UCL: FAHAMU MACHACHE MECHI YA REAL MADRID VS ROMA
Mechi itachezwa katika dimba la Santiago Bernabeu saa 4:00 usiku saa za Afrika Mashariki. Mwamuzi atakua ni Mfaransa Bjorn Kuipers. Madrid imeshinda mara 3 dhidi ya Roma katika mechi 3 zilizopita.
Timu hizi zimekutana mara 11 katika ligi hii ya mabingwa barani Ulaya wakati Madrid ikiwa na rekodi ya kushinda mara 6 katika mechi hizo ikisuluhu katika mechi 3 wakati Roma wamewahi kuifunga Madrid mara 1 tu.
Ni mechi 1 tu katika mechi 10 zilizopita ambayo Roma haikufungwa na Madrid na ilikuwa ni Oktoba 2002, ilishinda 1-0 katika dimba la Madrid Santiago Bernabeu goli lilifungwa na Fransesco Totti.
Msimu wa 2017/2018 Madrid ilikuwa timu ya kwanza kutwaa kombe hili mara 3 mfululizo ikilinganisha rekodi na Bayern Munich ya Ujerumani iliyowahi kushinda mara 3 katika mwaka 1974, 1975 na 1976.
Madrid wanacheza michuano hii mara ya 22 mfululizo na kuwa timu yenye rekodi ya muda mrefu katika michuano hii. Katika michuano 8 iliyopita Madrid walifika hatua ya nusu fainali.
Madrid wameshinda mara 22 katika michezo 25 kwenye hatua ya makundi wakiwa nyumbani, walisuluhu mara 3 na bila kupoteza. Walifungwa mara ya mwisho na AC Milan magoli 3 dhidi ya magoli 2. Hii ilikua ni msimu wa Oktoba 2009.
Madrid hawakufunga katika mechi 1 tu katika michezo 56 ya ligi hii ya mabingwa barani Ulaya katika hatua ya makundi na ilikua ni dhidi ya PSG, walitoka suluhu ya bila kufungana Oktoba 2015.
Roma wanashiriki mara ya 11 sasa katika ligi hii (UCL), Juventus wameshiriki mara 19, AC Milan mara 17 na Inter Milan mara 12, hizi ndizo timu 3 zilizoshiriki mara nyingi zaidi katika ligi hii katika timu za nchini Italia.
Katika msimu uliyopita Roma ilifikia hatua ya nusu fainali ambayo ilikua ni mafanikio makubwa kwao katika ligi hii tangu walipopoteza katika finali ya ligi hii mwaka 1984. Wameshinda mechi 1 tu katika 15 walizocheza ugenini, walisuluhu 5 na kupoteza 9.
Madrid wanashiriki bila Cristiano Ronaldo aliyejiunga na Juventus majira ya joto msimu uliopita baada ya michuano ya Kombe la Dunia. Mreno huyo amehusika kwa 50% katika magoli yote ya Madrid tangu msimu wa 2009/2010 hadi 2017/2018 katika ligi hii. Alifunga magoli 105 akisaidia magoli 27 yaliyofungwa.
Edin Dzeko mshambuliaji wa klabu ya Roma amefunga katika kila mechi katika 5 alizocheza na klabu ya Roma katika ligi hii.
Jesús Vallejo wa Madrid na Javier Pastore watakosa kushiriki mechi ya leo kutokana na majeraha.
Comments
Post a Comment