ALI KIBA - MVUMO WA RADI WATCH VIDEO & DOWNLOAD MP3


Ali Kiba ameachia audio na video ya Wimbo wake mpya Unaoitwa Mvumo wa Radi.

Kudownload audio    BOFYA HAPA

Kudownload video    BOFYA HAPA


Kutazama video hii hapa chini



GOODALL MWANASAYANSI WA AUSTRALIA (104) AMEJITOA UHAI WAKE NCHINI USWISI

David Goodall 
Mwanasayansi David Goodall, 104, aliyesafiri kutoka Australia hadi Uswisi ili kujitoa uhai amefariki katika kliniki moja nchini Uswisi, shirika linalotetea haki za watu wanaotaka kufa limetangaza.

Mwanaikolojia huyo ambaye pia alikuwa mtaalamu wa mimea hakuwa anaugua lakini alisema aliamua kujitoa uhai kutokana na kudhoofika kwa 'ubora wa maisha yake'.
Image result for david goodall
Goodall mwaka 1984 enzi za ujana.
Bw Goodall alikuwa amezua mjadala kutokana na safari yake ya kutoka Australia kwenda kujitoa uhai.
Muda mfupi kabla ya kifo chake, alisema alikuwa na "furaha kuhitimisha" maisha yake.

"Maisha yangu yamekuwa dhaifu sana kwa mwaka mmoja hivi uliopita na hivyo basi nina furaha kuyahitimisha," alisema akiwa amezingirwa na jamaa wake kadhaa.

"Nafikiria, kuangaziwa kwa kisa changu kutachangia kutetea haki za wazee kuruhusiwa kujitoa uhai, jambo ambalo nimekuwa nikitaka."

Mtazame Goodall katika video hii hapa chini:



Alifariki mwendo wa saa sita unusu mchana katika kliniki ya Life Cycle mjini Basel baada ya kudungwa sindano ya Nembutal, kwa mujibu wa Philip Nitschke mwanzilishi wa shirika la Exit International lililomsaidia kujitoa uhai.

"Najuta kufika umri huu," Dkt Goodall alisema mwezi uliopita katika sherehe ya kuzaliwa kwake, katika mahojiano na shirika la utangazaji la Australia.
Image result for david goodall

"Sina raha. Nataka kufa. Sio jambo la kuhuzunisha, kinachohuzunisha ni kwamba mtu anazuiwa kufa."
Ni jimbo moja pekee Australia lililohalalisha kujitoa uhai mwaka jana kufuatia mjadala mkali uliozusha mgawanyiko, lakini ili mtu kuruhusiwa, ni sharti awe anaugua mahututi.

Je ni mataifa gani mengine yanaruhusu kujitoa uhai?

  • Uswizi, ni nchi pekee iliyo na vituo vinavyotoa huduma hiyo kwa raia wa mataifa mengine.
  • Uholanzi, Ubelgiji na Luxembourg zinaruhusu, hata kwa watoto lakini katika hali maalum.
  • Colombia inaruhusu kujitoa uhai kwa hiari wakati mgonjwa akiwa hatibiki.
  • Majimbo sita ya Marekani - Oregon, Washington, Vermont, Montana, California na Colorado - yannaruhusu kwa wagonjwa mahututi wasio tibika.
  • Canada ililifuata jimbo la Quebec kuruhusu hilo mnamo 2016.
    Jamaa zake Goodall watajumuika naye huko Uswizi
    Jamaa zake Goodall walijumuika naye huko Uswisi kabla ya kifo chake.

Mjadala unazua mgawanyiko Afrika

Katika nchi nyingi tu Afrika, njia zote za kujitoa uhai zinatizamwa kama mauaji. Wataalamu barani Afrika wamepinga wito wa watu kutaka kujitoa uhai kwa hiari. Mjadala mkubwa umezuka kuhusu kinachotajwa kuwa 'kuuawa kwa huruma' hususani kwa wagonjwa walio mahututi na wasioweza kutibika

Lakini mkutano wa muungano wa wataalamu wa afya duniani katika mkutano mapema mwaka huu mjini Abuja Nigeria waliamua kwamba hatua hiyo inakwenda kinyume na kiapo cha matabibu na inakwenda kinyume na imani na maadili ya jamii za Kiafrika badala yake viongozi katika muungano hao wametaka kuboreshwa kwa huduma za kuwashughulukia wagonjwa mahututi wasioweza kutibika.

Masuala yaliozingatiwa katika kuptisha uamuzi huo ni sheria, dini, jamii na tamaduni, saikolojia na upana wa maadili kuhusu suala hilo. Wataalamu wa mataifa kutoka Afrika kusini, Kenya, Botswana, Zambia na Cote D'ivore (Ivory Coast) walipinga hoja hiyo ya kujitoa uhai kwa hiari wakisisitiza inakwenda kinyume na maadili ya utoaji matibabu.


 Chanzo: BBC

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI ATIMIZA MIAKA 93: TUJIKUMBUSHE HISTORIA YAKE KWA UFUPI

Mei 8, 1925 wkati huo Tanganyika ikiwa ni koloni la Uingereza alizaliwa Rais mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mzee Ali Hassan Mwinyi.

Image result for MWINYI in marathon 

Alipoingia madarakani kumpokea aliyekuwa Rais wa Awamu ya kwanza,Mwalimu Julius Nyerere mnamo tarehe 5 Novemba mwaka 1985, watanzania wachache sana (kama wapo) waliweza kutabiri kwamba miaka kumi baadaye na zaidi baada ya kustaafu rasmi, ataibuka kuwa mmojawapo wa maraisi wa Tanzania ambao watabakia kupendwa na kuheshimika kwa namna ya kipekee kabisa. Tunadiriki kusema “namna ya kipekee” kwa sababu ukweli unabakia kwamba inapofanyika tathmini ya uongozi wake, bado mtu au watu mbalimbali wanakuwa na maoni yao tofauti tofauti kuhusiana na suala hilo. Utoaji huo wa tathmini ni suala ambalo haliwezi kukoma leo wala kesho, ni tukio linaloendea na litakaloendelea, vizazi mpaka vizazi. Huo ndio uzuri au ubaya wa historia na muda (history and time) huwa vina jinsi ya kipekee katika kutoa hukumu zao.

Mpaka anakabidhi madaraka yake ya Urais kwa Rais wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa mnamo tarehe 23 November mwaka 1995, jina ambalo wengi tulipenda kulitumia ni “Mzee Ruksa” ingawa kamwe hatukuwahi kusahau kwamba jina lake kamili ni Ali Hassan Mwinyi, Raisi wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Ali Hassan Mwinyi alizaliwa tarehe 8 mwezi wa tano (Mei) mwaka 1923 katika kijiji cha Kivure,wilayani Kisarawe, mkoa wa Pwani,Tanzania Bara. Kama wengi wa viongozi wetu, Mwinyi naye alizaliwa katika iliyokuwa Tanganyika. Akiwa bado mwenye umri mdogo sana familia yake ilihamia Zanzibar. Kwa maana hiyo Mwinyi ni mzaliwa wa bara aliyekulia na kuendelea kuishi visiwani Zanzibar.

Alianza safari yake kielimu huko visiwani Zanzibar katika shule ya msingi Mangapwani kuanzia mwaka 1933 hadi 1936 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari Dole kwa ajili ya elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1937 mpaka mwaka 1942. Baada ya hapo alijiunga na Chuo Cha Ualimu Zanzibar kusomea ualimu kuanzia mwaka 1943 mpaka 1944.
Mwinyi katika picha rasmi ya wakati wa utawala wake.

Kuanzia mwaka 1945 mpaka mwaka 1950 alirejea tena katika shule ya Mangapwani,shule aliyosomea,safari hii akiwa sio mwanafunzi tena bali Mwalimu.Kuanzia mwaka 1950 mpaka 1954 alikuwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo wakati huo huo alikuwa akiongeza elimu yake kwa njia ya posta ambapo alijipatia General Certificate in Education (GCE) na pia alikuwa amejiunga na Durban University Institute of Education, United Kingdom (kwa njia ya posta tena) kusomea stashahada ya ualimu. Baada ya hapo alijiunga tena na Chuo Cha Ualimu Zanzibar kama mkufunzi kuanzia mwaka 1956 mpaka mwaka 1961 huku pia akiendelea kujisomea kwa njia ya posta kutoka Regent Institute kilichopo London nchini Uingereza ambapo alijipatia cheti cha ufundishaji lugha ya kiingereza.

Kuanzia mwaka 1961 mpaka 1962 alijiunga na Hall University, Uingereza katika Tutors’ Attachment Course. Mzee Mwinyi pia ana cheti ya lugha ya kiarabu alichokipatia Cairo nchini Misri kati ya mwaka 1972 na 1974.

Safari yake ya kisiasa aliianza rasmi mwaka 1964 alipojiunga na Afro Shiraz Party (ASP) huko Zanzibar ambapo alikitumikia chama katika ngazi na nafasi mbalimbali. Kati ya mwaka 1964 na 1965 alikuwa ni Katibu Mkuu wa muda katika wizara ya elimu Zanzibar kabla hajateuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi katika iliyokuwa Zanzibar State Trading Corporation (ZSTC).Hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1965 na mwaka 1970. Pia katika miaka hiyo hiyo,kuanzia mwaka 1966 mpaka 1970, Mwinyi alikuwa mweka hazina msaidizi katika tawi la ASP la Makadara,Zanzibar. Wakati huo huo pia kati ya mwaka 1964 mpaka 1977 alikuwa ni mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA)
Majukumu mengine aliyokuwa nayo miaka hiyo ni pamoja na uenyekiti wa Zanzibar Censorship Board (1964-1965), Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam na pia mwenyekiti wa Baraza la Chakula na Lishe.

Mwinyi (kushoto) akiwa na maraisi wenzake wastaafu Benjamini Mkapa (kulia) na Jakaya Mrisho Kikwete (katikati)

Kuanzia mwaka 1972 mpaka 1975, Mwinyi alikuwa ni Waziri wa Afya wa Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuanzia 1975 mpaka 1977. Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri cheo alichokitumikia mpaka mwaka 1982 aliporejea nyumbani na kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii cheo ambacho alikutumia kwa muda mfupi tu kwani mwaka 1983 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Raisi.
Mwaka 1984, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Raisi wa Zanzibar wakati huo,Alhaj Aboud Jumbe, Mwinyi alichaguliwa kuwa Raisi wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na wakati huo huo Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuanzia mwezi August mwaka huo huo wa 1984 Mwinyi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi cheo alichoendelea nacho mpaka mwaka 1990 baada ya kung’atuka kwa Hayati Mwalimu Nyerere kutoka katika kukiongoza Chama Cha Mapinduzi(CCM)

Mwinyi (wa pili kutoka kushoto) akishuhudia mchezo wa bao kati ya hayati Mwalimu Nyerere (wa pili kutoka kulia) na mzee mmoja wa Butiama(jina halijulikani).Wengine wanaoshuhudia ni Mama Maria Nyerere(kulia) na kaka yake Nyerere,Chief Burito(wa tatu kutoka kulia).Picha ilipigwa Butiama.

Lakini kabla ya hapo, mwaka 1985,Mwinyi alichaguliwa kuwa Raisi wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kustaafu kwa Mwalimu Nyerere. Mwinyi ni mtaalamu wa lugha ya Kiswahili na pia hupenda michezo hususani jogging. Mwinyi ameoa wake wawili (Sitti Mwinyi na Khadija Mwinyi), ana watoto na wajukuu. Anaishi Msasani jijini Dar-es-salaam.

Related image
Rai mstaafu Mwinyi akiwa na wastaafu wenziye Mkapa, Kikwete na Rais Magufuli. Picha kwa hisani ya Mwananchi Communication Limited.
MAKALA HII NI HAKIMILIKI YA JEFF MSANGI MWANDISHI WA TOVUTI YA BONGOCELEBRITY.

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda.

Zaidi ya watu milioni 15 katika bara hili huitumia lugha hii kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya Muungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika.

TANZANIA

Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa.
Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVITA, TATAKI (zamani TUKI pia TAKILUKI) na UKUTA. Pia vyuo vikuu mbalimbali vya Bara na Visiwani vilianza kufundisha Kiswahili kuanzia Shahada za Awali, Uzamili na Uzamivu kama vile Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha TanzaniA, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino n.k.

KENYA

Kiswahili nchini Kenya ni lugha rasmi na pia ni lugha ya Taifa. Rais wa kwanza wa taifa la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta alitoa kauli kwamba Kiswahili kinafaa kutumika kama lugha rasmi ya Kenya mwaka 1969. Mwaka 1975 kiswahili kilianza kutumika bungeni.Serikali ya Kenya ilianzisha somo la Kiswahili katika Idara ya Lugha za Kiafrika na Isimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Kuanzia miaka ya themanini mwishoni, takribani vyuo vikuu vyote vilivyoanzishwa na Serikali vilifundisha masomo ya Kiswahili kwa lugha ya hii.

UGANDA

Mwaka 1960, Serikali ya Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo. Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima. Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro hata kabla ya ukoloni mwaka 1862. Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.
Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi.
Wikendi hii Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, Keneth Cimara imeipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Katika warsha ya siku mbili iliyokamilika mwishoni mwa juma katika hoteli ya Imperial Royal mjini Kamapla iliyowajumuisha walimu wa vyuo vikuu, shule za upili na taasisi mbalimbali nchini Uganda.
Keneth Cimara amesema miaka ya themani raia wengi wa Uganda walikiona Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwanyanganya mali zao, aidha kuwatendea uhalifu.
Cimara ameongeza kwamba sasa Serikali ya Uganda ni miongoni mwa mataifa ya Jumuia ya Afrika Mashariki ambayo yameweka mikakati ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahi kama anavyosema tena Katibu mtendaji.


RWANDA

Kiswahili ni lugha rasmi nchini Rwanda. Kabla ya mwaka 1994, wakati wa mauaji ya kimbali lugha ya kiswahili ilizungumzwa kwenye miji tofauti nchini Rwanda.
Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.
Mwaka wa 1976-1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule za upili na chuo Kikuu Cha Rwanda

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Kiswahili kiliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya 19. Kiswahili kilianza kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo, kuelekea kandokando ya mto Kongo.

Pia kuna wazungumzaji wachache katika nchi za Burundi, Msumbiji, Comoros, Malawi , Madagascar na Zambia.


Chanzo: BBC

MIAKA 5 YA VENANCE BLOG NAWASHUKURU SANA KUWEPO HAPA TANGU KUANZISHWA KWAKE MEI 2013

VENANCE BLOG ilianzishwa Mei 2, 2013.

Alhamis ya tarehe 2 Mei, 2013 nilitimiza kiu yangu ya kufungua Blog hii, lilikuwa ni wazo lililoishi toka mwaka 2012 nilipoanza kufahamu matumizi ya mtandao na tarehe hiyo lengo hili lilitimia. Huu ni mwaka wa 5 sasa nikiwa katika tasnia hii.

Kuna wakati majukumu ya kitaaluma shuleni yanakaba sana mpaka nashindwa kuwa active kutokana na kufanya kazi hii nikiwa bado masomoni toka mwaka 2013 mpaka sasa.

Kuwepo kwa Blog hii kumesaidia baadhi ya watu kupata taarifa na habari nyingine kwa mfano zile za kielimu hasa wakati wa selection za vyuo vikuu. VENANCE BLOG imekua msaada kwa baadhi ya watu, nimekua nikiwapa taarifa za habari hizi hasa wale walio katika mazingira ya kutokua na access ya mtandao.

Pamoja na mengine mengi kama haya nimekua nikiitumia Blog hii kama platform ya kuchapisha mashairi yangu ambayo nimekua nikiyaandika kwa nyakati tofauti tofauti. Nawashukuruni sana wasomaji wangu kwa kutembelea Blog hii na kuyasoma mashairi hayo na pia kutumia muda wenu kutoa maoni kadiri inavyowapendeza. Asanteni sana.

Aidha nimekua nikiandika habari za kitaifa, kimataifa, siasa, udaku, nyimbo mpya, video mpya, habari za masuala ya anga, Teknolojia, Michezo, nimekua nikiandika pia nukuu kutoka kwa wanafalsafa wakubwa dunia na watu wengineo kama vile wanasiasa, wanamuziki, wanaharakati wa masuala tofauti tofauti n.k. Aidha nimekua nikiandika habari za mitindo na mambo mengine kadha wa kadha.

Habari, Picha, Matukio na mambo mengine ninayoyachapisha hapa nimekua nikipitia kwa ukaribu katika vyanzo makini kama vile Habari Leo, Mwananchi, BBC, DW, VoA, Jarida la Mitindo la Vogue, Forbes, Kitabu cha kumbukumbu cha rekodi za dunia Guinness, Blogs za watu binafsi, taasisi na kadhalika.

Katika mwaka huu wa 5 naahidi kuendelea kufanya kazi hii kwa ukaribu kabisa na watu, moja ya mpango wa hivi karibuni ni kuanza kuandika habari za matangazo ya kazi pamoja na kuongeza zaidi taarifa za nafasi za masomo ya nje ya nchi (scholarship) ambayo hii tayari nimeanza kuifanyia kazi. Pia kuna mengine mengi yanakuja katika Blog hii. Endelea kufuatilia VENANCE BLOG na nakushukuru sana kuendelea kuwa msomaji wa Blog hii.


Kwa maoni na mengineyo, wasiliana nami kwa moja kati ya njia hizi:
barua pepe: venancegilbert@gmail.com

Simu ya mkononi: 0753400208.

ZIFAHAMU TEKNOLOJIA 7 ZITAZOKAZOKUZA MAENDELEO YA MAJIJI MAKUBWA DUNIANI

Fikiria ulikuwa unafanya kazi katika taasisi ya maendeleo na kupunguza umasikini mwanzoni mwa miaka ya 1990. Mwandishi wa makala hii, Abhas Jha anasema yeye aliwahi kufanya kazi zama hizi. Anasema kipindi hicho kulikuwa na tovuti moja tu iliyokuwepo duniani mpaka kufikia Agosti mwaka 1991 (leo kuna zaidi ya tovuti bilioni 1.5 duniani kote). Anasema kipindi hicho simu za mkononi zilikuwa ghali sana, chache na zilikuwa nzito na za kishamba sana ukilinganisha na hizi za sasa. Ni watu wachache wangetazamia kuhusu hali iliyopo nchini India kwa sasa kwamba kungekua na idadi kubwa ya simu za mkononi kuilko idadi ya vyoo.

Bill Gates aliwahi kusema "tunayapa uzito sana mabadiliko ambayo yatatokea ndani ya kipindi cha muda mfupi sana na kuyapuuza yale yaliyotokea kwa muda mrefu sana". Teknolojia inakua kwa kasi sana na kufanya na mabadiliko makubwa sana kwenye majiji ili kufikisha huduma kwa jamii. Teknolojia inafanya hivi ili sio tu kufikisha huduma haraka kwa wateja bali pia kukuza uchumi na kuimarisha namna ya kufanya mikakati ya kuboresha njia za kuongeza ufanisi wa kifedha.

Hizi hapa ni teknolojia 7 zilizofanya na zitakazokuja kufanya mabadiliko makubwa sana katika majiji duniani na kufanya mabadiliko ya ufikishaji wa huduma kwa wateja:

1. TEKNOLOJIA YA MTANDAO (INTERNET) YA 5G


5G inasimama kwa kumaanisha "kizazi cha tano". Hii ni teknolojia ambayo itatumika kwa simu za mikononi na kompyuta kurahisisha uharaka wa mtanadao, inategemewa kuanza kutumika rasmi kuanzaia mwaka 2020 kwa sasa bado iko katika majaribio. Itakuwa na uwezo mara 40-60 ya uwezo wa teknojia ya sasa ya mtandao wa simu za mkononi. Benki ya Dunia inasema kwamba "kwa ongezeko la 10% la kasi ya mtandao, uchumi utaongezeka kwa 1.3% na kupelekea kile kinachoitwa kitaalamu uhuru wa ugunduzi. Kwa mujibu wa Jukwaa la Uchumi la Benki ya Dunia wanasema kwamba "kama 40% tu ya watu wote wangetumia mtandao duniani, tungeweza kuongeza pato la dunia kwa kiasi cha dola za Marekani $1 trilioni kwa kuunganisha watu wengine milioni 327". Mtandao wa 5G utasaidia matumizi madogo, matumizi madogo ya vifaa vya kuhisi (sensor) ambavyo vitawekwa kwenye majengo, magari, vifaa vingine n.k. Kiufupi utakuwa ni "mtandao wa muunganiko wa vitu" yaani Internet of Things (ToT)

Benki Kuu ya Dunia inakubaliana na miradi mikubwa ambayo ufikishwaji wake unategemea mtandao kwa mfano mradi mkubwa unaojulikana kama BridgeIT nchini Tanzania unaofanya urahisishaji wa kuangalia video za kidijitali madarasani wakati wa kufundisha na kujifunza kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi. Mtandao wa 5G utarahisisha sana matumizi ya mambo haya na mengineyo.

2. TEKNOJIA YA MALIPO YA KIFEDHA "BLOCKCHAIN"

Hii ni teknolojia ya malipo ambayo inafanywa na bitcoin. Teknolojia hii itaweza kurahisisha malipo kama jinsi mtandao unavyofanya kufikisha taarifa kwa haraka zaidi. Lengo la teknolojia hii ni kusambaza mifumo ambayo itasaidia kufanya malipo kwa njia ya mtandao kwa haraka ziadi hata ya mifumo mingine kama Western Union, PayPal, MasterCard na VISA. Hii itasaidia miamala ya kifedha kufanyika bila kuwepo na upatanishi kwa mfano kupitia soko la hisa ambayo kwa sasa inafanya kazi kama mpatanishi wa miamala.

Teknolojia hii inatumiaka kwa matumizi mbalimbali kama vile kurahisisha usajili wa maeneo na kurahisisha usalama wa chakula nchini China. Benki ya Dunia inasema imechapisha makala ambayo inaitambua teknolojia hii kama kichocheo cha maendeleo ya kimataifa. Pia teknolojia hii imesaidia kuwalipa mamilioni ya watu wanaofanya michezo ya upatu mtandaoni na hata wale wanaofanya baadhi ya kazi za bitcoin.

3. TEKNOLOJIA YA AKILI BANDIA "ARTIFICIAL INTELLIGENCE" INAYOHUSISHA KUJIFUNZA KWA VIFAA "MACHINE LEARNING" NA DATA KUBWA "BIG DATA"

Kuna baadhi ya wataalamu kama Stephen Hawking (mtaalamu wa Fizikia aliyefariki Machi 14 mwaka huu) na Elon Musk waliowahi kuonya dhidi ya matumizi ya teknolojia hii ambayo ina madhara makubwa  baadaye. Wengine kama vile Fei-Fei Li, ambaye ni profesa wa Sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu Stanford anasema kwamba "tunakaribia kwenye mashine ya kufua kuliko kuharibu mambo" akiwa na maana kwamba tunaelekea kwenye urahisi zaidi wa mambo kuliko hatari ambazo watu wanafikiria kuhusu teknolojia hii.

Aliongezea kwamba teknolojia hii ya akili bandia "Artificial Intelligence" na data kubwa, ni teknolojia ambazo zinarahisisha urahisi wa mambo hasa katika majiji ambayo yanahitaji matumizi makubwa ya data kama vile Shanghai, Hong Kong, Sydney na New York hususani katika maeneo ambayo yanafanya maegesho ya magari kwa teknolojia hii, kusimamia ubora wa hewa na kuongeza matumizi ya nishati katika majengo makubwa na marefu.
Kwanza, tufahamu Artificial Intelligence na Machine Learning ni nini? Artificial Intelligence ama kwa ufupi AI kwa lugha nyepesi tunaweza kusema ni Akili Bandia, inaitwa hivi kwa vile Akili Asilia anayo mwanadamu tu. AI ni matokeo ya Akili Asilia. Pia, Machine Learning (ML) ama kwa tafsiri yangu nyepesi Ujifunzaji wa Vifaa kwa Kujazwa Taarifa ni tokeo la AI. Kwa hivyo AI na ML ni dhana mbili zinazokwenda sambamba, dhana hizi zinahusika na utengenezaji wa kanuni ambazo zinaruhusu Kompyuta kufanya kazi ambazo zinahitaji akili ya mwanadamu. AI ni uwanda mpana wa Sayansi ya Kompyuta ambao unalenga kutengeneza mifumo inayoweza kufanya kazi ambazo zikifanywa na mwanadamu huhitaji akili. Mambo hayo ni utatuzi wa changamoto, ufahamu na utambuzi wa lugha, kutambua kanuni na mifumo ya asili na kufanya maamuzi. AI ipo katika aina mbili: Akili Bandia Nyembamba (Narrow AI) ambayo imetengenezwa na kufunzwa kwa kazi mahsusi na Akili Bandia ya Jumla (General AI) ambayo iko na utambuzi na sifa zote za akili ya mwanadamu. 
ML ni kipengele cha AI ambacho kinahusika na utengenezaji wa kanuni (algorithms) ambazo zinaruhusu Kompyuta kujifunza na kufanya maamuzi kutokana na taarifa zinawekwa katika kifaa husika. Badala ya kujazwa taarifa za kufanya kazi mahsusi, kanuni za ML zinatumia njia za kitakwimu kujifunza mambo mbalimbali kutokana na taarifa zinazowekwa katika kifaa husika. Kuna aina kadhaa za ML ambazo nitazitaja tu kwa lugha ya kigeni:

(i) Supervised Learning
(ii) Unsupervised Learning
(iii) Reinforcement Learning

AI na ML zinatumika katika uwanda mpana wa mambo mengi mathalani:
• Utambuzi wa Sauti na Uzungumzaji (Voice and speech recognition) kwa mfano katika huduma kama Siri au Google Assistant. 
• Utambuzi wa Picha (Image recognition)
• Vipimo vya Kitabibu (Medical diagnosis)
• Utabiri wa masuala ya fedha (Financial forecasting)
• Njia tofauti za masoko (Personalized marketing)
• Gari zinazojiendesha (Self-driving cars) na mengine mengi. 

Na pili, tuangalie Big Data ama kwa tafsiri yangu nyepesi nimeamuia kuita Data Kubwa. Kwa maana nyepesi kabisa data kubwa ni taarifa ambazo ni kubwa (kama jina lenyewe) na hivyo huwa ni changamoto kuzipangilia, kuzichakata na kuzichanganua kwa kutumia njia za kawaida/asili za uchanganuzi wa taarifa. Big data inasifika kwa kuhusu mambo matatu ambayo ni ukubwa (volume), kasi (volume) na namna nyingi (variety). Matumizi ya data kubwa yanasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi, kuchochea umaizi (insights) na maendeleo. Big data inasaidia katika nyanja zifuatazo:
(i) Afya, hapa teknolojia hii inasaidia kutabiri mlipuko wa magonjwa (disease outbreak prediction), namna ya kuboresha huduma ya afya kwa wagonjwa (optimized patient care), ugunduzi wa dawa (drug discovery) na mengine mengi.
(ii) Fedha, benki na taasisi nyingine za kifedha zinatumia teknolojia hii kugundua udanganyifu (fraud detection), kupima madhara (risk assessment), upangiliaji wa taarifa za kibiashara kutokana na mapendeleo ya mtu (algorithmic trading) na mgawanyo wa mateja (customer segmentation)
(iii) Elimu, taasisi na majukwaa ya kielimu yanatumia biga data kufahamu maendeleo ya wanafunzi katika masomo (student performance), kuboresha njia za ujifunzaji (personalized learning paths) na kutabiri kiwango cha idadi ya wanafunzi watakaoshindwa kuendelea na masomo (dropout rates).
(iv) Kilimo, wakulima wanatumia teknolojia hii kufanya kilimo kuwa cha kisasa (precision agriculture) ambacho kinatumia taarifa za kiteknolojia ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kupunguza hasara zitokanazo na shughuli za kilimo. Teknolojia hii inawasaidia wakulima kupitia picha za satelaiti kuhusu upatikanaji au ukosefu wa mvua na majanga ya asili, vifaa vinavyohisi (sensor) katika kilimo, matumizi ya ndege zisizo na rubani (drones) katika kilimo hasa upuliziaji wa madawa ili kuboresha uzalishaji na matumizi ya raslimali.
(v) Mauzo, big data inasaidia watoa huduma za mauzo kufahamu vitu wapendavyo wateja (customer preference), kuboresha mikakati ya mauzo (optimize pricing strategies), kusaidia ugunduzi (managing inventory) na ufikishaji wa huduma za masoko kwa wateja wa aina tofauti kwa njia mbalimbali (tailor marketing campaigns)
(vi) Burudani, big data inatumika kupendekeza mambo ya kutazama/kusikiliza kwa watazamaji wa huduma za mtandaoni (streaming) kulingana upendeleo wa mtazamaji na historia ya mambo aliyotazama katika kwa mfano watumiaji wa YouTube, Netflix, Hulu, Amazon Prime Video, Max, Disney+, Apple TV+, Spotify, Tidal, Apple Music, Paramount+ n.k. Hapa teknolojia hii inapendekeza nyimbo na picha mjongeo (video) pamoja na filamu ama michezo ya kuigiza (drama series)
(vii) Nishati, kampuni zinatumia big data kufahamu vifaa ambavyo vimeshindwa kufanya kazi (equipment failure), kuboresha namna ya usambazaji wa nishati (optimize energy distribution) na matumizi ya njia za nishati zisizo na madhara katika mazingira na zinazoweza kutumika kwa ufanisi (integrate renewable sources efficiently)
(viii) Uboreshaji wa miji na majiji, teknolojia hii inasaidia mipango miji (urban planning), upatikanaji wa hewa safi (monitoring air quality), uboreshaji wa huduma za usafiri wa umma (optimize public transport) na usafi wa miji (waste management).
(ix) Viwanda, big data inasaidia viwandani kufahamu vifaa vinavyohitaji matengenezo (predict maintenance), kuhakikisha ubora ya bidhaa inayozalishwa kiwandani (product quality assurance) na uboreshaji wa mnyororo wa thamani (supply chain optimization).
(x) Mitandao ya Kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram n.k. hutumia teknolojia hii kupendekeza maudhui anayoweza kuyapenda mtumiaji wa mtandao (tailor content suggestion), kufahamu maudhui yanayotazamwa au kufuatiliwa sana (detecting trending topics) na kupendekeza matangazo kulingana na tabia za mtumiaji wa mtandao (target advertisments)
(xi) Usafirishaji, teknolojia hii inasaidia kuboresha safari (route optimization), kupendekeza matengenezo ya vyombo vya usafirishaji (predictive maintenance of vehicles) na uchanganuzi wa taarifa za barabarani ili kupunguza msongamano barabarani na ucheleweshwaji wa huduma (analyzing traffic patterns to reduce congestion)
(xii) Michezo, walimu wa mpira wa miguu (coaches) na timu zao wanatumia big data kufahamu ufanisi wa wachezaji (evaluate player performance), kuboresha mikakati ya mchezo (strategize game plans), na kufatilia maendeleo na hatua za kumnunua na kumuajiri mchezaji katika timu (scouting and player recruitment)
(xiii) Biashara mtandao (E-commerce), watoa huduma za mauzo mtandaoni huchanganua taarifa za watumiaji (analyze customer behavior), kuboresha matokeo ya utafutaji wa bidhaa au huduma (optimize search results) na ufikishaji wa huduma za masoko kwa wateja wa aina tofauti kwa njia mbalimbali  (tailor marketing campaigns)
Hayo ni machache katika mengi ambayo teknolojia hii imesaidia utendaji kazi wa mambo kadha wa kadha.

4. TEKNOLOJIA YA MAGARI YANAYOJIENDESHA "AUTONOMOUS VEHICLES (AV)"

Licha ya kuwepo taarifa ya hivi karibuni kuhusu kifo cha mtembea kwa miguu kugongwa na gari linalojiendesha, teknolojia hii bado itakuwa ni ya kushangaza na bora zaidi na itakuwa na matokeo mazuri sana katika majiji makubwa na kwingineko ulimwenguni.
Mwaka 2016 John Zimmer ambaye ni miongoni mwa waanzilishi na Rais wa kampuni ya Lyft ambayo inahusika na utengenezaji wa magari hayo alichapisha chapisho refu ambapo alidai kuwa teknolojia hii ya magari yanayojiendesha itachukua nafasi ya teksi ndani ya miaka 5 na mpaka kufikia mwaka 2025 umiliki binafsi wa gari nchi Marekani katika majiji makubwa utafikia kikomo kutokana na teknolojia hii ya magari kuanza kutumika katika majiji hayo. Nimeamua kuiita teknolojia hii kama teknolojia ya magari huru kutokana na kutoendeshwa na mtu; ni magari yanayojiongoza yenyewe.


5. TEKNOLOJIA YA BEI RAHISI YA UTAFITI WA ANGA "LOW-COST SPACE EXPLORATION"

Kampuni ya Elon Musk, Heavy Reusable Rocket inao uwezo wa kutengeneza roketi kwa gharama za dola za Marekni 1000. Hii ni teknolojia ambayo itakuwa ni ya kushangaza na kurahisisha sana utafiti wa anga kwa maisha ya mwanadamu. Musk ana wazo la kufanya utafiti wa usafiri wa anga kutoka jiji moja hadi jingine kwa kutumia roketi ambayo kwa mawazo yake ni kwamba ingerahisisha kwenda mahala popote duniani ndani ya saa moja tu kwa kutumia teknolojia hii.
Kulingana na utafiti uliofanywa na taasisi ya tafiti ya Gartner, zaidi ya vitu bilioni 20 vitakuwa vimeunganishwa dunia nzima mpka kufikia mwaka 2020. Wanadai kuwa teknolojia hii itashirikiana na ile ya OneWeb ili kusambaza satelaiti ndogo ili kuunda mkusanyiko ambao utafanikisha kutataua changamoto kubwa ya kutoa urahisi wa kuunganisha watu zaidi ya bilioni 4 duniani kote kuwa na urahisi wa kupata huduma ya mtandao kwa wale ambao wasingefikiwa na huduma hii kutokana na kuwa katika maeneo ambayo mtandao ungekuwa kitendawili kwao. Huduma hii pia itaunganisha mambo bilioni 20 ambao yataletwa na teknolojia ya Mtandao wa Muunganiko wa Vitu "Internrt of Things (IoT)" 


6. TEKNOLOJIA YA UTAMBUZI YA KIELEKTRONIKI-BAIOMETRIKI (BIOMETRIC) INAYOHUSISHA VITAMBULISHO VYA KISASA (DIGITAL ID) NA MALIPO YA KISASA (DIGITAL PAYMENTS)

Idara ya Utambuzi kwa Mandeleo ya Benki ya Dunia (ID4D) imekediria kwamba takribani watu bilioni 1.1 hawana uwezo wa kuhakiki vitambulisho vyao (hii ni sawa na mtu 1 katika kila mkusanyiko wa watu 7) Haya ni mabadiliko ya haraka sana. Idara ya Aadhar nchini India imesajili takribani watu bilioni 1.1. Kwa kuruhusu Aadhar kama mfumo rasmi wa vitambulisho, kulingana na utafiti mmoja, kiwango cha ushirikishwaji wa kifedha nchini India umeongezeka kwa 24% miongoni mwa wanawake kati ya mwaka 2014 na 2015. Kwa pamoja, makadirio  yanaonesha kuwa akaunti takribani milioni 22o zilifunguliwa kufiki April 2016.
Kuunganisha malipo kwa mfumo huu kumesidia kufanya malipo ya ruzuku na pesa na mabo mengine kwa kutumia vitambylisho vya baiometriki kumepunguza udanganyifu, ujanja ujanja na rushwa kwa mfano kutambua watumishi hwa nchini Nigeria.

Mfumo wa Vitambulisho vya kisasa unaohusisha na progamu za simu za mkononi pia ulianzishwa nchini Algeria, Cameroon, Jordan, Italia, Senegal na Thailand ukienda sambamba na tangazo la kuwepo kwa matumizi ya mpango huu nchini Uholanzi, Bulgaria, Norway, Liberia, Poland, Jamaica na Sri Lanka pamoja na kujaribiwa jijini Mynmar nchini Burma. Teknolojia hii kwa sasa inahusisha mfumo ya kibaiometriki kwa mfumo wa alama za vidole (fingerprint).

7. TEKNOLOJIA YA VIFAA VYA ANGA VISIVYO NA WAONGOZAJI NDANI YAKE "UNMANNED AERIAL VEHICLES (UAVs) mathalani Drones

UAVs ni vifaa ambavyo vinajiongoza bila kuendeshwa na rubani ndani yake aidha kwa kuongozwa na mtu aliyeko chini au katika kifaa kingine ama kuongozwa na Kompyuta iliyoko ndani ya kifaa husika. Hii ni teknolojia ambayo kwa sasa imesaidia sana upatikanaji wa taarifa ndani ya muda mfupi sana hasa hasa kwa kamera ambazo huongozwa kwa kutumia rimoti. Mawasiliano yanakuwepo baina ya kamera hii na muongozaji ambaye anakua ardhini kuiongoza kamera hiyo. Wakati mwingine kamera hii inaweza kujiongoza yanyewe kwa kutumia kompuya inayokuwa ndani ya kamera hiyo. Teknolojia hii ilisaidia kupata taarifa kuhusu mafuriko yaliyosumbua jiji la Dar es Salaam mwezi April mwaka 2018.

Changamoto ya teknolojia hii ni nguzo za umeme, miti mirefu na upepo mkali ambavyo ni vikwazo vinavyozuia kamera hizi kwenda umbali mrefu sana. Kama kunakuwa hakuna vikwazo hivi, kamera hizi zinauwezo wa kusafiri kulingana jinsi kilivvyowekewa umbali husika.

Ndege zisizo na rubani (Drones) zimesaidia katika mambo mengi kwa sasa mathalani upuliziaji wa dawa na uangalizi wa afya ya mazao mashambani, ulinzi na usalama, upigaji picha za matukio mbalimbali, ukaguzi wa madaraja, nguzo za umeme, ufikishaji wa huduma kwa wateja na uangalizi wa mazingira hasa misitu, mbuga na kufatilia mabadiliko ya kimazingira.


Benki ya Dunia ina uwezo wa kufanya jambo la msingi katika teknolojia hizi ili kuhakikisha kuwa zinatumiaka kote duniani na kuzingatia kuwa hata masikini hawaachwi mbali sana na teknolojia hii. Kwa kuhitimisha ni kwamba Ripoti ya Mendeleo Duniani ya mwaka 2016 kuhusu mgawanyo wa teknolojia ya kisasa unatoe masomo  matatu:

1. Kutumia data ili kulenga maeneo ambayo yako mbali sana na upatikanaji wa mtandao kama jinsi Sao Paulo walifanya kuwa na taarifa za kijografia kufanya kipaumbele kuhusu makazi.

2. Kufungua data ili kurahisisha uwazi hii ikijumuisha kuwa na ramani za vitu, uchafuzi na mahitaji ya jamii huko Kiberia, eneo ambalo halina makazi yaliyipangiliwa jijini Nairobi; na

3. Kuwepo na teknolojia ya kuunganisha simu za mkononi ili kurahisisha ushiriki wa wanchi kama jinsi majiji ya nchini Ufilipino kwa kushirikisha wananchi wake katika bajeti za majiji hayo.


MAKALA HII IMENDALIWA NA BENKI YA DUNIA NA KUTAFSIRIWA NA KUONGEZWA MANENO MENGINE NA VENANCE BLOG.

MAWASILIANO
barua pepe: venancegilbert@gmail.com
simu: 0753400208

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: FIFA IMESEMA ITAZIPA DOLA MILIONI 2 NCHI ZA AFRIKA ZINAZOSHIRIKI KOMBE LA DUNIA



FIFA itatoa zawadi ya dola milioni mbili kwa kila mojawapo ya timu tano za Afrika zilizofuzu kucheza kombe la dunia kuzisaidia katika maandalizi, amesema rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF.
Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia, zimefuzu kushiriki katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi, na rais wa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad, alismea katika taarifa kwamba fedha hizo zitatumika "kushughulikia mapema, suala la bonasi za wachezaji."
"Migogoro juu ya malipo katika michuano iliyopita ilipelekea kuwepo na hali zilizoathiri vibaya taswira ya soka barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kuathiri kwa kiwango kikubwa utendaji wa timu viwanjani," aliongeza.
Mwaka uliopita, shirikisho la kandanda la Nigeria (NFF) lilisaini makubaliano na wachezaji wake wakiahidi kujiepusha na migogoro ya bonasi na malipo ambayo imeharibu kampeni zao za nyuma za kombe la dunia.
Wachezaji wa timu ya Nigeria, Super Eagles walihusika katika mzozo wa muda mrefu kuelekea mashindano ya kombe la shirikisho la mwaka 2013 nchini Brazil, na mgogoro juu ya bonasi pia ukavuruga kampeni yao ya kombe la dunia mwaka 2014.
Matatizo sawa na hayo yameziathiri timu nyingine na bara la Afrika.
Time 32 zinashiriki katika michuano ya kombe la dunia inayofanyika kuanzia Juni hadi Julai, hupokea kitita cha dola milioni 1.5 kila mmoja kutoka FIFA katika mfumo wa malipo ya maandalizi, na zinahakikishiwa kingine kisichopungua dola milioni 8 katika fedha za zawaidi baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

Chanzo DW

FACEBOOK KUANZISHA PROGRAMU YA KUWAPATANISHA WAPENDANAO HUKU IKIIMARISHA KIWANGO CHA FARAGHA

Mark Zuckerberg mmiliki wa mtandao wa Facebook
Kampuni ya Facebook inaongeza faragha kwa watumiaji wake kwa kuweka sehemu ya kufuta historia ya ulichokitafuta katika mtandao huo wa kijamii.
Aidha amesema kwamba programu hiyo itaangazia uhusiano wa muda mrefu na sio urafiki wa muda mfupi na itawatenganisha marafiki na watu wanaotarajiwa kuwa na uhusiano.
''Programu hii itakuwa na kiwango cha juu cha siri na usalama kutoka mwanzo'', aliongeza.
Hivi karibuni kampuni hiyo ilikumbwa na kashfa ya kutothamini faragha za watumiaje wake huku watumiaji zaidi ya millioni hamsini walidukuliwa katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani.
Facebook imekua katika sakata la faragha ya watumiaje hivi karibuni, mamilioni ya taarifa za watumiaji zilichukuliwa bila ridhaa na kampuni ya Cambridge Analytica kwa matumizi ya wanasiasa. Mark Zuckerberg amesema kuwa atahakikisha suala kama hilo halitajitokeza tena, kwa kutengeneza ulinzi zaidi wa mtandao huo. Kitendo hicho kilishusha mapato ya Facebook karibu asilimia 15 ya mapato ya awali.
''Kilichotokea kwa Cambridge Analytica ilikua uvunjifu wa uaminifu wa hali ya juu, walichukua data za watu na kuziuza, hivyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa suala hili halitokei tena, kwanza tunaweka vizuizi kwa data ambapo mtu atakua anaombwa kwa ridhaa yake, na pili tunahakikisha tunazijua program mbaya zote'' alisema Zuckerberg.
Katika mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo ya mjini California, Zuckerberg ameongeza pia wanaimarisha faragha ambapo itamruhusu mtumiaji kufuta historia ya kitu alichotafuta.

Chanzo BBC

MOHAMMED SALAH: ILIKUAJE AKAIMARIKA HARAKA? MAJIBU HAYA HAPA

Mohammed Salah
Huku wachezaji wakisherehekea kwa fujo baada 4-0 dhidi ya ENPPI, kocha Said Al Shesheni aliangalia upande mmoja na kugundua kwamba mchezaji mmoja wa kikosi cha al-Mokawloon wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16 hakuwa akifurahia michuano iliokuwa Cairo. Alikuwa akibubujikwa na machozi kwamba jina lake halikuwa katika orodha ya wafungaji mabao. Akicheza kama beki wa kushoto ilikuwa vigumu kuchukua jukumu kubwa kama alivyotaka.
Akiwa mzaliwa wa eneo la Nagrig, kijiji kimoja kilichopo kilomita 130 Kaskazini mwa mji mkuu wa Misri, mchezaji huyo alilazimika kupitia tatizo la kusafiri kwa saa tisa kila siku mara nyingine akilazimika kutumia mabasi 10, ili kuweza kufika mazoezini mbali na kushiriki mechi.
Na baada ya kufurahishwa na ari ya kijana huyo Al Sheheni alimpatia fursa na kumpeleka safu ya mbele. Tangu wakati huo Mohammed Salah hajarudi nyuma tena.
Kijana katika uwanja wa Mo salah
Mchezaji huyo wa Liverpool alilazimika kulipia uwanja mpya katika shule yake ya zamani.

Habari hiyo ni jibu kwa swali ambalo limekuwa katika fikra za mashabiki wa soka duniani: Mchezaji ambaye hakuwa na athari yoyote kimchezo katika ligi kuu za Ulaya mara moja amekuwa mfungaji bora akilinganishwa na Lionel Messi na Christiano Ronaldo.
Katika soka inasaidia wakati mchezaji anapojikuta katika eneo analohitajika kuwa na katika wakati ufaao. Lakini ni watu wachache waliokuwa na hilo wakati Liverpool ilipotangaza usajili wa Salah kutoka klabu ya Italia ya Rome mwaka uliopita .
Kitita cha $55.7m kinaonekana kuwa cha juu kwa mchezaji ambaye alikuwa amefeli kuonyesha umahiri wake katika soka ya Uingereza baada ya kuhudumu kwa zaidi ya mwaka mmoja akiwa Chelsea 2015.
Pia ni muhimu kuona kwamba Misri sio timu yenye umaarufu mkubwa katika soka duniani, ijapokuwa ina umaarufu mkubwa barani Afrika, baada ya kushinda taji la kombe la Afrika mara saba.
Lakini The Pharaoh wamecheza katika michuano miwili ya kombe la dunia 1934 na 1990 na hadi Salah alipoimarika, ilikuwa rahisi kutajwa kwa kuwa kipa Essam El-Hadary yuko katika harakati za kuwa mchezaji mkongwe zaidi kushirki katika kombe la dunia, wakati Misri iliporejea katika kinyang'anyiro hicho nchini Urusi.
Timu ya taifa ya Misri
Misri imeshiriki katika michuano miwili pekee ya kombe la dunia lakini wamefaulu kushiriki Urusi 2018

Ni nini kilichofanyika kimakosa kwa Salah mapema alipocheza Uingereza? Kwanza Salah alishiriki katika ligi ya Switzerland, ambayo haina ushindani mkubwa kama ile ya Uingereza.
Akiwa Chelsea pia alikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji walioimarika na hakupata fursa za kutosha kuonyesha umahiri wake.
Raia huyo wa Misri alicheza mechi 19 kwa klabu hiyo ya London huku akianzishwa katika mechi tisa pekee. Ni mara mbili pekee alipocheza dakika zote 90. Salah baadaye alipelekwa kwa mkopo kwa vilabu vya Italia kabla ya kusainiwa na Roma kwa msimu wa 2015/16
Ni wakati huo ambapo Salah alionyesha umahiri wake na kufunga mabao 34 katika misimu miwili kabla ya kuelekea Liverpool.
Image result for mohamed salah with mourinho at chelsea
Salah hakuweza kufanya vizuri chini ya usimamizi wa Mourinho akiwa Chelsea: Alicheza mechi 19 na kufunga mabao 2 pekee.
"Alikuwa mtoto alipowasili Chelsea na Chelsea ilikuwa na kikosi kizuri hivyo basi ilikuwa vigumu'', alisema mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp akizungumza na runinga ya Ujerumani wiki hii.
"Nadhani sote lazima tukubaliane kwamba Jose Mourinho ni kocha mzuri kwa hivyo mara nyengine mambo huwa hivyo. Kwa hivyo iwapo haiwezekani jiondoe ujaribu tena na hivyo ndivyo ilivyokuwa na Mohamed."
Katika ziara ya hivi karibuni Anfield, Mourinho, ambaye sasa ni mkufunzi wa Manchester United alionekana akimkumbatia raia huyo wa Misri.
Na mahojiano na ESPN Brasil yaliorushwa hewani Jumapili iliopita, raia huyo wa Ureno alizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na mchezaji huyo.
''Ni mimi ndiye niliyemsaini Salah na uamuzi wa kumuuza haukuwa wangu, bali ulikuwa wa Chelsea''.
''Ni mtu mzuri , lakini alikuwa mdogo na hakuwa amejiandaa kimaungo na kifikra wakati alipwasili. Pia alipata utamaduni tofauti. Nafurahi sana kumuona anaendelea vyema, hususan kwa sababu hajafunga dhidi ya United'', alifanya mzaha.
Image result for mohamed salah with klopp
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp akimkumbatia Mohammed Salah
Inawezekana kwamba magoli aliyofunga katika msimu wa 2017/18 yalipita kiwango ambacho mchezaji huyo alikuwa ametaka kuafikia. Katika mechi 48 alizochezea Liverpool katika mashindano yote, raia huyo wa Misri alifunga mabao 43 na kusaidia pasi za mabao 15.
Amekuwa nyota katika kombe la vilabu bingwa Ulaya ambapo ameisaidia Liverpool kukaribia kufika fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu 2007.
Raia huyo wa Misri ni baraka kwa aina ya mchezo wa Klopp kwa kasi na mashambulio.
Mbali na mafanikio yake, Salah anaweza kufanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza wa Afrika kushinda taji la mfungaji bora Ulaya, taji analokabidhiwa mfungaji bora katika ligi ya Ulaya.
Na msimu wa Salah hautakamilika katika wikendi ya mwisho ya ligi kuu ya Uingerza. Timu ya taifa imefanikiwa kufuzu katika kombe la dunia la 2018 ikiwa ni mara kwanza katika kipindi cha miaka 28 baada ya kampeni ya kuwania kufuzu ambapo Salah alifunga mabao matano kati ya manane huku akitoa usaidizi wa mabao mawili.
Ushujaa wake ulihusisha penalti ya dakika 94 dhidi ya Congo ambayo ilikamilisha kufuzu kwa taifa hilo katika kombe la dunia .
Mo Salah akiichezea Egypt
Salah alifunga mabao matano kati ya magoli ya Misri katika kombe la kombe la dunia.
Na kudhania kwamba kuimarika kwake kulianza kwa bahati. Mnamo mwezi Machi 2012, soka la Misri lilikuwa limedorora: ligi ya taifa hilo ilisitishwa kutokana na janga la uwanja wa Port Said - maandamano ambayo mapema takriban watu 70 walifariki huku wengine 500 wakijeruhiwa.
Huku wakitafuta kushiriki katika mechi kwa maandalizi ya michezo ya Olimpiki mjini London, timu hiyo ya Misri yenye wachezaji wasiozidi umri ya miaka 23 walipanga mechi za kirafiki hidi ya vilabu vya Ulaya.
Mojawapo ni klabu ya Uswizi ya Basel, ambaye rais wake, Bernhard Heusler, alimsajili Salah hapo kwa hapo.
"Kulikuwa na baridi kali lakini alionyesha mchezo mzuri. Alicheza kipindi cha pili pekee lakini sijaona mchezaji mwenye kasi katika maisha yangu yote'', alisema Heusler.
Wachezaji wenza wa Basel wanakumbuka kwamba Salah hakuchezshwa mara moja. Katika mwaka wake wa kwanza katika klabu hiyo mchezaji huyo alitumiwa kama mchezaji wa ziada na ni katika mechi 10 pekee kati ya 29 ambapo alicheza kwa zaidi ya saa moja.
Mchezaji mwenza Philipp Degen, aliambia Sky Sports habari kuhusu Salah alivyomshangaza kila mtu baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Chelsea katika mechi ya kombe la vilabu bingwa.
Salah akiichezea Basel
Salah alijiunga na Basel mwaka 2012 baada ya kucheza kipindi kimoja pekee ya mechi dhidi ya timu ya Usiwzi
"Tulijaribu kumpa hongera lakini hakukubali. Anasema kuwa alipiga nje mikwaju sita na ni wa saba tu pekee kwa kuwa klabu ilimuamini. Umaruufu wake pia unatokana na kuwa mfuasi mkuu wa dini ya Kiislamu.
Anapendwa sana nchini Misri wakati ambapo taifa hilo limegawanyika katika misingi ya kisiasa ilioanzishwa mika michache iliopita na maandamano ya Uarabuni na mapinduzi ya 2013, lakini Salah anapenda mizizi yake.



Amelipia ujenzi wa shule na hospitali na kuweka jina lake katika mashirika ya hisani ikiwemo kuchangisha $280,000 kwa hazina ya serikali inayolenga kuimarisha kiuchumi familia za Wamisri masikini.
Picha ya Mo Salah mjini Cairo
Mchezaji huyo ni shujaa wa taifa lake la Misri.
Utata unaozunguka jina la Salah unashirikisha madai kwamba alikataa kusalimiana na wachezaji kutoka klabu ya Israel ya Maccabi Tel-Aviv katika mechi dhidi ya Basel mwaka 2013 - alienda kubadili viatu vyake kabla ya mechi kuanza wakati huo raia wengi wa Misri walikuwa wamepinga vitendo vyake na hata kumtaka mchezaji huyo kutoshirikishwa katika mechi ya ugenini ya Israel.
Hata hivyo mbali na kuzomewa na mashabiki wa Maccabi Salah alicheza mechi ya ugenini na kufanikiwa kufunga bao.
Wiki iliopita baada ya raia huyo wa Misri kuisaidia Liverpool kushinda 5-2 dhidi ya Roma katika kombe la vilabu bingwa, Waziri wa Ulinzi Avigdor Lieberman alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter kwamba atampigia mkuu wa utumishi wa umma kumsaini Mohammed Salah kwa mkataba wa kudumu na jeshi la Israel.

Chanzo: BBC
Picha: Getty Images