URUSI NA QATAR HUENDA ZISIANDAE KOMBE LA DUNIA

Mkuu wa kamati ya uhasibu wa shirikisho la soka duniani FIFA Domenico Scala amesema huenda Urusi na Qatar zikapoteza nafasi za kuyaandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 mtawalia iwapo ushahidi utaonyesha kulikuwa na ufisadi katika shughuli ya kinyanganyiro cha kupata kibali cha kuandaa mashindano hayo. Scala hata hivyo amesema mpaka kufikia sasa hawajapokea ushahidi wowote wa kudhihirisha kuwa nchi hizo mbili zilitoa hongo. Matamshi yake ndiyo ya kwanza kutolewa na afisa wa ngazi ya juu wa FIFA kuwa kuna uwezekano nchi hizo zikapokonywa uenyeji wa mashindano hayo. Maafisa wa idara ya mahakama wa Uswisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu kutolewa kwa kandrasi hiyo ya kuandaa mashindano ya 2018 na 2022 kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ufisadi katika FIFA. 

Chanzo: DW

0 comments:

Post a Comment