa Uswisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu kutolewa kwa kandrasi hiyo ya kuandaa mashindano ya 2018 na 2022 kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ufisadi katika FIFA.  Chanzo: DW

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

Image
Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7 wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto duniani na athari zake. Chanzo: DW

KOMBE LA DUNIA KWA WANAWAKE

Image
Michuano ya kombe la dunia la wanawake,inaendelea huko canada katika miji tofauti tofauti.michuano hiyo ya kombe la dunia kwa wanawake liliendelea tena hapo jana kwa michezo miwili kupigwa kati ya Norway waliopepetana na Thailand. Ujeruman ilioonesha kazi pwani ya samawati naizungumzia Ivory Coast na matokeo yalikuwa hivi Norway waliibuka na mtaji wa magoli manne huku Thailand wakikubali matokeo na kutulia na yai. Kwa upande mwingingine kwenye mechi ya pili Ujerumani walijizolea magoli yao mawili na kuwaacha Ivory Coast mikono mitupu. Chanzo: BBC

WATU 400 WAFARIKI KATIKA MTO YANGTSE

Image
Meli iliyozama China Msemaji wa serikali nchini China anasema kuwa karibu watu 400 wanahofiwa kuaga dunia wakati feri ilipozama kwenye mto Yangtze siku ya jumatatu. Idadi hiyo imeongezeka kwa haraka baada ya makundi ya uokoaji kusaka vyumba vya feri hiyo. Kwa sasa meli hiyo imendolewa majini kwa kutumia mitambo mikubwa. Jumla ya watu 456 walikuwa ndani ya feri hiyo wakati ilipokumbwa na dhoruba ambapo ni watu 14 tu walioripotiwa kuponea ajali hiyo. Ajali hiyo inaripotiwa kuwa mbaya zaidi nchini humo tangu miaka 60 iliyopita. Chanzo: BBC

RAIS KIKWETE AELEKEZA NGUVU KATIKA ELIMU YA KIDATO CHA 5 & 6

Image
Rais Jakaya Kikwete akipokea tuzo maalum kutoka kwa Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jana. Picha na Ikulu Rais Jakaya Kikwete jana alitumia kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu kuaga wadau wa sekta hiyo, akisema sasa nguvu zielekezwe katika kujenga majengo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu ya sekondari. Rais Kikwete, ambaye alikiri kuwapo udhaifu katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, alisema mafanikio pia ni makubwa kiasi kwamba sasa hakuna wanafunzi wanaokosa nafasi ya kwenda sekondari baada ya kufaulu na hivyo nguvu sasa inatakiwa kuwekwa katika kuongeza miundombinu ya kidato cha tano na sita. Kikwete alitoa kauli hiyo jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa alipohutubia maelfu ya wakazi wa Dodoma, wakiwamo wanafunzi wa shule za sekondari na msing...

PINDA: CCM ITAELEZA HAYA KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU

Image
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, jana alihitimisha mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Ofisi yake ya Sh trilioni 5.7 ambayo ilipitishwa na Bunge, huku akifafanua hoja zitakazotumiwa na CCM kuomba kura za wananchi katika Uchaguzi Mkuu ujao. Pinda alisema hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo na kufafanua kuwa katika Uchaguzi Mkuu, CCM itatakiwa kueleza mafanikio ya Serikali katika nishati ya umeme vijijini, miundombinu ya barabara, elimu, maji na afya. Alitaka waliokuwa wakijiuliza nani atashinda katika uchaguzi huo, wapitie kidogo historia kuanzia mwaka 1995 mpaka katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika Desemba mwaka jana, ili waelewe nani alipata kipigo. Elimu Akifafanua kwa ufupi mafanikio yaliyopatikana katika elimu, Pinda alisema watakapoulizwa katika sekta hiyo nini kimefanyika, wataweka wazi kuwa ingawa bado kuna changamoto lakini yapo pia mafanikio makubwa. “Wacha tubebe lawama katika changamoto, lakini tutaeleza kuwa katika vyuo vya ufundi mwaka...

RAIS NKURUNZINZA KULIPIZA KISASI KWA WAASI

Image
 Burundi Pierre Nkurunziza amewapongeza wanajeshi wazalendo waliozuia mapinduzi na kurejesha hali ya usalama na utawala huru mjini Bujumbura. Rais Nkurunziza amewataka waburundi wazalendo kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi juni. Rais huyo alikuwa Mjini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumatano kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kundi la wanajeshi waasi walipotangaza ''Mapinduzi'' dhidi ya serikali yake. Viongozi watatu miongoni mwa makamanda 6 wa jeshi waliounga mkono tangazo hilo la ''mapinduzi'' ilikupinga muhula wa tatu wa rais huyo tayari wamekamatwa. Kufikia sasa watu 105,000 wameripotiwa kutorokea mataifa jirani kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. Baada ya kurejea kutoka Tanzania rais Nkurunzinza alielekea Kaskazini mwa Bujumbura eneo alikotokea kabla ya kurejea katika kasri la rais lililoko katika mji mkuu wa Bujumbura. Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni rais Nkurunzinza a...

JACKLINE WOLPER ANASWA LIVE AKITOKA JUMBA LA FREEMASONS

Image
Mshtuko! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameibua maswali kwa mashuhuda walimuona ‘live’ akiingia kwenye hekalu la watu wa Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemasons yenye nguvu duniani inayohusishwa na imani za kishetani. TUJIUNGE MTAA WA SOKOINE Tukio hilo lililoibua kizaazaa kwa mashuhuda waliomuona Wolper, lilijiri juzikati, mishale ya jioni kwenye hekalu hilo lililopo Mtaa wa Sokoine mkabala na Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar jirani na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). SIMU ZAMIMINIKA Likiwa kwenye majukumu ya kusaka habari kama kawaida yake, gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa mashuhuda hao wakiwataka wanahabari wetu kuwahi eneo la tukio. Kufuatia umbali waliokuwa mapaparazi wetu, ilibidi kuwaomba mashuhuda hao ‘kumfotoa’ picha ambapo mmoja wao alifanya hivyo na kuziwasilisha kwenye meza ya gazeti hili. ALINASWAJE? Akidadavua mazingira aliyonaswa Wolper, shuhuda huyo alikuwa na haya ya kusema: “Kwanza mwanzoni hatukumjua ...

HABARI LEO TAHARIRI: TFF IFANYIE KAZI KASORO ZA MSIMU ULIOMALIZIKA

Image
MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara umemalizika Jumamosi iliyopita, huku timu za Polisi Morogoro na Ruvu Shooting ya mkoani Pwani zikishuka daraja. Kushuka kwa timu hizo mbili kunatoa nafasi kwa timu nne kupanda daraja kukiwa na lengo la kuongeza timu shiriki kutoka 14 hadi 16 katika msimu ujao wa ligi hiyo. Timu zilizopanda daraja ni Majimaji ya Songea, African Sports ya Tanga, Toto African ya Mwanza na Mwadui ya Shinyanga, ambazo zinakamilisha timu hizo nne. Wakati msimu huo wa ligi ukifungwa, tayari Yanga na Azam FC walishajitangazia nafasi za kwanza na pili na kuwa na uhakika wa kuliwakilisha taifa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Shirikisho la Afrika. Baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi ndio mwanzo wa msimu unaokuja na timu zinatakiwa kujipanga vizuri kwa ajili ya msimu huo, ambao kama baadhi ya makosa yatarekebishwa, inaweza kuwa ligi bora zaidi. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), timu pamoja na wadau wengine wa ligi hiyo kama kamati mbalimbali, ambaz...

KUONDOKA KWA NGASA YANGA NI PENGO KUBWA KWA TIMU HIYO

Image
KATIBU Mkuu wa klabu ya Yanga, Jonas Tiboroha amekiri kuondoka kwa mshambuliaji Mrisho Ngassa ni pengo kubwa kwa timu yao, lakini amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuhakikisha wanapambana kumbakiza kiungo Haruna Niyonzima. Tiboroha alisema ana uhakika watafikia makubaliano na kiungo huyo bora Afrika Mashariki katika siku chache zijazo ili aendelee kuichezea timu yao msimu ujao na kwa kushirikiana na nyota wengine waliopo na watakaowasajili. Akizungumza na gazeti hili jana, Tiboroha alisema itakuwa wamefanya kosa kubwa endapo watamruhusu nyota huyo kuondoka kwani itakuwa ni pengo jingine baada ya Ngassa kuhamia Free State ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka minne. “Bado tupo kwenye mazungumzo na imani yangu kama Katibu Mkuu wa Yanga ni kwamba msimu ujao Niyonzima atabaki kuichezea Yanga kwa sababu mazungumzo yapo kwenye hatua nzuri na hata yeye mwenyewe ameonekana kutaka kubaki,” alisema Tiboroha. Kiongozi huyo alisema wamekuwa na vikao virefu na viongozi wa juu wa Yanga...

KAMANDA WA WAASI ADF KUREJESHWA UGANDA

Image
Waasi wa kikundi cha ADF. SERIKALI ya Tanzania inatarajia kumpeleka Uganda Kamanda wa Kikosi cha Waasi cha ADF cha Uganda, Jamil Mukumu aliyekuwa akitafutwa muda mrefu hapa nchini na Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol). Atapelekwa Uganda baada ya taratibu za kumfikisha mahakamani kukamilika. “Baada ya kukamatwa mtu huyo tuliwauliza Umoja wa Mataifa kama watamchukua, lakini walikataa njia iliyobaki sasa ilibidi tumfikishe mahakamani na kisha mahakama kwa kufuata sheria ya kubadilishana wafungwa na mahabusu atapelekwa Uganda kwenye mashitaka yake,” alisema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Alisema utaratibu huo wa kumpeleka Uganda unafanyika kisheria kwa sababu ndio njia pekee iliyobaki. Membe alisema pamoja na tukio la wanajeshi wawili kuuawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na wengine 15 kujeruhiwa, wanajeshi wa Tanzania wanafanya kazi nzuri. Kundi la waasi la ADF limejikita mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(...

ALBINO AKATWA VIUNGO KATAVI

Image
Katavi. Mwanamke mmoja mwenye ulemavu wa ngozi, Remi Luchoma (30), Mkazi Kijiji cha Mwamachoma, wilayani Mlele amekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana na kutokomea nacho. Luchoma alikatwa mkono juzi saa sita usiku akiwa nyumbani kwa wazazi wake na sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda. Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk Joseph Mkemwa alisema majeruhi huyo anaendelea vizuri na matatibu. Akisimulia tukio hilo, Luchoma alisema akiwa amelala chumbani, alishtukia akivamiwa na watu wawili baada ya mlango kuvunjwa. “Walipoingia ndani walinishika na mmoja alitoa panga na kunikata kiganja cha mkono wangu,” alisema Luchoma. Ndugu wa karibu wa Luchoma, Maliselina Jackson alidai kuwa alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa dada yake na alipoamka aliwaona watu wawili wakitoka chumbani. “Niliwaona watu wawili wakitoka chumbani alikolala dada wakiwa na kiganja cha mkono, nilipiga kelele za kuomba msaada,” alisema Jackson. Alisema ...